CHADEMA, uislam na waislam!

CHADEMA, uislam na waislam!

Status
Not open for further replies.
kumekuwa na upotoshaji au propaganda kwamba chadema hakipikiki chungu kimoja na waislam walio wengi(sio wote),je suala hili ukweli wake ukoje?na je ni wapi hasa kama papo wanapotofautiana na kushindwa kuaminiana?je tatizo kama lipo kweli lipo upande gani,kwa waislam ama kwa jinsi chadema yenyewe ilivyojiweka na kuikalia kimya propaganda hii hatari.

ushauri wangu kama tatizo lipo kwa waislam kutokana na kulishwa tu propaganda basi tuwasaidie na kama tatizo lipo upande wa pili kwa maana ya chadema basi muda upo ijirekebishe na kuondoa sintofahamu hii kwa maslahi yake binafsi kama chama cha siasa chenye hamu ya kushika dola siku moja kwa kuwa ni ukweli ulio wazi bila kura za watanzania wote ambao kwa asilimia kubwa ni waislam na wakristo kwa umoja wao hakuna uwezekano wala njia ya mkato ya kushinda uchaguzi wa rais na kuunda serikali.

Nawasilisha.

DSC08501.JPG

Viongozi wa dini ya kiislamu mkoa wa Kilimanjaro.



DSC08536.JPG

mbunge wa jimbo la Moshi mjini Philemoni Ndesamburo akiteta jambo na viongozi wa dini ya kiislamu,huu ni mfano wa kuigwa




SDC10404.JPG


safi sana hii


Chadema+na+Idd+1..JPG



Chadema+na+Idd+3..JPG


Hii ni namna bora zaidi ya kujenga mahusiano na kuaminiana,iendelezwe na viongozi wa chadema mikoani na wilayani,kamwe chadema isidhani hii propaganda itaondoka yenyewe tu hapana they have to do something kujionyesha hawako upande wa kanisa na hawawachukii waislam kama waislam wengi wanavyoaminishwa na pia wana chadema mmoja mmoja pia mkisaidie chama kwa kuwa polite kwa waislam na wala msiwakejeli kwa namna yeyote ile bali muwasaidie kukielewa chama chenu,muwe mabalozi wazuri wa chama chenu,waislam watawaelewa na kuwakubali tu
Haturudii kosa na wala hatudanganyiki. nyie kuleni umbwabwa wenu na hao mashehena ubwabwa yenu.
halafu nikuulize swali we mleta hii thread, nani kakuambia kuwa uislam ni kanzu na kofia?
 
Mliji changanya sana kumsimamisha Padri Mstaafu kuwa Mgombea Urais,na makanisa yakawa yanatoa approval kuwa hata kama Padri hajaoa sio tatizo kuongoza nchi! Na matamko ya Roman Catholic nayo kipindi yalizidi,siku hizi wameacha! Naona hapa ndipo mlipo jipambanua!
Una ushahidi? Unaweza ukatuwekea hapa hilo tamko la kanisa?
 
Mi nadhani hapa tatizo ni lilelile, Elimu..
Elimu ndogo inazuia uwezo wa kuchanganua mambo kwa upana wa kutosha, na ni hapo ndipo viongozi wa dini wenye hisia za siasa wanapoingia na kutumia ushawishi wao kuweka mambo ya siasa kwa interest zao.

Chukua watu wanaomlaumu dr slaa kama mdini, kikubwa wao wanasema aliwahi kuwa padri, lakini hiki hakiwezi kuwa kigezo cha mtu kutokuwa objective kwenye kazi yake. Rais mstaaf alhaji A.Mwinyi alikuwa rais muislam anaipenda hasa dini yake lakini dhahama inayotolewa sana mfano na waislam kama mfano wa unyanyasaji kwao ya mauaji ya Mwembechai ilitokea kipindi chake, sipati picha kama jambo kama hilo litokee na m2 kama dr slaa awe madarakani, wangesema aliingia madarakani kwa lengo hilo tu, la kuua watu wa imani tofauti na yake.

Mtu mwenye elimu nzuri anajua wapi anadanganywa na wapi anaambiwa kweli, kwahiyo anakuwa na nafasi ya kuamua yeye binafsi, mtu anaambiwa chadema haipendi waislam lakini uongozi wa juu kwa maana ya mwenyekiti na manaibu wake kuna waislamu wanne na wakristo wawili, kwa maana ya makamu wa bara na visiwani na naibu katibu hawa ni watu wakubwa ambao wanaingia vikao vyote vya siri vya chama, kama kina uadui na waislam lazima watajua ..ina maana hao ni wasaliti wa uslam? Dr slaa amewahi kuwa mbunge na kiongozi kwenye chama, ameuathiri vipi uislam? Hivi mtu kama Lipumba na Cuf yake wamewaathiri vipi wakristo? Waafrika tulio wengi hatupendi kufikiri kwa hiyo tunapenda watu wafikiri kwa niaba yetu, na wao hawawezi kuifanya kazi hiyo bure, watafanya kwa maslahi yao, na kama linagusa haraka hisia zetu basi hilo ndo linalipa zaidi..
 
CHADEMA ITAMKE WAZIWAZI JINSI ITAKAVYO TATUA TATIZO LA WAISLAM HAPA TANZANIA KUJIONA KUWA NI JAMII ILIYOBAGULIWA KATIKA ELIMU,AJIRA ZA UMMA,HUDUMA ZA AFYA,UMASIKINI KATIKA UKANDA WA PWANI WENYE WAISLAM WENGI,ITAMKE KUIVUNJA BAKWATA NA KUUNDA CHOMBO CHENYE TIJA KWA TAASISI ZOTE ZA KIISLAM,KUZIPA RUHUSA NA USALAMA KWA TAASISI ZA KIMATAIFA ZINAZOSAIDIA JAMII ZA WAISLAM DUNIANI KWANI KWA SASA HAZIPO TENA TANZANIA KWA KIGEZO CHA PROPOGANDA ZA UGAIDI ZINAZOENEZWA NA MAREKANI.hayo yakifanyika nina uhakika CHADEMA itakonga nyoyo za waislam kwani kwa sasa hawana wa kuwasikiliza

ipo dhana kwamba waislam wengi (sio wote)wanaiunga mkono ccm,kama hilo ni kweli unadhani ni kwanini ilhali ni wazi ccm pia haijaweza kuyafanya hayo uliyoshauri mfano kuivunja hiyo bakwata na mengine uliyosema kwenye andiko lako hapo juu?
 
Hata Nyerere alipohamia Daru ssalam na kukaribishwa na Waislam, aliacha kuvaa kaptura yaani suruali fupi na kuanza kuvaa kibaraka shehe na hata kufunga swaumu siku nzima mpaka kichwa kikamuuma na kuomba apewe aspirini lakini alinyimwa dawa na kuombwa asubiri mpaka futari na baada ya kufuturu na Waislamu Nyerere hakusikia maumivu ya kichwa tena!

Sasa viongozi wa chadema wanachotakiwa kufanya sio kula pilau na Waislamu bali kuingia mkataba na Waislamu kuwa wakishika dola basi watashughulikia kero na madai ya msingi ya Waislamu kuwa...

1. Elimu itakuwa haki ya msingi kwa kila raia na hakutakuwa na ubaguzi wa rangi, dini, jinsia au jiografia kama ilivyo sasa!
2. Shule zote za Waislamu zilizotaifishwa na Nyerere wakati wa azimio la Arusha 1967 wanarudishiwa wenyewe!
3. Mgawo sawa wa madaraka ya nchi na sio dini moja tu kuhodhi kila sehemu!
4. Waislamu wawe huru ndani ya nchi yao kutangaza dini yao bila kuingiliwa na Serikali au Kanisa! mradi wanafuata sheria!
5. na mengine mengi yatakayochangiwa!

Chadema wasijidanganye kuwa watarudisha imani ya Waislamu kwa kula nao Pilau au biriani bali wanatakiwa kutumia mbinu muafaka na mbinu kama hizi hutumiwa hata Marekani na nchi nyingi duniani! hata Kenya Odinga na ODM aliingia Mkataba na Waislamu wa Kenya ktk uchaguzi uliovurugika wa 2007!


kwenye hiyo namba mbili hapo juu,hebu tujiulize kwanza kabla ya kudai turejeshewe shule zilizotaifishwa,hivi hizi shule tulizonazo mfano kinondoni na al haramain pale kariakoo zipo kwenye mazingira gani?mi nadhani tungejikita kwenye kuziboresha tulizo nazo sasa kwanza,jk alipoingia madarakani viongozi wa bakwata walipomuomba arejeshe shule zilizotaifishwa nakumbuka ilikua arusha kwenye baraza la idd au maulid aliwauliza hili swali kuna marehemu gorogosi wakawa hawana jibu la maana
 
Haturudii kosa na wala hatudanganyiki. nyie kuleni umbwabwa wenu na hao mashehena ubwabwa yenu.
halafu nikuulize swali we mleta hii thread, nani kakuambia kuwa uislam ni kanzu na kofia?

uislam ni nini sheikh wangu?
 
waislamu feki hao au mambumbumbu, mwislamu wa kweli ambaye ni MUUMINI wa dini yake na anaielewa vizuri CHADEMA hawezi kuishabikia hata siku moja.km umeelewa hakuna haja ya kubishana hapo
 
Kuvaa kofia baraghashia na kupiga picha na waislam haitoshi hio cheap propaganda cha muhimu ni muhimu ni kufunguka ki sera na muelekeo
Bado kuna tatizo la kuamini malengo na nia ya CDM. Dhidi ya Waislam na uislam kwani hata zao ni za Mehemko kama ya kilokole so yaliyojificha ndani ya moyo zao ni makubwa kuliko yale wanayoengea wakivaa baraghashia kusanif waislam

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
Watu wasio na elimu ukiwalisha jambo fulani huwa wanalikariri kweli kweli na kuliondoa inakuwa taabu sana. Hata CDM ingeiwahi CCM na kuwaambia waisilamu kuwa CCM ni ya makafiri, nakwambia leo hii waisilamu wangekuwa wanaichukia CCM bila hata kufanya their own judgemement. Kwa hiyo hapa inategemea nani alianza kuwalisha sumu hawa jamaa!
 
CHADEMA.

Nyumbani kwetu kuna kitu kinaitwa "Kuhiga" ni uwindaji wa wanyama kwa staili ya kuiga sauti zao au kutengeneza umbo linalofanana na mnyama unayemuhitaji.


kwa hiyo, unakaa kwenye kichaka ambapo wewe unaweza kumuona kwa urahisi mnyama unayemuwinda, na wenzako wana Bunduki "Gobole". Unapuliza sauti ya mlio wa huyo mnyama kwa staili ya mwenzao anapowaita akiona chakula. wale wanyama wanakuja na wanapokaribia kichaka kile tu, wenzako wenye Bunduki wanachagua wanyama walionona na kuwapiga risasi na kuanguka palepale kwisha kazi.

Au unatengeneza sanamu linalofanana na mnyama na kulipaka mafuta yenye harufu ya mnyama unayemuhitaji kisha unaliweka pembeni jirani na njia wanayopenda kupita wanyama hao. Na kweli wanyama hao wakifika hapo wanasikia harufu ya mwenzao na kwa kuwa wanamuona ni mgeni hapo mawazo yao ni kumfuata. hapo ndipo mkiwa na Bunduki mnawatwanga risasi kama mchezo vile.

Mifano hii ni hao CHADEMA sasa wamejificha kwenye Kichaka wanapuliza sauti ya Kiislam ili waislam wajue ni wenzao.

CHADEMA wametengeza sanamu la picha ya Uislam ili waislam walifute kisha.........

NINAWAOMBA WAISLAM TUWE MACHO KICHAKA MNACHOTAKA KUKIFUATA MKIDHANI NI WENZENU SIYO WENZENU HAO
NINAWAOMBA WAISLAM TUWE MACHO HUYO ALIYESIMAMA SIYO MUISLAM NI SANAMU MKILIFUATA MMEUMIA
 
propaganda dhidi ya cuf na chdm hazijafanywa na ccm peke yake. vyombo vyetu vya habari navyo vimechangia. haviendeshwi kiueledi! kama alivyo sema mchangiaji mmoja kuwa picha za mbowe, slaa na ndesamburo wakiwa na waislamu huwa hazipewi front page coverage. kutokana na propaganda ya ccm na uzembe wa vyombo vya habari, mbowe na slaa huwa wanapewa front page photo wakiwa na maaskofu.

kwa upande mwengine, vyombo vya habari huwa vinaweka picha za wafuasi wa cuf wenye baraghashia, shungi, kanzu na ndevu. wafuasi wa cuf ambao hawana muonekano huu huwa hawaoneshwi. hali hii imewafanya wakristu waamini kuwa lisemwalo kuhusu cuf na waislamu ni kweli. vilevile waislamu huendelea kuamini kuwa lisemwalo kuhusu chdm na wakristu ni kweli.


piga, ua, garagaza, imani hizi haziwezi kufutika. wakristu wengi wataendelea kuamini kuwa cuf ni chama cha waislamu na waislamu wengi wataendelea kuamini kuwa chdm ni chama cha wakristu. mtanzania akisha lishwa imani fulani, kumbadilisha ni kazi ngumu! huo ndiyo ukweli. mtanzania akiamini simba au yanga kumtoa huko ni kazi ngumu.

ukiangalia nchi zilizo tuzunguka, utabaini kuwa vyama vingi vikongwe vya siasa vimeangushwa. vilabu vingi vya mpira vinapanda na kushuka. siyo hapa bongo. timu ni simba na yanga kila mwaka japo azam wanawasumbua kiasi fulani.

siyo kwamba nakukatisheni tamaa watanzania wenzangu. tuendelee kuunga mkono mageuzi lkn kwa hapa kwetu kazi ipo.
 
Mliji changanya sana kumsimamisha Padri Mstaafu kuwa Mgombea Urais,na makanisa yakawa yanatoa approval kuwa hata kama Padri hajaoa sio tatizo kuongoza nchi! Na matamko ya Roman Catholic nayo kipindi yalizidi,siku hizi wameacha! Naona hapa ndipo mlipo jipambanua!
Mti wenye matunda ndo unaopigwa mawe,wenye propaganda watashindana sana lakini hawatashinda,
nashauri CDM wajielekeza zaidi Zanzibar,Tanga n.k. Ushindi wa CDM upo wazi,
 
Hata mimi nilikuwa nikidhani haya maneno maneno ya migawanyiko ya dini na siasa yanaelekea kupamba moto. Ila hali ya Mtwara imenihakikishia kwamba masikini wa mali sio masikini wa akili,

Chadema mtafanikiwa iwapo tu mtaendelea kuelimisha wa Tanzania wajitetee kwa umoja bila kujali itkadi, dini au blah blah nyingine.
 
Mkuu amini usiamini nchi hii haitakaa ishikwe na muislam tena.

Muislam hana matatizo, udhaifu wa Kikwete usipelekwe na kusambazwa kwa waislamu woote, aidha, udini wa Kikwete na Mwinyi usihusishwe na waislamu wote. Hilo ni kosa.
 
Mi nadhani hapa tatizo ni lilelile, Elimu..
Elimu ndogo inazuia uwezo wa kuchanganua mambo kwa upana wa kutosha, na ni hapo ndipo viongozi wa dini wenye hisia za siasa wanapoingia na kutumia ushawishi wao kuweka mambo ya siasa kwa interest zao.

Chukua watu wanaomlaumu dr slaa kama mdini, kikubwa wao wanasema aliwahi kuwa padri, lakini hiki hakiwezi kuwa kigezo cha mtu kutokuwa objective kwenye kazi yake. Rais mstaaf alhaji A.Mwinyi alikuwa rais muislam anaipenda hasa dini yake lakini dhahama inayotolewa sana mfano na waislam kama mfano wa unyanyasaji kwao ya mauaji ya Mwembechai ilitokea kipindi chake,

..

Mwinyi hakuwa Rais mauaji ya Mwembechai bali Rais alikuwa Mkapa na mauaji hayo yalifanyika 28.2.1998 miaka mitatu baada ya Mwinyi kustaafu! historia haifutiki mkuu!
 
watu wasio na elimu ukiwalisha jambo fulani huwa wanalikariri kweli kweli na kuliondoa inakuwa taabu sana. Hata cdm ingeiwahi ccm na kuwaambia waisilamu kuwa ccm ni ya makafiri, nakwambia leo hii waisilamu wangekuwa wanaichukia ccm bila hata kufanya their own judgemement. Kwa hiyo hapa inategemea nani alianza kuwalisha sumu hawa jamaa!

dah kazi mnayo hiki kibanzi kwa namna hii hakiweki kukutokeni....badala ya kuona kwamba hii ni challenge unaanza watu wasio soma...hii ni changamoto ambayo chedema wanayo na wanapaswa kuindoa kwa vitendo na sio kusema watu wasio soma...wakati waislam walio soma ndio wengi wanayo ikataa chadema.....
Kujifanya mmesoma lakini hamkuelimika...tizo la necta...kuchakachua
mtu alosoma hajianiki na kutangaza mie nimesoma mie nimesoma..ukimuona hiyo basi ujue wa kocopy na ku paste
 
propaganda dhidi ya cuf na chdm hazijafanywa na ccm peke yake. vyombo vyetu vya habari navyo vimechangia. haviendeshwi kiueledi! kama alivyo sema mchangiaji mmoja kuwa picha za mbowe, slaa na ndesamburo wakiwa na waislamu huwa hazipewi front page coverage. kutokana na propaganda ya ccm na uzembe wa vyombo vya habari, mbowe na slaa huwa wanapewa front page photo wakiwa na maaskofu.

kwa upande mwengine, vyombo vya habari huwa vinaweka picha za wafuasi wa cuf wenye baraghashia, shungi, kanzu na ndevu. wafuasi wa cuf ambao hawana muonekano huu huwa hawaoneshwi. hali hii imewafanya wakristu waamini kuwa lisemwalo kuhusu cuf na waislamu ni kweli. vilevile waislamu huendelea kuamini kuwa lisemwalo kuhusu chdm na wakristu ni kweli.


piga, ua, garagaza, imani hizi haziwezi kufutika. wakristu wengi wataendelea kuamini kuwa cuf ni chama cha waislamu na waislamu wengi wataendelea kuamini kuwa chdm ni chama cha wakristu. mtanzania akisha lishwa imani fulani, kumbadilisha ni kazi ngumu! huo ndiyo ukweli. mtanzania akiamini simba au yanga kumtoa huko ni kazi ngumu.

ukiangalia nchi zilizo tuzunguka, utabaini kuwa vyama vingi vikongwe vya siasa vimeangushwa. vilabu vingi vya mpira vinapanda na kushuka. siyo hapa bongo. timu ni simba na yanga kila mwaka japo azam wanawasumbua kiasi fulani.

siyo kwamba nakukatisheni tamaa watanzania wenzangu. tuendelee kuunga mkono mageuzi lkn kwa hapa kwetu kazi ipo.

strong point member,umesema vizuri sana na kwa kuongezea tu ccm ndio kinajionyesha chama cha wote,hii haijaja bahati mbaya ni strategy ya muda mrefu lakini bahati mbaya wapinzani cuf na chadema wako usingizini wakiota ndoto za nani mpinzani mkuu wa ccm kati yao,yani kila mmoja anaota na kupigania kuwa chama kikuu cha upinzani tanzania!wapenzi wao wako tayari kutoana macho kwa ajili hiyo tu! shame on you guys
 
Kwahiyo chadema kiytachaguliwa na wakirisito tu?

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Jibu la SUALI/MASUALI lako utalipata hapa hapa, nakuomba usome kwa makini comment za wachangiaji 95% utapata majibu kama CHADEMA kipo kwa ajili ya nani na kimesimama kwa dhidi ya nani!
 
Wala haitaji kuwa na PhD kujua mlengo wa Chadema.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom