CHADEMA: Tujadili Utayari wa Kutawala Nchi 2015

Mchambuzi unachambua sana bana.. waTZ wavivu kusoma ujue.

Ebu nishauri dada yangu, niwe nafanya nini ili iwe rahisi zaidi; nimewahi andika fupi, lakini naishia kuambiwa na baadhi ya watu kwamba its too shallow and falls short of a good analysis;
 
Tuko pamoja Mchambuzi Mkuu! Kusema kweli nimependa uchambuzi wako wa kujenga, na kama ni wa kusikilizwa utaleta tija kubwa kwa chama.

Tatizo kubwa ninaloliona katika vyama vyetu, ni kuwa watu hukimbilia kupinga kila neno kwa kupinga tu, bila ya kuchukua hata dakika chache za kutafakari mawazo mbadala.

Kitu kilicho wazi ni kwa saa ya mabadiliko Tanzania imewadia - ingawaje njia bado ni ngumu.

Na kuongezea tu, ni dhahiri kwamba tumeshakomaa na tupo tayari kwa demokrasia ya kupokezana vijiti, na aliyepo karibu katika hilo ni Chadema, ndio maana ni muhimu tukabadilishana mawazo juu ya changamoto walizonazo; mimi ni mwana CCM lakini sioni tatizo kuwa chama cha upinzani mwaka 2015 iwapo Chadema itashinda, na mwana ccm yoyote mwenye msimamo tofauti na mimi ni aidha:

* CCM inampa immunity kutokana na ufisadi alioufanya akiwa madarakani na immunity hiyo itakufa siku chadema wakichukua uongozi wa nchi au
*Kwake yeye maana ya uongozi ni kutimiza mahitaji ya tumbo, sio ya wananchi;

Vinginevyo, let the people speak, na tutajua kwenye sanduku la kura; kama ni CCM 2015 au Chadema 2015 - LET THEM SPEAK!!!
 
.......Watanzania wapo (hasa vijijini) wapo katika mkao wa kupata uhuru wao wa kiuchumi miaka 50 baada ya TANU/CCM kushindwa kufanikisha hilo;
Ndio maana nakuambia kujihusisha sana na TANU bila kuweka rollback option kunaweza kusiwe na faida sana..Yaani wajihusishe na TANU kwa uangalifu basi wawe na jinsi ya kupunguza makali ya musiano yao kiasi ambacho wengine wakijenga hoja mbaya inakuwa rahisi wakata effects.TANU walikuwa big failure na kuna wazee wanakumbuka hilo.Uhuru wetu haukuwa taabu kihivyo kwani UN walihitaji kutuamini tuu halafu waingereza wajiandae ondoka.Hapo palitegemea sana uongozi uliokuwepo na ukomavu wa chama kama kinavyoonekana kwa vigezo vya wakoloni na jumuia ya kimataifa.Nyerere aliweza vifanyia kazi na kwa vile alisoma katika mifumo yao na alivuka sana viwango vyao ya ushupavu na ujanja.Haikuchukua muda kuaminika na kuachiwa nchi.Ndio uhuru unahusishwa na speech yake katika UN zaidi ya blah blah za wazee wa Dar,wanaodai matunda ya uhuru miaka yote na si kujiuliza ujenzi wa taifa.Wengi wa wazee wa mikoani wanakumbuka michango yao ya kumuwezesha kukamilisha safari hiyo.Hao wanaojiiita sijui wagombea uhuru walimpisha Nyerere kwa vile alikuwa na ujasiri na uwezo wa kujengea hoja,za kutosha mlainisha yeyote ajae mbele yake.hata wale wanaomchukia Nyerere walizungumza asipokuwa,ila walipokutana naye ana kwa na ama watubu n akujisikia fedheha kuwa hawakutumia akili kabla ya kutenda kuwa walikuwa wajinga.


kwahiyo nachosema hapa ni kwamba harakati za Chadema limeanza kuwakumbusha wananchi hasa wa vijijini vuguvugu la TANU, na baadhi yao wanaanza kuamini kwamba pengine malengo yale ya TANU ya kuwaletea ukombozi wa kiuchumi yatafanikishwa na Chadema; Kwahiyo Chadema hawana haja ya kuzama kwenye itikadi za TANU bali kuelewa watanzania hasa wa vijijini wamekuwa wanasubiri mapinduzi ya namna gani na kwanini waliamini TANU ingeweza kuwaletea mapinduzi hayo, thats all.
Sikatai kuwa kuna mambo mengi mazuri yanaweza anzia vijijini, ila nijuavyo vijijini kama si mazao, au magonjwa,vibarua, waganga wa jadi,wacheza ngoma hakuna mafanikio ya kuwavutia wanakijiji yanaweza anzia huko?Ndio maana CCM hawajafanikiwa sana pamoja na kuwa na idadi kubwa ya wanachama vijijini, pamoja na kuwa na unlimited access ana control ya fikra za watu wa vijijini.CCM wamekuwa dismantled kirahisi.Wanaonekana wa kizamani wakati CDM wanaonekana wa kisasa.Muulize Shigongo story zake characters wake walivyo inspirational vijijini,na kwa watu ambao hawana muda tangu watoke vijijini.Vijijini huwa wanaendeshwa na miji ndugu yangu.Wanazalisha kutokana na wapendavyo mjini.wanatafuta hela ili wapate mengi yapatikanayo mjini, wana kiu ya ustaarabu wa mjini.Kama una bisha uliza kwanini HIV haina mipaka vijijini?Kwa vile watu wa mijini huwa wanavutia sana vijijini, wanavumilika zaidi, wana dekezwa .Kama unabisha siku ukienda kijiji chochote au hama mji mmoja nenda mwingine uone jinsi unavyowe jikuta wanawake si tuu kuwa ukiwataka wanakuwa wepesi, bali wao wenyewe hawawezi subiri kukutaka.Na jinsi watu wengine wanavyopenda shirikiana nawe,mpaka pale utakapoji behave vibaya ndio watabadilika na kuwa kinyume.Ila bado kuna kitu utakiona"uvumilivu wao juu ya mapungufu yako".

CDM wanahitaji ku seize hii opportunity. Watu wana kiu ya mambo ya kisasa(Habari ya CDM ni km ya celebrity) huko vijijini, na kwa vile wameanzia MJINI wanafaninishwa wa usasa(modernity) na uwepo wa vijana(vijana wana haiba sana kwa uma-Kuwa kijana wa kiume katika jamii ya wanawake kunakufanya ugombaniwe, same kwa upande w wapili-Hii ni youth effect ambayo hata JK alitumia, cameron pia),Kung`ang`ania TANU ni kuwaambia watu kuwa upo boaring kama ngoma walizozichoka kijijini.Hii inauzika mjini kwa watu wanaopiga tumba kes uchovu wa kukosa IDENTITY wakitaka jidai kuwa wana feeling na African culture(huku hawaijui)


Bottom line is - Chadema wanaweza kabisa kumtupa jongoo (TANU) lakini sio mti wake (mambo ambayo TANU ililenga kimkakati kuwakomboa watanzania hasa wa vijijini).

Nicholas:
Naomba unisaidie kujibu swali hili: je, Chadema wana njia gani mbadala ya kuwakmboa small peasants vijijini ambao waliunga mkono TANU?

Kuitoa CCM(TANU ya Jana, wakivua gamba tutapa CCM mpya au TANU ingine) na kushika nchi, kurahisisha mambo kwa kuondoa urasimu katika michakato mbalimbali ya maisha katika nchi na hivyo kuondoa rushwa inayoleta vikwazo kwa masikini na wasiojua hizo njia, kuondoa ufisadi, kutekeleza mipango yote wanayoaminika kuitenda, kujaribu coordinate technologia mpya na za manufaa kwa nch,kuruhu uhuru wa habari na fikra, kuimarisha miundo mbinu, kupanua masoko na kudumisha haki.Mengine yatakuwa yakifanyika na raia wenyewe.

Mkulima atajikuta akiuza mazao ananunua vitu vya kumsaidia kufngua mradi, na huo mradi kufanyika bila vikwazo.Watu watadhamini kazi zao na kufurahia mapato yatokanayo na jasho lao.Leo hii nchi watu wanavunjwa moyo na wizi ufanyikao, wafanya kazi wanaumia kwamba hela yao ya mafao hawaurhisiwi ipata wakiwa vijana ili wajikomboe, wakati watu wasiochangia kwa vile hawakuawahia jiriwa wakizchukia wapendavyo na kuzirudisha watakavyo.Kidogo Mkapa alijitahidi kuwafanya watu waangalie kufanya kazi kama chanzo namba moja cha kujipatia kipato.sasa hivi watu wanaangalia rushwa, siasa, na wizi kama sehemu ya kwanza kupata hela.Watu hawasomi kwa umahiri kwani sasa hivi cheti ndio kikubwa kulika elimu ya kuweza kuongeza ufanisi katika utendaji ambao utaashiria kupata mafanikio ya kipato.
 
Nicholas,

Kimsingi nakubaliana na wewe, lakini nimejieleza zaidi katika majibu yangu mengine kwako kuhusu uwepo wa aspirations za watanganyika whether TAA au TANU au Nyerere alikuwepo au hakuwepo; alichofanya nyerere ni kutumia TANU kujaribu kufanikisha aspirations za wananchi wale; na hata kama ujamaa umefeli, bado haina maana kwamba aspirations za watu hawa huko vijijini ziliondoka na azimio la arusha; Je, unakubaliana na mimi kwamba mtanzania wa kijijini bado anasubiri uhuru wake wa kiuchumi kama alivyokuwa anasubiria mwaka 1961 TANU ilipoleta uhuru wa kisiasa na kuahidi kufanyia kazi changamoto za uhuru wa Kiuchumi? kama utakubaliana nami katika hili, then ni sahihi kufananisha TANU na Chadema in terms of aspirations za walio wengi Tanzania ni zipi pamoja na changamoto zilizopo.

Vinginevyo, mimi nadhani, hata Mzee Mtei akisoma leo hii kitabu cha Mwalimu titled "TANU NA RAIA", nina uhakika atakubaliana na Mwalimu kwa kiasi kikubwa sana, kwani TANU ilikuwa inajaribu kusoma aspirations za watanganganyika, kuelewa mazingira wanayoishi na kuja na njia sahihi ya kufanikisha ndoto zao, ndoto ambazo mpaka leo kwa kiasi kikubwa ni zile zile; tukijaribu kuweka pembeni ushabiki wa jina TANU versus Chadema, huku tukiwa na mentality ya Tanzania kwanza siasa baadae, kwa haraka tutaelewa cherished desires za watanzania walio wengi ni zipi, and subsequently come into agreement kwamba ni zile zile, na kwamba whether tunaijadili TANU, CCM, CHADEMA, TLP, NCCR Mageuzi, CCK n.k, bado ukweli huu hautabadilika;

Ni Muhumu Ukatambua kwamba:

TANU haikujenga aspirations za watanganyika bali aspirations zilikuwepo hata kabla ya TAA au TANU kuzaliwa; ilipozaliwa TANU mwaka 1954, ni kwamba uongozi wa TANU (under Nyerere) ukasoma, na kuelewa, hivyo kuamua kuziwekea mkakati wa kuzitimiza; leo hii hali hiyo haijabadilika; Chadema haiwezi kujenga aspirations za watanganyika walio wengi (ambao ni wanavijiji), kwani zipo hata kabla ya Chadema kuzaliwa mwaka 1995; what chadema can do ni kuzisoma, kuzielewa kisha kuziwekea mkakati wa kuzitimiza kama ilivyofanya TANU (na kushindwa); vinginevyo, bila ya bottom - up approach ya namna hii, na bila ya Chadema kukubali in principle kwamba Changamoto zake leo ni kama za TANU in 1950s, Chadema watakuwa wanapotea kwa kweli na hawatadumu madarakani iwapo watashinda 2015; bear in mind kwamba - Zambia, CCM Yao (UNIP) iliangushwa na Chadema Yao (MMD) lakini leo hii, sio CCM Yao wala Chadema yao ambao wapo madarakani bali Chama Cha PF chini ya Satta - sasa hatujui kama PF ni CCK, NCCR, au chama kipya siku za mbeleni, ndio maana mimi natatizwa na watu wanaosema vyama vimekuwa vingi, viwili vinatosha kuleta ushindani wa kweli (CCM na CDM); hii sio sahihi kwani neither of the two anaonyesha dalili ya kufanikisha ndoto za mwanakijiji, ndio maana sio CCM wala sio Chadema kwa hali ya leo, anaweza kujivunia kwamba atakaa madarakani kwa uhakika kwa muda mrefu; siri iliyopo hapa ni kurejea aspirations za mwanakijiji wa 1950s-1960s na kumuonyesha kwa kila hali kwamba kazi inayoendelea ni jitihada za kufanikisha ndoto zake!
 
ndg Mchambuzi, kumbuka kuwa mengi ya ulioorodhesa kuwa yanatoa advantage kwa CCM yanafanyika KWA BARAKA ZA ccm kinyume cha sheria, na nadhani yatatoweka CCM ikishaangushwa, labda tu useme kuwa yanafanya iwe vigumu kuiangusha CCM.

(a) Nitazungumzia hili la kwanza ambalo wana CCM wamekuwa wakilitumumia kuwa wao ndio walioleta mabadiliko ya kisiasa. Hilo siyo kweli, kwani awali mazingira ya chama kimoja yenyewe yalikuwa ni kinyume cha misingi ya haki za binadamu. halafu mabadiliko yale yalisababishwa na mageuzi yaliyotokea huko Ulaya ya mashariki, ambako ndiko CCM ilikokuwa imetoa model yake ya utawala. Kujidai kuwa tume ya Nyalali iliuliza wananchi kuhusu mfumu upi ufuatwe pia ilikuwa ni kutumia vibaya raslimali za nchi kwani mojawapo ya misingi ya haki za binadamu ni uhuru wa kuamini itikadi yoyote; jambo ambalo lilikuwa limezimwa na huo mfumo wa chama kimoja. Pili idadi kubwa ya watu walioulizwa swali hilo ni wale waliokuwa hawajui maana halisi ya demokrasi, hivyo wakiwa wanachukulia kuwa kuwepo kwa vyama vingi ni uhasama; jambo ambalo serikali makini ilitakiwa ilijue. Iwapo kweli serikali ilikuwa inataka kukusanya maoni ya wananchi, ilitakiwa kwanza iwafundishe wananchi maana halisi ya siasa za vyama vingi ndipo iwaulize kama wanataka mfumo huo.

(b) Jambo la pekee linalotakiwa kusimamiwa na CHADEMA kwa karibu sana sasa hivi ni uendeshaji wa uchaguzi na uhesabu wa kura. Ile tume ya UCHAGUZI na taratibu za kusimamia na kuhesabu kura ndiyo mambo yanayotakiwa kushughulikiwa kwa makini sana sasa hivi kabla ya uchaguzi; baada hapo, hayo mengine yote yatanyooka yenyewe. Nchi zote majirani zetu walifanikiwa kuondoa vyama vikongwe madarakani kutokana na kuwa na tume nzuri ya kusimamia uchaguzi; kwetu hapa hilo bado ni ndoto.
 
Last edited by a moderator:
ndg Mchambuzi, kumbuka kuwa mengi ya ulioorodhesa kuwa yanatoa advantage kwa CCM yanafanyika KWA BARAKA ZA ccm kinyume cha sheria, na nadhani yatatoweka CCM ikishaangushwa, labda tu useme kuwa yanafanya iwe vigumu kuiangusha CCM.

(a) Nitazungumzia hili la kwanza ambalo wana CCM wamekuwa wakilitumumia kuwa wao ndio walioleta mabadiliko ya kisiasa. Hilo siyo kweli, kwani awali mazingira ya chama kimoja yenyewe yalikuwa ni kinyume cha misingi ya haki za binadamu. halafu mabadiliko yale yalisababishwa na mageuzi yaliyotokea huko Ulaya ya mashariki, ambako ndiko CCM ilikokuwa imetoa model yake ya utawala. Kujidai kuwa tume ya Nyalali iliuliza wananchi kuhusu mfumu upi ufuatwe pia ilikuwa ni kutumia vibaya raslimali za nchi kwani mojawapo ya misingi ya haki za binadamu ni uhuru wa kuamini itikadi yoyote; jambo ambalo lilikuwa limezimwa na huo mfumo wa chama kimoja. Pili idadi kubwa ya watu walioulizwa swali hilo ni wale waliokuwa hawajui maana halisi ya demokrasi, hivyo wakiwa wanachukulia kuwa kuwepo kwa vyama vingi ni uhasama; jambo ambalo serikali makini ilitakiwa ilijue. Iwapo kweli serikali ilikuwa inataka kukusanya maoni ya wananchi, ilitakiwa kwanza iwafundishe wananchi maana halisi ya siasa za vyama vingi ndipo iwaulize kama wanataka mfumo huo.

(b) Jambo la pekee linalotakiwa kusimamiwa na CHADEMA kwa karibu sana sasa hivi ni uendeshaji wa uchaguzi na uhesabu wa kura. Ile tume ya UCHAGUZI na taratibu za kusimamia na kuhesabu kura ndiyo mambo yanayotakiwa kushughulikiwa kwa makini sana sasa hivi kabla ya uchaguzi; baada hapo, hayo mengine yote yatanyooka yenyewe. Nchi zote majirani zetu walifanikiwa kuondoa vyama vikongwe madarakani kutokana na kuwa na tume nzuri ya kusimamia uchaguzi; kwetu hapa hilo bado ni ndoto.

Kichuguu, tupo pamoja; msingi wa hoja yangu ni kama ulivyoelezea - kwamba CCM ina advantages na nachojaribu kusema ni kwamba bila ya Chadema kufanyia kazi maeneo haya na pengine mengi zaidi ambayo kimsingi nimeyataja kama "what went right for CCM" (ujenzi wa CCM as a brand, an institution and a politica party) - bila ya chadema kuyafanyia kazi haya, kazi ya kuiangusha CCM 2015 itakuwa ni ngumu sana, hasa iwapo focus itakuwa kwenye "what went wrong for CCM (mapungufu na madhaifu yanayokosolewa na Chadema)"

Kuhusu suala la utaratibu na uendeshaji wa uchaguzi, nakubaliana na wewe, lakini ningependa kuongeza pia kwamba - Chadema inatakiwa waangalie faida na hasara za utaratibu wa sasa ambapo mshindi ni mshindi, hata kama akishinda kwa 50.1% dhidi ya 49.1%; huku pia ikiangalia faida na hasara za muundo mpya ambapo mshindi atatakiwa avuke threshold fulani ya kura, vinginevyo uchaguzi urudiwe; vinginevyo mambo yakibakia kama yalivyo leo, mimi naona Chadema sana sana watafanikiwa kuunda serikali ya pamoja na CCM kama ilivyotokea Zanzibar, sasa tatizo litakuja pale Chadema watapokubaliana na utaratibu huu; au pengine watakataa na kupelekea Chadema kuonekana inataka kuleta machafuko nchini n.k; ni kwa bahati mbaya sana au nzuri (depending unaangalia vipi suala hili), chadema waliwabeza sana CUF kwamba wameingia ndoa na CCM baada ya uchaguzi wa 2010 bila ya kuangalia suala hili kwa kina; hili likiwatokea wao wataficha wapi nyuso zao? Ni moja ya changamoto kubwa sana and i hope wanaliangalia hili kwa kina;
 
Nicholas,

Kimsingi nakubaliana na wewe, lakini nimejieleza zaidi katika majibu yangu mengine kwako kuhusu uwepo wa aspirations za watanganyika whether TAA au TANU au Nyerere alikuwepo au hakuwepo; alichofanya nyerere ni kutumia TANU kujaribu kufanikisha aspirations za wananchi wale; na hata kama ujamaa umefeli, bado haina maana kwamba aspirations za watu hawa huko vijijini ziliondoka na azimio la arusha; Je, unakubaliana na mimi kwamba mtanzania wa kijijini bado anasubiri uhuru wake wa kiuchumi kama alivyokuwa anasubiria mwaka 1961 TANU ilipoleta uhuru wa kisiasa na kuahidi kufanyia kazi changamoto za uhuru wa Kiuchumi? kama utakubaliana nami katika hili, then ni sahihi kufananisha TANU na Chadema in terms of aspirations za walio wengi Tanzania ni zipi pamoja na changamoto zilizopo.
Nashukuru na kukubalina nawe kwa jinsi postings zakohadi sasa zinavyoonesha nia njema zaidi katika kujadili issue na si ghadhabu kama postings za watu wengine ambao huwa zinalipuka haraka.

Nakubalina na wewe katika uliyoyasema kuhusu TANU ambayo kwa upande mwingine naweza sema haina tofauti sana na hiii kemikali maarufu DDT ambayo kwa vipindi vingi baada ya kupigwa marufuku bado ina waumini wanopenda irudisha katika list ya chemikali muhimu katika maisha ya leo, ingawa kwa sura ingine.Museven alikuwa akiipigia debe irudi Uganda ikaue mazalia ya mbu huku aki downplay adhari zake kwa afy aya binadamu kwa vizazi kibao.Kama Slavery na outsourcing ya kazii(Kuna tofauti gani ya Kuifanya china kuwa kiwanda cha dunia huku mishahara ya wafanya kazi haizidi gharama za kutunza mtumwa katika dunia yenye watu wa haki za binadamu, tofauti ni kuwa mtumwa ana uhuru wa kulala kwake na kuangalia budget yake mwenyewe), Colonialism na neo-colonialism.

Uovu wa CCM ni sawa na wa TANU ni sawa ingawa TANU ilikuwa na advantage nyingi.hawakuwa na upinzani kwani dunia ile iliruhusu dictator ku cntrol kila kitu kuanzia fikra za watu hadi maisha binafsi na mpinzani kutoweshwa.TANU ilipa advantage ya kuishi katika ukombozi na cold war issue ilisaidi propaganda.Ila raia wengi hawakupenda na mpaka leo wanakumbuka shule za mkoloni na kuona fahari ya elimu yao(Inajadilika).Propaganda za TANU zilipelekea hata kumbukumbu zote zi glorify chama kuweka legacy.Na kupata kiongozi kama Nyerere aliyeamua chagua wema na kuacha uovu kwa kutumia busara zake na kutazama mapungufu in a positive way kama uchanga wa chama ndiko kuliko fanya historia iachie wema ushinde uovu.Mwenyewe alipa zuia uasi mara kibao ambao ulikuwa haufurahii njia njema aliyoamua ichagua.Ushahidi wa hayo ni Kuzima upinzani wa vyama, habari mbadala, uasi ndania ya serikali na TANU (unaonyesha-palikuwa aspirations tofauti au hawakuzifanyia kazi , Kauli ya Nyerere kuwa Katiba inampa madaraka makubwa angeweza yatumia vibaya sana ni ushahidi kuwa kwa kiasi fulani aliona mapungufu na uozo ila hakuutumia-hii ni kazi binfsi yake ), CCM ya leo ingekuwa malaika kama haka kaukoo ka tabaka la internet kama JF hakawezi pigwa marufuku.CCM wanalia sana kuhusu control ya kila kitu kinachoingia katika public na uhuru wa habari tofauti kwa raia, kwa vile kuna lies nyingi sana wanazoweza tumia kutengeneza supa hero party out of CCM.

Halfu ujue si kweli kuwa successful kila mara successful business wanafuata demands, sometimes wana create demands.wapo watu ambao huwa hawaoni sababu ya kufuata/tafuta masoko huwa wanatengeneza masoko tofauti na kwa jinsi wanavyotaka.Ni kuchagua tuu customer watarajiwa, kuangalia nini cha kuwauzia, na uwauzie vipi kwa kutumia uwezo binafsi wa kifikra. Sidhani kama jamaa waligundua "walkman" walifuata hamu za watu,kwani binadamu hawezi taka kituasichokijua au hata kukiota,au hata ku-experience,ila success yake wanajua wale Taiwanese.same kwa Apple wao.Tablet hawakufuata market kwani ilishakufa na walioajirbu ingia wlaishashindwa bila hata kuwa na upinzani, apple akaingia na kutengeza demand, na kafanya hivyo kwa category nyingi.

Binadamu huwa hana demands za kueleweka kama unavyoweza dhani?Ndio maana wapo very easy kuwa manipulated.CDM bado ni wapole sana na combinationa za karama nyingi zzinawafanya wakubalike inagwa hawafanyai ugaidi wa kumanipulate jamii ili iende wapendavyo kama wafanyavyo CCM,CDM hawajaamua kufanya attack katik amabi ya CCM na kuiboa toka ndani, wao wanafaya fair game ya kuwa detach na jamii.CCM ipo katika slef destruction ndio maana mambo yanawaharibikia kwa kasi na hawawezi nyoosha mikono kueleke wengine kwani wana maumivu kwa ndani.

Mkuu historia ina historia pia,Historia ya mashujaa wetu imepikwa na watu wengi, waandishi wetu wameandika ili kuwafagilia wakidhani ni uzalendo.Wakoloni wan version nyingi sana za mashujaa wetu.wana version ya kutuonyesha sisi,wana version ya kuwaonyesha maadui zao,pale inapotokea wanataka rekebisha mahusiano kwa kitu maalumu na wakati maalumu(wakati wakiwa technically at war.Kama sisi na malawi), wana version ya kuionyesha jumuia ya kimataifa na kuna walioificha kwa vile.Hii waliyoificha ndio inayobeba survival tools of their own kind(race and their civilization).
Ukifanya research utakuta machief wetu habari zao zipo version nyingi sana:

Mfano Mkwawa.
-Kuna tunazosoma shule:Jama ni shujaa sana, alipingana na mkoloni na aliunganisha makabila mengi ya ukanda wote wa uhehe, ubena, kuanzia sijui wapi hadi wapi.Dhana ya umoja ni nguvu inapata nguvu na nia yake ya umoja ili kumuondoa mkoloni.Very inspirational.

-halafu kuna hii ya waafrika utekaji na uvamizi ili kupora na kutawala.Historia za vitabu na kiukoo zinaonyesha kuwa zamani utekaji wa jamii nyingine kwa lengo la kuiba vyuma,mifugo, shanga, vibuyu, mazao ya chakula na mazao dawa na wanawake bila utumwa kipindi hicho mateka waliuwawa,ilikuwa kitu cha kawaida sana.Na kuaminiana kulikuwa kudogo sana hadi laana zikawekwa.

-halafu kuna hii ya waafrika walio chini ya ushawishi wa imani na tamaduni na dini za kigeni.Hapa utakuta jamii za kiislam wanamtazama Mkwawa kama ustaadhi,mwadilifu aliyemkomboa Mwafrika toka katika ukoloni.Mkristu aliyepitia shule za Kikristu wa makanisa makongwe wana historia zao kuhusu Vita ya mkwawa juu ya Ukristu na wamisionary wa mwanzo.

-Halafu kuna Historia ya wamissionary wenyewe wanamuona mkwawa kama mtu aliyetumika na waarabu kuuwateka waafrika wenzake na kuwauza kwa minajili ya dini, pia kama mtu katili sana aiyeshawishika na dini mpya yake akaamua ua wamissionary msaada wa Waarabu na hivyo wanahitaji weka kumbukumbu ya waliokufa kama mashahidi wa Iman.Na hivyo kumbukumbu hiyo inawavuta kuenzi iringa huku wakiibeba hisoria ya Mkwawa kwa mtazamoa utakaotufanya tusikwazike na kuwachukia.

-Halafu kuna historia ya mapepari na Kikwazo alichowawekea katika ushindani wao na waarabu katika kupora rasilimalia zetu.

-Halafu kuna Historia ambayo wanayo wazungu kwa ajili yao na survival yao(Inayojenga utamaduni wa kimagharibi) na hii ni version ambayo si kila mtu anapaswa ijua.Hii ndio inaonyesha historia ya Ustaarabu wa kimangaribi na matukio yaliyohatarisha uhai wao na njia zilizowaokoa.Huku ndipo wazungu wanaangalia Mzuguano wa tamaduni na madhaifu na nguvu za tamaduni za dunia.na njia za kuhakikisha hawafikii pahali pa kukumbwa na yaliyowakutakatika historia kiasi ch akufikia kuokoka kwa sadaka za viongozi mashujaa wa vipindi husika.Mkwawa anatajwa kama Kikwazo na kibaraka katika kusaidia Islamic civilization.na wanachukulia kuwa kawa inspire wengi katika jamii za kiafrika,kiarabu na kiislam kwa ujumla.

-Halafu kuna historia ya muarabu kwa muarabu na hata kwa muislam aliyeshindwa ufanya UIslam kwa minajili ya kiafrika.Hii inamtazama kama uislam safi lakini,pia kwa pembeni muarabu anatazama kama kipindi alichoweza tumia resources vizuri kumwadhibu mzungu bila kujali ni mzungu bepari au Mmissionary ila makafir kwa ujumla.Na hivyo kutazama jinsi atakavyoweza hakikisha survivala ya Arab supremacy kwa mgongo wa dini, na mshikamano na watu wa tabaka nyingine.

TANU ILIANZA CHINI YA WATU WA DINI MOJA, na baadaye dini kumezwa na Utashi wa Nyerere, watu hawakuweza eleweshwa na kuelewa uhalali na uadilifu wa kuondoa influence za dini,ndio maana "UDINI" haukuisha katika mioyo ya watu.Watu hao hao ndio hadi leo wapo CCM na wameibuka kwa nguvu na dhana ya udini kwa nguvu.

Uwezo wetu hautategemea tunakuja na ushahidi kiasi gani wa haya mambo,ila kwa kiasi gani tunaweza soma viashiria fulanifulani vitakavyotupelekea kuangalia Historia vizuri na kupata ukweli.Halafu nasi tufanye maamuzi magumu kwa ujasiri na fikra pana.
 
Nicholas,

Mimi nadhani wengi tunachukulia kama vile jamii zetu kabla ya ukoloni existed in a vacuum. Hii sio sahihi. Vile vile aidha kwa makusudi au bahati mbaya, wengi tuna mazoea ya kutazama jamii zetu kwa jicho la "WEST", kwani hoja zetu nyingi zinaleta tafsiri kwamba mkoloni aliikuta TANU madarakani, akaipokonya madaraka kwa nia ya kuiboresha nchi na watu wake, lakini TANU wakavuruga mipango hiyo, hivyo mkoloni akamrudishia mtanganyika nchi yake kupitia TANU, lakini TANU wakaharibu kila kitu in the long run. Ni vizuri umetaja societies kama zile zilizokuwa zinaongozwa na Mkwawa. Ebu tuzitazame kwa undani kidogo.

Kabla ya ukoloni, kulikuwa na jamii kuu za aina mbili: Kwanza ni zile centralized and highly politicized; pili ni zile zilizokuwa decentralized and stateless.

  • Tuanze na Decentralized societies: Hizi zilikuwa made of jamii/vijiji vidogo vidogo vilivyokuwa vinaishi jirani jirani na havikuwa na any meaningful political units na pia hazikuwa na political connection na jamii kubwa kama za mkwawa zaidi ya mahusiano ya kibisahara;

  • Tukija kwenye Centralized & Politicized Societies: Hizi zilikuwa chini ya himaya ya machifu (e.g Mkwana). Key characteristics za jamii hizi that differentiates na zile decentralized ni kwamba - the chiefs had absolute power; and there was no separation of powers- machifu na washauri wao controlled mfumo wote wa utawala as they carried both the Executive, Judiciary and Legislative duties.

Kumbuka, mpaka hapa hakuna Mkoloni, TAA, TANU wala Nyerere, na jamii hizi zilipiga hatua kubwa sana kimaendeleo. Jamii hizi zilikuwa na uwezo mkubwa kujiendesha kisiasa na kiuchumi, na uwezo huu ulitokana na ukusanyaji wa kodi na tributes mbali mbali hasa kupitia trade control; pia ziliweza kulinda mipaka isivamiwe na maadui. Jamii hizi zilikuwa na ndoto na malengo ya kukabiliana na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na kujitosheleza kwa chakula), kujitosheleza kifedha (kiuchumi) ili kuendesha shughuli za utawala, na muhimu zaidi, kudumisha uhuru wake kwa kulinda mipaka yake yake. Muhimu hapa ni kwamba Jamii hizi:


  1. Zilifanikiwa kukuza sana sekta ya uzalishaji wa Kilimo;
  2. Zilifanikiwa sana kuendeleza tekinolojia ya chuma/new metals technologies;
  3. Vile vile zilifanikiwa sana kukuza sekta ya biashara (trade expansion);

Mkoloni alipoingia Tanganyika, lengo lake kubwa ilikuwa ni kuvuruga mfumo na mafanikio yote haya, hasa uwezo wa kiuchumi uliotokana na efficient revenue system, nguvu za kijeshi, uhuru wa jamii kujiamulia sera kisiasa, kiuchumi, kijamii n.k; Mkoloni alifanikiwa kufanya haya kwa kuwarubuni machifu kadhaa, pia kupitia sera ya ‘divide and rule', na mara nyingine ‘military coercion'. Kwa kifupi, mkoloni alifanikiwa kuzima ndoto za Watanganyika na badala yake, akaleta muundo mpya kabisa wa mahusiano katika uzalishaji (uchumi), mahusiano katika utawala, huku pia akivuruga utamaduni wa mwafrika and install utamaduni na mfumo wake ambao ulilenga to serve interest za serikali ya kikoloni na pia za mataifa mama.

Mkoloni akaanzisha a new government, New Political Practices and New Political Institutions ambazo zilikuwa ni ngeni kabisa (so alien) kwa jamii ya watanganyika; Nahimiza kwamba hadi hapa hapakuwepo TAA, TANU wala Nyerere bali jamii iliyorundikwa kwa pamoja bila ya ridhaa yao, ikapewa jina la "Tanganyika", kisha kuanza kutawaliwa katika kila nyanja bila ya hiyari yao;

TANU na Harakati za Uhuru

Tujitahidi kutazama harakati za uhuru kwa kina zaidi kuliko ndani ya mazingira ya TANU. Harakati kama za Kinjeketile (Maji Maji) na Mkwawa dhidi ya mjerumani zililenga kuondokana na utawala wa kikoloni ambao ulivuruga taratibu za maisha ya watanganyika, huku ikizidi kupoteza uhuru wao wa kisiasa na kiuchumi. Kumbuka tena, hapa hapakuwa na TAA, TANU wala Nyerere. Pia niseme kwamba kidogo umenishangaza unapo downplay harakati za Nyerere kwamba ‘it was an easy walk to freedom' huku ukisahau kwamba kwa ujumla wake, Tanganyika na Kenya kwa mfano, hazipishani sana when it comes to umwagaji wa damu wakati wa mapambano dhidi ya ukoloni; tofauti kubwa iliyopo baina ya harakati za Kenya ni only in contextual terms (especially dates), lakini content wise, hatuna tofauti kubwa sana;

Bottom line mkuu Nicholas ni kwamba, aspirations za watanganyika zilikuwepo kwa muda mrefu sana, hata kabla ya ujio wa TANU na Nyerere, na ushahidi ndio huu wa Kinjeketile na Mkwawa. Kilichotokea ni kwamba TANU ilikuja kuongezea nguvu vuguvugu hili na ikafanikiwa kuwaletea watanganyika uhuru wa kisiasa (somewhat) na kuahidi kuwaletea uhuru wa kiuchumi.

TANU ndani ya Tanganyika huru ilikuwa na majukumu mawili:

a) To restore/reconstruct Tanganyika.
b) To Develop Tanganyika.

Tumeona katika historia jinsi gani Europe was reconstructed baada ya vita vikuu vya pili vya dunia. In actual fact, walijiundia chombo special kwa kazi hiyo – IBRD (International Bank for Reconstruction and Development), ambayo baada ya kufanikiwa, IBRD ikapewa jina jipya – the World Bank kwa lengo la kufanya shughuli ya reconstruction and development in the third woorld (former colonies) kama ilivyofanya kazi Europe. Lakini ili Tanganyika na mataifa mengine huru yafanikiwe to reconstruct and develop, ilikuwa ni lazima wajengewe mazingira kama yale ya Europe chini ya IBRD, lakini haikuwa hivyo, na badala yake, mfumo ule ule wa kikandamizaji ukaendelezwa, na ndio maana Nyerere ajijaribu to delink jamii yetu na mfumo huu wa kidhalimu, hence Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea ili tuweze kuanzia pale mkoloni alipokuja na kutuvuruga, na hii ndio moja ya sababu kubwa kwanini Ujamaa uliungwa mkono nna wengi. Logic ya Ujamaa was a simple as that! Tatizo likaja pale Nyerere aliposhindwa na mradi huu wa delinking, na badala yake kupelekea wananchi kuzidi kuumia;

Mfumo wa kibepari ulishaotesha mizizi mirefu sana, kwahiyo isingekuwa rahisi wa Nyerere kufanikiwa. Na sio kwa Tanzania tu, kwani hakuna nchi yoyote Africa iliyofanikiwa katika hili. Kilichofanya wenzetu kwa mfano wa Kenya au Zimbabwe watuzidi ni kwamba Kenya kwa mfano - mkoloni alitumia muda na rasilimali nyingi kujenga a an indigenous bourgeoisie class (hasa wakikuyu) ili wafanane nae in terms of kumiliki ardhi n.k kwasababu mkoloni alilenga kuishi Kenya moja kwa moja, na kwamba at independence, pasiwe na much ‘class struggle'; kwa bahati nzuri au mbaya (depending unaangalia kwa jicho gani), mkoloni hakufanya hivyo Tanganyika kwani hakuwa na nia ya kuishi (we were not a settler economy), ndio maana hakuwaendeleza watanzania kwa namna yoyote ya maana, badala yake aliwaacha as proletariats (wengi as manual laborers) na pia wakulima wadogo wadogo kama alivyowakuta.

Pia ni muhimu tusijisahau na kuanza kuijadili TANU kama vile Nyerere alipokea nchi (1961) ikiwa na:

· Uwezo wa kujiendesha (political capacity) na pia uwezo wa kuboresha maisha ya watanganyika kwa urahisi;
· Kama vile Nyerere alipokea nchi iliyokuwa inaheshimu human rights and democracy practices wakati wa ukoloni;
· Na pia kama vile watanganyika walikuwa ni homogenous society wakati ukweli ni kwamba ilikuwa na makabila mengi huku baadhi yao mkoloni tayari akiwa ameshayavuruga kiuchumi, kisiasa na kijamii kwa kutumia makabila mengine, huku baadhi ya makabila (na dini) yakiwa yame neemekana kuliko mengine - kiuchumi, kisiasa na kijamii.

Tutazame kidogo masuala ya political capacity na human rights.
1. Political/State Capacity Chini ya TANU: Huu ni uwezo wa serikali kufanya shughuli zake kama to guarantee protection and security kwa wananchi, guarantee haki za binadamu; kuwekeza kwenye miundo mbinu inayohitajika kwa ajili ya shughuli za kiuchumi, to encourage uwekezaji ambao utazaa ajira, kama njia ya kukuza uchumi; kutoa huduma za kijamii kwa wananchi wote – elimu, afya, nyumba, maji safi n.k.
Ili kufanikisha haya, Serikali lazima iwe na vitu kama:

a) Taasisi (institutions) - zinazojihusisha na kila sekta tajwa hapo juu, mfano shule (kutoa elimu), hospitali (kutoa huduma za afya), polisi na jeshi (kwa ajili ya ulinzi na usalama wa raia na mali zao); Pia ni lazima taasisi hizi ziwe na ufanisi wa hali ya juu. Lakini muhimu pia ni:
b) Bureaucrats – wenye ujuzi, ari na moyo wa kutumikia nchi yao; kila taasisi inahitaji watumishi wenye uelewa na ujuzi katika maeneo husika, vinginevyo malengo ya serikali hayawezi timia; lakini kumbuka pia kwamba - ili upate watumishi wa namna hii, ni lazima taasisi za afya na elimu ziwe katika ubora wa hali ya juu vinginevyo ili kuzalisha Human Capital ya maana, vinginevyo mambo hayataenda. Lakini pamoja na umuhimu wa taasisi na human capital, pia kuna suala la:
c) Mapato (Revenue) – bila ya mapato, taasisi na human capital zitakuwa useless unless kuna mapato ya kujenga na ku maintain taasisi hizi, kulipa mishahara mizuri n.k ili huduma bora zitolewe kwa wananchi;

Sasa tofauti na haya, Nyerere hakupokea nchi ikiwa na haya yote in place kwani taasisi, bureaucracy na revenue structure aliyokuta Mwalimu, mkoloni hakuiunda kwa ajili ya kutoa huduma kwa watanganyika milioni tisa on indendepence eve; Sote tunaelewa fika kwamba mkoloni hakufanya lolote la maana kuendeleza wananchi walio wengi kielimu na kiafya; vile vile, mkoloni hakutumia mapato kutoka kwenye kilimo na kodi kuendeleza to diversify uchumi, au to develop miundombinu kwa lengo la kuinua maisha ya walio wengi; Alichorithi Nyerere na TANU ni muundo uliokusudiwa kunufaisha serikali ya kikoloni na mataifa yao makubwa; given haya yote, haina ulazima wa mtu leo hii kujikuna sana kichwa kwa masikitiko kwamba Nyerere's idea to delink us from mfumo wa usiotendea haki wazalishaji wetu, hence sera ya UJAMAA na KUJITEGEMA, was a bad idea. When it comes to Ujamaa, tukijitahidi kutofautisha Malengo, Mchakato, Utekelezaji na Matokeo ya Ujamaa nadhani itakuwa ni hatua muhimu sana katika kuelewa changamoto zetu kama taifa (sio kama wana CCM, Chadema n.k). Tanzania kwanza, siasa baadae!

2. Human rights Chini ya TANU:
Wengi wetu tumekuwa na tabia za kum criticize Nyerere na TANU kama vile mkoloni alimwachia nchi iliyokuwa inaheshimu haki za watanganyika. Je, Nyerere alirithi taifa linalojali rights and freedoms for all individuals - without distinction of any kind, such as race, color, sex, language, religion, political or national/social origin? What about right to life, liberty and security of the people? Jibu ni HAPANA! Haya yote hayakuwahi kuwepo kabla ya mkoloni na hata baada ya mkoloni kuja. Sasa in the midst ya colonial legacy na madhara yake kwa jamii yetu, ili kusonga mbele ilibidi TANU na Nyerere to compromise mengi. Tutazame baadhi:

a) Political rights- Rights of individuals to participate in their own government and provide protection against abuse and oppression by governments. [Je. Nyerere alikuta such rights? NO]
b) Freedom of thought and religion – the notion that everyone has the right to freedom of thought, conscience and religion; hii ni pamoja na freedom to worship/practice religion…[Je. Nyerere alikuta such rights? NO]
c) Economic rights - These include the right to own property, right to employment, rights to an adequate standard of living… [Je. Nyerere alikuta such rights? NO]
d) Social/Distributive Rights - Includes rights to adequate health care for all, a safe and healthy childhood, adequate housing[Je. Nyerere alikuta such rights? NO]
e) Cultural Rights - hali ya kila mtu kuwa na right to freely participate in the cultural life of the community, to enjoy the scientific advancement za jamii n.k [Je. Nyerere alikuta such rights? NO]

Ni kweli Ujamaa ulifeli, lakini in the midst of all this, ningependa kusikia toka kwako je: Nyerere angefanya nini/ au better said – Je kwa mfano Chadema ndiyo ingekuwa Chama mbadala wa TANU, wangeweza kufanya nini? Nadhani majibu yako yatatusaidia kuboresha mjadala wetu juu ya similarities between TANU na Chadema – kwa maana ya changamoto zilizokuwepo waakti ule na zile zilizopo katika mazingira ya sasa. Iwapo utajikita katika kuuponda Ujamaa, jaribu kuujadili in the context of Malengo, Mchakato, Utekelezaji na Matokeo wa Sera hii.

Naamini hii itatusaidia sana kuzidi kusaidiana mawazo kuhusu changamoto za Chadema 2015, hasa tukiweka watanzania wa vijijini at the centre badala ya the periphery kama wengi wanavyofanya katika mjadala wa kuelekeo 2015.
 
Nicholas,

Mimi nadhani wengi tunachukulia kama vile jamii zetu kabla ya ukoloni existed in a vacuum. Hii sio sahihi. Vile vile aidha kwa makusudi au bahati mbaya, wengi tuna mazoea ya kutazama jamii zetu kwa jicho la “WEST”, kwani hoja zetu nyingi zinaleta tafsiri kwamba mkoloni aliikuta TANU madarakani, akaipokonya madaraka kwa nia ya kuiboresha nchi na watu wake, lakini TANU wakavuruga mipango hiyo, hivyo mkoloni akamrudishia mtanganyika nchi yake kupitia TANU, lakini TANU wakaharibu kila kitu in the long run. Ni vizuri umetaja societies kama zile zilizokuwa zinaongozwa na Mkwawa. Ebu tuzitazame kwa undani kidogo.
Sikatai ulichosema ingawa naweza kuwa na tafsiri ingine.Hata wakoloni pia huwa wanajisahau na kudhania kuwa walikujwa istaarabisha Africa kama kusudio la kwanza,ingawa ukweli ni kuwa lilikuwa ni baadaye.Ingawa sehemu kubwa ya ustaarabu uliohamia ulikuja kutokana na mahitajia ya mkoloni na kuelekeo wa dunia.Mfano. kina mtu anafahamua hasara ya kuwa namtumishi wa ndania siyeweza kumudu shughuli mbalimbali za Nyumbani,pamoja na usalama.Kwa mtumishi wa ndani kupelekwa shule ya upishi,shule ya udereva, au hata lugha haikuwa kusudio lakwanza, au hata kujua kutumia vifaa ghali na vya kisasa katika ile nyumba(airconditioner,Micorwave,tea makers etc).

Huyu mafanyakazi anaweza .bosi wake n awatu wa nje wanaweza kuwa na tafsiri tofauti sana katika kuelezea kilichofikisha hayo yote hapo.
Kabla ya ukoloni, kulikuwa na jamii kuu za aina mbili: Kwanza ni zile centralized and highly politicized; pili ni zile zilizokuwa decentralized and stateless.

  • Tuanze na Decentralized societies: Hizi zilikuwa made of jamii/vijiji vidogo vidogo vilivyokuwa vinaishi jirani jirani na havikuwa na any meaningful political units na pia hazikuwa na political connection na jamii kubwa kama za mkwawa zaidi ya mahusiano ya kibisahara;

  • Tukija kwenye Centralized & Politicized Societies: Hizi zilikuwa chini ya himaya ya machifu (e.g Mkwana). Key characteristics za jamii hizi that differentiates na zile decentralized ni kwamba - the chiefs had absolute power; and there was no separation of powers- machifu na washauri wao controlled mfumo wote wa utawala as they carried both the Executive, Judiciary and Legislative duties.
Mkuu hapa pako very illutional, kwani hapakuwa na tawala ya kiafrica iliyokuwa na ustaarabu wenye misingi ya haki kabla na kipindi wakoloni wanaingia.Na kuvuma kwao kipindi cha wakoloni kulichangiwa na watu nje wengi.
Haiwezekani jamii isiyo na mfumo makini wa kuhifadhi na upataji mzuri wa kumbukumbu wakaweza kuwa na haya uyasemayo.Mkwawa alikufa kaijua kiarabu vizuri,cha kuandika na kusoma.Kwa hiyo alikuwa tayari influenced na culture zingine.

Waafrika waliishi kwa hadithi na matambiko, huku wakiwa na wapiga ramli kama watu waliowapa watu muelekeo wa siku zijazo.

Walikuwa ni wababe tuu na hawakuwa na expansion kama invyodhaniwa, watu walivamia na kupora vitu kwa wengine huku wanaume wote wakiuwawa na wanawake kuchukuliwa, waliobakiw alikimbia mbali.So baada ya wavamizi kuchukua vyao wenyeji hurudi au kutokomea kabisa, wavamizi hawakubaki tena,labda pawe na vitu vya kudumu ndipo walibaki.
Kumbuka, mpaka hapa hakuna Mkoloni, TAA, TANU wala Nyerere, na jamii hizi zilipiga hatua kubwa sana kimaendeleo. Jamii hizi zilikuwa na uwezo mkubwa kujiendesha kisiasa na kiuchumi, na uwezo huu ulitokana na ukusanyaji wa kodi na tributes mbali mbali hasa kupitia trade control; pia ziliweza kulinda mipaka isivamiwe na maadui. Jamii hizi zilikuwa na ndoto na malengo ya kukabiliana na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na kujitosheleza kwa chakula), kujitosheleza kifedha (kiuchumi) ili kuendesha shughuli za utawala, na muhimu zaidi, kudumisha uhuru wake kwa kulinda mipaka yake yake. Muhimu hapa ni kwamba Jamii hizi:


  1. Zilifanikiwa kukuza sana sekta ya uzalishaji wa Kilimo;
  2. Zilifanikiwa sana kuendeleza tekinolojia ya chuma/new metals technologies;
  3. Vile vile zilifanikiwa sana kukuza sekta ya biashara (trade expansion);

Mkoloni alipoingia Tanganyika, lengo lake kubwa ilikuwa ni kuvuruga mfumo na mafanikio yote haya, hasa uwezo wa kiuchumi uliotokana na efficient revenue system, nguvu za kijeshi, uhuru wa jamii kujiamulia sera kisiasa, kiuchumi, kijamii n.k; Mkoloni alifanikiwa kufanya haya kwa kuwarubuni machifu kadhaa, pia kupitia sera ya ‘divide and rule’, na mara nyingine ‘military coercion’. Kwa kifupi, mkoloni alifanikiwa kuzima ndoto za Watanganyika na badala yake, akaleta muundo mpya kabisa wa mahusiano katika uzalishaji (uchumi), mahusiano katika utawala, huku pia akivuruga utamaduni wa mwafrika and install utamaduni na mfumo wake ambao ulilenga to serve interest za serikali ya kikoloni na pia za mataifa mama.
Hapa naona watu wanajisahau na kupeleka akili katika fikra kuwa mkoloni ni mzungi tuu.Na kudhani mwafrika alitibuliwa katika ukoloni.Sudan, Zanzibar, Sahara magharibi etc mkoloni wao alikuwa mwarabu.

Tanganyika haikuwepo ,ilikuwepo koloni la Mjerumani(tanganyika ya leo+burundi+rwanda-toa ukanda wa pwani na zanzibar waliokuwa chini ya mkoloni mwarabu ambaye pia alikuwa mwendesha utumwa kabla ya kuhamia katika Ukoloni),TAA,TANU hazikuwa na mtazamo wa kitaifa.Hardly vilifika morogoro.Nyerere ndio alikata mitaa nchi mzima kuvunja utawala machief ,huku akieneza TANU.Otherwise kulikuwa na uwezekano,by the time tunapata uhuru Mbeya isingekuwepo, dar, na mikoa mingine ya pwani ama wangebaki kinyao ama wangekwa sehemu ya Zenj, kanda ya Ziwe kagera ingekuwa Uganda,Kigoma ,Kilimnajaro arusha, manyara wangeweza kuwa nchi,huku Sehemu za Rombo zingekuwa Kenya, huku sehemu za Tanga zingewe kwenda Mombasa au hata kuungana na kilimnjaro.Mpaka Leo kuna mikoa bado haifanani sana Tanzania kwa mambo Mengi zaidi ya nchi jirani.

Na ukoloni si mbaya kama watu wanavyojaribu upaka rangi, Utumwa ndio ulikuwa mbaya kabisa na ndio ulioacha mazalia mabaya sana.Ukoloni watu walipelekwa shule,kuwa na hospital, miundo mbinu etc.Ingawa vyote hivyo vilikuwa kwa malengo fulani ya kufanikisha unyonyaji wao,lakini pia ndizo laws za ecomonics zinavyosema.Hakuna kitu kinafanyika bila faida.Na ikibidi wengine hufanya vitu vya kuongeza faida.

Utumwa haukujali prince wala,chief na wote walichukuliwa pale hapakauadhiri utendaji wa dhalimu.haukujali mila wala biashara.
Kwa africa mashariki mwarabu alikuwa ndio bado katika mfumo wa utumwa wakti wengine walikuwa katika ukoloni.Na hizo biashara na mambo mengine zilizotibuliwa ni zile za mwarabu na chini ya ustaarabu wa mwarabu.Ndio maana HISTORIA MBADALA huwa zinamshutumu mkoloni kuvuruga maeneo yaliyokuwa na shule, na biashara(Ila haikuwa African in anyway.).
Mkoloni akaanzisha a new government, New Political Practices and New Political Institutions ambazo zilikuwa ni ngeni kabisa (so alien) kwa jamii ya watanganyika; Nahimiza kwamba hadi hapa hapakuwepo TAA, TANU wala Nyerere bali jamii iliyorundikwa kwa pamoja bila ya ridhaa yao, ikapewa jina la “Tanganyika”, kisha kuanza kutawaliwa katika kila nyanja bila ya hiyari yao;

TANU na Harakati za Uhuru

Tujitahidi kutazama harakati za uhuru kwa kina zaidi kuliko ndani ya mazingira ya TANU. Harakati kama za Kinjeketile (Maji Maji) na Mkwawa dhidi ya mjerumani zililenga kuondokana na utawala wa kikoloni ambao ulivuruga taratibu za maisha ya watanganyika, huku ikizidi kupoteza uhuru wao wa kisiasa na kiuchumi.
Tayari watu hao walikuwa si huru kama unavyodhani, na pia hawakuwa tena waafrica kihivyo.Mkwawa alikuwa akijua kiarabu kizuri cha kuandika na kuongea,tayari alikuwa na jamii inayovaa kitwana, nahiyo ipo wazi kabisa hadi leo.Uvaaji wa wahehe katika ngoma unajisema wenyewe.

hayo majina yao ya Kiafrica hayasemi ukweli kama yakisemwa yote.Na hawa jamaa walikuwa proxy ya waarabu na walipata silaha na utaalamu toka kwa watawala wa pwni ambao walikuwa na mchanganyiko wa damu za kiarabu na hivyo kuwa na mausiano ya karibu na waarabu.

Watu wa magharibi(wamissionary+mabepari) wanaifuatilia sana hii historia ingawa wanayo katika documents zao,kwa vile ilihusisha mapamabno mengine kati yao na Waarabu(Islamic culture) katika fronts nyingine walizokuwa wakigombea himaya.
Attacks vyingi za akina Mkwawa zilikuwa dhidi ya wamissionary ambao nao walidai ulinzi kwa serikali zao, ndipo hawa mashujaa wa Kiafrika walipojikuta hali si nzuri sana.Ukifuatilia sana utaona hata zoezi la kuupinga utumwa lilipata nguvu baada ya wamissionary kufanya lobbying katika serikali zao ambazo nazo kwa kiasi fulani walilazimisha wammissionary washiriki nao ili wawape ulinzi.Hapo ndipo waandishi wetu wa Histroia wakamua husisha ukoloni+wammissionary.

Kumbuka tena, hapa hapakuwa na TAA, TANU wala Nyerere. Pia niseme kwamba kidogo umenishangaza unapo downplay harakati za Nyerere kwamba ‘it was an easy walk to freedom’ huku ukisahau kwamba kwa ujumla wake, Tanganyika na Kenya kwa mfano, hazipishani sana when it comes to umwagaji wa damu wakati wa mapambano dhidi ya ukoloni; tofauti kubwa iliyopo baina ya harakati za Kenya ni only in contextual terms (especially dates), lakini content wise, hatuna tofauti kubwa sana;
Umwagaji damu mwingine ulikuwa wa kijinga na ulikuwa zaidi wa kikabila na Kiustaarabu(kupigania mkoloni fulani) zaidi ya uhuru kwa mwafrica.
Tanzania tayari ilikuwa katika Transition period kuelekea uhuru.Na huwezi amin kuwa Uhuru unaweza kuwa uliletwa kwa ustadi wa mwalimu peke yake.Clue ipo katika nature ya TANU mwanzoni, na jinsi Nyerere alivyojiweka ndani na baadaye kuwa Kiongozi na baadaye kufikia hatua ya kulazimisha uhuru kabla ya Muda.TANU haikuwa na sura ya Kitaifa,ilikuwa na Waislam, na ilikuwa umbali kidogo sana toka dar na haikukubalika mikoani palipokuwa na Machief walikuwa tayari wametapatiwa nafasi katika serikali ya kikoloni.Nyerere kwa uwezo binafsi na karama Yake aliweza jiweka na kukubalika katika TANU kwa urahisi sana kiasi cha cha kuwashangaza hata wale watu wanaodai mgao wa matunda ya uhuru.TANU iliyokuwa haina kiongozi mwenye ushawishi ndani yake na hata kukosa sifa za kupewa nchi na UN ilimhitaji Nyerere kama Wachina Leo wanavyonunua akina Drogba.

Nyerere alipambana katika game hatari ya kuwashawishi machief kuikubali TANU na baadaye kuuvunja uchief kwa upinznaia mkubwa.Ndie aliitoa TANU toka chama cha Wazee wa Dar,wenye imani moja ya Dini na wney misimamo mikali, hadi kuwa Chama cha kitaifa (Kipindi hicho kiswahili hakikuwa kikijulikana sehemu kubwa sana Tanganyika).Nyerere huyo huyo alipata imani ya mzungu kwa vile alisoma katika seminary na baadaye katik mataifa ya magharibu alikuwa akijulika na kuaminiwa nao hivyo alibakiwa na kazi moja tuu kuwashawishi.Nyerere aliweza shawishi yeyote aliyekutana naye.Kunzia wazee wa TANU ambao ni masalia ya wale waliolazimisha wamissionary wa Kijerumani wakajenge Pugu kule mlimani, kwenda kwa machief, hadi mkoloni na UN na baadaye kujenga misingi.

Kwanini nasema ilikuwa rahisi, nyerere alikuwa kama Messi, alicheza mchezo aupendao na kuujua vizuri katika mechi ambayo tayari wapinzania wanatamani kombe liondoke.unless mtu happend hesabu,ila kupiga hesabu za kujenga jengo unalolisubiri kwa hamu si kitu kigumu.
Bottom line mkuu Nicholas ni kwamba, aspirations za watanganyika zilikuwepo kwa muda mrefu sana, hata kabla ya ujio wa TANU na Nyerere, na ushahidi ndio huu wa Kinjeketile na Mkwawa. Kilichotokea ni kwamba TANU ilikuja kuongezea nguvu vuguvugu hili na ikafanikiwa kuwaletea watanganyika uhuru wa kisiasa (somewhat) na kuahidi kuwaletea uhuru wa kiuchumi.

TANU ndani ya Tanganyika huru ilikuwa na majukumu mawili:

a) To restore/reconstruct Tanganyika.
b) To Develop Tanganyika.
hao akina Kinje na Mkwawa pia walikuwa na aspirations za wakoloni wengine.Na ukiwataja katika Black historians wa nje ay africa watakushangaa,kwani hao hao jamaa walihusika sana kuuza wenzao, na kulinda tawala wauza watumwa.

HUWEZI RESTORE KITU HAKIKUWAHI EXIST.Tanganyika haukiwahi exist.Ila koloni la ujerumani la africa mashariki(tanganyika ya leo+burundi+rwanda-toa ukanda wa pwani wote+zenj),TANU ilikuwa dar na dar, na Dar mwanzo haikuwa sehemu ya Tanganyika.Ndio maana wamissionary walikimbilia Pugu, Na Tanga wakakimbilia Lushoto.
Mfumo wa kibepari ulishaotesha mizizi mirefu sana, kwahiyo isingekuwa rahisi wa Nyerere kufanikiwa. Na sio kwa Tanzania tu, kwani hakuna nchi yoyote Africa iliyofanikiwa katika hili. Kilichofanya wenzetu kwa mfano wa Kenya au Zimbabwe watuzidi ni kwamba Kenya kwa mfano - mkoloni alitumia muda na rasilimali nyingi kujenga a an indigenous bourgeoisie class (hasa wakikuyu) ili wafanane nae in terms of kumiliki ardhi n.k kwasababu mkoloni alilenga kuishi Kenya moja kwa moja, na kwamba at independence, pasiwe na much ‘class struggle’; kwa bahati nzuri au mbaya (depending unaangalia kwa jicho gani), mkoloni hakufanya hivyo Tanganyika kwani hakuwa na nia ya kuishi (we were not a settler economy), ndio maana hakuwaendeleza watanzania kwa namna yoyote ya maana, badala yake aliwaacha as proletariats (wengi as manual laborers) na pia wakulima wadogo wadogo kama alivyowakuta.
unathibitisha urahisi uliokuwepo.Kwani mwingereza si hakuwa na nia,ila hakuruhusiwa kukaa forever, ndio maana hakuwa na haja ya kuweka resources zake.Na hata mashamba wali sub contract kwa wagiriki, wayahudi na wamrekani,huku barclay wakiwapa mikopo.hembu fikiria pressure aliyonayo US kuondoka Iraq, na Afghanistan,kilichobaki ni kujenga mazingira ya kuweka mifumo ya kuwapa control mara watakapokabidhi uhuru.
Pia ni muhimu tusijisahau na kuanza kuijadili TANU kama vile Nyerere alipokea nchi (1961) ikiwa na:

· Uwezo wa kujiendesha (political capacity) na pia uwezo wa kuboresha maisha ya watanganyika kwa urahisi;
· Kama vile Nyerere alipokea nchi iliyokuwa inaheshimu human rights and democracy practices wakati wa ukoloni;
· Na pia kama vile watanganyika walikuwa ni homogenous society wakati ukweli ni kwamba ilikuwa na makabila mengi huku baadhi yao mkoloni tayari akiwa ameshayavuruga kiuchumi, kisiasa na kijamii kwa kutumia makabila mengine, huku baadhi ya makabila (na dini) yakiwa yame neemekana kuliko mengine - kiuchumi, kisiasa na kijamii..

TANU Ilipata nchi ikiwa nzuri sana na kile kipindi cha re adjustment kilipoopita na hapakuwa tena hofu ya kupinduana.Tulinaguka baada ya kushindwa balance chnagamoto za Vita baridi na ukoloni mamboleo.

Kwa jamii za kiislam palitokea makosa kidogo ya ku re-adjust baada ya shift ya mwenendo wa dunia na nchi kwa ujumla.Waislam walikuwa jamii zilifanikiwa tokana na kuwepo kwa biashara zilizokuwa katika mifumo ya kiarabu na ustaarabu wa kiislam.
Baada ya nchi kuingia katika kujitawala hofu, na karaha ya kuingia mfumo wa kimagharibi amabo uliongozwa sana na wamissionary.Mbalia na waislam kuona kama fedheha kuingia katika shule za wamissionary, huku jamii zao zikiwa na maisha mzuri tuu na wasomi.Tazama miji mingi nchini nyumba za mijini ni za waislam wengi.Upepo wa kiuchumi na kubadilika kwa mitazamo ya waislam imepelekea wengine kuuza maeneo.So kiukweli hapakuwa na nia ya wazi ya kuwapiga waislam vita.Kwa makabila mikoani,wasomi wengi walikuwa watoto wa watumishi wa wamissionary,watoto wa machief, wafanyakazi wa mashamba ya wakoloni.Na hivyo waliimarika sana katika mambo mengi.DHAMBI ILIYOUWA MAKUNDI MENGI ni ile inayoua utajiri katika kizazi kimoja kwenda kingine.Utaoana Kuna UPs and DOWNs kwa uislam dunia nzima.Uislam ulishatawala dunia enzi Uturuki, na SPAIN.katika uhuru pia walifanikiwa sana.Hii pia hutokea kwa familia zilizofanya kazi sana kujenga misingi, wanapofanikiwa watoto wao huwa wanakuwa na vingi sana kiasi cho kutofanya kazi, nahuamua kufuja, na kuendekeza pongezi, na mwishowe kutowaachia watoto kitu zaidi ya madeni.
 
mchambuzi, kuweza jua jinsi gani habari inaweza potosha historia miaka ijayo,tazama hii picture.

halafu ujiulize haya maswali:
-Je imani nyingine hazina wazee?
-Je ni waislam tuu ndio wanachama wa CCM?
-Je CCM ikija tajwa katika historia kuwa chama kiovu kuliko ,ni vipi tutazuia watu wasitafsiri kwa minajili ya imani?
-je kama kuna wema wa CCM katika Historia,Itakuwa ni haki kuihusiasha na Uislam katika mafanikio?
-Je mpiga picture alikuwa akifahamu kuwa picture aliyopiga haikutazama utaifa zaidi?
-Je kuna shida katik ukaaji wa wanachama wa CCM?Kwani raia wapendano hukaa kutokana na vyeo vya kichama,maeneo watoakayo na si kidini.Au ndio kusema CCM ina makundi ya namna hiyo?

Ukitaka kujua madhara ya haya mambo katika historia, mfano patokee maangamizi makubwa ama ya mafuriko au tetemeko na kuangamiza kila kitu katika eneo hilo.Halafu ikapita miaka kadhaa akaja mtaalamu wa mabaki ya zamani.Katika kuchimba mbali na kupat amabaki mengi yasiyoelezea sura na tamaduni kabaatika pata hiii picture.Kwa kumbumbuku chache za magazeti kutoka library za nje ya mkoa akajua kuna chama kilikuwa kikitwa CCM na viongozi wakaonekana na magazeti yanaonyesha tarehe ya mkutano.Ktik kutafsiri picture unadhania watasema nini?Ukiongezea na picture za wazee wa dar wakiwa na rais?

Naandika haya kwa vile si waandishi tuu wa kalamu,hata wapiga picture na watafiti wetu,huwa wana tabia ya kuchukua mambo haraka haraka kiasi cha kufanya habari zao baada ya miaka kadhaa kuwa ama hazina dhamani au hata zikawa zinagawanya watu.Na mfano mmoja wa watue hubomboa z ambao wanaweza tumia vibaya ni wale watanzania wanaojaribu dai matuunda ya uhuru kwa minajili ya dini.Pia kejeli tuionayo hata humu hatika picture za mikutano ya marais na wazee wa dar.Haya yote hubomoa zaidi ya kujenga.

Na hivi ndivyo hata maeneo mbalimbali ya historia yetu yalivyopindishwa na kuandikwa kizembe.Yaani hapa ndipo panakuwa na historia ya historia.
 
Chadema ikishinda 2015, Najiondoa Jamii Forum.
Mood nukuu maneno yangu.
 
mchambuzi, kuweza jua jinsi gani habari inaweza potosha historia miaka ijayo,tazama hii picture.

halafu ujiulize haya maswali:
-Je imani nyingine hazina wazee?
-Je ni waislam tuu ndio wanachama wa CCM?
-Je CCM ikija tajwa katika historia kuwa chama kiovu kuliko ,ni vipi tutazuia watu wasitafsiri kwa minajili ya imani?
-je kama kuna wema wa CCM katika Historia,Itakuwa ni haki kuihusiasha na Uislam katika mafanikio?
-Je mpiga picture alikuwa akifahamu kuwa picture aliyopiga haikutazama utaifa zaidi?
-Je kuna shida katik ukaaji wa wanachama wa CCM?Kwani raia wapendano hukaa kutokana na vyeo vya kichama,maeneo watoakayo na si kidini.Au ndio kusema CCM ina makundi ya namna hiyo?

Ukitaka kujua madhara ya haya mambo katika historia, mfano patokee maangamizi makubwa ama ya mafuriko au tetemeko na kuangamiza kila kitu katika eneo hilo.Halafu ikapita miaka kadhaa akaja mtaalamu wa mabaki ya zamani.Katika kuchimba mbali na kupat amabaki mengi yasiyoelezea sura na tamaduni kabaatika pata hiii picture.Kwa kumbumbuku chache za magazeti kutoka library za nje ya mkoa akajua kuna chama kilikuwa kikitwa CCM na viongozi wakaonekana na magazeti yanaonyesha tarehe ya mkutano.Ktik kutafsiri picture unadhania watasema nini?Ukiongezea na picture za wazee wa dar wakiwa na rais?

Naandika haya kwa vile si waandishi tuu wa kalamu,hata wapiga picture na watafiti wetu,huwa wana tabia ya kuchukua mambo haraka haraka kiasi cha kufanya habari zao baada ya miaka kadhaa kuwa ama hazina dhamani au hata zikawa zinagawanya watu.Na mfano mmoja wa watue hubomboa z ambao wanaweza tumia vibaya ni wale watanzania wanaojaribu dai matuunda ya uhuru kwa minajili ya dini.Pia kejeli tuionayo hata humu hatika picture za mikutano ya marais na wazee wa dar.Haya yote hubomoa zaidi ya kujenga.

Na hivi ndivyo hata maeneo mbalimbali ya historia yetu yalivyopindishwa na kuandikwa kizembe.Yaani hapa ndipo panakuwa na historia ya historia.

Nimekuwa najaribu kukusoma lakini kidogo napata wakati mgumu kuelewa msingi wa hoja zako kuhusu suala la udini. Can you be a little bit specific? Maana yako ni nini hasa - je unajaribu jenga hoja kwamba CCM ni chama cha kidini? Au CCM haithamini wanachama wa dini fulani? Au mafanikio ya CCM yanatokanana dini fulani...? sikupati bado.
 
Mchambuzi
Tufike mahali kila serikali iwe na achievement za kujivunia badala ya kungangana na umoja na amani ambavyo ni vizuri lakini kwa kizazi cha sasa sio jambo pekee la kulizungumzia.

Kwenye namba 4. kumenisononesha kutokana na ukweli kuwa ninakotoka uko Mvomero ( iliyokuwa Morogoro vijijini ) hawajui lini watapata umeme...ni wazazi wengi wanapata bahati ya kujifungua watoto hospitalini mana hutakufa kabla ya kufika uko. ulizia eneo liitwalo msepa/bunduki kuhusu huduma za jamii nazani utafuta hiyo point namba 4 na ndicho kinachowafanya vijana wengi kufikilia chama mbadala na kwa mazingira yalivyo CDM ndo kina mwelekeo, nahitimisha kwa kusema kwamba suala si CDM kuwa tayari ila watu kuichoka CCM, Chadema wajiandae wasijiandae, wawe wakuleta matumaini kweli au hisiwe hivyo ila wananchi wnegi wamefika state ya kusema CCM sasa basi na mbadala wake ni Chadema na kwa utaratibu huu wa wao kutembea mikoani hadi kwenye kata nazani kiu ya kuiweka CCM pembeni itatimia.

Kuna mfano wa mpangaji mmoja aliyechoka manyanyaso ya mwenye nyumba hivyo akaamua kuichoma hiyo nyumba ingawa vyombo vya mpangaji huyo navyo vikiwa ndani na kuungua pia, kiu ya mpangaji ilikuwa ni kuhakikisha nyumba inachomwa.

Nlikuwa Kilema kwa Lazari wilayani Himo uko Moshi nlishangaa wamama na wabibi kuonyesha kuchoka na kupewa khanga...waliniacha hoi walipokuwa wanajiuliza kwa nini BEI YA BIA IKO CHINI KULIKO YA SUKARI???? kwao wanaona serikali iko tayari wao walewe kuliko kunywa chai...ndugu yangu kama watu wa aina hiyo wanafikiri na kuichoka serikali yao kiasi hicho then kuna tatizo.
 
Last edited by a moderator:
....ndicho kinachowafanya vijana wengi kufikilia chama mbadala na kwa mazingira yalivyo CDM ndo kina mwelekeo, nahitimisha kwa kusema kwamba suala si CDM kuwa tayari ila watu kuichoka CCM, Chadema wajiandae wasijiandae, wawe wakuleta matumaini kweli au hisiwe hivyo ila wananchi wengi wamefika state ya kusema CCM sasa basi na mbadala wake ni Chadema na kwa utaratibu huu wa wao kutembea mikoani hadi kwenye kata nazani kiu ya kuiweka CCM pembeni itatimia...

Nakubaliana na wewe, lakini tatizo linakuja pale ambapo bado hakuna chama (including CCM) chenye solution ya kweli kwa matatizo ya watanzania wanaoishi vijijini. Kwa mfano, maeneo ya huko mvomero morogoro, shida za wananchi zinaeleweka kwa uwazi kabisa lakini utatuzi wake (na katika maeneo mengi ya vijijini tanzania kwa ujumla) - utatuzi wake haupo anywhere close, regardless chama gani kipo ikulu; hii ni kwa sababu hakuna chama chenye ideological orientation inayo challenge soko huria na mfumo mzima wa kibepari usiotendea haki wasio nacho; hii haina maana kwamba tunahitaji chama cha kijamaa kukomboa wenzetu hawa, lakini chama chenye ideology ya kukemea soko huria na kulirekebisha kila inapobidi kwa manufaa ya wengi; kwa sasa sio chadema wala ccm wa kufanya hilo;
 
Tarehe 10, August, 2012 mchambuzi mahiri wa masuala ya siasa hapa jamvini, Ndugu Mchambuzi, licha ya kukiri wazi udhaifu wa sasa wa chama tawala kiutendeja, kinadharia na kimaadili, alijadili sababu kadhaa alizoamini zinakifanya chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuonekana hakipo tayari kukamata dola mwaka 2015.

Nikisukumwa na mapenzi yangu kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, na pia hamu yangu ya kuusaka ukweli, niliamua kuafanya jitihada ya kutafuta vyanzo mbali mbali vya maarifa na taarifa ili kupata ungavu wa kifikra katika kuzikabili hoja za Mchambuzi. Pamoja na mambo mengine, dhumuni la andiko hili ni kuhakiki na kuangalia ukweli wa hoja hizo na kukuza mjadala sawia.

1. Hoja kuhusu Uongozi wa Mageuzi ya kisiasa nchini.
Katika eneo hili tunaelezwa na Ndugu Mchambuzi kuwa CCM ilimiliki mchakato wa Mageuzi nchini na kwamba kuingia kwa ''Mfumo wa Vyama Vingi'' ilikuwa ni jitihada ya CCM. Hoja hii imedumu katika uwanja wa kisiasa kwa muda sasa na tumekuwa tukielezwa na waandamizi takribani wote wa CCM, kuwa bila CCM kuridhia kuingiza mfumo huo leo tusingekuwa na siasa za upinzani nchini. Sote tunatambua, hata hivyo, kuwa mfumo wa vyama uliingia nchini mwanzoni mwa miaka ya 1990 ikiwa ni matokeo ya mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi yaliyokuwa yakitokea duniani kote hasa Ulaya Mashariki yaliyoshuhudia kuanguka kwa ukuta wa Berlin uliokuwa ukitenga Ujerumani Magharibi na Ujerumani Mshariki na kupata Jamhuri ya Muungano wa Ujerumani.

Mabadiliko hayo yalipekea kuundwa kwa Tume ya Jaji Nyalali iliyokuja na mapendekezo ya kuanzishwa mfumo wa vyama vingi licha ya 80% ya wananchi waliohojiwa kupendekeza mfumo wa chama kimoja uendelee na 20% kupendekeza mfumo wa vyama vingi.Hii ilipelekea kutungwa na kupitishwa kwa sheria ya vyama vya siasa namba 15 ya mwaka 1992 na Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania wakati huo likiwa ni la wabunge wa CCM pekee, enzi za ''Chama kushika Hatamu''.

Hata hivyo yafaa pia kukumbuaka ya kuwa mfumo wa vyama vingi nchini ulikuwepo kabla na baada ya Uhuru kabla ya kufutwa mwaka 1965 na sheria ya Bunge.Vyama vya Upinzani vya wakati huo vilikuwa ni AMNUT, PDP, PCP, NEP na AIM. Huu ni ushahidi kuwa dai kuwa wapinzani hawana shukrani kwa kuwa ''walipewa'' fursa ya kushitiki katika siasa za vyama vingi halina msingi kwa kuwa kilichofanyika kilikuwa ni kurejesha tena 'Mfumo wa Vyama vya Vingi vya Siasa'' uliokuwepo tangu miaka ya 1960.

2. Hoja kuwa Ujamaa ni relevant na maisha ya wananchi wa vijijini na bado ni itikadi inayokidhi matamanio,ndoto na matarajio yao kuwa mbinu za CHADEMA za sasa hazipo coherent and consistency.
Yafaa pia tuangalie dainamiksi za kidegrafia hapa nchini kuanzia mwaka 1967 hadi mwaka 2002. Kwa kuzingatia report ya sensa ya Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania iliyotolewa mwaka 2003,mchango wa mikoa katika idadi ya watu kitaifa ilikuwa kama ifuatavyo.Mkoa wa Mwanza (8.5%),Shinyinga (8.1%), Dar Es Salaam (7.2%) na Mbeya (6.0%). Wakati Lindi na Pwani kwa ujumla wake ilichangia 5% katika idadi ya watu kitaifa. Na takwimu zinaonyesha kuwa kuna kiwango kikubwa sana cha umijinishaji (urbanization) katika jiji la Dar es Salaam.

Kwa kuzingatia Idadi ya Watu katika Kilometa Moja ya Mraba (Population Density) tunaona kuwa Lindi ina watu ( 12),Rukwa (17) ,Shinyanga (55%),Tabora (23) Dar Es Salaam (1793), Dodoma(41), Arusha (35), Kilimanjaro (104), Tanga (61) Morogoro (25),Pwani (17), Mtwara(68),Ruvuma (18),Iringa(26), Mbeya(34), Singida(22), Kigoma(45), Kagera(72), Mara(70), Mwanza(150), Manyara(23).

Mtawanyiko wa Watu katika maeneo unaamuliwa na mambo kadhaa muhimu:
Tabia ya nchi, Uoto wa Asili, Uwepo wa maeneo yanayohidhiwa kwa sababu za kimazingira, Mbuga za wanyama na Uwepo wa misitu minene isiyovutia ukaazi na shughuli za kibinadamu.

Tuangalie pia mtawanyiko wa watu kwa kuzingatia ukaazi.
Mwaka 1967, wakazi wa mijini waliokuwa wakiishi vijijini walikuwa 12,313,469 sawa na 93.8% wakati wakaazi wa mijini walikuwa 6.2%. Mwaka 1978,wakazi wa vijiji walikuwa ni 17,512,610, sawa na 86.2% wakati wakazi wa Mijini walikuwa 13.8%. Mwaka 1988, wakazi wa vijijni walikuwa ni 23,174,336, sawa na 81.6% wakati wakaazi wa Mijini walikuwa ni 18.4%.Mwaka 2002, wakazi wa vijijini walikuwa ni 34,443,603, sawa na 76.1%, wakati wakazi wa Mijini walikuwa ni 23.1%.
(SOURCE:Ndalahwa F.Madulu, Istitute of Resource Assessment, IRA,University of Dar-Es-Salaam.)

Takwimu hizo hapo juu zinaonyesha dhahiri kuwa idadi ya wakazi wa vijijiji inapungua kwa kasi na yawezekana katika sensa ya mwaka huu tukawa na 60% ya Watanzania wanaoishi vijijini na Watanzania waishio Mijini kuwa 40%. Takwimu hizi zinaonyesha wazi kabisa kuwa ipo haja ya kutambua mabadiliko ya kidegrafia yaliyojitokeza tangu mwaka 1967kupitia mwaka 2002 na hadi sasa 2012. Ukweli huu unatutaka kubuni, kutunga ama kuboresha sera ,programu na mikakati,miradi na kwa kuzingatia mabadliko hayo muhimu ya kijamii.

Hoja hapa inatakiwa kuwa wakazi wa vijijini wanahitaji uboreshaji wa miundombinu ya kiuchumi kama vile bara bara ,umeme, kuwa uhakika wa masoko, umeme wa uhakika kwa ajili ya kuwa na agro -processing industries kwa ajili ya kuongeza tahamani ya mazao yao na kufaidika na kazi za mikono yao, Kuboersha huduma bora za afya, kutoa mikopo yenye riba nafuu kwa ajili ya kuwezesha wakazi wa vijijini kujihussisha na shughuli za kujiongezea kipato, upatikanaji wa uhakika wa pembejeo nk. Haya yote yanaweza kufanywa kama chama cha Demokrasia na Maendeleo kitaingia madarakani kwa kuweka nyenzo ya kufanikisha adhama hiyo. Kwa kuanzia, kama maandalizi ya mwaka 2015, wakazi wa vijijini wameamua kukiunga CHADEMA kwa kupata wabunge kadhaa katika maeneo ya Vijijini kama vile Mbulu,Singida Mashariki, Meatu, Mbozi Magharibi nk.

3. Hoja kuhusu Tanzanian Political Culture/Utamaduni wa kisiasa Tanzania.
Ni kweli ulio wazi kuwa, hapa nchini utamaduni wa kisiasa, unaojumuisha thamani, tunu, mitazamo, mienendo na miiko haujakita mizizi katika maisha ya wengi na hii ina athari zake katika dainamiksi za kisiasa na kwamba moja ya matokeo ya ombwe la ukosefu huu wa utamaduni huu ni wanasiasa kuendesha siasa za kushambulia watu badala ya kupambanisha hoja.Kama tutachukulia kuwa viongozi wa kisiasa wana angalau kiwango cha kutosha cha Elimu basi tulitarajia kuwa wangeendesha shuguli za kisiasa tofaiti na kundi la wananchi wengi ambao hawakubahatika kusoma.

Tutakumbuka kuwa, Salim Ahmed Salim, mwaka 2005, alikuwa ni mhanga wa utamaduni huu dhaifu wa kuchafuana badala ya washindani wake, ndani ya CCM ,kuamua kutoshindana naye kwa hoja kuhusu masuala muhimu ya kiuchaguzi. Hali hii iliendelea pia katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 na yameendelea kuonekana katika Chaguzi Ndogo za Ubunge katika maeneo mbalimbali nchini, inaonekana hakuna dalili kama hali hii itakoma hivi karibuni.

Kwa kawaida, utamaduni wa kisiasa, kwa kuzingatia uhusiano wa mpiga kura na mtawala, utagundua masuala muhimu yafuatayo:
Utambuzi, uelewa na ufahamu wa wananchi kuhusu maana na majukumu ya serikali, matarajio yao kwa serikali na ushiriki wao kisiasa.

Aidha, zipo aina tatu za Tamaduni za Kisiasa: parochial political culture, subject political culture,na participant politicalculture.
Katika parochial political culutre, wananchi huwa na uelewa, utambuzi na ufahamu wa chini juu ya maana na majukumu ya serikali yao, na huwa wana matarijio ya chini kutoka serikali. Na katika subject political culture, huwa kuna kiwango kikubwa cha utambuzi, ufahamu na uelewa wa wananchi na kwa kawaida huwa na matarajio makubwa kutoka kwa serikali lakini hawashiriki katika michakato ya kisiasa kama vile kupiga kura na kutoa maoni yao.Na katika participant political culture, wanannchi wana uelewa wa juu kuhusu maana na majukumu ya serikali,na hushiriki kikamilifu katika michakato ya kisiasa ikiwemo kujadili masuala yanayowahusu na kushiriki katika kupiga kura katika chaguzi.

Political awereness ama utambuzi wa kisiasa, husababishwa na wakala wa ujamiishaji wafuatao
:

Ngazi ya familia
:
Kwa watoto kutengeneza mtazamo kuhusu nini maana ya mamlaka na nguvu kwa kuzinagatia malezi yanayohusisha pia utiifu kwa wazazi

Shuleni
:
Serikali huamua jinsi ingependa wananchi wake wawe baadaye, kwa kuzingatia mahitaji ya kisiasa kiuchumi, kijamii na kiutamaduni, mitaala mwafaka hutungwa na kutekelezwa kukidhi lengo hilo

Marafiki wa rika na tabia zinazofanana
:
Hii huweza huunda mitazamo ya kisiasa kwa wahusika

Aina mbalimbali ya vyombo vya habari
:
Hivi vina kawaida ya ku- set agenda na kuwa vyanzo vya mawasialiano ya kisiasa na kuwezesha mijadala na hivyo watunga sera kupata fursa kuelewa matarajio na matanmanio ya wananchi juu ya masuala mbalimbali. Kwa hiyo, ni dhahiri, namna tunavyoenesha siasa zetu leo, ni matokeo ya moja kwa moja ya namna tulivyo manipulate hizo varibles hapo juu. Na hapa taasisi inayostahili lawama ya udhaifu wa utamaduni wa kisiasa nchini ni serikali ya CCM na hii ni sababu mwafaka kuiondoa madarakani kwa kuwa haikuwekeza kwa makusudi katika kujenga wananchi wanaofahamu haki zao,wajibu wao na pia majukumu ya watawala.

4. Hoja kwamba CHADEMA haina itikadi iliyo wazi.
Hoja hii imekuwa ikisika sana kwa muda mrefu sasa ,katika ulingo wa kisiasa.Binafsi, nimepata faraja sana kugundua kuwa hatimaye CHADEMA inayo itikadi tofauti na madai ya baadhi ya wananchi wenzetu.

Kwa nini itikadi ni muhimu? Chama chochote cha kisiasa kinahitaji kuwa na itikadi ili kuweza ku -base programme, sera,miradi, mikakati na misimamo mbalimbali, kudhibiti matendo na mienendo ya wanasiasa na wanachama wake na kuwezesha kupata msimamo kuhusu masuala muhimu katika jamii. Itikadi inaeleza namna jamii inavyotakiwa kuwa ,mbinu mwafaka na bora za kufikia lengo hilo,hubainisha vile vile ,namna kinavyotaka jamii ienende baada ya kukamata dola. Mathalani tungependa kuona vyama vya sisasa vinashindana mwaka 2015 juu ya mtazamo na misimamo yao kuhusu NEPAD,EAC,AGOA,CPA,na EPA ama hata dhana ya Pan Africanism na ndoto ya Serikali ya Umoja wa Afrika.

Tutazame aina mbalimbali za itikadi za kisiasa kisha tuamue kama kweli CHADEMA haipo katika kundi lolote la itikadi.

(a)Maxsism
:
Itikadi hii inatetewa na Karl Marx pamoja na Fredrich Engels,wote wakiwa wana-nadharia wa Kijerumani,wakipingana na itikdai ya Kibepari.Wao wanapendekeza kuwa, mabadiliko ya kijamii yataletwa na Mapinduzi yatakayoratibiwa na kutekelezwana na tabaka tawaliwa(ploreterarian) ama wavuja jasho, wasio na mtaji dhidi ya tabaka tawala (buorgeoisies) wenye mtaji na wanaonufaika na jasho la Walalahoi.Itikadi hii inalenga kukomesha mahusiano ya kinyanyaji na kikandamizaji kati ya tabaka moja na lingine.Bila shaka Chama cha Mapinduzi kimepata kuamini katika itikadi hii!

(b)Radicalism:
Hii ni itikadi iliyoanzia Great Britain katika karne ya 18,ikipendekeza mabadiliko makubwa ya kimfumo katika vyombo na taasisi za Uchaguzi; Uwakilishi wa Haki na ulio sasa katika Mfumo wa Kibunge,; Ikipendekeza Ujamuhuri,Ugawanyaji wa mali na uhuru wa mawazo.Ikiwa co opted katika Liberalism, katika karne ya 19 ilipendekeza Ufalme wa Kikatiba badala ya Ufalme Kamili, huku ikiendesha migomo na maandamano kwa lengo la kushinikiza mabadiliko ya kimsingi ya kisiasa na kiuchumi. Baadaye, ikiwa na matunda ya juhudi za watetezi wa dhana hii,ilipitishwa na Bunge Sheria ya Mabadiliko( Reform Act ,1832,ikiwa sambamba na Chartists.Kwa sasa itikadi hii inatekelzwa na chama cha Liberal Democracy,nchini Uingereza.Hapa utaona kuwa kimatendo ,CHADEMAimekuwa ikipigania mabadiliko hapa nchini na agenga kuu sote zote imekuwa ni "Mabadiliko"'

Vile vile, CDM imepigania sana mabadiliko ya Katiba na Mabadiliko ya Mfumo wa Uchaguzi.

(c) Conservatism:
Hii ni itikadi inayopinga kila aina ya mabadiliko yanayopendekezwa na wanamabadiliko na na ni itikadi ambayo ingependa kuona hali iliyopo iendelee kuwa jinsi ilivyo (status quo), maana inawafaidika watetezi wake.Iliasisiwa na Francois-Rence de Chateaubriand, 1819 akiungwa mkono na Edmund Burka waliokuwa wakipinga Mapinduzi ya Ufaransa. Sasa hapa tuanaiona wazi CCM ikiangukia katika kundi hili.

(d) Classical Liberalism:
Itikadi hii iliibuka katika karne 19 huko Ulaya na America,ikitetewa na akina John Stuart Mills,Thomas Hobes,,Jean Baptiste Say,Thamas Mathulus,na David Ricado.Watetezi wake wa itikadi hii wanaamini katika ''limited government power'' katika maisha ya kisiasa,kijamii , kiuchumi na kiutamaduni.Ni itikadi inayoamini katika ukuu wa kikatiba (constitutionalism),utawala wa sheria,due process (kupata haki ya kusikilizwa kabla ya kuhukumiwa ,haki za kibinafsi(individual liberties), ikihisisha uhuru wa mawazo na maoni,uhuru wa vyombo vya habari, na soko Huria.Huku David Ricado akipata inspiration kutoka kwa Adama Smith,alikuja na dhana ya utilitarianism,natural law, na Maendeleo.Hapa naiona CHADEMA kama chama cha Kidemokrasia kikiangukia katika kundi hili.

(e)Libertarianism( Neo - Classical Liberalism)

Itikadi hii inatetewa na Wahafidhina Mamboleo, na Waliberali wa Mrengo wa Kulia kama Emmanuel Kant.Wao wanaamini katika maximum Freedom and minimum government intervetion. Hii ni itikadi inayozingatia uhuru na haki za kibinafsi na kwamba watu wanaamua kutenda ama kutotenda baada ya ku-calculate faida na hasara za maaumuzi yao. Assumption hapa ni kuwa wananchi wana uwezo wa kung'amua mema na yasiyofaa. Kwa mfano kwa kuwa mwananchi anaogopa njaa atalazimaika kufanya kazi.

(f) Social Capitalism:

Hii ni itikadi inayoamini katika uendeshaji makini wa uchumi mkubwa(macro economy) na ingependa kuacha nguvu ya soko(invisible hands ya demand and supply ifanye kazi.Serikali inaweza kuingilia tu katika mazingira mahsusi,kwa lengo la kupunguza pengo linaloweza kujitokeza kati ya ''wenye nacho'' na ''wasio nacho'' kwa kuwalinda wananchi /wapiga kura dhidi ya ubinafsi wa wafanyabiahara wanaotafuta faida katika soko. Katika mazingira ya sasa sioni nchi inayoweza kupinga itikadi hii.Hata Marekani na Uingereza, nchi zenye ubepari uliokamaa,inatekeleza sera hizi.

Faida ya itikadi hii ni
(i)kuongeza uimara katika soko kuepusha unyonyaji dhidi ya walaji wa mwisho wabidhaa/wananchi/wapiga kura .
(ii)kutoa ruzuku ama pesa kwa familia maskini na hata kuzipatia nyumba za kuishi hata ikiwezekana chakula
(iii) Kutoa pesa kwa wazee ambao hawana uwezo tena wa kufanya kazi kuweza kupata kipato kuweza kuishi
(iv)Kutoa elimu ya bure kwa watoto wa maskini ili kuwapunguzia wazazi wao mzigo wa kugharamia masomo yao na kutumia sehemu ya akiba ya pesa zao kwa ajili kugharamia mahaitaji mengine na kuwekeza kwa faida ya baadaye.
(v) Kugharamia gharama za Afya kwa familia maskini.

Ili kuwezesha haya kutokea, Serikali hutoza kodi kubwa wananchi hasa matajiri ili kugharamia huduma za Afya, Elimu na Makazi kwa maskini na sasa wanatoa employment benefits kwa vijana wasio na ajira. Hapa, hata Ilani ya Uchaguzi ya CHADEMA ilizungumzia baadhi ya masuala hayo hapo juu.

(g) Social Democracy/ Ujamaa wa Soko:
Hapa, nyenzo za uzalishaji kama vile viwanda na migodi humilikiwa na umma kupitia serikali na zinaendeshwa kwa lengo la kupata faida katika uchumi wa soko. Faida inayopatikana inatumiwa kuongeza mishahara ya watumishi wake,ama kugharamia gharama za uwekezaji katika miundombinu ya kiuchumi kama vile barabara, umeme, hospitali, zahanati. Hizi ni faida zinazorudishwa kwa wananchi kupita social dividend. Katika itikadi hii hakuna unyonyaji wa jasho. Hapa pia CHADEMA inakusudia kujenga viwanda, na kuboresha maslahi ya Watumishi wa Umma.

Hitimisho.
Ni hali ya kawaida kabisa ya Chama cha Siasa kuamini ,kuhubiri ama kutekeleza Itikadi zaidi ya moja kutokana na mazingira ya kiuchumi ,kijamii (kidemografia) na kiutamaduni yanayobadilika.Kwa hiyo CHADEMA ina Itikadi.
Nawasilisha.
 
Baada ya kuweka hoja zangu hapo juu,zilizokuwa ni majibu kwa Ndugu Mchambuzi, kuweza kuzifanya hoja zangu zieleweke kiurahisi nimeonelea kuweka ufafanuzi kidogo.

Kwa kutilia maanani bandiko langu hapo juu ni matarajio yangu, kuwa ,sasa tumeweza kuelewa kuwa CHADEMA kama taasisi ya kisiasa inayo itikadi tena inayoeleweka. Kimsingi hoja kuhusu itikadi inayofuatwa ama kutekelezwa na vyama huweza kuangaliwa na kueleweka kwa wananchi kiurahisi katika mazingira ambayo kuna utamaduni wa kisiasa aina ya ''participant'' ambayo moja ya conditions zake ni uwepo wa kiwango cha juu cha ufahamu wa masuala ya kisiasa na/au uchumi (civil political competence).

Nchini Marekani, kwa mfano, wapiga kura hupiga kura kwa kuzingatia sana itikadi za vyama kwa kuwa wananchi wake wana kiwango kizuri cha uelewa. Katika kampeni za uchaguzi nchini humo kiwango cha mfumuko wa bei na/au kasi ya ukuaji wa uchumi, huweza kuamua mshindi. Na chama kilicho madarakani na mgombea wake, huweza kabisa kupoteza ushindi ikiwa hakikufanya jitihada za kukuza uchumi na kupunguza kasi ya mfumuko wa bei. Chama kinachoshinda uchaguzi huongozwa na itikadi yake katika kuamua aina ya sera na sheria zinazoweza kutekeleza ilani yake ya uchaguzi. Ni kwa sababu hii, Chama cha Democrats,baada ya kuingia madarakani,kilisukuma na kuweza kufanikisha marekebisho ya sheria kuhusu sekta ya Afya.

Katika mazingira yaliyo na kiwango kidogo cha uelewa wa kisiasa, kama hapa Tanzania, wanasiasa na /au wagombea,nyakati za uchaguzi, huwa hawajishughulishi sana na masuala ya kimsingi na badala yake hujadili maisha kibinafsi ya wagombea na mara nyingi huwa katika namna ya kuchafuana. Kama walivyo wanasiasa na wagombea wapiga kura nao huwa hawajishughulishi sana kujua itikadi, falsafa, ilani sera na mikakati ya vyama vya kisiasa. Kwa hiyo, suala la itikadi hueweka sana kwa watu wachache wenye kiwango fulani cha uelewa wa masuala unaotokana na kiwango na aina ya elimu.

Pamoja na mapungufu hayo, wananchi huweza kuelewa dira na mikakati ya kisiasa ya vyama iwapo vinavyogombea, ikiwa wanasiasa na wagombea watafafanua ilani sera na mikakati yao katika lugha wanayoweza kuielewa. Ni kwa sababau hii, kwa mfano, CHADEMA, katika uchaguzi mkuu wa 2010, iliweza kuvutia kura, baada ya kuahidi kutoa Elimu ya Msingi na Sekondari bure.

Idadi ya wananchi waishio maeneo ya vijijina, ambao huchukuliwa kuwa wana kiwango cha chini cha uelewa wa kisiasa, katika uchaguzi mkuu wa 2010, wameonyesha utayari wao kukiunga mkono CHADEMA. Bila shaka hili lilitokea kama moja ya matokeo ya CHADEMA kuwaendea wananchi wa vijijini na kuzungumza nao katiak lugha wanayoweza kuielewa. Aidha, kama nilivyoweza kuonyesha, kutokana na sababu mbalimbali, wananchi walio wengi wamekuwa wakihama vijijini na kuhamia mijini.

Sasa hapa tunapata changamoto moja:
Je, ni kweli wananchi wa mijini wana utayari wa kushiriki siasa kikamilifu?

Bila shaka jawabu ni ndio, ingawa sio mara zote. Ili kuweza kufikia matumaini, matarajio, matamanio na ndoto za wapiga kura wa maeneo ya vijijini na wale wa vijijini, ni vyema CHADEMA itunge sera na mikakati inayoweza kunufaisha makundi yote haya mawili na sio kuweka mkazo tu kwa wananchi wa vijijini.Muhimu zaidi ni kuwa, sasa, tunapaswa kutambua ukweli kuwa hakuna taifa lolote lililopata kupiga hatua kubwa ya maendeleo bila kuhamasisha na kuvutia umijinishaji (urbanization).

Vile vile, nadharia za uchumi zinaelekeza kuwa ili kuweza kupiga hatua za maendeleo, tunapaswa kuweka mazingira yatakayowezesha kupunguza idadi za wananchi wanaotegemea kilimo kama chanzo chao cha kipato. Kwamba zitungwe sera na mikakati inayohamasisha usasa katika kilimo (agricultural modernization) inayoenda pamoja na mechanization (utumiaji wa zana na mbinu za kisasa katika kilimo). Lengo hapa ni kuwa na wananchi wachache zaidi wanaojishughulisha na kilimo. Lile kundi la wananchi litakaloacha kutegemea sekta ya kilimo litaenda mijini kutafuta ajira katika sekta nyingine kama vile viwanda. Ili hili liweze kutokea, kunahitajika mazingira(sera, mipango na mikakati) yanayohamasisha maendeleo ya viwanda. Tutakubaliana bila shaka kuwa kuna uhusiano wa wazi na wa moja kwa moja, kabisa kati ya maendeleo ya sekta ya kilimo na maendeleo ya sekta ya viwanda.

Ndio maana tunaye mtawala aliyepata kudai kuwa ''alisahau'' kilimo. Haishangazi kuona kuwa waliamua kuua na kuuza viwanda. Hakika ''asingesahau'' kilimo wangefikiria mara mbili mbili uamuzi wake huo wa kuua viwanda.

Kama nilivyoweza kufafanua hoja yangu kuhusu population density, ni wazi kuwa yapo maeneo hayafikiki kiurahisi kutokana na Jiografia ya maeneo. Maeneo mengi nchini yana miinuko ,milima na misitu minene na hivyo kufanya maeneo haya kukaliwa na idadi ndogo ya wakazi. Hali hufanywa kuwa mbaya zaidi kunapokuwa na kiwango kikubwa cha uhamaji kuelekea mijini. Matokeo yake ni kukwaza mchakato wa ''political socialization'' na hatimaye political culture.

Hoja hii ililenga kueleza kuwa, hii ni changamoto ya kiasili, haitokani na makosa wala matendo yetu kama wanadamu, na kwa hakika, ipo juu ya uwezo wa udhibiti wa vyama vya siasa katika jitihadi zao za kujitangaza na kufahamika. Hata hivyo, changamoto hii inaweza kupatiwa ufumbuzi kwa kubuni na kupanaga mikakati maridhawa.
 
Last edited by a moderator:
Hoja ya "Mchambuzi" kuwa kutokuwa tayari Chadema kushika dola haijajengeka kwa upana wa kuridhisha, kwani tofauti ya kizazi cha leo na kile tulipopata uhuru ni kubwa sana. Wakati ule uelewa wa watu ulikuwa mdogo sana na wasomi walihesabika kwa nchi nzima, ndio maana wasomi wachache ndio walionekana wenye uwezo huo ingawa wengi wao walipata nafasi sababu tu ya kigezo cha elimu waliyokuwa nayo lakini si kigezo cha uwezo katika stahili zao.

Timu haiwezi kupewa sifa za ubora kama haijapambanishwa na timu nyingine na ikaonekana inafaa. Kupambanishwa na timu kadhaa na ikaonekana inatokeza, ni dalili wazi kuwa inao uwezo wa kuhimili vishondo vya ligi kwa kuwa imejipima nguvu vyakutosha. Mazingira kama hayo yananipa tumaini kubwa kuhusu uwezo wa Chadama katika kuongoza nchi kutokana na mengi ambayo wamepambana nayo na kushinda, kwani kuna vyama vingi vya siasa kama NCCR Mageuzi kilipokuja juu lakimi mizegwe ya CCM iliwamaliza mapema tu, lakini Chadema wanaonekana kuwazidi ujanja CCM na mwamko wa wananchi ni mkubwa sina shaka ni dalili tosha na wazi kwa chama hiki kuwa na uwezo wa kushika dola.

Sera wanazo nzuri, wanachotakiwa ni kujaribu kuangalia mapungufu kadhaa katika sera zao na pia mapungufu kadhaa hasa yanayoweza kusababisha kuleta nyufa kama baadhi wanapoamua kuonyesha dhamira za kuwania nafasi fulani za uongozi wakati hata uchaguzi mkuu haujawadia. Wanachotakiwa ni kuelekeza nguvu zaidi kwa sasa kuweka mizizi vijijini ambako ndiko kwenye chimbuko kubwa la wapiga kura, kwani huko ndio CCM wanakojivunia hazina ya ushindi kwa miaka mingi.

Kuna mapungufu kadhaa ya kawaida ambayo nitayajadili baadaye katika mada hii ambayo ni muhimu kuyafanyia kazi, la sivyo mambo ya siasa ni kama kamali, ubora wako unaweza ukawa katika mikutano na mizengwe ya kampeni na mengineyo yakampisha asiyestahili tukaendelea na vyama stahili kushika dola vikabaki ni ndoto za kufikirika.
 
Back
Top Bottom