PreGE2025 CHADEMA njooni na hoja zinazomtoa nyoka pangoni

PreGE2025 CHADEMA njooni na hoja zinazomtoa nyoka pangoni

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Labda husikilizagi Nondo za heche na Tundu Lissu hebu kazibue masikio yako
Wahana nondo, ila wanataka zamu yao ya kwenda Ikulu, yaani CCM haifanyi kitu kikubwa na wao hawatafanya kitu kikubwa pia. Maana masoko ya bidhaa zetu na kanuni za mchezo wa kuuza na kununua zitabaki kuwa zilezile; sanasana tutabaki vilevile au tutazidi kurudi nyuma zaidi na zaidi.
 
Katiba hii iliandikwa kwa kuzingatia mazingira fulani, walioandika sio wajinga. Kuwalaumu ni sawa kumlaumu mtu aliyejenga nyumba na kuweka nondo kwenye madirisha yote kiasi cha kushindwa kutokea dirishani kama moto ukiwaka na kuzingira sehemu ya mlangoni. Kama ukimuuliza vizuri atakwambia kuwa nimeweka nondo ili kuzuia wezi, vibaka, popobawa, nk. Kama ukiwauliza walioandika katiba kama hii watakwambia maskini na asiekuwa na elimu huwezi kumpatia demokrasia pana sana, atai misuse. Watu wetu ni maskini sana na bado ujinga ni mwingi sana kulinganisha na wale wa Ulaya na marekani; kama ukiwapa demokrasia pana sana lazima wataimisuse.

Wacha demokrasia itamalaki polepole kuanzia kwenye ngazi ya familia, mitaani na mashuleni kabla ya kuingiza demokrasia pana kwenye Katiba; tutaanguka tu. Wazazi siku hizi wameshaanza kuwapa watoto wao badhi ya uhuru wa kuchagua; ndio maana unaona siku hizi baadhi ya wazazi wanaruhusu watoto wao wa kike kucheza mpira wa miguu, kusomea sanaa, kufanya biashara, nk, zamani haikuwa hivyo. Hata demokrasia yetu lazima iende polepole sawa na mabadiliko ya kwenye jamii zetu. Mfano, ona akina Lissu wanatukana na kukebehi viongozi wakuu ati kwa kivuli cha demokraia kama ya ulaya. upuuzi mtupu, hatujafika huko sisi. Sisi tuko bado kwenye level ya kumlazimisha mtoto asome kozi anayoitaka mzazi. Demokrasia pana lazima ianzie majumbani mwetu kwanza. Wazungu demokrasia yao pana iko hata kwenye majumba yao wanamoishi.
 
Kwa unaona bora sisi tusiwe na tume huru tu kwa mifano hiyo??
Tume huru ni nzuri lakini tume iwe huru kiasi gani?

Tume iruhusu na huyu apite? anawaza wazungu tu waseme Tanzania iweje huku akijua wazungu wanshindwa kusema kitu kule Ukraine, Gaza, Sudan, Somalia, DRC, Neymar, NKorea. Waulize watoto wao wako wapi?


View: https://www.youtube.com/watch?v=YBMD4hlmKm8
 
No reforms no election ndio tamko la hovyo kabisa chadema imefanya tangu chama hiki kianzishwe. Kama kusipokuwa na election maana yake CCM itatawala milele. Kule Ukraine hakuna uchaguzi hivyo Zelensky yupo tu milele pale.
 
Kama Tume ya Zanzibar ingekuwa huru Jecha angefuta ushindi wa Maalim Seif kidhalimu namna ile?

Wewe sifa za Tume huru unazozijua ni zipi?
They can not allow their country go to the dogs.
Chadema tafadhalini tena naomba mje na hoja nzito kuliko hizi za kusema mnataka kuifanya Tanzania iwe kama Singapore, Malasya, Vietnam.
Kilichopoa mbele ya watanzania ni tume huru ya Uchaguzi, hii ndio itakuwa hakkimu sahihi wakuyadhihilsha haya..!!. Hofu ya nini kupata refa ambaye atakuwa huru kufanya maamzi yasiyopendelea upande wowote?.
Hatutaki demokrasia na tume huru ambayo hata muongo, mwizi, shoga, mlaghai anaweza kupenya na kuwa Rais. Watanzania bado wanashinda kutofautisha kati ya ahadi za kweli na ahadi feki, mtu mwenye dhamira nzuri na mwenye dhamira mbaya, halisi na mamluki. Mfano, mgombea anawaambia wapiga kura kuwa Tanzania ina rasilimali nyingi sana kuliko Malaysia na Singapore lakini hata toothpicks tunaagiza kutoka China, hivyo chagueni chadema tuifanye Tanzania kama Malaysia na Singapore.

Jiulize, hivi ni kweli serikali ya CCM au Chadema ndiyo inapaswa kutengeneza toothpicks, magunia ya kupakia korosho na vifungashio? Ni kweli kwamba serikali ya Marekani na Uingereza ndizo zinazotengeneza vinywaji na nguo?. Wanawadanganya watanzania.
 
Watanzania bado wanashindwa kutofautisha kati ya ahadi za kweli na ahadi feki...
Hii hoja yako imeniwazisha Sana. Yaani miaka 64 baada ya Tanganyika kupata madaraka na miaka 61 baada ya Tanganyika kuungana na Zanzibar na kuunda Tanzania. Yaani watanzania bado wanashindwa kutofautisha kati ya ahadi za ukweli na Ahadi za uongo?

Sasa miaka yote hiyo CCM na wazazi wake TANU na ASP walikuwa wanajenga Taifa la wajinga?
 
Hii hoja yako imeniwazisha Sana. Yaani miaka 64 baada ya Tanganyika kupata madaraka na miaka 61 baada ya Tanganyika kuungana na Zanzibar na kuunda Tanzania. Yaani watanzania bado wanashindwa kutofautisha kati ya ahadi za ukweli na Ahadi za uongo?

Sasa miaka yote hiyo CCM na wazazi wake TANU na ASP walikuwa wanajenga Taifa la wajinga?
Kaka bado tunao watanzania ambao wanachagua mtu kwa chakula, T-shirt na kofia, khanga na ahadi tamu, na hao ndio wengi. Chadema nao wameingia kwenye mtego huohuo wa ahadi zilizovunda. Hawasemi namna watakavyofanya ili tanzania ya chadema iwe kama Singapore, kilo ya korosho inunuliwe kwa 10,000, nani atachimba chuma chetu na kututengenezea mataluma ya reli na viwanda vya matrekta hapa, hawasemi walimu wazuri watawapaje na mishahara yao mikubwa, hawasemi namna watakavyofanya ili bidhaa zetu zipenye kwenye masoko yote duniani bila bughudha, hawatuambii namna watakavyofanya ili Trump atuondolee Tafiff kwenye bidhaa zetu na kuturejeshea misaada ya USAID aliyositisha, hawasemi fedha za kufanya tafiti kwa wanataaluma wetu watatoa wapi, hawasemi namna watakavyomnyang'anya mkulima kijembe cha mkono. Muda mwingi ni katiba mpya, tume huru,, Kaakaaa!! Tume huru kwaajili ya nani na kwanini?
 
Kaka bado tunao watanzania ambao wanachagua mtu kwa chakula, T-shirt na kofia, khanga na ahadi tamu, na hao ndio wengi.
Hapo wa kulaumiwa ni CHADEMA au CCM?

Halafu CHADEMA hawatoi chakula, Khanga, T-shirt au kofia. Sasa utawafananishaje na wanaotoa hivyo vitu?
 
Hapo wa kulaumiwa ni CHADEMA au CCM?

Halafu CHADEMA hawatoi chakula, Khanga, T-shirt au kofia. Sasa utawafananishaje na wanaotoa hivyo vitu?
Ni kuonyesha kuwa watanzania baaaado kabisa kuwa na akili ya kupambanua mambo, bado hawezi ku-link siasa na aina ya shuka wanalojifukika usiku. Wako ambao hawajui kama hata kama cdm ikiingia Ikulu hali yao itabaki ileile au kuzidi kuwa mbaya zaidi. Leo hii ukimuuliza mkenya akwambie kati ya Uhuru Kenyata na Willium Ruto nani ana anfuu kwao watashindwa kukupa jibu la moja kwa moja. Hata wapinzani wanadanganya tu, maana zimwi linalotutafuta liko nje ya mipaka yetu; linakuja kuiba na kuondoka kwa kutumia uzuzu wetu, akili zao na nguvu zao za kifedha, kijeshi na kiteknolojia. Wapinzani wanadanganya pia kama wanavyodanganya CCM.

Hebu ona uzuzu wa cdm, kama wakizuia uchaguzi usifanyike maana yake walioko sasa madarakani wataendelea kuweko hadi hapo uchaguzi utakapofanyika tena. Kwahiyo kuzuia uchaguzi usifanyike ni akili au matope?
 
Tunatumia fedha nyingi sana kuzuia wapinzani wasiende Ikulu badala ya kuzuia watu wabaya wasiende Ikulu. Hata CCM pia kuna watu ambayo tumeyapa majukumu ya kutuongoza katika ngazi mbalimbali wasiostahili kuweko hapo. Kuna watu wanaotuibia sana sasa sasa lakini tunashindwa kuwashitaki wala kuondoa. Hatusemi kuwa wapinzani wako off-point kabisa, lakini hata wao bado hawatuambii ni kwa vipi wao hawatakuwa na majizi.
 
Hao CCM wanawatumia tu kama toilet paper wakishakuwa hawana kazi nao basi watawatupilia mbali
Kaka hebu sikiliza hoja hizi nyepesi sana za Heche za mlima mrefu, dhahabu, maziwa mapana na marefu. Hivi yeye akiingia Ikulu atafanya nini na dhahabu na samaki hao ili mwananchi wa mbagala asilale na njaa? Kuna wakati mm ninaona ni sahihi serikali kuwazuia watu hawa; hawana tofauti na wahuri wanaouza mafuta ya upako ya korie kujipatia fedha.

View: https://www.youtube.com/watch?v=2rnV9xwHSgc
 
Kaka hebu sikiliza hoja hizi nyepesi sana za Heche za mlima mrefu, dhahabu, maziwa mapana na marefu. Hivi yeye akiingia Ikulu atafanya nini na dhahabu na samaki hao ili mwananchi wa mbagala asilale na njaa? Kuna wakati mm ninaona ni sahihi serikali kuwazuia watu hawa; hawana tofauti na wahuri wanaouza mafuta ya upako ya korie kujipatia fedha.

View: https://www.youtube.com/watch?v=2rnV9xwHSgc

Wapeni nafasi, wasipoweza watatolewa nao
 
Chadema yenye uwezo wa kujenga hoja za kumtoa nyoka pangoni iliishia 2015 baada ya Dr Slaa, professor Mkumbo, na sisi kuondoka chama kilipokodishwa kwa Lowassa (rip) ili kugombelea urais.
Hii ya sasa hivi, ya lisu, tegemea zaidi porojo, matusi, fujo, kukinukisha, na maozo mengine yanayofanana na hayo.
 
Kuna vitu vizuri na vibaya ambavyo watanzania wanavijua kuhusu CCM, Serikali, viongizi na Katiba yao, lakini wananchi bado wanaona kuwa mazuri bado ni mengi kukiko mabaya yao.

Ndio maana bado watu wanavaa mashati ya kijani mitaani bila hofu. Watanzania pia wanafahamu mazuri na mabaya ya vyama na viongozi wa upinzani lakini bado wanaona mabaya yao ni mengi kuliko mazuri, ndio maana mitaani kuko shwari hata kama viongozi wa upinzani wakikutana na masahibu gani ya kisiasa.

Na hii inatokana na viongozi wa upizani kuwa na tabia ya kuorodhesha matatizo tu bila kusema wao watafanya nini kuyaboresha katika mazingira kama haya ya dunia ilivyo. Kuna wakati wapinzani wanarudi CCM kila wakinyimana maslahi kuonyesha kuwa dhamira zao ni maslahi yao tu sio shida za wananchi orodha ya wapinzani waliorejea CCM ni ndefu sana na inayokatisha tamaa wananchi kuviamini vyama hivi kama vyama kimbilio kwao.

Kama utadhani kuwa hakuna watu wameichoka CCM utakuwa unakosea tena sana. Inafahamika kuwa ccm imekusanya watoto wanaccm wa zamani na sasa kuwapa zawadi na fadhila za kutuongoza hata kama wengine hawana uwezo wa kuongoza. Lakini hawaoni nani wa kumpa uongozi mbadala wa ccm bado.

Kuna kiongozi wa upinzani unasema naaam huyu ni madhubuti, lakini mara utasikia ameenda au amerudi ccm.
Hoja yao kubwa ni WATAKINUSHA.Tundu raia wa Ubeligiji , LEMA raia wa Canada.Watoto wao wote wapo kwenye hizo nchi,hawapo hapa. AMKENI VIJANA !!
 
Duuuuh kakaaa!! Ikulu ni tamu. Lissu akiingia Ikulu hatoki tena, ni zamu yao ya kutesa na cCM kuteseka.
Kama tukiweza kupata katiba mpya itakayo set standards nzuri, tukapata tume huru ya Uchaguzi ambayo ipo neutral, na vyombo vya ulinzi na Usalama vikawa unbiased, nakuhakikishia hata kama Lissu akiingia madarakani akafanya ndivyo sivyo basi na yeye Kwa uhakika atatolewa Kwa haraka
 
Back
Top Bottom