CHADEMA ndani ya Songea mjini

Pipoooooooooooooooooooooooozzzzzzzzzzzzzzzzzzzz Poweeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeer! HAyupo wa kuizuia inakuja kwa mwendo kasi wa umeme
 
attachment.php

Ndugu wanaJF!
Kuna kila dalili za ukweli fulani katika haya maandamano pasipo ushabiki, mie mwenyewe si mwanachama wa chama chochote ila nafuatilia siasa za nchi hii kwa ukaribu sana.
Haya maandamano nakumbuka ndio yalikua yakitokea mwaka ule 2005 wakati JK akiwa kabeba matumaini ya Watanzania ambao leo hii kawaangusha vibaya kwa mapenzi yao waliyo mpa. Kweli inabidi atafakari kwa makini kile alichowatenda Watanzania hadi wamemgeuka namna hii.

kwa bahati nzuri nilipata kushudia maandamano ya kumuunga mkono jk mwanza 2005 kweli barabara kuu siku ile hazikupitika na nikashuhudia mkutano wake wa kampeni morogoro 2010, umati uliomiminika uwanjani kwenda kumsikiliza ulikua balaa hadi nikaona upinzani hasa Dr. Silaa amechemka lakini nilipigwa na butwaa pale alipoanza kuhutubia, watu walianza kuondoka kama vile watu wanavyotoka uwanjani mpira ukiisha huku yeye akiendelea kuhutubia, kumbe bwana siri ya kuwavuta watu ilikua ni kundi la wasanii aliokua akitembea nao kwa kutoa burudani.
CDM hawana hata msanii mmoja lakini nyomi yake yanitisha kwamba kweli watu wamevutika kusikiliza watakachoambiwa na sio burudani ya watumbuizaji.

Nawaasa sana CHADEMA kuhusu umati huu wa watu wanaokuja kwenye mikutano yenu msiwapuuze hata kidogo, wamehamishia matumaini yao kwenu na msiwaangushe kwa vitendo na si kwa maneno kama JK.
Safisheni kila mahali patakapo leta dalili ya kuwaondolea matumaini yao watu hawa kwenu.

Nashauri tu jamani.
 
kudadadeki hapo lazima kieleweke kama hata huko Songea ambako kura hazikusimamiwa vizuri hatukupata hata mbunge 1 mwamko ni mkubwa hivyo ni jambo la kufurahia nguvu ya umma ni kubwa na walatin wanasema Vox Populi vox Dei
 
Ngoja nipige magoti niendelee na sala yangu....

"Mungu baba mtakatifu, uketie mahali pa juu patakatifu..... nakuja mbele zako nalileta taifa lako hili teule, Tazama wanao sisi (watz) kwa namna ya peke tumepata imani ya ukombozi wa taifa letu kupitia watu wako wateule ambao kwa uwezo wako wameweza kumgusa kila mtz mwenye dhiki na aliyekandamizwa na umasikini wa kutisha, ninaomba ukazidi kuwatia nguvu katika mapambano haya ya haki, ukawaepushe na dhuruba zote za mitafaruku ya kisiasa, ukawaimarishe wakaendelee kusimama vyema katika kuendelea kupigania hadhi ya maisha ya heshima ya mtanzania. Sana na zaidi kabisa ukatupe jicho la kimapinduzi kwa kadiri tunavyoikaribia 2015 tukaendelee kuwa na moyo huu wa kufikia mabadiliko tunayoyatamani kwenye nchi yetu.
Kwa jina lako lililokuu, nmeomba.... wote tuseme, Ameeeeeen"
 
Nasema tena-Ameen!
Nikiangalia picha hii ya CDM Songea na kuilinganisha na ile ya Singida kwenye mkutano wa Nnauye ninaona kule Singida ulikuwa ni vikongwe tu. Je wewe unaona tofauti gani?
1.
2.
3.
 
Ninachowaomba viongozi wa CHADEMA wajitahidi kuandikisha wanachama wapya na kufungua matawi

mengi sehemu mbalimbali wanazopita hasa huko Vijijini ambako kuna wapiga kura wengi.
 
Mkuu asante sana kwa hotuba hiyo ya mh.Zitto na kama ulichukua na ya Mh.Mbowe tuwekee maana jumbe hizi zinztujenga sana
 
Siku Moja kabla kulikuwa na mkutano wa CCM ambao uliwatisha na kuwazuia watu wasiende kwenye mkutano wa chadema,walifanya mkutano katika kata zote nakuwaambia mabomu yatapigwa kwakuwa chadema ni chama cha wahuni na fujo,baada ya kuona hii moyo wangu umekuwa na amani sana.
 
Naona kuna siku sasa wataamua kuwashikia wananchi bunduki au kutangaza amri ya kutotoka nje siku Chadema watakapoamua kufanya maandamano kabla ya mwaka 2014/15 karibia na uchaguzi mkuu.Wanasiasa uchwara wakishazidiwa wana-resort kwenye vitisho.

Wasubiri kiama chao chaja
 
Ngoja nipige magoti niendelee na sala yangu....
"Mungu baba mtakatifu, uketie mahali pa juu patakatifu..... nakuja mbele zako nalileta taifa lako hili teule, Tazama wanao sisi (watz) kwa namna ya peke tumepata imani ya ukombozi wa taifa letu kupitia watu wako wateule ambao kwa uwezo wako wameweza kumgusa kila mtz mwenye dhiki na aliyekandamizwa na umasikini wa kutisha, ninaomba ukazidi kuwatia nguvu katika mapambano haya ya haki, ukawaepushe na dhuruba zote za mitafaruku ya kisiasa, ukawaimarishe wakaendelee kusimama vyema katika kuendelea kupigania hadhi ya maisha ya heshima ya mtanzania. Sana na zaidi kabisa ukatupe jicho la kimapinduzi kwa kadiri tunavyoikaribia 2015 tukaendelee kuwa na moyo huu wa kufikia mabadiliko tunayoyatamani kwenye nchi yetu.
Kwa jina lako lililokuu, nmeomba.... wote tuseme, Ameeeeeen"

Ameeeeen
 
Mbona kwenye hizo picha nawaona vijana tu,tena wale waliokaa kibange bange!

Ndo maisha magumu yamewafanya waonekane kukaa kibangi bangi hivyo ndugu yangu ( a heri weye upo vyema), na mwingine anaweza wapiga kwa kuonekana ni vibaka kisa hawajakaa kimjini mjini ( alaaniwe aliyewafikisha hapo), nashukuru wamemjua mchawi na ndo hao hao watawaondoa nyie mliokaa kisharobaro na kimjini mjini. BTW wengi waonekao watanashati wanatumia hizo bangi kuliko hao waonekanao kibangi bangi! Nitakupa data baadae na picha juu.
 
Ngoja nipige magoti niendelee na sala yangu....
"Mungu baba mtakatifu, uketie mahali pa juu patakatifu..... nakuja mbele zako nalileta taifa lako hili teule, Tazama wanao sisi (watz) kwa namna ya peke tumepata imani ya ukombozi wa taifa letu kupitia watu wako wateule ambao kwa uwezo wako wameweza kumgusa kila mtz mwenye dhiki na aliyekandamizwa na umasikini wa kutisha, ninaomba ukazidi kuwatia nguvu katika mapambano haya ya haki, ukawaepushe na dhuruba zote za mitafaruku ya kisiasa, ukawaimarishe wakaendelee kusimama vyema katika kuendelea kupigania hadhi ya maisha ya heshima ya mtanzania. Sana na zaidi kabisa ukatupe jicho la kimapinduzi kwa kadiri tunavyoikaribia 2015 tukaendelee kuwa na moyo huu wa kufikia mabadiliko tunayoyatamani kwenye nchi yetu.
Kwa jina lako lililokuu, nmeomba.... wote tuseme, Ameeeeeen"

Amee! amee!amee!
 
Back
Top Bottom