bwana Jasusi
Tanzania kinachotusumbua ni kuwa na watu wanaopenda kitu kidogo,hii nchi hata wakipewa chadema,kama hatutakuwa na watu wanaofanya kazi kwa uzarendo itakuwa ni kila siku kuilaumu serikali itakayokuwa serikalini,unadhani ni kwanini viwanda hivyo vimekufa? je hatukuweza kusimamia visife? ni kwanini viwanda vya kurosho toka 25 mpaka hakuna kitu,je korosho hazilimwi tena? je waliopewa kazi ya kusimamia mashirika ya umma hawayaoni hayo? KITU KIDOGO
watendaji tuliowapa mamlaka ya kusimamia mali za umma hawafanyi kama inavyotakiwa,ni lazima tubadili mfumo wetu wa utendaji kazi,narudia hata chadema wakiingia madarakani,kama watu hawatatimiza wajibu wao ktk maneo yao ya kazi itakuwa ni lawama hata ktk hiyo serikali itakayo ongozwa na chama kingine.
Tanzania si masikini,ila watendaji waliopewa mamlaka ndio tatizo.
sheria zetu ni nzuri sana,mipango yetu ni mizuri sana na sera zetu ni nzuri sana,tatizo ni wanaopewa kazi ya kusimamia hayo yote niliyoyataja
Mkuu unayoyasema ni kweli kabisa. Na hapo ndipo tunaona kuwa CDM angalau inaonyesha kuwa sheria zipo nzuri lakini kwa makusudi kabisa hazifuatwi kwa sababu au za kifisadi au uzembe wa kepeana vyeo kirafiki na kichama chama zaidi bila kujali utaalamu na kutukuzana kijinga jinga tu huku ubabe ukitumika kuteketeza wale wazalendo wenye nia thabiti ya kuiendeleza nchi. Sheria ndiyo tunazo nzuri nyingine tuliiga tu lakini kwa maslahi ya CCM hazifuatwi! Umeona hata Bunge linavyoendeshwa, kibabe babe tu! sasa kama mhimili muhimu kwa Taifa unaendeshwa kwa siasa za kibabe namna ile unashauri nini?
Itakuwa busara kabisa Chadema ikaingia nayo ikafanya makosa yake lakini tunaamini yapo watakayoyamudu na wengine tena watafuata na ndiyo maana ya Demokrasia na maendeleo ndivyo yanavyochangiwa katika nchi. Siyo chama kimoja kikae madarakani mika 70 kikituzalishia familia za kifalme zenye ubinafsi zinazojali elimu na afya za familia zao tu.