Boss,
I hope hilo jina la Mkwawa unajua maana yake.
Pili unatakiwa ujue sababu zilizowafanya wanafunzi wafeli na baada ya hapo hata ukiandamana mie nitakuunga mkono kwani tutajua nani au nini kilisababisha wanafunzi kufeli, sio kuandamana kila kukicha kama vile hakuna kazi nyingine ya kufanya.
KESHO MVUA ZISIPONYESHA NA MAZAO YAKAHARIBIKA UTAANDAMANA WAZIRI WA KILIMO AJIUZURU?
Chris Lazima ujue wewe unasimamia nini, Je unasimamia tumbo au unasiamamia sera na wananchi.
Hakuna nchi duniani iliyoendelea inamchekea mtendani mbovu hasa pale wizara au taasisi yake inaposhindwa ispokuwa kwa masikini kama wewe.
Nionyeshe ni nchi gani makini duniani pamoja na hiyo ambayo wewe ni mkimbizi wa kiuchumi na kielimu baada ya serikali ya CCM kukunyima elimu na ajira ikabidi ukimbie kama ina viongozi ambao hawawajibiki pale wanapoharibu.
Kila waziri au kiongozi anayeshindwa kuongoza taasisi au wizara yake lazima aondoke.
Sisi hatuko tayari kuona tena watoto wanakosa elimu kwa ajili ya Maccm kuwagawana fedha za elimu. Ndio maanadamo yataongeza bajeti ya wizara, ndio maandamano yatawafanya watawala kutekeleza wajibu wao, ndio maandamao wajibishi ndio silaha iliyotumiwa duninani na wote waliodai haki na ilipatikana. Ndio maandamono hata leo yanatumika hata huko ulipo kudai haki.
Njia za mazungumzo zikishindikana njia nyingine zitatumika. Hatuna muda wa kubembeleza wazembe, wezi, mafisadi, na wavivu. wewe subiria ninaamini siku moja utaona matunda ya hawa wanaojitoa kwa ajili ya ndugu, watoto na kizazi hiki na cha kesho.
Hata afrika ya kusini kulikuwa na wasaliti ila leo wanashangilia uhuru haki na usawa. Hata kwenye kudai uhuru tulikuwa na watu walituuza kwa kutetea wakoloni, hata kwenye harakati za Martin luther king baadhi ya weusi walisaliti leo wanashangilia Mweusi kuwa raisi. Hata Yesu alisalitiwa na mwanafuzi wake hivyo hujaanza wewe kuwasaliti watanzania.
Kwa sababu unatetea chama huoni, mateso ya Watanzania, kwa sababu unajikomba huoni madhara ya elimu mbovu Tanzania, Kwasababu hujawahi kupimwa malaria na kupewa majibu fake kwasababu ya ukosefu wa ujuzi, Kwasababu hujawahi kuona uzembe wa kujenga barabara chini ya kiwango na kusababisha hasara kwa walipa kodi.
Huna uchungu na kodi zetu wala hujui mwananchi ni nani?
Na nisikusikie ukilalalmikia huduma bora za jamii. wewe tuache sisi na Tanzania yetu na lazima tumwajibishe yeyote mzende, mvivu, mwizi, fisadi kwa gharama zozote zile.
Maandamano ni kilele cha serikali kuwa kikteta.
Siku moja tutakuona ukiyakubali haya kwa aibu.