Kamanda The Commissioner
Uko sawasawa kwa kiasi kikubwa mno. Waratibu wa maandamano na mgomo huo siku ya Jumatatu, BAVICHA kupitia kwa Katibu wa Baraza hilo taifa, Deo Munishi, wametuma taarifa kwa vyombo vya habari wakitoa tahadhari kwa Jeshi la Polisi kuacha kuwa kichocheo cha vurugu siku hiyo, badala yake litimize wajibu wake wa kulinda raia na mali zao.
Amesema kuwa uongozi wa chama katika kanda husika ambako watu wake watakutana kwenye centre moja kwa ajili ya shughuli hiyo, umeshafanya mawasiliano na Jeshi la Polisi kwa maana ya kutoa taarifa ili kuhakikisha uwepo wa ulinzi wa raia na mali zao.
Wamesisitiza siku zote CHADEMA kimekuwa kikiitisha maandamano ya amani, ambayo yamekuwa yakifanyika bila rabsha yoyote, isipokuwa pale ambapo Jeshi la Polisi linapotumwa au kutumika vibaya, kuvuruga na kusababisha fujo! Mifano iko hai.
Wamesisitiza pia kuwa, kama alivyosema Mwenyekiti wa Taifa, Freeman Mbowe, maandamano hayo ni ya Watanzania wote wanaoipenda nchi yao. Itakumbukwa Mwenyekiti alisema yatamhusu kila mtu, waendesha daladala, bodaboda, mamantilie, walimu, wanafunzi (wote kuanzia msingi hadi vyuo vikuu), wasukuma mikokoteni, madaktari na wengine wote, watu wa kada zote nchini.