CHADEMA mwendo mdundo

kwahio na wale wanao toa tuhuma kwa mafisadi hawana haja ya kuwachukulia hatua kwa vile siasa haiko kiivyo sana? mie naona tuhuma za mbowe kufuja mil 35 ni nzito sana ukiangalia wananchi wengi wana moyo na chadema sasa kupatikana tuhuma kama hizi inatufanya tuone mambo ni yale yale kote kote.
bwana wenger, ni kwamba tunaposema Chenge , Lowasa, RA, Karamagi, nk kua ni mafisadi tunakua na malengo mawili.
1. tunataka waliowapigia kura wapime na waamua kua waliowapa dhamana ya uongozi ni wezi wa mali ya umma, ili wasiwapigie kura tena.
2. Tunatoa taarifa kwa DPP,Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa na kwa raisi kuwa wateule hawa ni wezi na wanastahili kutiwa jela. sasa watu hawa hawatimizi wajibu wao.
sasa kama hao kina kafulila na mwenzie wanahisi kuna wizi CHADEMA wa pesa za ruzuku eti kwasababu Mbowe ni signatory CAG amesikia, atakuja kukagua, report yake itawasilishwa na mamlaka husika zitapima maoni yake kuona kama kuna wizi ama hakuna, maana sikila report Chafu maana yake ni wizi, zingine ni uzembe wa kufanya marejesho tu.....elimika ujue na utambue, jikomboe wakati ni huu mtanzania mwenzangu.
 
Wanabodi,
Madai haya ni mazito sana kiasi kwamba yanaweza kukichafua chama vibaya sana. Ni tuhuma ambazo hazina tofauti na zile za kesi nyingi hapa nchini zinazohusu Ufisadi ikiwa ni pamoja na Matumizi mabaya ya madaraka - Ufisadi una tafsiri kubwa zaidi ya wizi wa fedha za EPA.

Mimi sioni tatizo hapa kufikia kuanza kumshambulia mtu wakati hatuna majibu ya tuhuma zilizotolewa....Kwa wanachama wa Chadema, Ukaguzi ufanyike tutakuwa tumemaliza ubishi!..Na kama kuna mtu mwenye taarifa nzuri kuhusiana na mahesabu ya chama ayaweke wazi kinyume cha madai ya Danda, Siku zote ukweli utajitenga!

Kwa mujibu wa taarifa hii inaonyesha wazi kwamba danda kafukuzwa kazi kutokana na madai yake ambayo yananipa wasiwasi kubwa zaidi kutokana na kauli za Zitto hapa JF kwamba kuna matumizi mabaya ya fedha za ruzuku. Na picha nzima inaonyesha wazi kwamba yapo makundi mawili ndani ya chama Chadema na yametokana na matumizi ya hizi ruzuku.

Haiwezekani kuwa kila anayeondoka Chadema swala liwe hili hili la matumizi mabaya ya ruzuku, hata kama Mbowe hutoa fedha zake mfukoni na kukikopesha chama..Bado haipotoshi madai ya matumizi mabaya ya fedha...Swala sii fedha ngapi zimechangishwa ama zimeibiwa isipokuwa ni matdai yote yanahusu matumizi mabaya ya RUZUKU.. Hizi ni fedha za walipa kodi wala sii za CCM ama Chadema ni fedha za wananchi ambazo zinatakiwa vyombo hivi kuwakilisha matumizi yake ktk vyombo husika kama Wizara, mashirika na Taasisi nyinginezo..Tunabishana ktk jambo ambalo lipo wazi kabisa...

Mimi sina wasiwasi na Mbowe najua fika kwamba amekisaidia sana chama Chadema kwa fedha yake mwenyewe lakini ikiwa kuna madai yasiyokuwa na msingi kama haya ni bora kuondoa nuksi hii kwani Chama kilipoamua kuwaondoka wahusika ktk madaraka walikuwa wakijua wazi ni kitu gani kinachofuatia. Na kuwatukana wahusika kwa maneno mazito na machafu haiwezi kusaidia kitu kabisa kwani hata mimi nimeanza kuwa namashaka makubwa na Uongozi ndani ya Chama hasa pale wanaposhindwa kutoa majibu yanayohusiana na madai isipokuwa wanakwenda Personal.. Swali linabakia palepale - Je, ni kweli, fedha za ruzuku na michango inatumiwa vibaya na huyu msaini aitwaye KOMU ambaye inadaiwa yuko karibu na Mbowe hivyo hupewa kinga inapofikia kuwakilisha mahesabu?..

Nitashangaa sana kuona viongozi wa Chadema na wanachama wake wataendelea kuyabeba madai kama haya kwa majibizano..Hawa wote walikuwa ama ni wanachama wa Chadema, na inasemekana wote wamefukuzwa uongozi kutokana na madaia yao kuhusiana na Matumizxi mabaya ya ruzuku..Chadema onyesheni mfano wa kuigwa na vyama vingine vyote iwe CCM, TLP, NCCR - Mageuzi.. Vyama hivi vyote vinatakiwa kukaguliwa mahesabu yao kwani ndio utaratibu unaoheshimika ktk ngazi zote za Uchumi..
 
Nawaonea huruma vijana wenzangu. Kuanza Siasa bila tabia njema ni aibu kubwa. Sasa ikigundulika hakuna Ufisadi hao vijana waliko kimbilia wataaibika na hawataaminika hata kidogo. Hata huko walikokwenda watakutana na hayo hayo.
Pili kuwa signatory haina maana ya kuwa Mwizi. Basi tuombe wakurugenzi wote wasiwe masignatory. mbona maofisini masignatory ni hao watoa majukumu mbona hatuogopi kama ni wezi.

Unapoona umedhalilishwa huwa wanaenda mahakamani na huko ukishinda ,unaweza mwachia mtuhumiwa na wananchi kukuelewa, ama kuamulu mahakama itende unavyotaka.

Sasa Juju kwa kutambua hilo kawaambieni wzi ya kuwa, kama tuhuma ni za uongo basi mwende mahakamani kwa kuruhusu kwanza NGAG ikague mahesabu ,na mkishinda basi jamaa yuko radhi kuingia jela. simple and clear
 
Yuko tayari kuingia jela kwa kosa gani? Hebu nielimishe hapa.
 
kama tuhuma za uongo wapelekeni mahakamani basi kwani wanawachafulia sana.kila siku hapa tunasema mafisadi wanaotajwa kama tuhuma ni za uongo waende mahakamani sasa leo swala liko kwenu chadema onyesheni mfano kwa kumpeleka huyu kijana mahakamani kwa kutoa tuhuma za uongo kuhusu ufujaji wa pesa ndani ya chama chenu,

tumechoka watukutupiana maneno kila siku kama swala uongo mnaweza kumshitaki na hapo mwenye nguvu ya ushaidi ndio atapona.lakini hayo mambo yakutupiana maandishi na maneno kila siku hayatupeleki popote.

Arsene Wenger,

Dunia nzima imejisahahu na uenezi na ufujaji wa habari(kama hii iko sawa)kwa tekenolojia iliyopo sasa-haijirudii (not reversable) na ni vigumu kula hata muogo ulioutema.

Nitarudia...'kuna umuhimu wa "Serikali" kupitia mifumo mingi...mengi ya kienyeji na ya kigeni ambayo kwa namna moja au nyingine yana wagusa maisha ya "Mwananchi" kwa namna yeyote! na kuyapatia ufumbuzi yakinifu-yanayowezekana kwa karne hii bila ya kupiga mabusu ya ******! yap!
 
kusema uongo kama upo, udhalilishaji kama kweli aliyosema si sahihi.

Mfano anapokusia wabunge wanawake wanavyofanywa.
Tangu lini kusema uwongo limekuwa kosa la jinai? Mnawadanganya akina nani?
 
hapo ndio tofauti ya siasa na sihasa inapoonekana.............vijana kibao,wanaingia upinzani na CCM pia kwa maslahi ya matumbo badala ya kubadilisha hali iliyopo...NATAMANI WATU WAPYA!!!!
 
Kazi ipo!! inaonekana uongozi wa kasoro wa mbowe ni sababu ya zitto kutaka uenyekiti
 
Yafaa Danda awekwe ndani kwanza kwa kutoleta hizo data mapema, alikuwa wapi kufanya hivo na sasa aone ni muda mwafaka? ni kati ya waleawle walioingia upinzani kwa kazi moja ya kuvuruga upinzani nionavo sasa wanarudi kundini kwao,
acha hizo bwanaaaaaa!
 
Wanabodi,
Madai haya ni mazito sana kiasi kwamba yanaweza kukichafua chama vibaya sana. Ni tuhuma ambazo hazina tofauti na zile za kesi nyingi hapa nchini zinazohusu Ufisadi ikiwa ni pamoja na Matumizi mabaya ya madaraka - Ufisadi una tafsiri kubwa zaidi ya wizi wa fedha za EPA.

Mimi sioni tatizo hapa kufikia kuanza kumshambulia mtu wakati hatuna majibu ya tuhuma zilizotolewa....Kwa wanachama wa Chadema, Ukaguzi ufanyike tutakuwa tumemaliza ubishi!..Na kama kuna mtu mwenye taarifa nzuri kuhusiana na mahesabu ya chama ayaweke wazi kinyume cha madai ya Danda, Siku zote ukweli utajitenga!

Kwa mujibu wa taarifa hii inaonyesha wazi kwamba danda kafukuzwa kazi kutokana na madai yake ambayo yananipa wasiwasi kubwa zaidi kutokana na kauli za Zitto hapa JF kwamba kuna matumizi mabaya ya fedha za ruzuku. Na picha nzima inaonyesha wazi kwamba yapo makundi mawili ndani ya chama Chadema na yametokana na matumizi ya hizi ruzuku.

Haiwezekani kuwa kila anayeondoka Chadema swala liwe hili hili la matumizi mabaya ya ruzuku, hata kama Mbowe hutoa fedha zake mfukoni na kukikopesha chama..Bado haipotoshi madai ya matumizi mabaya ya fedha...Swala sii fedha ngapi zimechangishwa ama zimeibiwa isipokuwa ni matdai yote yanahusu matumizi mabaya ya RUZUKU.. Hizi ni fedha za walipa kodi wala sii za CCM ama Chadema ni fedha za wananchi ambazo zinatakiwa vyombo hivi kuwakilisha matumizi yake ktk vyombo husika kama Wizara, mashirika na Taasisi nyinginezo..Tunabishana ktk jambo ambalo lipo wazi kabisa...

Mimi sina wasiwasi na Mbowe najua fika kwamba amekisaidia sana chama Chadema kwa fedha yake mwenyewe lakini ikiwa kuna madai yasiyokuwa na msingi kama haya ni bora kuondoa nuksi hii kwani Chama kilipoamua kuwaondoka wahusika ktk madaraka walikuwa wakijua wazi ni kitu gani kinachofuatia. Na kuwatukana wahusika kwa maneno mazito na machafu haiwezi kusaidia kitu kabisa kwani hata mimi nimeanza kuwa namashaka makubwa na Uongozi ndani ya Chama hasa pale wanaposhindwa kutoa majibu yanayohusiana na madai isipokuwa wanakwenda Personal.. Swali linabakia palepale - Je, ni kweli, fedha za ruzuku na michango inatumiwa vibaya na huyu msaini aitwaye KOMU ambaye inadaiwa yuko karibu na Mbowe hivyo hupewa kinga inapofikia kuwakilisha mahesabu?..

Nitashangaa sana kuona viongozi wa Chadema na wanachama wake wataendelea kuyabeba madai kama haya kwa majibizano..Hawa wote walikuwa ama ni wanachama wa Chadema, na inasemekana wote wamefukuzwa uongozi kutokana na madaia yao kuhusiana na Matumizxi mabaya ya ruzuku..Chadema onyesheni mfano wa kuigwa na vyama vingine vyote iwe CCM, TLP, NCCR - Mageuzi.. Vyama hivi vyote vinatakiwa kukaguliwa mahesabu yao kwani ndio utaratibu unaoheshimika ktk ngazi zote za Uchumi..

Mkandara
Nawe umeshakumbwa na upepo wa kusi? Au ndivyo tulivyo?
 
Huyu Danda ni mtu wa umri gani? Yaani anaalika CAG CHADEMA, huko CCM alishamuona CAG?

Eti mulipa kodi wa nchi hii! Stupidity
“There is no sin except stupidity.” Oscar Wilde
 
Wapendwa wanaJF wenzangu:

Nimekuwa mchangiaji wa nadra sana wa JF kutokana na sababu ambazo nilishawahi kueleza hapa siku za nyuma, mojawapo ukiwa ni ushauri wa baadhi yenu ambao niliuheshimu.

Nimekuwa msomaji wa majadiliano yanayoendelea kuhusu mustakabali wa taifa letu, na katika baadhi ya mijadala imetajwa CHADEMA na jina langu limekuwa likijitokeza tokeza. Aidha baadhi yenu mniandikia ujumbe nije hapa kufafanua baadhi ya mambo yanayohusu CHADEMA hususani yale yanayonihusisha kwa namna moja au nyingine.

Niliwahi kuandika hapa kwa kirefu naichukuliaje JF, lakini moja ya mtazamo wangu kuhusu JFni kuwa hivi ni chombo cha habari, pia ni kama kijiwe cha kijamii cha mijadala, lakini pia ni kama mkutano wa majadiliano katika mji(town hall meeting), naitazama pia JF kama mkutano wa hadhara ambao kila mmoja yuko huru kuhutubia!.

Katika muktadha huo, kama ambavyo nashiriki mijadala katika matukio yenye sura ya hayo hapo juu, najihisi nina wajibu kwangu binafsi na kwenu kuja kushiriki mijadala mara kadhaa.

Kwa kuanzia nawaletea taarifa hii rasmi, ambayo nimeitoa leo kwa niaba ya ya CHADEMA. Taarifa hii inajibu baadhi ya maswali ambayo yamekuwa yakiulizwa hasa kuhusu yanayoendelea ndani ya chama katika siku za karibuni.

Tamko hilo mnaweza kulipata kwa kubonyeza hapa: http://www.chadema.or.tz/habari/habari.php?id=103

Kesho tutakuwa na Kongamano la Vijana, halafu kuanzia tarehe 30 Novemba, 2009 mpaka tarehe 3 Disemba 2009 tutakuwa kwenye mfululizo wa vikao vya juu vya chama tukiutathmini mwaka 2009 na kupanga mwelekeo wa chama kwenda mwaka 2010.

Hivyo, naomba muendelee na mjadala na kama kuna maswali yatakayoulizwa nitakuja kuyajibu moja baada ya jingine baada ya tarehe hizo.

Salamu zangu za baraka ya Iddi kwa waislamu, ni siku nzuri ya kutafakari aya kwenye kurani tukufu mathalani Al Heed 57:25, Al-Nisa 4:35, Al-Maidah 5:8
 
Panapofuka moshi ni dalili kwamba kuna moto

Afichaye uginjwa/maradhi kifo kitam-umbua

Kelele zote hizi bado hamjui tatizo lenu....ama kweli sikio la kufa halisikii dawa...
 
Panapofuka moshi ni dalili kwamba kuna moto

Afichaye uginjwa/maradhi kifo kitam-umbua

Kelele zote hizi bado hamjui tatizo lenu....ama kweli sikio la kufa halisikii dawa...

Tumaini

Asante kwa mchango wako, ugonjwa upi huo? Kelele zipi hasa unatushauri tuzingatie kama sauti maridhawa za kuchochea mabadiliko ndani ya CHADEMA na taifa letu kwa ujumla? Naomba uziweke kwenye mpangilio ili tuzielewe maana tuliwahi kufundishwa tukiwa watoto kuwa kelele ni sauti zisizo katika mpangilio maalum?

Iddi njema kwa watanzania wote hususan waislamu.

JJ
 
Hongereni CHADEMA kwa kuwa chama imara, angalieni msijekuwa infiltrated na kukoseshwa welekeo!
 
Back
Top Bottom