CHADEMA mwendo mdundo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA mwendo mdundo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Serayamajimbo, Nov 27, 2009.

 1. S

  Serayamajimbo Senior Member

  #1
  Nov 27, 2009
  Joined: Apr 15, 2009
  Messages: 191
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  JUMA lililopita nilipigiwa simu nyingi sana na wasomaji wa safu hii, hoja kubwa ikiwa walihitaji kupata maoni yangu kuhusu kile kilichokuwa kinaendelea ndani ya CHADEMA kufikia David Kafulila na Danda Juju, kuvuliwa nyadhifa zao za uofisa wa makao makuu ya CHADEMA.
  Ndiyo maana nikaona nichukue nafasi hii japo kidogo kujaribu kuchangia kwa faida ya Watanzania wengi vijana na wazee ambao wanaonekana kuguswa sana na siasa za CHADEMA.
  Kinachofanya Watanzania wengi kuguswa sana na mwenendo wa mambo ndani ya CHADEMA kama ilivyo kwa CUF nimekielezea kwa kina sana huko nyuma tena mara nyingine nikirejea maandishi ya waandishi wengine kama Edward Kinabo, Charles Mullinda (mhariri wangu wa makala) na hata Mhariri wangu Mtendaji ndugu Absalom Kibanda.
  Hivyo ni vema nichangie japo kidogo ili wale wanaopenda kusikia mtazamo wangu kuhusu hili wapate nafasi ya kunisikia na kuchambua maoni yangu kuhusu sakata hili ambalo kwa bahati mbaya baadhi wameliita mgogoro ndani ya CHADEMA.
  Kwanza kabisa nikiri kwamba Kafulila ni rafiki yangu wa siku nyingi hususan kwa sababu amekuwa mchambuzi wa mambo ya siasa kwa muda mrefu akiwa ameandika makala muda mrefu kabla yangu, lakini pia ni kijana ambaye kwa muda mrefu nimemwona kama mwenye mtazamo unaofanana nami. Anapozungumzia juu ya kujenga upinzani wenye nguvu anagusa jambo ambalo wanaharakati wengi wa mageuzi tunaliimba kila siku na sisi wa Tanzania Daima tumeliimba kwa muda mrefu tukiongozwa na jemedari wetu, Mhariri Mtendaji, Absalom Kibanda.
  Tunafanya hivi si kwa sababu Tanzania Daima ni gazeti la chama fulani cha upinzani ama ni la vyama vya upinzani, la hasha! Ni kwa sababu tunazijua faida za nchi hii kuwa na upinzani wenye nguvu mithili ya ule uliopo nchi kama Marekani, Uingereza, Ujerumani, Ufaransa, na kwingineko ambako chama fulani hakina hatimiliki ya kuiongoza nchi na hivyo hufanya kila jambo kwa tahadhari kubwa na muhimu zaidi kwa kuangalia masilahi ya watu wao kwa kuwa kuteleza hata kidogo tu na kujifanyia mambo ya binafsi au mambo ambayo ni kwa maslahi ya chama chao kama tunavyoona hapa nchini kwetu, itakuwa ni tiketi ya wao kuondolewa madarakani.
  Katika hilo tumekuwa pamoja na Kafulila kwa kipindi kirefu. Na ndiyo maana amekuwa huru sana kunieleza mambo mengi mara kwa mara yanayoendelea ndani ya CHADEMA na mara zote nimekuwa nikitumia upeo wangu mdogo wa kuelewa ambao nimejaliwa na Mwenyezi Mungu kubaini yepi ni halisi yapo CHADEMA, yepi ni imani potofu ya Kafulila, yepi ni hofu tu ndani ya Kafulila mwenyewe, yepi amejikuta akiyatamka kwa sababu ya kutojua na yepi anayaongea kwa makusudi kwa sababu zake binafsi.
  Wakati wa mchakato wa uchaguzi wa CHADEMA tuliwasiliana sana na Kafulila kwa kupigiana simu na kutumiana sms, baada ya uchaguzi ule tumeendelea kuwasiliana naye mara nyingi tu, wakati wa kuvuliwa uofisa pia tumeongea sana na baada ya kutangaza kujitoa CHADEMA nilimpigia simu tukaongea naye zaidi ya dakika 18, na siku hiyo alinitaarifu kwamba angejiunga NCCR – Mageuzi. Mimi pia ni miongoni (kama kuna wengine) wa watu waliotumiwa ujumbe mfupi wa simu na Kafulila akinieleza comment ambayo alikuwa ameitoa kwa vyombo vya habari kuhusiana na kitendo cha katibu mkuu wa CHADEMA kutengua uteuzi wake kama Ofisa Habari na Uenezi wa CHADEMA. Na hatimaye nimesoma statement yake kwa vyombo vya habari wakati akizungumzia suala la yeye kuondolewa kwenye nafasi yake na azima yake ya kujitoa CHADEMA.
  Na mwisho nimesoma kile alichokiandika akiwa anachangia kwenye mtandao wa WANABIDII kuhusu kitendo cha yeye kujitoa CHADEMA.
  Naweza kusema sasa bila kuumauma maneno kwamba Kafulila ameshindwa kubadili mwenendo wake ili kuwa compatible (mtanisaidia Kiswahili chake) na wenzake.
  Nadiriki kusema hapa kwamba binafsi nilishiriki kumshauri Kafulila kuachana na siasa zake alizokuwa akiziendesha ndani ya CHADEMA na naamini wapo wengine hususan ndani ya chama chake hicho cha zamani waliomshauri pia. Lakini kwa sababu hakusikia yakamfika yaliyomfika. Na mara moja akatangaza kukihama chama.
  Napenda niwaeleze tu wasomaji kwamba hoja nyingi alizozitumia Kafulila ni za kale mno na ambazo zimepitwa na wakati na zile zile ambazo wakati fulani akiwa vizuri ndani ya CHADEMA alishiriki kuzitetea.
  Ni hoja zile zile za ukabila, viti maalumu vya ubunge, matumizi mabaya ya ruzuku, ubaya wa Mbowe, nk. Ni hizo hizo.
  Mambo mengine yanayozuka hivi sasa ya vikao vya siri vya kummaliza Zitto kisiasa na kuwavua uanachama wote waliomuunga mkono Zitto wakati wa uchaguzi mkuu wa chama, Mbowe kuita wahariri watano wa magazeti ili kuwatumia kummaliza Zitto na hatimaye mmoja akakataa, Mbowe kufuja sh milioni 35 za chama, na mengineyo mengi ni kusaidia tu kukoleza hoja hizo hapo juu. Lakini soma kwa mfano nukuu hii hapa chini:
  “Wakizungumza na waandishi wa habari jana katika makao makuu ya chama hicho, Kinondoni, Mkurugenzi wa Habari na Uenezi, Erasto Tumbo, alisema taasisi hiyo inayojishughulisha na masuala ya utawala bora inapotosha umma kwa kudai kuwa Mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo, amechota sh milioni 100 za chama hicho. Alisema kauli ya Ngawaiya si ya kweli na kwamba fedha hizo zilikuwa ni deni ambalo Ndesamburo alikikopesha chama katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005. “Ngawaia anatakiwa kufahamu fedha hizo ni za Ndesamburo ambaye ndiye alikopesha chama, ili kufanikisha uchaguzi mwaka 2005 na tayari katika kipindi cha miaka mitatu tumekamilisha kurudisha fedha hizo, kwa hiyo Ngawaia hana hoja labda ana chuki zake za kisiasa ambazo anatumiwa na CCM,” alisema Tumbo.
  Tanzania Daima, Jumanne Januari 20, 2009. Ukisoma habari hiyo utagundua Kafulila alikuwa pamoja na Mkurugenzi wake Erasto Tumbo. Lakini leo anatangaza kitu hicho hicho alichokipinga kwa Ngawaiya yeye akijielekeza kwa Mbowe wakati Ngawaiya alikuwa kwa Ndesamburo.
  Ni Kafulila ambaye amekuwa akiisifia CHADEMA, mfano kwenye Tanzania Daima Jumatano ya Juni 13, 2007 Mwanaidi anasema: “David Kafulila, mwandishi hodari hupenda kusema: ‘CCM works with a clock while CHADEMA works with a compass.’ Yaani CCM inafanya kazi kwa kutumia saa wakati CHADEMA inafanya kazi kwa kutumia dira.” Maneno haya hawezi kuyatamka leo baada ya kuvuliwa wadhifa wake lakini ameyahubiri sana akiwa mstari wa mbele wa CHADEMA.
  Ndiyo maana naiona hatua ya kufutwa kwa Kafulila wadhifa wake na hatimaye kuamua kukikimbia chama kama hatua isiyo na shida yoyote hasa kwa upande wa chama.
  Ni kama mtu aliyeshindwa kubadilika tu ili kufikia kwenye mstari unaomkutanisha na wenzake akaamua kutimua mbio.
  Lakini CHADEMA kitabaki kuwa chama makini kama kilivyo na kwa kweli binafsi napenda niseme, hivyo kilivyo CHADEMA ndivyo kinavyopaswa kuwa. Mwendo mdundo CHADEMA, chama cha siasa kinahitaji kuwa makini na hakihitajiki kuogopa kuchukua hatua pale inapobidi hata ikibidi kumvua wadhifa wake makamu mwenyekiti au hata mwenyekiti wa taifa, achilia mbali ofisa wa kawaida makao makuu.
  Wale waliokuwa wakiniuliza sana kwamba mbona chama kinaingia katika mgogoro itakuwaje? Jibu analitoa Kafulila mwenyewe kwenye makala yake ya Februari 12, 2006 pale aliposema:
  “Tunaelewa janja ya Bagenda ilikuwa nini? Bagenda alikuwa na agenda ya kuupotosha umma wa Watanzania kuwa vyama vya upinzani na hususan CUF na CHADEMA ni vyama hovyo hovyo.
  Kitu ambacho si kweli! Lakini hatuwezi kumshangaa Bagenda kwani anayo yafanya Bagenda ndiyo yaliyofanywa na karibu wasomi wote kila walipotaka kuhama upinzani.
  Haya ndiyo aliyafanya Nsanzugwanko, Wasira na sasa - Ngawaiya, ni gia ya kurejea kundini.”
  Ingawa Kafulila hakuelekea CCM lakini bado maneno yake mwenyewe dhidi ya Bagenda yaweza kuwa maneno yangu dhidi yake.
  Nani ajuaye, yawezekana kabisa kwamba kuingia CCM kwa Bagenda kwa mujibu wa Kafulila ilikuwa ni kurejea kundini na kuingia NCCR kwa Kafulila kwa mujibu wa mtu mwingine ikawa ni kurejea kundini, maana kwa maneno yake mwenyewe amenitamkia kwamba ndani ya jimbo lake NCCR ina nguvu kushinda CHADEMA.
  Muhimu kwa wana - CHADEMA na wanaharakati wanaoiunga mkono CHADEMA na kuitazama kama mbadala tunaoutafuta, ni kwamba Kafulila mwenyewe anasimama kukanusha akisema si kweli kwamba CHADEMA na CUF ni vyama vya hovyo hovyo tofauti na anavyotaka umma uamini sasa, baada ya kuamua kujitoa na kuingia NCCR. Pengine niwapongeze tu viongozi wakuu wa CHADEMA kwa busara ambayo wamekuwa nayo tangu kuanzishwa kwa chama.
  Busara ya kutojibishana hovyo hovyo kwenye vyombo vya habari. Hata katika hili muda mwingi wametulia.
  Ni mara chache sana ilipomlazimu Katibu Mkuu kutoa ufafanuzi kwenye vyombo vya habari. Hiyo ndiyo hulka inayotakiwa na hakika chama kitaendelea kuwa imara na pengine kuimarika zaidi bila Kabourou, bila Kafulila, bila Kyara, bila Akwilombe, na bila kiongozi yeyote wa CHADEMA ambaye ana mpango kama wa Kafulila bila kujali cheo ama wadhifa wake ndani ya CHADEMA ama umaarufu wake ndani ya nchi.
  Mabadiliko hayatakuja kwa askari laki moja waliojiunga na jeshi wakiwa wamejaa ubinafsi na kujiona kama wao ni wataalamu wa vita kuliko wengine. Mabadiliko halisi yataletwa na askari wachache waliojitoa wakaacha ubinafsi, kujisifu na kujiona wataalamu zaidi badala yake wakawa kitu kimoja katika kusikiliza sauti ya kamanda wa kikosi na kwa pamoja kusonga mbele kumkabili adui.
  Rejea makala yangu: “Idadi si kikwazo katika kupigania haki.” Tanzania Daima, Jumatano Aprili 9, 2008. Tuwasiliane kwa muda kupitia 0719 795 222 baada ya simu yangu kukwapuliwa na kibaka aliyeahidiwa na JK mwaka 2005 kwamba atapewa moja kati ya ajira milioni moja alizokuwa azitengeneze. Baada ya kuzikosa kajiajiri kuwakwapulia simu wale wanaomtetea, na si ajabu mwakani akamchagua tena aliyemwahidi ajira hewa na akikosa baada ya 2010 atapandisha ajira yake mwenyewe na kuwa mporaji wa kutumia sime na silaha nyingine ndogo ndogo.
   
 2. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #2
  Nov 27, 2009
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 217
  Trophy Points: 160
   
 3. Shalom

  Shalom JF-Expert Member

  #3
  Nov 27, 2009
  Joined: Jun 17, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Bado sijajua mwandishi ni nani? ni wewe sera ya majimbo au. Kuna njia nzuri tu za kuweza kuonesha kama ulileta habari hii ndiye mwandishi au umenukuu sehemu fulani.

  Kabla atujaanza kuchangia hebu tufafanulie nani nimwandishi wa hii habari
   
 4. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #4
  Nov 27, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,578
  Likes Received: 3,877
  Trophy Points: 280
  Sidhani kama ni busara ya Chadema kuendeleza endeleza hii ishu. Pia wengine wanaamini kabisa kuandika nakala kunasawazisha mambo fulani.Kumbe wakati unaandika nakala unawapa watu information mpya ambayo ni negative kwa Chadema.

  Tatizo langu ni kuwa ishu za CHADEMA zimekuwa uchi mno kiasi mabacho CHADEMA wanaweza wakawa wanaona wanafukia mashimo kumbe mvua ikija wanasababihsa matope.Ishu za hawa viongozi kama akina kafulila ni very sensitive.Kafulila ana weza akawa wrong 100% na anaweza akawa right 100%.Akiwa wrong,je watu wote watapokea hiyo meseji kuwa KAFULILA ana makosa?Chadema iko vitani, yet wamefumba macho na kujiona wameshafika.

  Believe me or not for any reasons that made Kafulila to be move, lazima kaacha athari za muda mfupi na mrefu, hizi ni hatari kwa uchaguzi jamani!

  Ishu hii wenyewe akina Slaa walishindwa kuidhibiti tangu walipoanza uchaguzi,mikutano ya siri.n.k, rekodi ya uchaguzi ya Chadema ni poor tangu ilipoanzishwa na hamna ukuaji, for sensible person anakata tamaa, yakiongeza na haya malumbano yenu ndiyo kabisaaaaa.

  Halafu naona mwandishi anasema leo kafulila hawezi tena kutamka hayo maneno, mwanaume kamili anaweza kula matapishi yake ili atoke sehemu moja kwenda nyingine! haina aibu hiyo!!! is aprt of life unless unampa chakula!

  Sijajua ila naamini, akina Kafulila walishakuwa excommunicated from Chadema society, piga ua, hata wewe huwezi ukakaa na kusema hapa wananipenda wakati watu kila ukitoa maoni bado wata recall yaliyotokea nyuma!''msaliti'' this is simple saiokoloji.

  Kafulila, kafulila, hajawa wa kwanza wala wa mwisho, chadema wameondokewa na watu mahiri zaidi ya huyu, who is this guy anyway! maana mnasababisha attention kwa kila mtu, huu udhaifu mkubwa sana wa chadema, kila mtu tishio???? siamini!!! mnaua chama, udhaifu wenu uko kwa kuwaogopa watu fulani, na sio kuheshimu katiba.ADUI YENU ATA WA STRIKE VIBAYA SANA, MTABAKI KUSEMA TULISEMA ONA SASA ZITO KAONDOKA, kumbe wenyewe mmeshaonyesha udhaifu tangu awali.VITA HII JAMANI!!! Kafulila kaacha makovu adui zenu wanashangilia, na msipoona ni vita basi kuna walakini kikubwa sana lengo lenu ni nini!-YIU ARE IN BATTLE FIELD!!

  kwenye ishu za mahusiano, hawa watu wabaya wasiitwe wabaya! wakiitwa wabaya watatoka tu , HUWEZI UKAMUITA MTU MNAFIKI KWENYE VYOMBO VYA HABARI UKATEGEMEA ATAENDELEA KUKAA KWENYE HICHO CHAMA!! hii haipo jamani! mtu yeyote atatoka tu

  CHADEMA sit down stay focused, mjue mko vitani hawa mnaoona wanaandika kuwapamba, believe wanawaharibia sana, sijajua intelijinsia yenu ya siasa imekaa vipi hapa!
   
 5. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #5
  Nov 27, 2009
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  CHADEMA, inawindwa na magaidi wa kisiasa wa TZ , watasubiri sana ili waione ikifa lakini hawatashinda. daima itazidi kunawiri maana haina sera ya kuoneana haya kwa wahujumu na wasaliti wa nidhamu ndani ya mchakato wa mabadiliko na maisha ya kisasa Tz
   
 6. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #6
  Nov 27, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Chadema ni malimbukeni...
   
 7. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #7
  Nov 27, 2009
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Nadhani kuna jambo linafichwa hapa, tunapigana changa la macho hivi hivi
   
 8. Kubwajinga

  Kubwajinga JF-Expert Member

  #8
  Nov 27, 2009
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,190
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Eti Mwendo Mdundo halafu yaliyoandikwa ni kupakana matope.

  Hivi ni nani anayefikiri mwandishi mwenye jina la SERAYAMAJIMBO ataandika ukweli juu ya Kafulila? Fool yourself.
   
 9. S

  Serayamajimbo Senior Member

  #9
  Nov 27, 2009
  Joined: Apr 15, 2009
  Messages: 191
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwandishi wa makala hiyo sio mimi na mwanahabari anayeitwa Samson Mwigamba

  serayamajimbo
   
 10. M

  Masatu JF-Expert Member

  #10
  Nov 27, 2009
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Jahazi linazama hilo jamani nyie kaeni na ubishi wenu mficha ugonjwa mauti humfichua....
   
 11. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #11
  Nov 28, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Viva Chadema . Hakuna mkamilifu na Chadema wanajifunza kwa kasi . Tuwaombee mazuri muda wote waungwana CCM life na lisizikwe liozee njiani .
   
 12. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #12
  Nov 28, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  That's the worst you can say?
   
 13. k

  kanda2 JF-Expert Member

  #13
  Nov 28, 2009
  Joined: Apr 22, 2007
  Messages: 1,318
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Kutokana na tuhuma zinazomkabili za kufuja ruzuku na kuwa muweka saini wa hundi za chadema
   
 14. IronBroom

  IronBroom JF-Expert Member

  #14
  Nov 28, 2009
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 524
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Chadema hakujatulia, Mbowe ashambuliwa

  Imeandikwa na Theopista Nsanzugwanko; Tarehe: 27th November 2009

  ALIYEKUWA kiongozi wa mambo ya Bunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Juju Danda, amejiondoa katika Chama hicho.

  Danda amesema jijini Dar es Salaam kuwa, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) anapaswa kukagua hesabu ya Chadema na kwamba, hati zikiwa safi yupo tayari kufungwa jela.

  Amedai kuwa, taratibu za manunuzi hazifuatwi katika chama hicho, na kwamba, manunuzi yote ya chama yanafanywa na Antony Komu ambaye ni mtu wa karibu na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe.

  Danda amedai kuwa, Mbowe ameifanya Chadema kama kampuni yake binafsi.

  “Nikiwa mmoja wa walipa kodi wa nchi hii, nina wajibu wa kuhakikisha fedha zinazotolewa kama ruzuku kwa vyama vya siasa zinatumika kwa mujibu wa sheria hivyo basi naomba mkaguzi mkuu wa fedha za Serikali aikague Chadema na ikipata hati safi mkondo wa sheria uchukue hatua dhidi yake” amesema Danda.

  Kwa mujibu wa Danda, Mbowe tu anafahamu zilipo fedha za ruzuku, makusanyo yanayopatikana kupitia ujumbe wa simu, na fedha zinazotoka kwa wahisani.

  Amesema, wananchi wengi wanakichangia chama hicho lakini Mbowe amekuwa akibadili michango hiyo kuwa yake binafsi na kudai kukikopesha Chama.

  Ametoa mfano kwa kudai kuwa, kuna mfanyabiashara jijini Dar es Salaam aliyechangia milioni 43 kwa ajili ya uchaguzi wa ubunge Tarime mwaka 2008 lakini Mbowe alidai kukikopesha chama.

  “Chadema wamekuwa wakilia na wimbo wa ufisadi kila siku lakini,shilingi milioni 35 alizochota Mbowe katika ruzuku ya Desemba mwaka jana ni sawa na asilimia 52 ya ruzuku ya chama kwa mwezi, wakati Sh.bilioni 133 za EPA ni sawa na asilimia 23 tu ya matumizi ya serikali kwa mwezi” amedai Danda.

  Danda amesema,yeye na aliyekuwa afisa habari wa chadema, walifukuzwa kwa kuwa walitofautiana kimtazamo na 'mmiliki huyo' hasa baada ya kuonesha hisia zao za kumuunga mkono Zitto Kabwe alipotaka kugombea uenyekiti wa chama hicho.

  Amedai kuwa, baada ya kufukuzwa alitakiwa kuomba msamaha ili arudishwe kwenye chama lakini alikataa.

  Danda amedai kuwa, hajafikiria atahamia chama gani lakini akishaamua ataondoka na wanachama wengi toka Chadema.

  Alisema ndani ya Chadema kuna makundi mawili, kundi la Mbowe lenye maisha mazuri na magari ya kifahari na lile la Zitto lenye wanachama wanaomuunga mkono mwanasiasa huyo.
   
 15. M

  Mayolela JF-Expert Member

  #15
  Nov 28, 2009
  Joined: Sep 21, 2009
  Messages: 383
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Haya tusubiri na tuone?
   
 16. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #16
  Nov 28, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  kuna watu walijiunga vyama vya upinzani bila kujua nini hasa maana ya upinzani, na kuna watu wanashindwa kuelewa kwamba wanasiasa wengi bado wanaangalia pesa kuliko wananchi
   
 17. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #17
  Nov 28, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,563
  Likes Received: 18,295
  Trophy Points: 280
  Danda ni Kafulila type, afadhali madai ya Kafulila yanasubstance japo uamuzi wa kujivua uanachama was a wrong move, na kuamua kudandia NCCR, is another wrong move, sasa huyu Danda yeye ni empty kabisa hoja zake hazina mashiko.

  Hii hoja eti Mkaguzi akague hesabu za Chadema wakipata hati safi, yuko tayari kuchukuliwa hatua za kisheria, yaani Chadema wamchukulie hatua yeye nkwa lipi?.

  Kwa mujibu wa Danda, hati safi ndio kipimo cha matumizi mazuri!. Hana habari kuna hati safi za matumizi ya mabovu ajabu na kuna hati chafu za matumizi safi na halali kabisa.

  Hebu tusubiri tuone huyu atadandia jahazi gani ila kwa maoni yangu, jamaa ni finito, kwisha, hakuna kitu hapa!.

  Kwa Chadema, hizi ni hatua muhimu, lazima pumba zitoke ili ubaki mchele safi, vinginevyo mtajikuta mnakwenda kwenye uchaguzi mkidhani mna watu, kumbe ni makapi matupu.
   
 18. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #18
  Nov 28, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  huyu nae anatuletea upupu sasa, yaani ufungwe kwasababu CHADEMA wana hati safi ya ukaguzi wa mahesabu? kwanza ajue kuita auditors sio kushitaki na pia unaweza ukawa na hati chafu bado auditors wananihii, tunawajua
   
 19. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #19
  Nov 28, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  good one pasco, hebu tujiulize halmashauri ngapi zina hati ya ukaguzi wakati yanayotokea tunayajua??

  anazungumzia komu na procurement, sijui yanayotokea lakini again ameonyesha mapungufu, ni lazima procurement person awepo sasa alitaka kila mtu afanya manunuzi? tatizo ni kama CHADEMA hawafuati procurement procedure, tatizo lisiwe Komu!!! hayo ya miko nk. tumeshayasikia na inaonyesha kuna haja kubwa ya kuweka darubini lisemwalo lipo, kama halipo laja!
   
 20. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #20
  Nov 28, 2009
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Who is ths Danda anyways kwenye siasa za Bongo, ndip kwanza namsikia leo after almost 2 decades ya vyama vingi kuoperate tena Tz
   
Loading...