CHADEMA msijidanganye, Dr. Slaa hayuko peke yake

watanzania tusipokuwa makini tutaishia kusikiliza porojo tu na matatizo yatabaki palepale....
 


Maneno mazito haya; sasa tunajua na tumeona tofauti ya watu wanaotaka mabadiliko ya kweli na wanaotaka mabadiliko tu. Wanaotaka mabadiliko tu hawana cha kusimamia isipokuwa kitu kibadilike tu. Hawajali ni mabadiliko gani, ya nini, kwanini na kwa vipi tu. Ni kama watu wanaopigishana stori kijiweni; mtu anaweletea stori za mpirani jinsi magoli yalivyofungwa na watu wanashangilia na kurudia jinsi kona ilivyopigwa n.k kumbe aliyewasimulia alisikia redioni tu. Wanataka tuamini kuwa Lowassa anawakilisha kweli mabadiliko! Hata kusema "CHADEMA" Lowassa maskini wa Mungu anapata tabu, halafu juu yake anatakiwa awakilishe UPAWA vile vile! Ili watu wapewe!

Ndio maana toka mwanzo nilishapuuzia huu UPAWA niliamini wakati ule kuwa ni dubwasha baya zaidi lililovuruga harakati za mabadiliko na litatusumbua baadaye. Lakini sikudhania lingetokea na la Lowassa vile vile. Sasa hivi CCM wala hawana haja ya kupiga kelele tena, wanasubiri vichinjio vyao wafutilie mbali upinzani tarehe 25 liwe onyo na somo kwa wengine!

Umefika golini kabisa na umebaki wewe na kipa mtu anakuonesha kisura halafu unabutua juu; hata wakionesha replay zile unashindwa kuangalia kwani ni aibu.
 

Ccm wewe kamnadi magufuli .tuachie lowasa wetu.
 
Ndiyo tunajua kuwa ccm na serikali yake iko nyuma ya huyu mzee Slaa.
 
Slaa muongo, Mbowe muongo, Lowassa ndio kabisa.

Chama cha kutawala mpaka sasa ni CCM pekee.
 
Hamna kiongozi yoyote yule mashuhuli duniani ambaye huwa hapitii matatizo na ukiona kiongozi yoyote ambaye hajapitia misukosuko ujue huyo hafai kuwa rais kama makufuri hajapitia misukosuko yoyote ile kwanza ile nafasi aliipata kwa zali tu sasa kwa mfano akiwa rais atatuambia nini wakati siku zote matatizo ndio yanamjenga mtu kisiasa kama muheshimiwa lowassa kwa 100% anafaa kuwa rais kwa misukosuko mingi aliyo pitia anamengi ya kutuambia watanzania na amejifunza mengi kwenye maisha yake kwanza anasema anauchukua umaskini inamaana ameisha jua yote yanayo tokea tatizo ni umaskini. Kwanza tu hiyo ni point ya kwanza na kwa kusema hivyo tayari uchaguzi ameshinda.
 
Dr.W.Slaa hayuko peke yake ndio,
Yuko na Gambaz
 
Last edited by a moderator:
Dr. Slaa amesema kinachomsumbua moyoni mwake na hawezi kufuta kauli zake kwani hana imani na Mh. Mgombea wa Ukawa. Tunamshukuru kwani tunahitaji kujua mengi ili tuwapime wagombea wetu lkn hatuwezi kumpuuza kirahisi bila kuwa na majibu ya hoja zake kwani ni mtu anayeaminika na watanzania
 

Wepesi wa hoja zake unakujaje? EMB kumbuka kuhusu list of shame af fananisha na press conference yake pale Serena yani iko wazi kuna kitu kama mfatiliaji na si mlopokaji
 
tanzania niya watu wachache lowasa kutoka huko inawaumiza kichwa sana hawa coz wanaona ulaji unaenda kukwatwa coz anafahamu kila kitu. DAH najuta sana kuzaliwa tanzania bora hata uganda mara mia duh
 

Mimi bado najiuliza swali moja tu. Baada ya maaskofu kutoa tamko lao, Kardinali Pengo alilipinga peupe. Ghafla akatokea Gwajima from nowhere akichukizwa na kitendo cha kupingwa kwa tamko hilo. Hewa ilichafuka kwa muda. Leo hii tunasikia tena kauli kuwa Gwajima alishuhudia maaskofu 30 wakipokea rushwa ili wamuunge mkono mgombea fulani. Je hili jambo laweza kuwa na uhusiano?
 

Tazama hiyo sentensi yako ya mwisho. Nainukuu, "Dr Slaa ni kioo, msimamo wake usiyoyumbishwa ni tunu pia ana mapenzi ya dhati kwa Taifa na watu wake" mwisho wa kunukuu.
Hivi umesukumwa na nini kusema hayo? Mtu mwenye sifa hizo na akiwakilisha upinzani anaweza kuandaliwa mkutano na kulipiwa gharama zote za ukumbi, matangazo ya moja kwa moja ya Radio na Television kwa vituo kadhaa na serikali anayoipinga? Anaweza kufanya kikao cha siri hotelini na Waziri wa serikali mwandamizi kwa masaa kabla hajaongea na waandishi?
Hatukatai, kama sifa hizo anaweza kuwa nazo HAPO AWALI lakini kwa sasa hana sifa hizo tena, amebadilika na ameamua kubadilika. Sababu hakuna anayeijua kwa dhati ila yeye mwenyewe. Wapo wanaosema ni mchumba, hakuna mwenye uhakika. Wapo wasemao ni kukosa nafasi aliyokuwa ameiweka akilini kwa muda mrefu na kujiaminisha ni yake, sijui.
Lakini wapo wasemao ni mchanganyiko wa sababu hizo zingine kisha ukakolezwa na PESA.
DR Slaa kama kapokea pesa ya hongo ili asaliti hizo sifa ulizozitaja wala haitakuwa jambo la ajabu kwa binadamu na nitashangaa atakaye sema kuwa Slaa hawezi kufanya hivyo. Kama Yuda mfuasi wa Yesu na miongoni mwa mitume na aliyeshuhudia miujiza na nguvu za Yesu aliweza kukubali kumsaliti Yesu kwa fadha ndio itakuja kuwa Slaa ambaye tayari ana hiyo historia ya kusaliti mamlaka nyingine?
Ni bahati mbaya kwake kuwa mission ime backfire na atashusha mvi zake kaburini kwa fedheha kubwa na kukiachia kizazi chake huzuni ya aibu yake.
 
Hatusikilizi majungu mwenye ushahidi peleka mahakamani. LOWASSA NI RAIS
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…