Hizo taarabu za kusoma namba peleka chimwaga na Lumumba
Mpaka sasa ukawa wanaongoza kwa 94.5 %
Mnazunguka na wasanii kwenye kampeni
Mnafanya fiesta show nchi nzima
Hata ivyo mnawapa promote wasanii kazi zao zinaonekana ila kura ni lowasa na wabunge Wa ukawa
Siku ukifika hata kama hujui hesabu lazima namba utaisoma.Hizo hesabu za kura za Ufipa?
Hizo hesabu za kura za Ufipa?
unajua maneno yako yanaonesha ulivyo kata tamaa kutokana na mtu mlie mtegemea angemaliza kazi kuiangamiza CHADEMA amepiga mpira nje kabisa na umekuwa wa kurusha kwahiyo mnafikiri bado kuna mtu mwingine mnaweza kumtumia!! mnaweza kumpata na akatumika lakini CHADEMA ITAZIDI KUIMARIKA ZAIDI NA ZAIDI. Jiulize pesa mlizotumia, muda na rasilimali zote mlizowekeza kwa Dr slaa ili aianmgamize CHADEMA n MLICHOPATA VINAUWIANA?? ni bora fedha hizo mngezielekeza kwenye kampeni za wagombea wenu ambao wengi hawajaanza kampeni kwa kukosa fedha halafu ninyi mnahangaika na Dr aliye expire!!Baada ya Dr. Slaa kung'atuka siasa za kitapeli za CHADEMA na washirika wake, tumeshuhudia manguli na viwanda vya propaganda wa CHADEMA wakitumia kila mbinu kutuaminisha kuwa kila kitu ni shwari ndani ya Chama hicho na kikundi cha UKAWA. Hoja nyingi zinazokosoa kitendo cha CHADEMA hususani UKAWA kuonyesha taswira ya kununuliwa na mgombea wake wa urais ambaye walipita nchi nzima na kutumia rasilimali nyingi ikiwemo damu na wengine kupata ulemavu kwa kumnadi ni FISADI papa pamoja na wenzake alioambatana nao. Hoja hizi hazijibiwi badala yake viwanda vya propaganda vimekuwa vikifanya CYBER BULLYING kwa yeyote anayehoji ama kukosoa.
Vinara wa uhuni huo wamekuwa wakiongea kwa kusema Dr. Slaa amechelewa na hakuna kinachobadilika na kinachoshangaza zaidi, yule waliyekuwa wanamnadi ni Rais wa mioyo ya Watanzania amepewa majina mapya ya Babu, Mzee, Kizee n.k. Pia wazungumzaji wanaotulazimisha tuwasikilize wao pekee wanajinasibu kuzungumza kwa niaba ya Watanzania wote. Hili ni kosa ambalo si muda mrefu watakuja kujutia na anguko lake si dogo.
Najua, nafahamu, natambua kuwa yeyote asomaye huu uzi anaelewa namaanisha nini lakini kwa kuwa tayari wengi wameshakula kiapo cha giza, wataporomosha matusi, kebehi na kubeza.
CHADEMA mnaodhani mmeshika mpini, tambueni kwamba Dr. Slaa hayupo peke yake. Kuna kundi kubwa la wanamageuzi wa kweli ambao wanamuunga mkono na wanajua cha kufanya ili kuondokana na upuuzi wa viongozi waroho kutaka kutumia njia za mkato kufanikisha malengo yao huku wakisigina misingi iliyofanikisha Chama kukubalika na wengi. Misingi ya kupambana na Ufisadi, ukiukwaji maadili ya uongozi na wizi wa amali za umma.
Dr. Slaa ni kioo, msimamo wake usiyoyumbishwa ni tunu pia ana mapenzi ya dhati kwa Taifa na watu wake.
Jibu sahii kwa wakati sahii ameongeza mwingine mwakwembeNi kweli kabisa hayupo peke yake hata chadema wanajua.kweli kabisa hayupo peke yake yupo na JOSEPHINE .hilo tunajua wote !!!!!
Hakuna tukio lisilokuwa na wafuasi wake,hata shetani alikuwa ni malaika mzuri na mtiifu wa mwenyezi Mungu.
Siku alipoasi na kutimliwa na mwenyezi Mungu aliondoka na kundi kuubwa la wafuasi wake na ndio hawa wanaotutesa hapa dunia.
Pamoja na shetani kuondoka na kundi lake kubwa,Mungu aliendelea kuwa Mungu yuleyule,mwenye weledi uleule,huku kundi kuubwa la malaika wakiendelea kumzingira na kumsudia kwa kusema kuwa wewe ni Bwana.
Na hakuna kilichoharibika kinyume na matarajio ya shetani pamoja na wafuasi wake.
Kwa hiyo hakuna jambo geni unaloweza ukalifanya ukiamini kuwa wewe ndiye wa kwanza kumbe hilo jambo lilishafanyika kabla yako.