CHADEMA msijidanganye, Dr. Slaa hayuko peke yake

CHADEMA msijidanganye, Dr. Slaa hayuko peke yake

Msanii

Platinum Member
Joined
Jul 4, 2007
Posts
26,355
Reaction score
39,825
Baada ya Dr. Slaa kung'atuka siasa za kitapeli za CHADEMA na washirika wake, tumeshuhudia manguli na viwanda vya propaganda wa CHADEMA wakitumia kila mbinu kutuaminisha kuwa kila kitu ni shwari ndani ya Chama hicho na kikundi cha UKAWA. Hoja nyingi zinazokosoa kitendo cha CHADEMA hususani UKAWA kuonyesha taswira ya kununuliwa na mgombea wake wa urais ambaye walipita nchi nzima na kutumia rasilimali nyingi ikiwemo damu na wengine kupata ulemavu kwa kumnadi ni FISADI papa pamoja na wenzake alioambatana nao. Hoja hizi hazijibiwi badala yake viwanda vya propaganda vimekuwa vikifanya CYBER BULLYING kwa yeyote anayehoji ama kukosoa.

Vinara wa uhuni huo wamekuwa wakiongea kwa kusema Dr. Slaa amechelewa na hakuna kinachobadilika na kinachoshangaza zaidi, yule waliyekuwa wanamnadi ni Rais wa mioyo ya Watanzania amepewa majina mapya ya Babu, Mzee, Kizee n.k. Pia wazungumzaji wanaotulazimisha tuwasikilize wao pekee wanajinasibu kuzungumza kwa niaba ya Watanzania wote. Hili ni kosa ambalo si muda mrefu watakuja kujutia na anguko lake si dogo.

Najua, nafahamu, natambua kuwa yeyote asomaye huu uzi anaelewa namaanisha nini lakini kwa kuwa tayari wengi wameshakula kiapo cha giza, wataporomosha matusi, kebehi na kubeza.

CHADEMA mnaodhani mmeshika mpini, tambueni kwamba Dr. Slaa hayupo peke yake. Kuna kundi kubwa la wanamageuzi wa kweli ambao wanamuunga mkono na wanajua cha kufanya ili kuondokana na upuuzi wa viongozi waroho kutaka kutumia njia za mkato kufanikisha malengo yao huku wakisigina misingi iliyofanikisha Chama kukubalika na wengi. Misingi ya kupambana na Ufisadi, ukiukwaji maadili ya uongozi na wizi wa amali za umma.

Dr. Slaa ni kioo, msimamo wake usiyoyumbishwa ni tunu pia ana mapenzi ya dhati kwa Taifa na watu wake.
 
Babu Slaa yuko na CCM waliomtuma na kumuhonga ,, Slaa amekodishiwa private jet kumpeleka Afrika Kusini akale ela alizohongwa na CCM
 
Lowassa anasonga mbeele.Silaha yao ya mwisho imebuma.
 
Tuna mambo muhimu ya kufanya zaidi ya Porojo za Dk!
Kura kwa Lowassa
 
Watanzania wengi mnaonekana mu wachanga wa siasa...

Mioyo yenu yapata tabu kwa kuwa imani zenu zimewekwa juu ya watu...

Mtu anahangaika kuwa na mahaba na Lowassa au Slaa n.k

Hao wanapita tu nchi na vyama vitabaki
 
Hakuna tukio lisilokuwa na wafuasi wake,hata shetani alikuwa ni malaika mzuri na mtiifu wa mwenyezi Mungu.

Siku alipoasi na kutimliwa na mwenyezi Mungu aliondoka na kundi kuubwa la wafuasi wake na ndio hawa wanaotutesa hapa dunia.

Pamoja na shetani kuondoka na kundi lake kubwa,Mungu aliendelea kuwa Mungu yuleyule,mwenye weledi uleule,huku kundi kuubwa la malaika wakiendelea kumzingira na kumsudia kwa kusema kuwa wewe ni Bwana.

Na hakuna kilichoharibika kinyume na matarajio ya shetani pamoja na wafuasi wake.

Kwa hiyo hakuna jambo geni unaloweza ukalifanya ukiamini kuwa wewe ndiye wa kwanza kumbe hilo jambo lilishafanyika kabla yako.
 
Ni kweli ulichosema kuwa Dr Slaa hayuko peke yake, kwa kuwa inajulikana wazi kuwa yupo sambamba na 'washikaji' wake wakubwa wa Sisiem, ambao ndiyo waliompa full support kwenye kikao chake na waandishi wa habari pale Serena Hotel!
 
Kama huna hela njoo kijijini tulime, Dunia ya sasa hela ndo kila kitu. Endelezeni porojo tu wenzenu wanajiendeleza pitia migongo yenu.

Safi Mbowe, Safi Lowassa, Safi R Azizi na wengine wote mnaoziona fursa na kuzitumia.
 
Babu Slaa yuko na CCM waliomtuma na kumuhonga ,, Slaa amekodishiwa private jet kumpeleka Afrika Kusini akale ela alizohongwa na CCM
Zamani Slaa alipokuwa anamshambulia Lowasa akiwa CCM alikuwa sawa hajaongwa, lakini sasa hivi kwa kuwa Lowasa yuko CHADEMA Slaa yule yule aliyekuwa akiyasema yale yale anaposema sasa amehongwa na CCM!!! Kisa Lowasa safi baada ya kuhamia CHADEMA!! Ni kweli?
 
Leo Nimeshtuka kusikia eti Rostam naye anaisemea CHADEMA. Bado Chenge tu sasa.

kuna alisema yeyote atakayemjibu slaa awe askofu au yeyote aliyetuhumiwa basi atakuwa anabeba lowasa au cdm coz walishambuliwa wote so ulitaka tostam aseme ni kweli anafadhili cdm?
 
Zamani Slaa alipokuwa anamshambulia Lowasa akiwa CCM alikuwa sawa hajaongwa, lakini sasa hivi kwa kuwa Lowasa yuko CHADEMA Slaa yule yule aliyekuwa akiyasema yale yale anaposema sasa amehongwa na CCM!!! Kisa Lowasa safi baada ya kuhamia CHADEMA!! Ni kweli?

Hivi ni uvivu wa kufikiri au makusudi tu? Katibu mkuu wa chama anapofanya jambo kwa maslahi ya chama anachokiongoza atakuwa amenunuliwa na nani? Amenunuliwa na mwenyekiti? Kajinunua?
 
Wapigwe tu
 

Attachments

  • 1441255960014.jpg
    1441255960014.jpg
    48.2 KB · Views: 805
Zamani Slaa alipokuwa anamshambulia Lowasa akiwa CCM alikuwa sawa hajaongwa, lakini sasa hivi kwa kuwa Lowasa yuko CHADEMA Slaa yule yule aliyekuwa akiyasema yale yale anaposema sasa amehongwa na CCM!!! Kisa Lowasa safi baada ya kuhamia CHADEMA!! Ni kweli?
Kama wengi walimkubali lowassa ndani ya chama demokrasia ilifuata mkondo
 
Back
Top Bottom