Maneno mazito haya; sasa tunajua na tumeona tofauti ya watu wanaotaka mabadiliko ya kweli na wanaotaka mabadiliko tu. Wanaotaka mabadiliko tu hawana cha kusimamia isipokuwa kitu kibadilike tu. Hawajali ni mabadiliko gani, ya nini, kwanini na kwa vipi tu. Ni kama watu wanaopigishana stori kijiweni; mtu anaweletea stori za mpirani jinsi magoli yalivyofungwa na watu wanashangilia na kurudia jinsi kona ilivyopigwa n.k kumbe aliyewasimulia alisikia redioni tu. Wanataka tuamini kuwa Lowassa anawakilisha kweli mabadiliko! Hata kusema "CHADEMA" Lowassa maskini wa Mungu anapata tabu, halafu juu yake anatakiwa awakilishe UPAWA vile vile! Ili watu wapewe!
Ndio maana toka mwanzo nilishapuuzia huu UPAWA niliamini wakati ule kuwa ni dubwasha baya zaidi lililovuruga harakati za mabadiliko na litatusumbua baadaye. Lakini sikudhania lingetokea na la Lowassa vile vile. Sasa hivi CCM wala hawana haja ya kupiga kelele tena, wanasubiri vichinjio vyao wafutilie mbali upinzani tarehe 25 liwe onyo na somo kwa wengine!
Umefika golini kabisa na umebaki wewe na kipa mtu anakuonesha kisura halafu unabutua juu; hata wakionesha replay zile unashindwa kuangalia kwani ni aibu.