CHADEMA msijidanganye, Dr. Slaa hayuko peke yake

CHADEMA msijidanganye, Dr. Slaa hayuko peke yake

Zamani Slaa alipokuwa anamshambulia Lowasa akiwa CCM alikuwa sawa hajaongwa, lakini sasa hivi kwa kuwa Lowasa yuko CHADEMA Slaa yule yule aliyekuwa akiyasema yale yale anaposema sasa amehongwa na CCM!!! Kisa Lowasa safi baada ya kuhamia CHADEMA!! Ni kweli?

Kama unataka kuisaidia nchi ili kupata kiongozi mzuri huwezi kumshambulia mmoja tu na kuwaacha wengine as if hawana kosa lolote. Ni ajabu na kweli kwamba Dr Slaa anaisaidia CCM kushinda uchaguzi. Hizi ni hasira za mkosaji
 
Nikweli Hayuko Pekeake Yuko Na Josefhine Mshumbushi
 
wANAJAVI NAOMBA KUULIZA MPAKA DR SLAA ANAZUNGUMZA BEI YA SLAA HAIKUWA IMEPATIKANA KWA WANAOJUA BEI YA DR SLAA NI BEI GANI NAOMBA ATUJUZE
 
Maneno mazito haya; sasa tunajua na tumeona tofauti ya watu wanaotaka mabadiliko ya kweli na wanaotaka mabadiliko tu. Wanaotaka mabadiliko tu hawana cha kusimamia isipokuwa kitu kibadilike tu. Hawajali ni mabadiliko gani, ya nini, kwanini na kwa vipi tu. Ni kama watu wanaopigishana stori kijiweni; mtu anaweletea stori za mpirani jinsi magoli yalivyofungwa na watu wanashangilia na kurudia jinsi kona ilivyopigwa n.k kumbe aliyewasimulia alisikia redioni tu. Wanataka tuamini kuwa Lowassa anawakilisha kweli mabadiliko! Hata kusema "CHADEMA" Lowassa maskini wa Mungu anapata tabu, halafu juu yake anatakiwa awakilishe UPAWA vile vile! Ili watu wapewe!

Ndio maana toka mwanzo nilishapuuzia huu UPAWA niliamini wakati ule kuwa ni dubwasha baya zaidi lililovuruga harakati za mabadiliko na litatusumbua baadaye. Lakini sikudhania lingetokea na la Lowassa vile vile. Sasa hivi CCM wala hawana haja ya kupiga kelele tena, wanasubiri vichinjio vyao wafutilie mbali upinzani tarehe 25 liwe onyo na somo kwa wengine!

Umefika golini kabisa na umebaki wewe na kipa mtu anakuonesha kisura halafu unabutua juu; hata wakionesha replay zile unashindwa kuangalia kwani ni aibu.

Nyie wote washabiki wazamani wa chadema mnaona haifai kwa sasa ni bora mkakaa kimya ndio tutawaona mna busara tena heshima yenu itaendelea kutukuka kwa yale mliyoifanyia chadema huko nyuma. Kuliko kushusha tuhuma lukuki tena mkisaidiwa na wale waliokuwa wabaya wenu mlipokuwa chadame, mnatufanya tuamini kama kuna shinikizo mnalopata na linawapelekea kufanya haya mnayo yafanya sasa
 
Hamna kiongozi yoyote yule mashuhuli duniani ambaye huwa hapitii matatizo na ukiona kiongozi yoyote ambaye hajapitia misukosuko ujue huyo hafai kuwa rais kama makufuri hajapitia misukosuko yoyote ile kwanza ile nafasi aliipata kwa zali tu sasa kwa mfano akiwa rais atatuambia nini wakati siku zote matatizo ndio yanamjenga mtu kisiasa kama muheshimiwa lowassa kwa 100% anafaa kuwa rais kwa misukosuko mingi aliyo pitia anamengi ya kutuambia watanzania na amejifunza mengi kwenye maisha yake kwanza anasema anauchukua umaskini inamaana ameisha jua yote yanayo tokea tatizo ni umaskini. Kwanza tu hiyo ni point ya kwanza na kwa kusema hivyo tayari uchaguzi ameshinda.

Rudia kusoma ulichoandika..utatijua una upeo gani wa kufikiria
 
Zamani Slaa alipokuwa anamshambulia Lowasa akiwa CCM alikuwa sawa hajaongwa, lakini sasa hivi kwa kuwa Lowasa yuko CHADEMA Slaa yule yule aliyekuwa akiyasema yale yale anaposema sasa amehongwa na CCM!!! Kisa Lowasa safi baada ya kuhamia CHADEMA!! Ni kweli?

umekula kiapo cha gizani
 
Hata kama Slaa alijenga mageuzi kwa jinsi alivyoongea ni kuua mageuzi. Sasa kuna faida gani kujenga nyumba nzuri kisha ukabomoa?
 
Hivi CCM ni lini mtaanza kumnadi mgombea wenu aliyepoteza mvuto? Au kama mnaona anafaa sana mpeni dk slaa agombee urais ili tupambane nae. Mnasahau kuwa adui ya maendeleo ya mtanzania ni CCM hivyo no matter what lazima tuiondoe ifikapo Oktoba 25. Ndio maana CCM inahaha kila mbinu lazini watanzania tumeamua kwa dhati
 
Dr. kawatibulia wahuni wa siasa sasa wanakataliwa kila kona ya nchi ..mbowe ametuhujumu watz wote
 
Chadema citak hata kuisikia, mmetuangusha wana mageuzi wa kwel
 
Ni kweli hayupo peke ake, yupo na kundi la vijana wahuni wa ccm wanaojifanya ni chadema
lowasaaa...mabadilikoooo
 
jaman watu wanasema wanatka kukitoa shama tawala madarakan hata waletewe rozitamu au shenge wao lao ni kuitoa tuu shishiem
 
Kweli Slaa hayuko Pekee ... Masaburi, Sitta, Mwakyembe... isitoshe anampunga wa kutosha na sasa ameenda kula bata ughaibuni ... so what? Maandamano feki yameumbuliwa ... what next?
 
Baada ya Dr. Slaa kung'atuka siasa za kitapeli za CHADEMA na washirika wake, tumeshuhudia manguli na viwanda vya propaganda wa CHADEMA wakitumia kila mbinu kutuaminisha kuwa kila kitu ni shwari ndani ya Chama hicho na kikundi cha UKAWA. Hoja nyingi zinazokosoa kitendo cha CHADEMA hususani UKAWA kuonyesha taswira ya kununuliwa na mgombea wake wa urais ambaye walipita nchi nzima na kutumia rasilimali nyingi ikiwemo damu na wengine kupata ulemavu kwa kumnadi ni FISADI papa pamoja na wenzake alioambatana nao. Hoja hizi hazijibiwi badala yake viwanda vya propaganda vimekuwa vikifanya CYBER BULLYING kwa yeyote anayehoji ama kukosoa.

Vinara wa uhuni huo wamekuwa wakiongea kwa kusema Dr. Slaa amechelewa na hakuna kinachobadilika na kinachoshangaza zaidi, yule waliyekuwa wanamnadi ni Rais wa mioyo ya Watanzania amepewa majina mapya ya Babu, Mzee, Kizee n.k. Pia wazungumzaji wanaotulazimisha tuwasikilize wao pekee wanajinasibu kuzungumza kwa niaba ya Watanzania wote. Hili ni kosa ambalo si muda mrefu watakuja kujutia na anguko lake si dogo.

Najua, nafahamu, natambua kuwa yeyote asomaye huu uzi anaelewa namaanisha nini lakini kwa kuwa tayari wengi wameshakula kiapo cha giza, wataporomosha matusi, kebehi na kubeza.

CHADEMA mnaodhani mmeshika mpini, tambueni kwamba Dr. Slaa hayupo peke yake. Kuna kundi kubwa la wanamageuzi wa kweli ambao wanamuunga mkono na wanajua cha kufanya ili kuondokana na upuuzi wa viongozi waroho kutaka kutumia njia za mkato kufanikisha malengo yao huku wakisigina misingi iliyofanikisha Chama kukubalika na wengi. Misingi ya kupambana na Ufisadi, ukiukwaji maadili ya uongozi na wizi wa amali za umma.

Dr. Slaa ni kioo, msimamo wake usiyoyumbishwa ni tunu pia ana mapenzi ya dhati kwa Taifa na watu wake.

hata na ww umeandika!! dr wa bei rahisi yule! kwaio kundi ni kubwa lililonunuliwa na ccm!! wengine ni kina nani!! Tujuze!!
 
Back
Top Bottom