CHADEMA mna machaguo mawili tu, kuhakikisha Makonda hapati watu wengi kwenye ziara zake au mmshitaki, la sivyo mtapata tabu sana!

Nsanzagee

JF-Expert Member
Jun 28, 2023
1,939
4,117
Kuwa na mvuto wa watu, hahitaji kuwa na madigere na au PhD ili ukubalike na watu

Ukiniuliza mimi, kwa yale tuliyoyasikia miaka hiyo ya utawala ya JPM hasa kumhusu Makonda, namna vyomba vya habari vilivyokuwa vikimwandama, kumchafua na kubezwa karibu na kila mtu, kwa akili yanfu naliamini kuwa, Makonda atakuwa kachukiwa saana na wananchi na pengine hatakuwa na ushawishi wowote kwenye jamii kwa masuala ya kisiasa

Hakuna jina ambalo hakuwahi kuitwa huyo kijana, alitwa muuwaji, kiongozi wa wasiojulikana na majina yoote mabaya

Kibinafisi niliamini kuwa, huyo jamaa, kwa majina hayo tu, inatosha kuwa kaburi lake na hatoinuka tena na haitawekana kuwa na ushawishi wowote kwa jamii

Tumeona wenye CCM yao, wamempa tena nafasi ambayo ni ya juu zaidi na ambayo inahitaji mtu uwe na ushawishi mkubwa wa kuvuta watu kwenye mikutano hiyo ili kupenyeza ajenda na sera za chama

Kwa ilivyo sasa, mtu huyu, amekuwa na ushawishi mkubwa huku akifuatwa na watu wengi kwenye mikutano yake na ambapo unapoilinganisha na mikutano ya vyama vya upinzani, havifikii kwa ujazo ule

Kwa namna hiyo, mimi najiuliza nakosa majibu, Wapinzani wake hasa Chadema, Wafanye nini ambacho kitakuwa mwarobaini kwa mtu huyu ili asiwe na ushawishi kabisa..!

Karibu kila agenda zinazotupwa kwake kutoka upinzani, ni kama zinamwongezea umarufu zaidi

Ni wakati sasa umefika kwa Chadema, wafanye kila wawezalo ili mikutano ya Paul Makonda isiwe inapata watu kabisa na au wamshitaki mahakamani

Kama hayo mawili hawawezi kuyafanya, basi Chadema inawapasa waanze sasa kampeni zao rasimi na waache kumpa jina kubwa Paul Makonda

Imekuwa kama, kila wakimsema sana huyu Makonda kwa mabaya yake, ndio inakuwa kana kwamba wanamwongezea umaarufu

Mikutano ya Makonda inafurika watu wengi kiasi kwamba, Chadema hawaezi kukusanya watu kiasi hiko kwa sasa!

Chadema acheni kumtangaza makonda, kabilianeni naye kwa hoja, kama huo siyo mwafaka, basi mpelekeni mahakamani ili muondokane na utumwa wa kuraja taja jina lake!

Matusi ruksa!

Ila kumbukeni, Kura yangu siwezi kuwapa masisiemu hata wanitoboe macho!
 
Ccm ni Chama Cha kizamani Sana mda wake ulisha pita.Hakielewi maana demokrasia ya sasa iliyo duniani.
 
Watu wanaolipwa mshahara na Makonda kumtangaza yeye binafsi badala ya Chama , wameongezeka… huyu bwana yuko kujitangaza binafsi na kujitafutia Madaraka ya miaka ijayo tena waziwazi

AJUE tunatizama na hawezi kufanikiwa kuyumbisha Chama na ubinafsi wake , naona hakujifunza
 
Kuwa na mvuto wa watu, hahitaji kuwa na madigere na au PhD ili ukubalike na watu

Ukiniuliza mimi, kwa yale tuliyoyasikia miaka hiyo ya utawala ya JPM hasa kumhusu Makonda, namna vyomba vya habari vilivyokuwa vikimwandama, kumchafua na kubezwa karibu na kila mtu, kwa akili yanfu naliamini kuwa, Makonda atakuwa kachukiwa saana na wananchi na pengine hatakuwa na ushawishi wowote kwenye jamii kwa masuala ya kisiasa

Hakuna jina ambalo hakuwahi kuitwa huyo kijana, alitwa muuwaji, kiongozi wa wasiojulikana na majina yoote mabaya

Kibinafisi niliamini kuwa, huyo jamaa, kwa majina hayo tu, inatosha kuwa kaburi lake na hatoinuka tena na haitawekana kuwa na ushawishi wowote kwa jamii

Tumeona wenye CCM yao, wamempa tena nafasi ambayo ni ya juu zaidi na ambayo inahitaji mtu uwe na ushawishi mkubwa wa kuvuta watu kwenye mikutano hiyo ili kupenyeza ajenda na sera za chama

Kwa ilivyo sasa, mtu huyu, amekuwa na ushawishi mkubwa huku akifuatwa na watu wengi kwenye mikutano yake na ambapo unapoilinganisha na mikutano ya vyama vya upinzani, havifikii kwa ujazo ule

Kwa namna hiyo, mimi najiuliza nakosa majibu, Wapinzani wake hasa Chadema, Wafanye nini ambacho kitakuwa mwarobaini kwa mtu huyu ili asiwe na ushawishi kabisa..!

Karibu kila agenda zinazotupwa kwake kutoka upinzani, ni kama zinamwongezea umarufu zaidi

Ni wakati sasa umefika kwa Chadema, wafanye kila wawezalo ili mikutano ya Paul Makonda isiwe inapata watu kabisa na au wamshitaki mahakamani

Kama hayo mawili hawawezi kuyafanya, basi Chadema inawapasa waanze sasa kampeni zao rasimi na waache kumpa jina kubwa Paul Makonda

Imekuwa kama, kila wakimsema sana huyu Makonda kwa mabaya yake, ndio inakuwa kana kwamba wanamwongezea umaarufu

Mikutano ya Makonda inafurika watu wengi kiasi kwamba, Chadema hawaezi kukusanya watu kiasi hiko kwa sasa!

Chadema acheni kumtangaza makonda, kabilianeni naye kwa hoja, kama huo siyo mwafaka, basi mpelekeni mahakamani ili muondokane na utumwa wa kuraja taja jina lake!

Matusi ruksa!

Ila kumbukeni, Kura yangu siwezi kuwapa masisiemu hata wanitoboe macho!
unawashauri mambo ya msingi kisiasa but watakupuuza na kukuporomoshea mvua ya mitusi balaaa....
 
Back
Top Bottom