CHADEMA kinajinadi kuwa ni chama cha kidemokrasia lakini ukweli ni kwamba ukaribu wao na dhana ya demokrasia uko kwenye jina tu

CalvinKimaro

JF-Expert Member
Sep 11, 2017
215
500
CHADEMA kinajinadi kuwa ni chama cha kidemokrasia lakini ukweli ni kwamba ukaribu wao na dhana ya demokrasia uko kwenye jina tu.

Kiutendaji na kifalsafa ni chama cha kidikteta. Mifano michache:

1. Kina Mkiti ambaye kabadili katiba na kuondoa ukomo wa nafasi ya Mkiti. Hii ni falsafa ya kidikteta perce.
2. Hakina mgawanyo wa madaraka unaoleweka. Ndio maana kwa mfano wenyewe walidai Katibu Mkuu aliyeondoka hawakuwa wanamuamini. Ndio maana wanatuhumiana kuna "inner cabinet". Ndio maana yeyote anayejisikia kuitisha press conference anaitisha na anahutubia kwa niaba ya chama.
Haya mawili yameongelewa sana. Leo nitaishia hapa.

Lakini kuna moja halijaongelewa japo nalo ni kigezo kikubwa cha kukosekana demokrasia ndani ya chadema.
Demokrasia inakataza kulimbikiziana madaraka. Lakini tizama chadema:
Mbunge kwa wakati mmoja anakuwa Mkiti wa Kanda, Mjumbe wa Kamati na Halmashauri Kuu, Katibu Mkuu au Naibu Katibu Mkuu!

Mtu huyohuyo bungeni anakuwa mjumbe au Mkiti wa Kamati ya bunge! Vyeo vyote hivi anarundikiwa mtu mmoja!
Lakini ni chadema haohao wanalalamika kuhusu serikali kurundikia watu vyeo? Itakuwa nyani haoni uso wake?
Hii ndio demokrasia na utawala wa sheria ambao chadema hujifanya machampioni!
Hebu tuitizame CCM!

Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu na wabunge wake wana majukumu yapi? CCM inazo kanda zake lakini zinaongozwa na wasio wabunge. Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu bara na visiwani sio wabunge! Mkiti wa CCM ana muda unaojulikana. Ukiisha anaondoka.

Sasa kati ya CCM na CHADEMA ni chama kipi cha kidikteta?
Kulimbikiziana madaraka kunaiponza chadema kuliko kuinufaisha. Chukulia mifano ya kina Lema na Matiko. Wakiwa na kesi mahakamani au wakiwa jela vyeo vingi ndani ya chadema navyo vinakuwa mahakamani au jela!
CHADEMA ikitaka iaminike kuwa ina demokrasia na utawala wa haki lazima wao wenyewe waondoe haya makandokando. Ama sivyo wabadili jina! Ni sawa ujiite Juma lakini unafuga na kubugia kitimoto!

Lakini pia nadhani inabidi msajili aitizame upya sheria ya vyama. Aangalie jinsi ya kuzuia wanasiasa kurundikiana vyeo, majukumu na madaraka ili kutoa nafasi kwa vijana wengi kushika madaraka, kukuza demokrasia na kuondoa umangi meza kwenye vyama vya siasa.
Naomba kutoa hoja!
NB makala ijayo nitawaangazia wanaojiita wazalendo.
 

Sangatitti

Senior Member
Apr 5, 2020
180
500
Huyo Magufuli atapita kwa kipi alichofanya bhana mbona mnampaisha huyo jamaa si tunatamani asigombee Kama itawezekana sijui anaongozaje mbabe anàtaka kusifiwa tu binadamu gani huyo ni bora tusiwe na rais kuliko alud huyu jamani maisha magum mvua hazinyesh zikinyesha zinazid mara korona sijui ana gundu vitu vya muhimu Bei juu Bora tuongozwe na jeshi tu Kama hamna mtu mwingine kwa kweli.
 

Drone Camera

JF-Expert Member
Jul 25, 2017
10,930
2,000
Hold one for a moment mkuu....Tupo na corona sasa nasikia leo imeufikia mji wetu pendwa😉😉
 
Top Bottom