CHADEMA mna chaguo za kubaki salama

CHADEMA mna chaguo za kubaki salama

Hakuna chama cha upinzani kimejipanga kwenda ikulu. Na hakuna chenye ndoto hiyo pia kwa kipindi hiki.

Ninaposema kipindi hiki, simaanishi kipindi cha magufuli. Hapana, namaanisha kipindi ambacho watanzania bado ni wajinga. Hawajui lolote kuhusu faida za kuchagua viongozi. Watanzania wanauchukulia uchaguzi kama siku kuu zozote zile. Yaani ikishapita imepita. Na wengine wanauchukulia uchaguzi kama ni wakati wa wagombea kutafuta nafasi za ulaji.

Siku watanzania watakapoelewa maana halisi ya uchaguzi na faida za kuwa na viongozi tunaowataka, ndipo utakapokua mwisho wa ccm.

Swali ni je, ujinga utawaisha lini watanzania wakati wanaotakiwa kuwatoa huo ujinga bado wanataka kuwatawala hawa watanzania?
Nakubaliana na wewe kwa asilimia kubwa, lengo la chama chochote ni kushika dola ukiacha vichache sana yenye malengo yao aidha ya kuchafua uchaguzi au kiko planted kukivurugia chama fulani. Ila naweza kusema CUF Zanzibar ilijipanga kushika dola hata Chadema bara ilijipanga ingawa bado inapwaya kwa baadhi ya maeneo.
 
Inawezekana kweli kuna wajinga wengi sana wanaodhani haya ni mapambano kati ya CCM na CHADEMA au kati ya Magufuli na Mbowe. Siku “CHADEMA” itakapotoweka kabisa kwa hizi harakati za mauaji ndipo fahamu zitakapowarejea wengi kuhusu mshindi halisi na “loser” ni nani hasa.

Hata ndani ya CCM yenyewe wenye akili hawachekelei ujinga unaoendelea. Hili hapa ni bandiko la wasiojitambua kabisa.
-ve forces
 
Nitaenda moja kwa moja kwenye msingi wa hoja yangu.

Option ya kwanza: Chadema ya leo inahitaji viongozi watakaokirudisha chama kwenye misingi yake ya zamani, misingi ya ujasiri, misingi ya hoja, misingi ya uanaharakati. Kuirudisha Chadema ya kina Slaa, Chadema ya kina Heche wakisema tukawatoe viongozi mahabusu vijana wanakwenda. Leo viongozi na wanachama wanauawa, wanatekwa, wanapotezwa, sijasikia tamko lolote la nguvu la chama zaidi ya press conference. Utawala huu sio wa press conférence, ni utawala wa kutunishiana misuli ni utawala wa Ukuta.

Option ya pili: Ili kukirudisha chama kwenye mstari, tangazeni maandamano ya amani kama yale ya Ukuta kushinikiza katiba mpya ninaimani taasisi mbalimbali na watanzania wengi watawaunga mkono na chama kitarudi kwenye hadhi yake.

Option ya tatu: Kupitia kamati kuu, chama kiamue kuunga mkono maandamano ya trh 26/4 yaliyoandaliwa na wananchi, kitendo hiki kitakaishitua serikali na kuilazimisha kuwaita kwa lengo la kukaa pamoja ili kuzungumza na kumaliza tofauti zilizopo. Hii option ina risk kubwa lakini ina faida nyingi na za haraka, the more the risk the more the profit.

Option ya Nne: Najua hii itaonekana kuwa ngumu kidogo lakini nyepesi. Hakika uchaguzi ujao utakuwa ngumu kwa Chadema, chama kisipobadili mbinu za ushindi karibu wabunge wote wa Chadema hawatarudi bungeni (fact). Bunge halitakuwa na Msigwa wala Lema wala Mdee wala Mnyika, wala Bulaya. Ili kujiweka salama aidha Chama au wabunge wote waamue kumuunga mkono Magufuli kama wenzenu wanavyofanya au wabunge wakae kimya kusubiri mafao yao yawasaidie kuanza maisha mpya ya uraiani baada ya uchaguzi wa 2020.

Ili kubaki salama lazima chama kiamue kuchagua option mojawapo vinginevyo kitaendelea kupukutika na pengine kubaki jina kama vyama vingine.
Katibu mkuu awe Jacob Steven meya wa ubungo huyu anajua mbinu zote chafu za ccm
 
Mbowe is a coward na Shakespear alisema nanukuu "Cowards die many time before their actual death".
 
Hapa nimekuelewa mbowe ni kama hayupo serious i wish mtu kama john heche ndo angekua katibu mkuu na lema awe mwenyekiti lisu awe mgombea urais na mnadhimu.mbowe abaki mtu wa mipango ila wasiruhusu maamuzi ya kilokolelokole.magufuli sio wa kumchekea hata kidogo na tukikaa vibaya tutajikuta tuko north krea.upinzani gani unanyamaza kwakutishiwa?
 
Hakuna option ninayoiunga mkono hata moja hapo! Waendelee kujijenga taratibu japo wanapigwa vibaya mpaka Siku watanzania watakapochoshwa vilivyo na watawala. Haiwezekani wakajiteeesa hku watz wengine wakijilalia makwao kusubiri mafanikio ya wakipiganiacho. Tazama Kenya serikali inajua wananchi sio waoga lkn hapa tunatishwa kama watoto na tunanywea nywiiii. Wapinzani msibebe saaana mzigo nendeni mdogomdogo wananchi nao waamke. Kina mbowe wako jela watu hawapazi sauti unadhani wamejitakia bhana
 
Mkuu naona point yako ina mantiki fulani ngoja niwashirikishe wadau.
 
Mkuu Quinine, kwanza naiunga mkono hoja hii, this is the best option, kwa sababu siku zote, haki haombwi, wala hailetwi kwenye kisahani cha chai, haki inadaiwa!, Chadema watangaze maandamano ya kifo, wamthibitishie rais Magufuli na polisi wake wote na jeshi lake lote kuwa siku hiyo, wataingia mitaani kuandamani na wote wako tayari kufa, ni heri kufa ukipigania haki, kuliko mtumwa anayelishwa makombo. Kama ni kweli polisi wetu na jeshi letu limegeuka gestapo na kutumia risasi za moto kama Soweto ile tarehe 16/6/1976, au Tiananmen Squire kule Uchina, then damu hiyo ndio itapanda mbegu ya ukombozi na amini usiamini, Karma itawashughulikia wauaji hao mmoja mmoja na hakuna hata mmoja wao ataondoka kwa amani, Malipo ni hapa hapa duniani.
Tatizo la uamuzi huu, hauwezi kufanyika Chini ya Kamanda MBOWE, ili hili lifanyike, MBOWE akubali tuu kupisha, akabidhi chama kwa vichaa kama Lissu na Lema kwa lengo tuu la kusimamia Mapambano.
"The Power of 'Karma'- Ndio Hukumu Pekee ya Haki Kamili Hapa Duniani!, Unahukumiwa kwa Matendo Yako!

Hiki ndicho kitu kinachokwenda kutokea 2020, Chadema inakwenda kupoteza majimbo yote hadi MBOWE mwenyewe hatorudi, hivyo mbunge au diwani yoyote wa Chadema, anayetaka kurudi Bungeni au kitini, ni ama aamue kupumzika siasa, ama ajiunge CCM!.

Hili nimelisema vizuri hapa.
Trend Reading: Wanaohamia CCM wasibezwe! Wanaona mbali, 2020 Majimbo yote kurejeshwa. Je tunarejea nchi ya Chama kimoja?
P.
Mbowe mnamsingizia tu, kumbuja mbowe kama.single human entity hawezi kukabiliana na Jeshi zima la policcm waka JWTccm.

Watanzania wenyewe hawako tayari kwa mabadiliko, mbowe hawezi kurisk maisha yake kwa watu wasiijitambua hiyo ni hasara.
 
Hakuna option ninayoiunga mkono hata moja hapo! Waendelee kujijenga taratibu japo wanapigwa vibaya mpaka Siku watanzania watakapochoshwa vilivyo na watawala. Haiwezekani wakajiteeesa hku watz wengine wakijilalia makwao kusubiri mafanikio ya wakipiganiacho. Tazama Kenya serikali inajua wananchi sio waoga lkn hapa tunatishwa kama watoto na tunanywea nywiiii. Wapinzani msibebe saaana mzigo nendeni mdogomdogo wananchi nao waamke. Kina mbowe wako jela watu hawapazi sauti unadhani wamejitakia bhana
Mnyika, Mbowe, Peter, Salum, Heche, Lema, mdee hawawezi kuleta mabadiliko wao peke yao. Tena ningeshauri hata akina Mbowe wajikalie kimya tu. Ili huyu mhutu wa rwanda aendelee kukandamiza zaidi ili hawa maskini wa tz wasio na akili waisome sawasawa.
 
Sawa, lkn tuende mbele turudi nyuma akina Nyerere wangeamua kukaa kimya uhuru ungepatikana mapema?
 
Nikimuangalia JJ kwenye politics, huyu ni mjamaa halisi wa Nyerere type, politics ndio full job yake kama Dr. Slaa, hii survive na heathy ya Chadema inayoonekana sasa, inatokana na ruzuku, Chadema bila wabunge, hakuna kitu, sasa kwa watu wanaotegemea politics as full time job, have no choice but to cross, hata Lema Arusha atapoteza, lakini kwa Lema, kuliko ku cross, ataamua bora afe kizungu na tai shingoni, ila he will be he has made enough kufanya biashara, vinginevyo atarudia kazi yake ile, ila this time kwa kuwatuma vijana!. JJ is too young to sink with Chadema na hayuko peke yake.

P.

ahahahahahh, Ila Paskali wewe!!! hapa ni wachache sana watakao kuelewa (Red). hahahahhah
 
Sawa, lkn tuende mbele turudi nyuma akina Nyerere wangeamua kukaa kimya uhuru ungepatikana mapema?
Wewe binafsi unauelewa na kuuhitaji huu ukombozi unaopiganiwa na CHADEMA?

Mada yako imelenga kuangalia mustakabali wa CHADEMA tu lakini umesahau lengo kubwa zaidi. Suala la msingi hapa ni kuangalia kama hicho wanachopigania CHADEMA kina umuhimu kwa Watanzania? Kama kina umuhimu, CHADEMA ikishindwa na kufa, wananchi wafanye nini? Manake hii si mechi ya mpira kati ya Simba na Yanga. Huu ni mustakabali wa Tanzania na Watanzania wote. Kutegemea kwamba Mbowe, Mnyika, Mdee, Mashinji, Mwalimu, Bulaya, Lissu, Heche, Sugu, Msigwa, Kubenea, n.k. na jukwaa lao la CHADEMA ndio washikilie mustakabali huo, itakuwa ni ujinga uliopitiliza kwetu sote.

Hatuwezi kukaa kujadili kufa kwa chama cha siasa au kwa wanasiasa kama vile hilo ni shauri lao binafsi; eti sie ni mashuhuda na mashabiki tu wa "mpambano" huo! Au ndio tunasubiri CHADEMA na wapinzani wote wafe tubaki na chama kimoja ndipo tuzinduke kuwa washindi and washindwa (losers) ni akina nani hasa? Tutakuwa nchi ya ajabu sana.

Heri waliokwishatoa kauli zao hadharani kuonyesha uozo unaoendelea kuliko wanaoushabikia. Na ninavyowafamu Watanzania wenzangu wengi siku karata zikigeuka, sitashangaa kutokea mashabiki wa leo wa mfumo wakiwahi microphone za media kujidai bila aibu jinsi walivyokuwa "wakikerwa na yanayoendelea na walivyokuwa wakipambana ndani kwa ndani ya mfumo ili kuliokoa taifa"! Si ajabu hata kusikia wengine wakijinasibu kuvujisha siri kwa Mange na Ngurumo! Interesting fellas!
 
Nitaenda moja kwa moja kwenye msingi wa hoja yangu.

Option ya kwanza: Chadema ya leo inahitaji viongozi watakaokirudisha chama kwenye misingi yake ya zamani, misingi ya ujasiri, misingi ya hoja, misingi ya uanaharakati. Kuirudisha Chadema ya kina Slaa, Chadema ya kina Heche wakisema tukawatoe viongozi mahabusu vijana wanakwenda. Leo viongozi na wanachama wanauawa, wanatekwa, wanapotezwa, sijasikia tamko lolote la nguvu la chama zaidi ya press conference. Utawala huu sio wa press conférence, ni utawala wa kutunishiana misuli ni utawala wa Ukuta.

Option ya pili: Ili kukirudisha chama kwenye mstari, anzisheni harakati za kudai katiba mpya na tume huru ya uchaguzi, ikiwezekana tangazeni maandamano ya amani kama yale ya Ukuta kushinikiza katiba mpya ninaimani taasisi mbalimbali na watanzania wengi watawaunga mkono na chama kitarudi kwenye hadhi yake.

Option ya tatu: Kupitia kamati kuu, chama kiamue kuunga mkono maandamano ya trh 26/4 yaliyoandaliwa na wananchi, kitendo hiki kitaishitua serikali na kuilazimika kuwaita kwa lengo la kukaa pamoja ili kuzungumza na kumaliza tofauti zilizopo. Hii option ina risk kubwa lakini ina faida nyingi na za haraka, the more the risk the more the profit.

Option ya Nne: Najua hii itaonekana kuwa ngumu kidogo lakini nyepesi. Hakika uchaguzi ujao utakuwa ngumu kwa Chadema, chama kisipobadili mbinu za ushindi karibu wabunge wote wa Chadema hawatarudi bungeni (fact). Bunge halitakuwa na Msigwa wala Lema wala Mdee wala Mnyika, wala Bulaya. Ili kujiweka salama aidha Chama au wabunge wote waamue kumuunga mkono Magufuli kama wenzenu wanavyofanya au wabunge wakae kimya kusubiri mafao yao yawasaidie kuanza maisha mpya ya uraiani baada ya uchaguzi wa 2020.

Ili kubaki salama lazima chama kiamue kuchagua option mojawapo vinginevyo kitaendelea kupukutika na pengine kubaki jina kama vyama vingine.
==========≠=========
Huu hapa chini ni mchango wa mwanaJF mwenzetu, binafsi nimeona kuna kitu cha kujifunza. Kwanini kina Mbowe wateseke kwa Watanzania waliolala wasioonyesha hata kuguswa na juhudi zao?
CHADEMA kinachowatokea ni matunda ya kuminya haki ndani ya chama chao; wakati wa mchakato wa uchaguzi badala ya kufanya teuzi za wagombea wa wanachama wao waliojitoa kwa hali na mali kukijenga chama wao macho na masikio yao huelekeza kwa CCM kuangalia nani anaachwa wamchukue na kumsimamisha.

Hata madiwani na Mbunge aliyerudi CCM naamini ni wale wale tuu waliochukuliwa dakika la lalal salama na kusimamishwa kugombea; mbona madiwani wa ACT hawahami?
 
Nikimuangalia JJ kwenye politics, huyu ni mjamaa halisi wa Nyerere type, politics ndio full job yake kama Dr. Slaa, hii survive na heathy ya Chadema inayoonekana sasa, inatokana na ruzuku, Chadema bila wabunge, hakuna kitu, sasa kwa watu wanaotegemea politics as full time job, have no choice but to cross, hata Lema Arusha atapoteza, lakini kwa Lema, kuliko ku cross, ataamua bora afe kizungu na tai shingoni, ila he will be he has made enough kufanya biashara, vinginevyo atarudia kazi yake ile, ila this time kwa kuwatuma vijana!. JJ is too young to sink with Chadema na hayuko peke yake.

P.
Kwahiyo unatarajia kuna siku jj ata cross.
 
Inawezekana kweli kuna wajinga wengi sana wanaodhani haya ni mapambano kati ya CCM na CHADEMA au kati ya Magufuli na Mbowe. Siku “CHADEMA” itakapotoweka kabisa kwa hizi harakati za mauaji ndipo fahamu zitakapowarejea wengi kuhusu mshindi halisi na “loser” ni nani hasa.

Hata ndani ya CCM yenyewe wenye akili hawachekelei ujinga unaoendelea. Hili hapa ni bandiko la wasiojitambua kabisa.
CCM ipo tangu zamani na Chadema ipo tangu 1992, kwa mawazo yako unadhani kwanini siasa za mauaji zimeshamiri siku za hivi karibuni.
 
Slaa hatokuja kuitwa shujaa, shujaa hakimbii vita anafia vitani historia imeshaandikwa tayari.
Mkuu, kuna kitu kinaitwa falsafa ya vita ambayo inaongozwa na two schools of thoughts, falsafa ya kwanza ni falsafa ya ushujaa, inayowatumia wapiganaji mashujaa, hawa motoo yao ni "fight, fight, fight", inaamini katika kupambana tuu, Mapambano!, yaani pigana, pigana, pigana, na hata kama unapigwa, "no retreat no surrender", endelea tuu kupigana mpaka mwisho, mpaka risasi ya mwisho na tone la mwisho la damu limwagike, hata mkifa wote na kuwa wiped out, mtakumbukwa kama mashujaa mlioipigania na kuifia nchi yenu, ila mmeshindwa vita na sasa wote ni mateka, wake zenu wanabakwa, na Watoto wenu wanafanywa watumwa!.

Falsafa ya pili ni falsafa ya umakini, inayowatumia wapiganaji makini, hawa hawapeleki jeshi vitani hadi kwanza waijue nguvu ya adui, kwa Imani kuwa "never fight a loosing battle", usipigane vita ambayo unajua hutashinda. Na ukiwa vitani, ukiona dalili za kushindwa vita, ama una surrender ili msiuawawe wote, au una retreat kwa kurudisha nyuma majeshi yako, kwenda kujipanga upya.

Kundi hili la wapiganaji makini, baada ya kujaribu kupigana na kushindana na kushindwa mara kadhaa kwa sababu adui yuko vizuri Zaidi yao, huamua kutumia kanuni inayoitwa, "If you can't beat them, join them". kama huwezi kuwashinda, jiunge nao, jifunze siri zao, jijenge upya na pigana nao kutokea ndani kwao!, yaani " fight from within". Hiki ndicho wanachokifanya baadhi ya wana CCM ambao wanajiunga CCM akiwemo Dr. Slaa. Hili nimelizungumzia hapa.
Tuko Vitani Tuna Wapiganaji Shupavu, Wapiganaji Makini na Watazamaji, Je! Wewe Uko Kundi Gani ?
Katika mazingira ya Tanzania, kati ya Dr. Slaa na MBOWE, ni nani shujaa wa kweli?. Kwa sisi tuliomsikiliza Dr. Slaa akizungumza kutoka moyoni mwake, huwezi amini amejiunga CCM kwa sababu anaipenda au anamuamini Magufuli, bali amejiunga CCM because he has to, its the only way!.
If you can't beat them, join them! He is the worst dictator. Let's pray for him!

P.
 
Dawa ni kuamua moja tu hata kama ni kufa bora kuliko huu unyanyasaji.
 
Ili kujiweka salama aidha Chama au wabunge waamue kumuunga mkono Magufuli kama wengine wanavyofanya au wabunge wakae kimya kusubiri mafao yao yawasaidie kuanza maisha mapya ya uraiani baada ya uchaguzi wa 2020.

Ili kubaki salama lazima chama kiamue kuchagua option mojawapo vinginevyo kitaendelea kupukutika na pengine kubaki jina kama vyama vingine.
==========≠=========​

Nadhani wazo hili ni nzuri. Warudi kwa wanachama wakawaombe ridhaa ya kufanya hivyo. Siku CCM wakiwa tayari kwa shughuli za vyama vingi wawaarifu.
 
Back
Top Bottom