CHADEMA mna chaguo za kubaki salama

CHADEMA mna chaguo za kubaki salama

Quinine

Platinum Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
25,169
Reaction score
60,528
Nitaenda moja kwa moja kwenye msingi wa hoja yangu.

Option ya kwanza: CHADEMA ya leo inahitaji viongozi watakaokirudisha chama kwenye misingi yake ya zamani, misingi ya ujasiri, misingi ya hoja, misingi ya uanaharakati. Kuirudisha CHADEMA ya kina Slaa, CHADEMAya kina Heche wakisema tukawatoe viongozi mahabusu vijana wanakwenda.

Leo viongozi na wanachama wanauawa, wanatekwa, wanapotezwa, sijasikia tamko lolote la nguvu la chama zaidi ya press conference. Utawala huu sio wa press conférence, ni utawala wa kutunishiana misuli ni utawala wa UKUTA.

Option ya pili: Ili kukirudisha chama kwenye mstari, anzisheni harakati za kudai katiba mpya na tume huru ya uchaguzi, ikiwezekana tangazeni maandamano ya amani kama yale ya UKUTA kushinikiza katiba mpya ninaimani taasisi mbalimbali na watanzania wengi watawaunga mkono na chama kitarudi kwenye hadhi yake.

Option ya Tatu: Najua hii itaonekana kuwa ngumu kidogo lakini nyepesi. Hakika uchaguzi ujao utakuwa mgumu sana kwa CHADEMA, chama kisipobadili mbinu za ushindi karibu wabunge wote wa CHADEMA hawatarudi bungeni (fact).

Bunge halitakuwa na Msigwa wala Lema wala Mdee wala Mnyika, wala Bulaya. Ili kujiweka salama aidha Chama au wabunge waamue kumuunga mkono Rais Magufuli kama wengine wanavyofanya au wabunge wakae kimya kusubiri mafao yao yawasaidie kuanza maisha mapya ya uraiani baada ya uchaguzi wa 2020.

Ili kubaki salama lazima chama kiamue kuchagua option mojawapo vinginevyo kitaendelea kupukutika na pengine kubaki jina kama vyama vingine.

================
Huu hapa chini ni mchango wa mwanaJF mwenzetu, binafsi nimeona kuna kitu cha kujifunza. Kwanini kina Mbowe wateseke kwa Watanzania waliolala wasioonyesha hata kuguswa na juhudi zao?
Hakuna option ninayoiunga mkono hata moja hapo! Waendelee kujijenga taratibu japo wanapigwa vibaya mpaka Siku watanzania watakapochoshwa vilivyo na watawala. Haiwezekani wakajiteeesa hku watz wengine wakijilalia makwao kusubiri mafanikio ya wakipiganiacho. Tazama Kenya serikali inajua wananchi sio waoga lkn hapa tunatishwa kama watoto na tunanywea nywiiii. Wapinzani msibebe saaana mzigo nendeni mdogomdogo wananchi nao waamke. Kina mbowe wako jela watu hawapazi sauti unadhani wamejitakia bhana
 
Option ya tatu: Kupita kamati kuu, chama kiamue kuunga mkono maandamano ya trh 26/4 yaliyoandaliwa na wananchi, kitendo hiki kitakaishitua serikali na kuilazimisha kuwaita kwa lengo la kukaa pamoja ili kuzungumza na kumaliza tofauti zilizopo. Hii option ina risk kubwa lakini ina faida nyingi na za haraka, the more the risk the more the profit.
Mkuu Quinine, kwanza naiunga mkono hoja hii, this is the best option, kwa sababu siku zote, haki haombwi, wala hailetwi kwenye kisahani cha chai, haki inadaiwa!, Chadema watangaze maandamano ya kifo, wamthibitishie rais Magufuli na polisi wake wote na jeshi lake lote kuwa siku hiyo, wataingia mitaani kuandamani na wote wako tayari kufa, ni heri kufa ukipigania haki, kuliko mtumwa anayelishwa makombo. Kama ni kweli polisi wetu na jeshi letu limegeuka gestapo na kutumia risasi za moto kama Soweto ile tarehe 16/6/1976, au Tiananmen Squire kule Uchina, then damu hiyo ndio itapanda mbegu ya ukombozi na amini usiamini, Karma itawashughulikia wauaji hao mmoja mmoja na hakuna hata mmoja wao ataondoka kwa amani, Malipo ni hapa hapa duniani.
Tatizo la uamuzi huu, hauwezi kufanyika Chini ya Kamanda MBOWE, ili hili lifanyike, MBOWE akubali tuu kupisha, akabidhi chama kwa vichaa kama Lissu na Lema kwa lengo tuu la kusimamia Mapambano.
"The Power of 'Karma'- Ndio Hukumu Pekee ya Haki Kamili Hapa Duniani!, Unahukumiwa kwa Matendo Yako!
Option ya Nne: Najua hii itaonekana kuwa ngumu kidogo lakini nyepesi. Hakika uchaguzi ujao utakuwa ngumu kwa Chadema, chama kisipobadili mbinu za ushindi karibu wabunge wote wa Chadema hawatarudi bungeni (fact). Bunge halitakuwa na Msigwa wala Lema wala Mdee wala Mnyika, wala Bulaya. Ili kujiweka salama aidha Chama au wabunge wote waamue kumuunga mkono Magufuli kama wenzenu wanavyofanya au wabunge wakae kimya kusubiri mafao yao yawasaidie kuanza maisha mpya ya uraiani baada ya uchaguzi wa 2020.
Ni ukweli mchungu.
Hiki ndicho kitu kinachokwenda kutokea 2020, Chadema inakwenda kupoteza majimbo yote hadi MBOWE mwenyewe hatorudi, hivyo mbunge au diwani yoyote wa Chadema, anayetaka kurudi Bungeni au kitini, ni ama aamue kupumzika siasa, ama ajiunge CCM!.

Hili nimelisema vizuri hapa.
Trend Reading: Wanaohamia CCM wasibezwe! Wanaona mbali, 2020 Majimbo yote kurejeshwa. Je tunarejea nchi ya Chama kimoja?
P.
 
Hiki ndicho kitu kinachokwenda kutokea 2020, Chadema inakwenda kupoteza majimbo yote hadi MBOWE mwenyewe hatorudi, hivyo mbunge au diwani yoyote wa Chadema, anayetaka kurudi Bungeni au kitini, ni ama aamue kupumzika siasa, ama ajiunge CCM!.
Naisubiri 2020
 
Wewe watu tumechoka bhnaaa
Binafsi nimekubali hata kufaa lakini kutetea haki yangu na yawatanzania wenzangu!
Cjigamb kisa nipo nyuma ya keybod but nauchungu sanaaa na nchi laxima nifanye KITU
 
Acha kupotosha watu, kuhamia ccm ni kuona mbali! Ukiona mcha Mungu anahamia kwa shetani jua ameangamia, kati ya vitu navojivunia hapa duniani ni kutokua ccm.
When faced in between the two devils, choose the lesser!, kwenye siasa zetu kuna kambi kuu mbili tuu, the wishful thinkers and the realists, the wishful thinkers kazi yao ni just to wish, just like gambling kwenye probability, the realist wako certain,
Magufuli is a game changer, amechange game lote la siasa za Tanzania, tunaelekea kuwa nchi ya chama kimoja, hakuna either or, japo CCM ni li zimwi, lakini ndilo zimwi likujualo!, 2020 ni CCM tuu!. Hivi uliamini kuwa kuna siku Dr. Slaa angerudi CCM, 2020 utashangaa, hata usiowategemea kabisa, watahamia CCM.

P.
 
Hakuna chama cha upinzani kimejipanga kwenda ikulu. Na hakuna chenye ndoto hiyo pia kwa kipindi hiki.

Ninaposema kipindi hiki, simaanishi kipindi cha magufuli. Hapana, namaanisha kipindi ambacho watanzania bado ni wajinga. Hawajui lolote kuhusu faida za kuchagua viongozi. Watanzania wanauchukulia uchaguzi kama siku kuu zozote zile. Yaani ikishapita imepita. Na wengine wanauchukulia uchaguzi kama ni wakati wa wagombea kutafuta nafasi za ulaji.

Siku watanzania watakapoelewa maana halisi ya uchaguzi na faida za kuwa na viongozi tunaowataka, ndipo utakapokua mwisho wa ccm.

Swali ni je, ujinga utawaisha lini watanzania wakati wanaotakiwa kuwatoa huo ujinga bado wanataka kuwatawala hawa watanzania?
 
Nitaenda moja kwa moja kwenye msingi wa hoja yangu.

Option ya kwanza: Chadema ya leo inahitaji viongozi watakaokirudisha chama kwenye misingi yake ya zamani, misingi ya ujasiri, misingi ya hoja, misingi ya uanaharakati. Kuirudisha Chadema ya kina Slaa, Chadema ya kina Heche wakisema tukawatoe viongozi mahabusu vijana wanakwenda. Leo viongozi na wanachama wanauawa, wanatekwa, wanapotezwa, sijasikia tamko lolote la nguvu la chama zaidi ya press conference. Utawala huu sio wa press conférence, ni utawala wa kutunishiana misuli ni utawala wa Ukuta.

Option ya pili: Ili kukirudisha chama kwenye mstari, tangazeni maandamano ya amani kama yale ya Ukuta kushinikiza katiba mpya ninaimani taasisi mbalimbali na watanzania wengi watawaunga mkono na chama kitarudi kwenye hadhi yake.

Option ya tatu: Kupitia kamati kuu, chama kiamue kuunga mkono maandamano ya trh 26/4 yaliyoandaliwa na wananchi, kitendo hiki kitakaishitua serikali na kuilazimisha kuwaita kwa lengo la kukaa pamoja ili kuzungumza na kumaliza tofauti zilizopo. Hii option ina risk kubwa lakini ina faida nyingi na za haraka, the more the risk the more the profit.

Option ya Nne: Najua hii itaonekana kuwa ngumu kidogo lakini nyepesi. Hakika uchaguzi ujao utakuwa ngumu kwa Chadema, chama kisipobadili mbinu za ushindi karibu wabunge wote wa Chadema hawatarudi bungeni (fact). Bunge halitakuwa na Msigwa wala Lema wala Mdee wala Mnyika, wala Bulaya. Ili kujiweka salama aidha Chama au wabunge wote waamue kumuunga mkono Magufuli kama wenzenu wanavyofanya au wabunge wakae kimya kusubiri mafao yao yawasaidie kuanza maisha mpya ya uraiani baada ya uchaguzi wa 2020.

Ili kubaki salama lazima chama kiamue kuchagua option mojawapo vinginevyo kitaendelea kupukutika na pengine kubaki jina kama vyama vingine.
Katika Ranki



1. Option ya Kwanza ya kutunishiana Misuli sio Ngeni. Hii ndio iliowaletea maswahibu ya kifo cha Akwilina. Hivyo si kweli kua haijawahi kufanyika. Ufanisi wake unaweza kufunikwa na vielementi vya uhalifu.

2. Option ya Pili ya kuandaa Maandamano ya Amani. Hii haitafanikiwa kama ambavyo UKUTA ulivyo feli. Dola hawatatoa kibali cha aina yoyote ya Siasa za kiuanaharakati.
.

3. Hii options ya 3 ya kuunga mkono maandamano ya tarehe 26 aprili, ni nzuri na applicable zaidi.

Prons:-
√Uzuri wake ni kwakua taasisi nyingine zisizoza kichama na za kidini zinaonesha kuibariki.

√Hailengi kuing'oa CCM madarakani. Hivyo inaweza kuwashawishi wana CCM WASIORIDHIKA KUIUNGA MKONO KWA 100%.

√Timing yake ni nzuri, ukichukulia inakwenda sambamba na Nyaraka za viongozi wa dini.

√So haitakua kazi kwao kuwaandaa wafuasi kisaikolojia na kimwili.

Cons:-
√Ina risky nyingi kama kuwepo kwa Visasi na Mauaji, Utekaji na Upotevu wa watu muhimu ndani ya Chama Na nje ya Chama, kama njia ya kudhibiti isifanikiwe.

√Pia Ajenda ya maandamano ya 26 Aprili yana tafsiriwa kua ni uhaini. Hivyo itawalazimu kama chama kubadili ajenda ili wasiingie Matatizoni zaidi.

√Viongozi wote muhimu wa CDM mpaka sasa wako Mahabusu, hivyo kuyaandaa inaweza kua changamoto.


4. Hii ndio best of all. Wakae kimya kisha wasubiri Mafao yao ya kustahafu Siasa. Lets nature takes it toll.
 
Back
Top Bottom