Mkuu Quinine, kwanza naiunga mkono hoja hii, this is the best option, kwa sababu siku zote, haki haombwi, wala hailetwi kwenye kisahani cha chai, haki inadaiwa!, Chadema watangaze maandamano ya kifo, wamthibitishie rais Magufuli na polisi wake wote na jeshi lake lote kuwa siku hiyo, wataingia mitaani kuandamani na wote wako tayari kufa, ni heri kufa ukipigania haki, kuliko mtumwa anayelishwa makombo. Kama ni kweli polisi wetu na jeshi letu limegeuka gestapo na kutumia risasi za moto kama Soweto ile tarehe 16/6/1976, au Tiananmen Squire kule Uchina, then damu hiyo ndio itapanda mbegu ya ukombozi na amini usiamini, Karma itawashughulikia wauaji hao mmoja mmoja na hakuna hata mmoja wao ataondoka kwa amani, Malipo ni hapa hapa duniani.
Tatizo la uamuzi huu, hauwezi kufanyika Chini ya Kamanda MBOWE, ili hili lifanyike, MBOWE akubali tuu kupisha, akabidhi chama kwa vichaa kama Lissu na Lema kwa lengo tuu la kusimamia Mapambano.
"The Power of 'Karma'- Ndio Hukumu Pekee ya Haki Kamili Hapa Duniani!, Unahukumiwa kwa Matendo Yako!
Hiki ndicho kitu kinachokwenda kutokea 2020, Chadema inakwenda kupoteza majimbo yote hadi MBOWE mwenyewe hatorudi, hivyo mbunge au diwani yoyote wa Chadema, anayetaka kurudi Bungeni au kitini, ni ama aamue kupumzika siasa, ama ajiunge CCM!.
Hili nimelisema vizuri hapa.
Trend Reading: Wanaohamia CCM wasibezwe! Wanaona mbali, 2020 Majimbo yote kurejeshwa. Je tunarejea nchi ya Chama kimoja?
P.