CHADEMA mna chaguo za kubaki salama

CHADEMA mna chaguo za kubaki salama

Wewe binafsi unauelewa na kuuhitaji huu ukombozi unaopiganiwa na CHADEMA?

Mada yako imelenga kuangalia mustakabali wa CHADEMA tu lakini umesahau lengo kubwa zaidi. Suala la msingi hapa ni kuangalia kama hicho wanachopigania CHADEMA kina umuhimu kwa Watanzania? Kama kina umuhimu, CHADEMA ikishindwa na kufa, wananchi wafanye nini? Manake hii si mechi ya mpira kati ya Simba na Yanga. Huu ni mustakabali wa Tanzania na Watanzania wote. Kutegemea kwamba Mbowe, Mnyika, Mdee, Mashinji, Mwalimu, Bulaya, Lissu, Heche, Sugu, Msigwa, Kubenea, n.k. na jukwaa lao la CHADEMA ndio washikilie mustakabali huo, itakuwa ni ujinga uliopitiliza kwetu sote.

Hatuwezi kukaa kujadili kufa kwa chama cha siasa au kwa wanasiasa kama vile hilo ni shauri lao binafsi; eti sie ni mashuhuda na mashabiki tu wa "mpambano" huo! Au ndio tunasubiri CHADEMA na wapinzani wote wafe tubaki na chama kimoja ndipo tuzinduke kuwa washindi and washindwa (losers) ni akina nani hasa? Tutakuwa nchi ya ajabu sana.

Heri waliokwishatoa kauli zao hadharani kuonyesha uozo unaoendelea kuliko wanaoushabikia. Na ninavyowafamu Watanzania wenzangu wengi siku karata zikigeuka, sitashangaa kutokea mashabiki wa leo wa mfumo wakiwahi microphone za media kujidai bila aibu jinsi walivyokuwa "wakikerwa na yanayoendelea na walivyokuwa wakipambana ndani kwa ndani ya mfumo ili kuliokoa taifa"! Si ajabu hata kusikia wengine wakijinasibu kuvujisha siri kwa Mange na Ngurumo! Interesting fellas!
Mkuu, heading yangu inazungumzia Chadema sio kwamba matatizo mengine ya kitaifa siyajui, karibu tuzungumuzie options.
 
Hakuna chama cha upinzani kimejipanga kwenda ikulu. Na hakuna chenye ndoto hiyo pia kwa kipindi hiki.

Ninaposema kipindi hiki, simaanishi kipindi cha magufuli. Hapana, namaanisha kipindi ambacho watanzania bado ni wajinga. Hawajui lolote kuhusu faida za kuchagua viongozi. Watanzania wanauchukulia uchaguzi kama siku kuu zozote zile. Yaani ikishapita imepita. Na wengine wanauchukulia uchaguzi kama ni wakati wa wagombea kutafuta nafasi za ulaji.

Siku watanzania watakapoelewa maana halisi ya uchaguzi na faida za kuwa na viongozi tunaowataka, ndipo utakapokua mwisho wa ccm.

Swali ni je, ujinga utawaisha lini watanzania wakati wanaotakiwa kuwatoa huo ujinga bado wanataka kuwatawala hawa watanzania?
fact
 
Mbowe ameendesha siasa za kistaarabu kupita ustaarabu wenyewe, hayo ndo matokeo yake akitoka ajue kumbe jela atakwenda hata asipoita maandamano ya aman
naaam kama asipo badilika niwazi anakiingiza chama kwnye tanuri la moto
 
Hakuna option ninayoiunga mkono hata moja hapo! Waendelee kujijenga taratibu japo wanapigwa vibaya mpaka Siku watanzania watakapochoshwa vilivyo na watawala. Haiwezekani wakajiteeesa hku watz wengine wakijilalia makwao kusubiri mafanikio ya wakipiganiacho. Tazama Kenya serikali inajua wananchi sio waoga lkn hapa tunatishwa kama watoto na tunanywea nywiiii. Wapinzani msibebe saaana mzigo nendeni mdogomdogo wananchi nao waamke. Kina mbowe wako jela watu hawapazi sauti unadhani wamejitakia bhana
Nadhani uko sahihi,inaonekana jamii haijawa tayari kuunga mkono kile wanachopigania.
 
Mkuu, kuna kitu kinaitwa falsafa ya vita ambayo inaongozwa na two schools of thoughts, falsafa ya kwanza ni falsafa ya ushujaa, inayowatumia wapiganaji mashujaa, hawa motoo yao ni "fight, fight, fight", inaamini katika kupambana tuu, Mapambano!, yaani pigana, pigana, pigana, na hata kama unapigwa, "no retreat no surrender", endelea tuu kupigana mpaka mwisho, mpaka risasi ya mwisho na tone la mwisho la damu limwagike, hata mkifa wote na kuwa wiped out, mtakumbukwa kama mashujaa mlioipigania na kuifia nchi yenu, ila mmeshindwa vita na sasa wote ni mateka, wake zenu wanabakwa, na Watoto wenu wanafanywa watumwa!.

Falsafa ya pili ni falsafa ya umakini, inayowatumia wapiganaji makini, hawa hawapeleki jeshi vitani hadi kwanza waijue nguvu ya adui, kwa Imani kuwa "never fight a loosing battle", usipigane vita ambayo unajua hutashinda. Na ukiwa vitani, ukiona dalili za kushindwa vita, ama una surrender ili msiuawawe wote, au una retreat kwa kurudisha nyuma majeshi yako, kwenda kujipanga upya.

Kundi hili la wapiganaji makini, baada ya kujaribu kupigana na kushindana na kushindwa mara kadhaa kwa sababu adui yuko vizuri Zaidi yao, huamua kutumia kanuni inayoitwa, "If you can't beat them, join them". kama huwezi kuwashinda, jiunge nao, jifunze siri zao, jijenge upya na pigana nao kutokea ndani kwao!, yaani " fight from within". Hiki ndicho wanachokifanya baadhi ya wana CCM ambao wanajiunga CCM akiwemo Dr. Slaa. Hili nimelizungumzia hapa.
Tuko Vitani Tuna Wapiganaji Shupavu, Wapiganaji Makini na Watazamaji, Je! Wewe Uko Kundi Gani ?
Katika mazingira ya Tanzania, kati ya Dr. Slaa na MBOWE, ni nani shujaa wa kweli?. Kwa sisi tuliomsikiliza Dr. Slaa akizungumza kutoka moyoni mwake, huwezi amini amejiunga CCM kwa sababu anaipenda au anamuamini Magufuli, bali amejiunga CCM because he has to, its the only way!.
If you can't beat them, join them! He is the worst dictator. Let's pray for him!

P.
Pascal kwa falsafa hizo za vita mashujaa wengi wa mataifa yao wanaangukia kundi la falsafa ya ushujaa ideology ya National patriotism, hawa ndio mashujaa wa kweli wafia nchi, wazalendo, wanaoamini wanachopigania kina Mandela, Nkuruma, Nyerere, Lumumba. Hao wengine unaosema mashujaa makini naweza kuwaita ma opportunist hawana uchungu na wanachokipigania hao ndio type ya kina Slaa.
 
Mkuu Quinine, kwanza naiunga mkono hoja hii, this is the best option, kwa sababu siku zote, haki haombwi, wala hailetwi kwenye kisahani cha chai, haki inadaiwa!, Chadema watangaze maandamano ya kifo, wamthibitishie rais Magufuli na polisi wake wote na jeshi lake lote kuwa siku hiyo, wataingia mitaani kuandamani na wote wako tayari kufa, ni heri kufa ukipigania haki, kuliko mtumwa anayelishwa makombo. Kama ni kweli polisi wetu na jeshi letu limegeuka gestapo na kutumia risasi za moto kama Soweto ile tarehe 16/6/1976, au Tiananmen Squire kule Uchina, then damu hiyo ndio itapanda mbegu ya ukombozi na amini usiamini, Karma itawashughulikia wauaji hao mmoja mmoja na hakuna hata mmoja wao ataondoka kwa amani, Malipo ni hapa hapa duniani.
Tatizo la uamuzi huu, hauwezi kufanyika Chini ya Kamanda MBOWE, ili hili lifanyike, MBOWE akubali tuu kupisha, akabidhi chama kwa vichaa kama Lissu na Lema kwa lengo tuu la kusimamia Mapambano.
"The Power of 'Karma'- Ndio Hukumu Pekee ya Haki Kamili Hapa Duniani!, Unahukumiwa kwa Matendo Yako!

Hiki ndicho kitu kinachokwenda kutokea 2020, Chadema inakwenda kupoteza majimbo yote hadi MBOWE mwenyewe hatorudi, hivyo mbunge au diwani yoyote wa Chadema, anayetaka kurudi Bungeni au kitini, ni ama aamue kupumzika siasa, ama ajiunge CCM!.

Hili nimelisema vizuri hapa.
Trend Reading: Wanaohamia CCM wasibezwe! Wanaona mbali, 2020 Majimbo yote kurejeshwa. Je tunarejea nchi ya Chama kimoja?
P.
Umesema kweli mkuu wangu na huo ndio uamuzi unaofaa katika kipindi hiki. Dharau inayoendelea sasa hatukupata kuiona katika tawala zote zilizopita. Hata wana CCM wanaoipenda nchi yao zaidi ya chama hawafurahishwi na huu uadui unaojengwa sasa.
Tunakuwaje maadui wakati zamani ndani ya nyumba moja mke anavaa kijani na mume yuko kwenye kombati na usiku wanapeana unyumba bila tatizo?
 
Kutetea wala vumbi wasiojielewa ni kazi sana ..viongozi wa juu wakiona watu hawataki kusaidiwa wawaache tu ili kila mtu aonje joto la jiwe alie na familia yake mpaka apoteze maisha labda atapata fahamu akiwa kaburini.
Mbowe nae betri imeisha chaji aachie vijana ambao hawana cha kupoteza.
 
Mkuu, kuna kitu kinaitwa falsafa ya vita ambayo inaongozwa na two schools of thoughts, falsafa ya kwanza ni falsafa ya ushujaa, inayowatumia wapiganaji mashujaa, hawa motoo yao ni "fight, fight, fight", inaamini katika kupambana tuu, Mapambano!, yaani pigana, pigana, pigana, na hata kama unapigwa, "no retreat no surrender", endelea tuu kupigana mpaka mwisho, mpaka risasi ya mwisho na tone la mwisho la damu limwagike, hata mkifa wote na kuwa wiped out, mtakumbukwa kama mashujaa mlioipigania na kuifia nchi yenu, ila mmeshindwa vita na sasa wote ni mateka, wake zenu wanabakwa, na Watoto wenu wanafanywa watumwa!.

Falsafa ya pili ni falsafa ya umakini, inayowatumia wapiganaji makini, hawa hawapeleki jeshi vitani hadi kwanza waijue nguvu ya adui, kwa Imani kuwa "never fight a loosing battle", usipigane vita ambayo unajua hutashinda. Na ukiwa vitani, ukiona dalili za kushindwa vita, ama una surrender ili msiuawawe wote, au una retreat kwa kurudisha nyuma majeshi yako, kwenda kujipanga upya.

Kundi hili la wapiganaji makini, baada ya kujaribu kupigana na kushindana na kushindwa mara kadhaa kwa sababu adui yuko vizuri Zaidi yao, huamua kutumia kanuni inayoitwa, "If you can't beat them, join them". kama huwezi kuwashinda, jiunge nao, jifunze siri zao, jijenge upya na pigana nao kutokea ndani kwao!, yaani " fight from within". Hiki ndicho wanachokifanya baadhi ya wana CCM ambao wanajiunga CCM akiwemo Dr. Slaa. Hili nimelizungumzia hapa.
Tuko Vitani Tuna Wapiganaji Shupavu, Wapiganaji Makini na Watazamaji, Je! Wewe Uko Kundi Gani ?
Katika mazingira ya Tanzania, kati ya Dr. Slaa na MBOWE, ni nani shujaa wa kweli?. Kwa sisi tuliomsikiliza Dr. Slaa akizungumza kutoka moyoni mwake, huwezi amini amejiunga CCM kwa sababu anaipenda au anamuamini Magufuli, bali amejiunga CCM because he has to, its the only way!.
If you can't beat them, join them! He is the worst dictator. Let's pray for him!

P.
Hamna ambaye anataka kufa ila kutaka ushujaa kila mtu anautaka huko chagademx
 
Bandiko linaonesha unaamini chama chako kipo nje ya msitari kimekosa mvuto
Tukiwaambia chadema hawapo kwa maslahi ya wananchi unatokwa povu
Mkiambiwa CCM imepoteza dira vyombo vyote vya ulinzi na usalama vinaingia mitaani kukilinda chama
 
Dawa ni kuamua moja tu hata kama ni kufa bora kuliko huu unyanyasaji.
AAnza kufa wewe kama unadhani ni rahisi! Wabongo mboyoyo nyingi sana halafu mnajitia kutaka ushujaa wa kuwazidi ccm.
Mapinduzi kwa Africa wanayaweza nchi zenye asili ya warabu tu!
 
Umesema kweli mkuu wangu na huo ndio uamuzi unaofaa katika kipindi hiki. Dharau inayoendelea sasa hatukupata kuiona katika tawala zote zilizopita. Hata wana CCM wanaoipenda nchi yao zaidi ya chama hawafurahishwi na huu uadui unaojengwa sasa.
Tunakuwaje maadui wakati zamani ndani ya nyumba moja mke anavaa kijani na mume yuko kwenye kombati na usiku wanapeana unyumba bila tatizo?
Huu ubaguzi umepandikizwa na uongozi wa awamu hii dhambi hii wasifikiri itaishia kizazi chao tu hawaangalii kizazi cha watoto wao na watoto wa watoto wao.
 
Huu ubaguzi umepandikizwa na uongozi wa awamu hii dhambi hii wasifikiri itaishia kizazi chao tu hawaangalii kizazi cha watoto wao na watoto wa watoto wao.
Mkuu watu kama Bashite ambao Mungu amekataa kuwapa kizazi kinacho endelea unadhani ni kwa nini? hata kama Mungu hafikiri kama sisi lakini waweza kuhisi tuu kuwa hataki kizazi hicho kiwepo baada ya yeye kutoweka.
Ni kwamba anataka kifutike
 
Nitaenda moja kwa moja kwenye msingi wa hoja yangu.

Option ya kwanza: Chadema ya leo inahitaji viongozi watakaokirudisha chama kwenye misingi yake ya zamani, misingi ya ujasiri, misingi ya hoja, misingi ya uanaharakati. Kuirudisha Chadema ya kina Slaa, Chadema ya kina Heche wakisema tukawatoe viongozi mahabusu vijana wanakwenda. Leo viongozi na wanachama wanauawa, wanatekwa, wanapotezwa, sijasikia tamko lolote la nguvu la chama zaidi ya press conference. Utawala huu sio wa press conférence, ni utawala wa kutunishiana misuli ni utawala wa Ukuta.

Option ya pili: Ili kukirudisha chama kwenye mstari, anzisheni harakati za kudai katiba mpya na tume huru ya uchaguzi, ikiwezekana tangazeni maandamano ya amani kama yale ya Ukuta kushinikiza katiba mpya ninaimani taasisi mbalimbali na watanzania wengi watawaunga mkono na chama kitarudi kwenye hadhi yake.

Option ya tatu: Kupitia kamati kuu, chama kiamue kuunga mkono maandamano ya trh 26/4 yaliyoandaliwa na wananchi, kitendo hiki kitaishitua serikali na kuilazimika kuwaita kwa lengo la kukaa pamoja ili kuzungumza na kumaliza tofauti zilizopo. Hii option ina risk kubwa lakini ina faida nyingi na za haraka, the more the risk the more the profit.

Option ya Nne: Najua hii itaonekana kuwa ngumu kidogo lakini nyepesi. Hakika uchaguzi ujao utakuwa mgumu sana kwa Chadema, chama kisipobadili mbinu za ushindi karibu wabunge wote wa Chadema hawatarudi bungeni (fact). Bunge halitakuwa na Msigwa wala Lema wala Mdee wala Mnyika, wala Bulaya. Ili kujiweka salama aidha Chama au wabunge waamue kumuunga mkono Magufuli kama wengine wanavyofanya au wabunge wakae kimya kusubiri mafao yao yawasaidie kuanza maisha mapya ya uraiani baada ya uchaguzi wa 2020.

Ili kubaki salama lazima chama kiamue kuchagua option mojawapo vinginevyo kitaendelea kupukutika na pengine kubaki jina kama vyama vingine.
==========≠=========
Huu hapa chini ni mchango wa mwanaJF mwenzetu, binafsi nimeona kuna kitu cha kujifunza. Kwanini kina Mbowe wateseke kwa Watanzania waliolala wasioonyesha hata kuguswa na juhudi zao?
Ni option ya 4 tu ndiyo inayoweza kutufanya na sisi wananchi tuone kama tunaweza kuuchagua upinzani.wananchi tunaona wazi jinsi Rais wetu anavyotupigania kwa moyo mmoja na kwa kukemea mabaya.leo hii tunaanza kuona nidhamu ya watendaji wa serikali inarudi,watu walioanza kua miungu watu hapo nyakati za nyuma.leo unaibuka eti upinzani wa kumponda mtu kama huyu kweli?yaani upinzani umesahau miaka kidigo ya nyuma ulisema nini na leo unasema nini.hawajielewi hata kidogo,wananchi tunaona kwa macho yetu na masikio yetu yanasikia pia,kumuunga mkono Rais wala siyo aibu maana juhudi zae tunaziona.badala yake upinzani umekua wa kupinga kila kitu,yaani eti ni kama serikali hii hakuna ilichofanya kwetu,sijui hawa watu wanadhani sisi ni watoto! leo wanaishia aibu ya kupelekwa mahabusu wakidhani ndiyo sifa ya upambanaji kisiasa ili vyombo vya habari viandike habari za kiumbea.badilikeni tutawaelewa

JAH RASTAFARI MORNING AFRICA
 
Mkuu Quinine, kwanza naiunga mkono hoja hii, this is the best option, kwa sababu siku zote, haki haombwi, wala hailetwi kwenye kisahani cha chai, haki inadaiwa!, Chadema watangaze maandamano ya kifo, wamthibitishie rais Magufuli na polisi wake wote na jeshi lake lote kuwa siku hiyo, wataingia mitaani kuandamani na wote wako tayari kufa, ni heri kufa ukipigania haki, kuliko mtumwa anayelishwa makombo. Kama ni kweli polisi wetu na jeshi letu limegeuka gestapo na kutumia risasi za moto kama Soweto ile tarehe 16/6/1976, au Tiananmen Squire kule Uchina, then damu hiyo ndio itapanda mbegu ya ukombozi na amini usiamini, Karma itawashughulikia wauaji hao mmoja mmoja na hakuna hata mmoja wao ataondoka kwa amani, Malipo ni hapa hapa duniani.
Tatizo la uamuzi huu, hauwezi kufanyika Chini ya Kamanda MBOWE, ili hili lifanyike, MBOWE akubali tuu kupisha, akabidhi chama kwa vichaa kama Lissu na Lema kwa lengo tuu la kusimamia Mapambano.
"The Power of 'Karma'- Ndio Hukumu Pekee ya Haki Kamili Hapa Duniani!, Unahukumiwa kwa Matendo Yako!

Hiki ndicho kitu kinachokwenda kutokea 2020, Chadema inakwenda kupoteza majimbo yote hadi MBOWE mwenyewe hatorudi, hivyo mbunge au diwani yoyote wa Chadema, anayetaka kurudi Bungeni au kitini, ni ama aamue kupumzika siasa, ama ajiunge CCM!.

Hili nimelisema vizuri hapa.
Trend Reading: Wanaohamia CCM wasibezwe! Wanaona mbali, 2020 Majimbo yote kurejeshwa. Je tunarejea nchi ya Chama kimoja?
P.

Mkuu kwa mfano wote wakapoteza majimbo na ndani kukawa na wabunge wa ccm tu kutakuwa na changamoto ya maendeleo?? Ninachoamini upinzania ni kioo kwa chama tawala ambapo hoja wanazoleta ndio chachu ya maendeleo kwa chama tawala. Sasa bunge likiwa na chama kimoja kutakuwa na hali gani!!
 
Kila jambo lina risk yake ukiogopa risk hutafanikiwa, sawa siasa za hoja zinatakiwa kwa mtu anayekusikiliza.
Siku hizi hata kupanda daladala ni risk, unakumbuka polisi walisema Akwilina alipigwa risasi kwenye mlango wa daladala wakati akiteremka! Baadaye wakapinduapindua ka Vodacom.
 
Mkuu watu kama Bashite ambao Mungu amekataa kuwapa kizazi kinacho endelea unadhani ni kwa nini? hata kama Mungu hafikiri kama sisi lakini waweza kuhisi tuu kuwa hataki kizazi hicho kiwepo baada ya yeye kutoweka.
Ni kwamba anataka kifutike
Naunga mkono hoja kwa 100% kwani Mungu si mjinga kwa kweli, Kitendo cha Maliyamungu idd Amin Bashite kutokuwa na mtoto hata wa kisingiziwa ni mipango ya Mungu ina maana Mungu hataki kizazi cha Roho mbaya kama za Maliyamungu Bashite kisambae Tanzania. Mungu Oyee oyee
 
Mkuu kwa mfano wote wakapoteza majimbo na ndani kukawa na wabunge wa ccm tu kutakuwa na changamoto ya maendeleo?? Ninachoamini upinzania ni kioo kwa chama tawala ambapo hoja wanazoleta ndio chachu ya maendeleo kwa chama tawala. Sasa bunge likiwa na chama kimoja kutakuwa na hali gani!!
Njia pekee ya kuwaokoa chadema wasipotezwe na kufutwa na Msajili wa vyama ni wao kwenda kufungua kesi mahakama za uhalifu wa kimataifa, pasipo kufanya hivyo watambue 2020 ndiyo utakuwa mwisho wa chadema na upinzani kwa ujumla.
 
Msajili hana ubavu wa kuifuta Chadema mwisho wake ni kutishia tu.
 
Back
Top Bottom