Drifter
JF-Expert Member
- Jan 4, 2010
- 5,407
- 5,584
Unfortunately, there are no options for CHADEMA or any credible opposition in Tanzania where state tyranny prevails and the citizenry is cowed into total submission. All that you've put forward are NON-OPTIONS:Mkuu, heading yangu inazungumzia Chadema sio kwamba matatizo mengine ya kitaifa siyajui, karibu tuzungumuzie options.
Kama wananchi wanafurahia serikali yao inavyoenenda na hawakubali au hawako tayari kwa mapambano dhidi ya udikteta uliopo unaodaiwa na CHADEMA, basi waarifu CHADEMA wafunge virago na kutoweka. HAKUNA NAMNA NYINGINE.
CHADEMA ya Dk. Slaa HAIWEZEKANI. Sijui kwa nini watu wanapenda kudanganyana kwenye hili. HII SIO ENZI YA KIKWETE. Siku hizi Polisi na dola wanapiga risasi waandamanaji mchana kweupe na kuua wanasiasa bila kificho. Dk. Slaa ashukuru Mungu kuwa aliachana na upinzani mapema na kufikia bei muafaka na utawala huu. Angekuwa bado huko angekuwa target number one badala ya Lissu. Yaani angeshakuwa R.I.P. na tungekuwa tumeshamsahau kama Ben Saanane alivyosahaulika.
Maandamano ya kudai Tume huru na Katiba mpya? Ni siku wananchi watakapokuwa tayari kujitoa mhanga mbele ya risasi za dola ndipo itakapowezekana kama ilivyokuwa Kenya na kwingineko. Wananchi wasipoona umuhimu huo, hakuna haja ya vitu hivyo.
CHADEMA kuunga mkono maandamano ya Mange? A gift on a golden plate for the State! Leo hii serikali inavyohangaika kutafuta namna ya kubandika sura ya CHADEMA (kama sio ya Mbowe kabisa) kwenye maandamano hayo na kwenye waraka wa KKKT halafu ikute sura hizo zimejibandika zenyewe, sio sherehe hiyo! Itakuwa ni mwendokasi wa mahakamani, jela na vipondo vya uhakika hadi watu wa R.I.P. kwa uhaini!
CHADEMA imuunge mkono Magufuli? Well, that's a sarcastic mode of ridiculing the defeated chaps. Inawezekana kweli ndio wamefikia mwisho wao wa safari. Wanachotaka kufanya hakiwezekani Tanzania. Watanzania ni watu wa amani na utulivu; hawataki shida na serikali yao. Basi, waambie CHADEMA waamue tu kukaa kimya, watulie na kujilia vijisenti vyao kimyakimya kama Kinana na joka la makengeza walivyoamua. Inatosha.