CHADEMA mikutano ya hadhara kila siku inakera

Siku za hivi karibuni kumejitokeza wimbi la wabunge wa cdm kufanya mikutano ya hadhara sehemu nyingi za nchi, nakubaliana na ukweli ya kwamba cdm imepata umaarufa hasa baada ya uchaguzi wa mwaka 2010.

Ninachoaasi viongozi cdm na wafuasi wao ni kwamba binadamu yoyote ana hulka ya kukosa hamasa na kitu chochote hasa baada ya kuwa na mazoe na kitu husika, rai yangu ni kwamba hii mikutano ya hadhara mnayofanya imeanza kuwachosha wananchi na sitashangazwa na cdm kukosa kabisa wasikilizaji ama wahudhuriaji wa mikutano yao 2015.

Ninavyoamini mimi ni kwamba kuna baadhi ya sehemu za nchi hii CHADEMA hawajawahi kufanya mikutano au kama wamefanya basi ni mara chache sana tena wakati wa uchaguzi tu. Wanachotakiwa sasa hivi ni kuweka msisitizo maeneo kama hayo ambayo chama bado hakijajulikana sana badala ya kuwaambia waache kabisa. Kumbuka chama kama CCM kilikuwepo tangu 1977 lakini bado kinafanya mikutano kila kukicha kupitia makada wao sasa iweje kwa vyama vya upinzani vilivyoanza 1992
 
Mbona bado kabisa, binafsi naona CDM bado hawajafanya mikutano ya kutosha inatakiwa hadi 2015, wawe wamepita kila kijiji cha Tanzania. Mikutano hiyo si ya siasa zile za majitaka ya CCM, ni mikutano ya kutoa elimu ya URAIA
 
Kwanin kichwa kiumize kiwili wili? kata hicho kichwa maana umejaa pumpa tu! CDM ndaima
 
Mikutano ya siasa ni lazima ndiyo inajenga chama hata hao CCM wanatamani lakini wanashindwa kwa sababu hawapati watu na wakiwapata wanawazomea kila wanachokisema.
 
Wanafanya mikutano kila siku kwa sababu wana vitu vingi ya kuwambia wananchi. Kwani wewe huoni kila siku serikali yako inaboronga na watu hawataki kujiuzulu, habari hizi lazima watu waelezwe vizuri na wajue ili itakopofika 2015 itakuwa ni kama kumsukuma mlevi tu.
 
Mbona bado wanafanya mikutano michache sana? Wananchi wanabidi kuelezwa maana ya "Upepo unaopita tu"
 
sema unakereka binafsi na kukubalika na mahudhurio ya mikutano unaiogopa mpaka umeamua kundika ...halafu tunawalipa kodi zetu kwa kazi hio..muulize nape nini kilimchosha mbona mikutano yake ya kujivua gamba imeishia wapi na matokeo yake?
 
Acha kuwasemea wananchi wa TANZANIA....kwa siku nyingi sana watu walikosa wa kuwaambia UKWELIWamepatikana CDM acha wafanye kazi yao ya siasa....KUMBUKA UKWELI HAUCHUJI WALA HAUMCHOSHI MSIKILIZAJI MAKINI!!!Kama watakosa hamasa kwa kuambiwa ukweli wa namna nchi yao inavyoporwa na umaskini wao unavyolazimishwa na wajanja wachache ndani ya CCM historia itawahukumu!!! Huu ni mwanzo tu bado tegemea makubwa....Kwingineko wananchi wenyewe bila hata kufanyiwa mikutano ulazimika kuacha kazi zao, nyumba zao na jamaa zao huku wakimiminika mitaani kuoneshwa kukerwa na watawala wao....Huku hata meli iue mamia...mabomu yalipuke....pesa ziibwe bado mnataka watu wasiamshwe kuambiwa ukweli wa mambo....Hata kama wasikilizaji watakosa hamasa na kususia mikutano ya CDM....Mimea, rasilimali na viumbe vingine vitafurahia ukweli unaosemwa make hata vyenyewe havitendewi haki chini ya watawala tulionao sasa!!!! ALUTA CONTINUA CDM.....
 
Back
Top Bottom