CHADEMA mbona hamueleweki?

CHADEMA mbona hamueleweki?

Hahahaa....unajua hawa watu hawako sawa kabisa vichwani mwao.

Na kadri siku zinavyosonga mbele ndo zile sifa alizozielezea rais mstaafu Mkapa zinazidi kudhihirika.

Ushindi wa huyo Uhuru huko Kenya unahusiana nini nyie CHADEMA?

Badala ya kupambana na hali yenu hapa Tanzania mnahangaika na kushangilia mambo ya wengine huko tena ambayo hayawahusu.

Halafu pia kuna watu eti wanawashangaa hawa CHADEMA kuwa kwa nini kama wao ni chama cha upinzani hapa nchini wakiunge mkono chama tawala cha huko Kenya.

Kwa akili ya kawaida watu wangedhani labda upinzani wa Tanzania ungetaka upinzani wa Kenya ushinde.

Kama CHADEMA walibadili gia angani kuhusu babu Lowasa na kumtimua mtu aliyekijenga chama chao kwa hali na mali [Dkt. Slaa], sasa ni nini cha kushangaza kuhusu wao kukiunga mkono chama tawala cha Kenya?

Laana ya Dkt. Slaa itawaandama hawa CHADEMA hadi siku ya kiama. Na wataishia kufurahia ushindi wa wengine huko kwingine na kamwe hawatokuja kufurahia mafanikio yao hapa Tanzania kwa sababu wapo kama vile ambavyo rais Mkapa alivyowaita!!
 
huo utakua ushindi wa kwanza wa chadema kwenye nafasi ya Urais.

Aisee nimecheka sana baada ya kuona mtu kaanzisha uzi akisema kwamba ushindi wa Uhuru ni ushindi wa CHADEMA.

Hawa watu naona wanaishi kwenye ulimwengu wao peke yao.
 
Hapana wewe ndiye mkurupukaji Mwanasheria msomi. Nimekuuliza maswali lakini umeshindwa kuyajibu sasa unabaki kutoa povu tu. Jiongeze na utafakari kwa kina.

Ni jambo la kimantiki tu. CHADEMA wamekurupuka.
 
Hahahaa....unajua hawa watu hawako sawa kabisa vichwani mwao.

Na kadri siku zinavyosonga mbele ndo zile sifa alizozielezea rais mstaafu Mkapa zinazidi kudhihirika.

Ushindi wa huyo Uhuru huko Kenya unahusiana nini nyie CHADEMA?

Badala ya kupambana na hali yenu hapa Tanzania mnahangaika na kushangilia mambo ya wengine huko tena ambayo hayawahusu.

Halafu pia kuna watu eti wanawashangaa hawa CHADEMA kuwa kwa nini kama wao ni chama cha upinzani hapa nchini wakiunge mkono chama tawala cha huko Kenya.

Kwa akili ya kawaida watu wangedhani labda upinzani wa Tanzania ungetaka upinzani wa Kenya ushinde.

Kama CHADEMA walibadili gia angani kuhusu babu Lowasa na kumtimua mtu aliyekijenga chama chao kwa hali na mali [Dkt. Slaa], sasa ni nini cha kushangaza kuhusu wao kukiunga mkono chama tawala cha Kenya?

Laana ya Dkt. Slaa itawaandama hawa CHADEMA hadi siku ya kiama. Na wataishia kufurahia ushindi wa wengine huko kwingine na kamwe hawatokuja kufurahia mafanikio yao hapa Tanzania kwa sababu wapo kama vile ambavyo rais Mkapa alivyowaita!!
Zamani niliamini Ulaya na Marekani hakuna ' wambeya na vizabizabina' kumbe sikuwa sahihi mkuu unathibitisha hilo!
 
Nyani nyani tu, akili za kinyani nyani tu. Vyovyote vile, tumeokoa EAC kutaliwa na watu wa aina fulani. Asante Mungu kwa hilo. Hivi ile Airport ya chattle uzinduzi si aliandaliwa jamaa awe mgeni rasmi akiwa presdaaa, chali, tupa kule
 
Mkuu,tangu Laigwanan ajiunge CDM mawazo yake ndo kama msimamo wa chama,cha kushangaza hata umafia anaoufanya Uhuru,hata kuuawa kwa kiongozi wa IEBC wiki moja kabla ya uchaguzi,hawakukemea kabisa,sababu wameshashikwa akili.

Ila wasisahau hapa tz haitotokea tena watu kuzungusha mikono,kudeki lami wala kujifanya kuzimia kama ilivyotokea 2015, wananchi wameshajua rangi halisi za CDM.Hawana sera tena.
 
upload_2017-8-9_17-13-34.jpeg
 
Uzi unaoujibu night huu hapa chini japo umehamishwa jukwaa●

CCM wataongea weee ila Unaweza kuwajibu hamadi kibindoni.
Unaweza pia kuwajibu Kimfaacho mtu chake!
Mimi nasema Hongera Uhuru , hongera CHADEMA.
Kwanini hongera CHADEMA?
Ni upuuzi, Actually ni wapuuzi tu wanaoweza kuubeza ushindi wa kimkakati wa CHADEMA kuwa na rafiki anayeongoza uchumi mkubwa kuliko yote Africa Mashariki.
Kenya ni kubwa karibu kila nyanja Africa Mashariki;
☞Ndio wenye uchumi mkubwa kuliko yote Africa mashariki .
☞Wana jeshi kubwa na la kisasa.
☞Wana kambi pekee ya Special Forces ya USA- Camp Simba hapa Africa mashariki.
☞Ni demokrasia iliyokomaa ukilinganisha na zote hapa Africa Mashariki.
Kuna msemo usemao, Ukitaka kumfahamu mtu basi waangalie marafiki zake.
Ukitaka kumfahamu Magufuli na CCM basi muangalie;
☞Paul Kagame
☞Yoweri Museveni
☞Nkurunzinza
Na Ukitaka kumfahamu Lowassa na CHADEMA basi muangalie Uhuru Kenyatta!
Leo nimejikumbushia kidogo miaka nikiwa Seminari na nikamkumbuka Yesu na familia ya kina Martha na Lazaro ambayo Yesu aliipenda sana. Unaweza kusema familia rafiki kwa Yesu.
Basi wakati Lazaro ameugua sana, Martha dadaye alituma ujumbe kwa Yesu kuwa rafiki yako anaumwa sana, hawezi tena.
Nakumbuka Yesu alimjibu kuwa, 'Ugonjwa huu sio kwaajili ya Mauti ila kwaajili ya utukufu wa Mungu'.
Naomba kwa leo niwaache na neno hilo hapo juu ndugu zangu!
 
Mwaka 2016,wakati wa uchaguzi wa kule nchini Ghana, nyinyi CHADEMA mlikuwa mkimuunga aliyekuwa mgombea wa Upinzani, Rais wa sasa wa Ghana Mhe. Nana Akufo-Addo aliyekuwa akichuana na Rais wa wakati huo, Mhe. John Dramani Mahama. Kwakuwa wote mlikuwa wapinzani, uungaji wenu mkono ulikuwa unaeleweka.

Mwaka huu, katika uchaguzi wa Kenya, CHADEMA mmemuunga mkono waziwazi Rais wa sasa wa Kenya na mgombea wa Jubilee Mhe. Uhuru Jomo Kenyatta. Ndiyo kusema, mmeunga mkono chama tawala ili kiendelee kutawala kule nchini Kenya. Mpinzani kuunga mkono chama tawala, ambacho nchini mwake anapambana kukiondoa madarakani, ni jambo la kustaajabisha.

Mwanachama wenu na Mjumbe wa Kamati Kuu, Ndugu Edward Ngoyai Lowassa amejitokeza mubashara jukwaa la Jubilee kukipigania chama tawala Kenya ili kiendelee kutawala. Kama Rais Uhuru Kenyatta atashinda tena, naye atapanda jukwaa la CHADEMA mwaka 2020 kuwanadi? Imekuwaje hadi nyinyi wapinzani muunge mkono chama tawala?

Tuamini kuwa hata Tanzania nyinyi CHADEMA mnazuga tu kupambana na chama tawala CCM huku mkiwa mnapenda CCM iendelee kuongoza? Kwakweli, CHADEMA hamueleweki kirahisi katika hili!
mbona nawewe hueleweki mbona mtaani unafanya ujinga lini umeeleweka?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu kwakweli umeonyesha haujui Siasa za kimataifa na diplomasia.....uliza uelekezwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Raila Odinga Aeleza Kenya Ilivyopokea Ushindi Wa Magufuli Na Kama Aliwahi Kumgusia Kuutaka Urais
2 years ago Comments Off on Raila Odinga Aeleza Kenya Ilivyopokea Ushindi Wa Magufuli Na Kama Aliwahi Kumgusia Kuutaka Urais
Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya, Raila Odinga ambaye ni rafiki wa Dkt. John Magufuli ameeleza jinsi ambavyo chama chake cha ODM na Kenya walivyoupokea ushindi wa kada huyo wa CCM kugombea kiti cha urais wa Tanzania.

Akiongea na kituo cha runinga cha ‘Azam Two’, Odinga alisema kuwa wameufurahia sana ushindi wa Magufuli. Alisema wana imani kubwa kuwa kwa utendaji wake atasaidia kuimarisha zaidi umoja wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

“Sisi kama rafiki wa Tanzania tumefurahishwa sana na ambayo yamefanyika. Kuteuliwa kwa bwana maguguli kama yule ambaye atabeba bendera ya chama cha CCM, imetufurahisha sana hapa Kenya. Ndio maana sisi tunasema pongezi na heko kwa bwana Magufuli,”alisema Raila Odinga.

Odinga alieleza kuwa amemfahamu Dkt. Magufuli kwa kipindi kirefu na wamekuwa wakishirikiana kwa ukaribu na kushauriana tangu walipokuwa wanafanya kazi kama mawaziri wa wizara za ujenzi na barabara wa nchi zao. Hivyo, anatambua uwezo wake wa kutenda kazi kwa ufanisi.

Akielezea jinsi alivyomfahamu Magufuli na kama aliwahi kumdokezea kuwa na mpango wa kuwa rais wa Tanzania siku za usoni, Odinga alisema, “ni mtu mpole, si mtu ambaye ana hamaki. Anafuatilia mambo kabla hajafanya. Yeye mwenyewe amesema tu mara kwa mara eti hawezi kujilazimisha katika hili, lakini watanzania wakiamua yeye atakuwa tayari kuwahudumia hata katika cheo cha urais.”

Alisema chama cha ODM ni rafiki wa Chama Cha Mapinduzi hivyo watakiunga mkono katika mbio hizo za urais wa Tanzania japo hawatajihusisha moja kwa moja na kampeni kwa kuwa kampeni zinapaswa kufanywa na watanzania wenyewe.

CC: Mwanasheria msomi Petro E. Mselewa
 
Mwaka 2016,wakati wa uchaguzi wa kule nchini Ghana, nyinyi CHADEMA mlikuwa mkimuunga aliyekuwa mgombea wa Upinzani, Rais wa sasa wa Ghana Mhe. Nana Akufo-Addo aliyekuwa akichuana na Rais wa wakati huo, Mhe. John Dramani Mahama. Kwakuwa wote mlikuwa wapinzani, uungaji wenu mkono ulikuwa unaeleweka.

Mwaka huu, katika uchaguzi wa Kenya, CHADEMA mmemuunga mkono waziwazi Rais wa sasa wa Kenya na mgombea wa Jubilee Mhe. Uhuru Jomo Kenyatta. Ndiyo kusema, mmeunga mkono chama tawala ili kiendelee kutawala kule nchini Kenya. Mpinzani kuunga mkono chama tawala, ambacho nchini mwake anapambana kukiondoa madarakani, ni jambo la kustaajabisha.

Mwanachama wenu na Mjumbe wa Kamati Kuu, Ndugu Edward Ngoyai Lowassa amejitokeza mubashara jukwaa la Jubilee kukipigania chama tawala Kenya ili kiendelee kutawala. Kama Rais Uhuru Kenyatta atashinda tena, naye atapanda jukwaa la CHADEMA mwaka 2020 kuwanadi? Imekuwaje hadi nyinyi wapinzani muunge mkono chama tawala?

Tuamini kuwa hata Tanzania nyinyi CHADEMA mnazuga tu kupambana na chama tawala CCM huku mkiwa mnapenda CCM iendelee kuongoza? Kwakweli, CHADEMA hamueleweki kirahisi katika hili!
wewe ndiye huelewi.chadema wameunga mkono uhuru kwasababu mkuu wetu alimuunga mkono odinga.sasa ulitaka wote wawe wamoja?Na unajua mkuu wetu asivyowapenda chadema.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom