CHADEMA mbona hamueleweki?

CHADEMA mbona hamueleweki?

Mkuu, kila mpinzani analenga kuwa mtawala. Mnapaswa kupambana mtawale. Si kuwaunga mkono watawala.
Mkuu kwani ni kosa
Uhuru ana mapungufu gani labda tuanzie hapa.....
Kwani Kila chama tawala lazima kisichaguliwe ?
What if Uhuru anatekeleza maazimio kwa wananchi?
So upinzani ni nini?
 
Boss na MwanaSheria Msomi Petro E. Mselewa nakumbuka nilisoma au kuisikiliza Mh. Mbowe alilitolea ufafanuzi ili jambo. Kwanini Chadema walibadilisha Gia Angani. Kama ulipitiwa walisema, wameamua kum support Uhuru kwa sababu wakati wa uchaguzi uliopita walim support Odinga akashindwa. Uchaguzi ulipokuja Tanzania. Odinga hakuwa support Chadema, Odinga alimSupport Mh. Rais Magufuli.

My Take: Haya si maneno yangu.

Mwaka 2016,wakati wa uchaguzi wa kule nchini Ghana, nyinyi CHADEMA mlikuwa mkimuunga aliyekuwa mgombea wa Upinzani, Rais wa sasa wa Ghana Mhe. Nana Akufo-Addo aliyekuwa akichuana na Rais wa wakati huo, Mhe. John Dramani Mahama. Kwakuwa wote mlikuwa wapinzani, uungaji wenu mkono ulikuwa unaeleweka.

Mwaka huu, katika uchaguzi wa Kenya, CHADEMA mmemuunga mkono waziwazi Rais wa sasa wa Kenya na mgombea wa Jubilee Mhe. Uhuru Jomo Kenyatta. Ndiyo kusema, mmeunga mkono chama tawala ili kiendelee kutawala kule nchini Kenya. Mpinzani kuunga mkono chama tawala, ambacho nchini mwake anapambana kukiondoa madarakani, ni jambo la kustaajabisha.

Mwanachama wenu na Mjumbe wa Kamati Kuu, Ndugu Edward Ngoyai Lowassa amejitokeza mubashara jukwaa la Jubilee kukipigania chama tawala Kenya ili kiendelee kutawala. Kama Rais Uhuru Kenyatta atashinda tena, naye atapanda jukwaa la CHADEMA mwaka 2020 kuwanadi? Imekuwaje hadi nyinyi wapinzani muunge mkono chama tawala?

Tuamini kuwa hata Tanzania nyinyi CHADEMA mnazuga tu kupambana na chama tawala CCM huku mkiwa mnapenda CCM iendelee kuongoza? Kwakweli, CHADEMA hamueleweki kirahisi katika hili!
 
Kwa akili ya kawaida tu, mnategemea wakati wa kampeni za 2020 Kenyatta akiwa rais wa Kenya aje kwenye kampeni za upinzani Tanzania na apande jukwaa moja na Lowassa?.

..sasa labda ulitaka wasiunge mkono mgombea yeyote mwenye uwezekano wa kuwa Raisi.

..Uhuru hawezi kuja Tz na kupanda majukwaani kuwa support CDM, unless unataka kusema ana busara sawa na yule Waziri wa serikali ya JK aliyempanda jukwaani kumsupport Raila Odinga.

..Pia msaada hata wa ushauri kuhusu mbinu na mikakati ya uchaguzi unatosha.

NB.

..Tumefika hapa kutokana na urafiki wa Raila Odinga na bwana mmoja huku Tz.

Cc Nyani Ngabu
 
Siasa ya Tanzania imekuwa kiasi ya kusaidia za majirani zetu.

Mwenyezi Mungu aendelee kutupa busara zaidi za kusaidia wenzetu.

Demokrasia yetu imebalance na ya majirani zetu.
Iwapo moja ya washindani wa Kenya atashindwa faraja yake ataipata Tanzania.

Katika hili tusiangalie Chama bali Amani ya Jamhuri ya Kenya,kwani Kenya ni moja na sisi Tanzania ni ndugu zao/Afrika moja.

Tuwasaidiane kuwafariji na kuwatia moyo katika kipindi hiki kifupi na kigumu.

Lakini pia tuwaombe washirikiane pamoja kuijenga Kenya Mpya itakayowakumbuka waasisi wa Taifa hilo Hayati Mzee Jomo Kenyatta na Hayati Mzee Jalamongi Oginga Odinga.
 
..sasa labda ulitaka wasiunge mkono mgombea yeyote mwenye uwezekano wa kuwa Raisi.

..Uhuru hawezi kuja Tz na kupanda majukwaani kuwa support CDM, unless unataka kusema ana busara sawa na yule Waziri wa serikali ya JK aliyempanda jukwaani kumsupport Raila Odinga.

..Pia msaada hata wa ushauri kuhusu mbinu na mikakati ya uchaguzi unatosha.

NB.

..Tumefika hapa kutokana na urafiki wa Raila Odinga na bwana mmoja huku Tz.

Cc Nyani Ngabu
Tatizo letu watanzania tunapenda sana kuongea mpaka tunajikuta tunawawekea maneno mdomoni watu wengine. Na hilo ni kosa kisheria.

Katika kipindi chote hiki serikali imekuwa kimya kabisa, lakini ni watu humu ndani wanaojaribu kujenga mazingira ili ionekane kwamba serikali ipo pamoja na Raila Odinga na inamhujumu Kenyatta.

Mleta mada amejenga hoja makini kwa kuwakumbusha CHADEMA kwamba sio tu waweke akiba ya maneno bali pia wakumbuke kuweka akiba ya matendo yao. Kila jambo lina matokeo yake tena yanayodumu kwa miaka mingi ijayo.

Chama cha siasa makini, huwa na watu wenye kuelewa faida na hasara za maamuzi ya leo.
 
Analosema au alofanya EL ndo jambo la CDM cause ni mali yake, alisha uziwa na mbowe. Akiwa Kenya alishatangaza atagombea urais kupitia ' chama chake CDM'
Mtabwabwaja lakini ukweli mnaufahamu. Wananchi wa Kenya wameonesha pasipo shaka kwamba udikteta hauna nafasi katika siasa zao na kama kuna kiongozi alijinadi hivyo imekula kwake. Demokrasia imeshinda na mtake msitake utawala wa mabavu umekataliwa na Wakenya, period.

Kuna uzi humu humu mkidai jina la Magufuli kutawala kampeni huko Kenya na kwamba wapo wagombea wanajinadi kwa kuahidi kuiga vitendo vya huyu...bonyeza hapa!

Na kwa wasiofahamu Raila anajulikana Kenya kama tinga (tinga tinga kwa kijaluo) na huku kwetu Magufuli alipewa jina hilo hilo tinga tinga kwa anavyowapondaponda wapinzani wake bila huruma na kuwaziba midomo. Well, the Kenyans dont want a tinga tinga, they want a leader who abides by the constitution and respects the rule of law...
 
We mwanasheria mbona na sisi hatukuelewi?umefanya homework ya kutosha kabla haujaja na uzi huu?mbona walishatoa maelezo kwa nini hawako na wapinzani wa kenya safari hii.Kati ya sababu ambazo walitoa ni kuwa Raila na wenzake waliwageuka kwenye uchaguzi uliopita wa kwetu.hata ungekuwa wewe mwanasheria ungefanyaje?dawa ya moto ni moto
 
Mkuu, unatamani niwe CHADEMA? Kweli una Magonjwa Mtambuka
Wewe Mngoni naona unatafuta matusi ya bure hapa. Kwani wewe hujui kwanini wanampigia kampeni Uhuru? Hata wewe ukitaka kuitwa msaliti kosoa makamanda wao. Tatizo siyo kuunga mkono Uhuru wao wanafikiri wanamkomoa Odinga kwa urafiki wake na JPM. Na kuhusu 2020 Uhuru hata wasaidia kukampeni maana anajua hawawezi kushinda.
Ndiyo maana nimekuomba tuanzishe chama chetu chenye wanachama wapya na ambao hawana makandokando ya u ccm ama ukawa kama wengi wa humu jf.
 
Aisee nimecheka sana baada ya kuona mtu kaanzisha uzi akisema kwamba ushindi wa Uhuru ni ushindi wa CHADEMA.

Hawa watu naona wanaishi kwenye ulimwengu wao peke yao.
Lugha hasi ya magufuli wanaita "cloud cuckoo land" ndiyo nchi wanayoishi hawa wajemeni
 
Wewe Mngoni naona unatafuta matusi ya bure hapa. Kwani wewe hujui kwanini wanampigia kampeni Uhuru? Hata wewe ukitaka kuitwa msaliti kosoa makamanda wao. Tatizo siyo kuunga mkono Uhuru wao wanafikiri wanamkomoa Odinga kwa urafiki wake na JPM. Na kuhusu 2020 Uhuru hata wasaidia kukampeni maana anajua hawawezi kushinda.
Ndiyo maana nimekuomba tuanzishe chama chetu chenye wanachama wapya na ambao hawana makandokando ya u ccm ama ukawa kama wengi wa humu jf.
Sawa,nipo tayari mtani. Na mtani Nyani Ngabu awepo.
 
Mkuu kwakweli umeonyesha haujui Siasa za kimataifa na diplomasia.....uliza uelekezwa

Sent using Jamii Forums mobile app
Tueleweshe hizo za kmataifa. Maana huwezi kubadilisha kila kukicha mwaka 2013 upo na nasa mwaka unaofuata upo na chama kingine. Nigel Farage alimkampenia Trump sababu Trump ni kama yeye ni far right ila aliyejificha kama conservative, Labour hata siku moja wanaweza kwenda kukampeni kwa Republican Marekani sababu wana itikadi za mrengo tofauti. Na kama Labour wapo madarakani ni nadra kwenda kukampeni marekani sijui hizo siasa zako za kimataifa ni mataifa gani. Labda mataifa ya kenya na kenya. Mwisho Petro japo ni mwanasheria lakini sidhani kama si muelewa wa haya masuala kama unavyojitahidi kumdhalilusha.
 
Sawa,nipo tayari mtani. Na mtani Nyani Ngabu awepo.
Huyo tena lazima awemo maana chama chetu bora kisiwe na mamilioni ya wanachama lakini kiwe na wenye umakini. Nimepitia comments hapa mpaka najiuliza kama watu huwa wana research ama wanaamua tu kujibu sababu wana bundle za data za kuchezea.
 
Mwaka 2016,wakati wa uchaguzi wa kule nchini Ghana, nyinyi CHADEMA mlikuwa mkimuunga aliyekuwa mgombea wa Upinzani, Rais wa sasa wa Ghana Mhe. Nana Akufo-Addo aliyekuwa akichuana na Rais wa wakati huo, Mhe. John Dramani Mahama. Kwakuwa wote mlikuwa wapinzani, uungaji wenu mkono ulikuwa unaeleweka.

Mwaka huu, katika uchaguzi wa Kenya, CHADEMA mmemuunga mkono waziwazi Rais wa sasa wa Kenya na mgombea wa Jubilee Mhe. Uhuru Jomo Kenyatta. Ndiyo kusema, mmeunga mkono chama tawala ili kiendelee kutawala kule nchini Kenya. Mpinzani kuunga mkono chama tawala, ambacho nchini mwake anapambana kukiondoa madarakani, ni jambo la kustaajabisha.

Mwanachama wenu na Mjumbe wa Kamati Kuu, Ndugu Edward Ngoyai Lowassa amejitokeza mubashara jukwaa la Jubilee kukipigania chama tawala Kenya ili kiendelee kutawala. Kama Rais Uhuru Kenyatta atashinda tena, naye atapanda jukwaa la CHADEMA mwaka 2020 kuwanadi? Imekuwaje hadi nyinyi wapinzani muunge mkono chama tawala?

Tuamini kuwa hata Tanzania nyinyi CHADEMA mnazuga tu kupambana na chama tawala CCM huku mkiwa mnapenda CCM iendelee kuongoza? Kwakweli, CHADEMA hamueleweki kirahisi katika hili!
Unapounga mkono chama fulani kwenye uchaguzi hasa wa urais unasukumwa na mgombea aliyeko kweye chama kile. Itoshe tu kukuambia ndugu yamgu, maana inaonekana umekwepa kuliseme hili. Mwaka 2015, Raila alikuwa upande wa chadema kama mpinzani mwenzao, kilichotokea ni kwamba baada ya jpm kupitishwa na ccm (jambo ambalo alikuwa hategemei ofcourse), ghafla akageuka akaelekea kwa jpm. Hapo ndipo palipoleta shida. Na mengine aliyofanya Odinga kwa chadema anafahamu mwenyewe maana (hata matokeo ya leo
ni adhabu ya aliyoyatenda wakati huo kupitia mfumo huu huu). Sasa unategemeaje umuunge mkono mtu aliyekusaliti kwenye mapambano? Pili, huyu odinga ni rafiki mkubwa wa jpm, unategemeaje upinzani hasa chadema wamuunge mkono basi tu kwa kuwa ni mpinzani? Kumbuka upinzani hutegemea na unakosimamia na si swala la 'tawala'. Hata Jubilee ni upinzani ukiwa upande wa odinga, na the viceversa is true also. Furaha yangu imesimamia tu pale ambapo yatakayowapa upinzani huko Kenya pamoja na kwamba si ya kufurahiwa na yeyotte, lakini yatatoa somo na ujumbe tosha kwa kina jpm ambao kwa namna moja au nyingine watahusika kutoa neno la busara. Tusishangae uhuru akiapishwa harakaharaka na kumuweka ndani Raila haraka sana. Unafikiri jpm atakuwa anapata ujumbe gani? Atakapoenda kushauri atasemaje huku magerezani nchini kwake kila kukicha akiwa anarundika upinzani? Inafikirisha, ni ngumu lakini ni kuimeza tu ndo dawa hakuna nyingine...
 
Mwaka 2016,wakati wa uchaguzi wa kule nchini Ghana, nyinyi CHADEMA mlikuwa mkimuunga aliyekuwa mgombea wa Upinzani, Rais wa sasa wa Ghana Mhe. Nana Akufo-Addo aliyekuwa akichuana na Rais wa wakati huo, Mhe. John Dramani Mahama. Kwakuwa wote mlikuwa wapinzani, uungaji wenu mkono ulikuwa unaeleweka.

Mwaka huu, katika uchaguzi wa Kenya, CHADEMA mmemuunga mkono waziwazi Rais wa sasa wa Kenya na mgombea wa Jubilee Mhe. Uhuru Jomo Kenyatta. Ndiyo kusema, mmeunga mkono chama tawala ili kiendelee kutawala kule nchini Kenya. Mpinzani kuunga mkono chama tawala, ambacho nchini mwake anapambana kukiondoa madarakani, ni jambo la kustaajabisha.

Mwanachama wenu na Mjumbe wa Kamati Kuu, Ndugu Edward Ngoyai Lowassa amejitokeza mubashara jukwaa la Jubilee kukipigania chama tawala Kenya ili kiendelee kutawala. Kama Rais Uhuru Kenyatta atashinda tena, naye atapanda jukwaa la CHADEMA mwaka 2020 kuwanadi? Imekuwaje hadi nyinyi wapinzani muunge mkono chama tawala?

Tuamini kuwa hata Tanzania nyinyi CHADEMA mnazuga tu kupambana na chama tawala CCM huku mkiwa mnapenda CCM iendelee kuongoza? Kwakweli, CHADEMA hamueleweki kirahisi katika hili!

Hivi kila unae msupport kama chama lazima awe madarakani , it doesnt make sense at all, Unaweza ukasupport chama kilicho madarakani au kisiwepo madarakani ili mradi mnaona kwamba mna uhusiano mzuri
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom