CHADEMA mbona hamueleweki?

CHADEMA mbona hamueleweki?

alivyoondoka slaa chama kikafa , alipokuja lowasa kikazikwa rasmi.



chadema wanyonge tulikipenda ila mafisadi wamekipenda zaid wameni disappoint sana binafsi.
 
Mwaka 2016,wakati wa uchaguzi wa kule nchini Ghana, nyinyi CHADEMA mlikuwa mkimuunga aliyekuwa mgombea wa Upinzani, Rais wa sasa wa Ghana Mhe. Nana Akufo-Addo aliyekuwa akichuana na Rais wa wakati huo, Mhe. John Dramani Mahama. Kwakuwa wote mlikuwa wapinzani, uungaji wenu mkono ulikuwa unaeleweka.

Mwaka huu, katika uchaguzi wa Kenya, CHADEMA mmemuunga mkono waziwazi Rais wa sasa wa Kenya na mgombea wa Jubilee Mhe. Uhuru Jomo Kenyatta. Ndiyo kusema, mmeunga mkono chama tawala ili kiendelee kutawala kule nchini Kenya. Mpinzani kuunga mkono chama tawala, ambacho nchini mwake anapambana kukiondoa madarakani, ni jambo la kustaajabisha.

Mwanachama wenu na Mjumbe wa Kamati Kuu, Ndugu Edward Ngoyai Lowassa amejitokeza mubashara jukwaa la Jubilee kukipigania chama tawala Kenya ili kiendelee kutawala. Kama Rais Uhuru Kenyatta atashinda tena, naye atapanda jukwaa la CHADEMA mwaka 2020 kuwanadi? Imekuwaje hadi nyinyi wapinzani muunge mkono chama tawala?

Tuamini kuwa hata Tanzania nyinyi CHADEMA mnazuga tu kupambana na chama tawala CCM huku mkiwa mnapenda CCM iendelee kuongoza? Kwakweli, CHADEMA hamueleweki kirahisi katika hili!
Wewe ndo hueleweki. Ni kipi usichokijua kuhusu CHADEMA kuanza kumuunga mkono Uhuru?
 
Katika watu niliokuwa nawaheshimu katika hili jukwaa ni wewe ila kwa hichi ulichoandika nimegundua Tanzania yangu bado NANGA ni wengi mno. Adui wa adui yako lazima awe rafiki yako. Wewe kweli umesoma sheria kama unavyojinadi? Ila siwezi kushangaa kwani kuna wanaomaliza mlimani hata mkataba wa kuuza shamba hawezi kuandaa.
 
  • Thanks
Reactions: Mdf
Kama ni chama rafiki cha muda hakuna tatizo. Jubilee na CHADEMA hawakuwahi kuwa marafiki isipokuwa sasa
Mbona unaendelea kuonyesha ujinga wako!!! kuna sehemu imeandikwa urafiki unatakiwa kuanza muda gani? Duu ujinga haujawahi kufichka leo umeonyesha ujinga wako wote
 
Vyeti fake havijawahi kumwacha mtu bila kujionyesha akili yake, huwezi amini mtu anasema amesoma sheria anauliza maswali ya kitoto kabisa au ni sheria ngazi ya cheti? hata ya cheti tu lazima awe anajitambua.
 
Wapinzani nchini wanamshangaa Raila anaposema kaibiwa kura.Ati siku hizi wapinzani hawaamini kama kura zinaweza kuibiwa!!

Wapinzani nchini wanamshauri rais Uhuru wa Kenya kumsweka ndani Raila kwa tuhuma za uchochezi!!!!!

Siasa za hii nchi burudani sana siku hizi.
 
Unapounga mkono chama fulani kwenye uchaguzi hasa wa urais unasukumwa na mgombea aliyeko kweye chama kile. Itoshe tu kukuambia ndugu yamgu, maana inaonekana umekwepa kuliseme hili. Mwaka 2015, Raila alikuwa upande wa chadema kama mpinzani mwenzao, kilichotokea ni kwamba baada ya jpm kupitishwa na ccm (jambo ambalo alikuwa hategemei ofcourse), ghafla akageuka akaelekea kwa jpm. Hapo ndipo palipoleta shida. Na mengine aliyofanya Odinga kwa chadema anafahamu mwenyewe maana (hata matokeo ya leo
ni adhabu ya aliyoyatenda wakati huo kupitia mfumo huu huu). Sasa unategemeaje umuunge mkono mtu aliyekusaliti kwenye mapambano? Pili, huyu odinga ni rafiki mkubwa wa jpm, unategemeaje upinzani hasa chadema wamuunge mkono basi tu kwa kuwa ni mpinzani? Kumbuka upinzani hutegemea na unakosimamia na si swala la 'tawala'. Hata Jubilee ni upinzani ukiwa upande wa odinga, na the viceversa is true also. Furaha yangu imesimamia tu pale ambapo yatakayowapa upinzani huko Kenya pamoja na kwamba si ya kufurahiwa na yeyotte, lakini yatatoa somo na ujumbe tosha kwa kina jpm ambao kwa namna moja au nyingine watahusika kutoa neno la busara. Tusishangae uhuru akiapishwa harakaharaka na kumuweka ndani Raila haraka sana. Unafikiri jpm atakuwa anapata ujumbe gani? Atakapoenda kushauri atasemaje huku magerezani nchini kwake kila kukicha akiwa anarundika upinzani? Inafikirisha, ni ngumu lakini ni kuimeza tu ndo dawa hakuna nyingine...

Kenya wanaruhusu wafungwa kupiga kura. Raila kashinda kwa wafungwa. Pia wanaruhusu diaspora kupiga kura, aka CIA agents. Raila kashinda tena.

Sawa kabisa na Chadema hapa - bodaboda; richmond; nafisadi; wabafunzi hewa; wanafunzi wenye mimba etc. Hata Narok na Kajiado naona Wamasai wamewagana 50-50 hata baada ya Lowassa kujaribu kuwarubuni.
 
Mimi Sio Chadema, ila vyama vya siasa huwa na mirongo inayofuta, kuna vya mrongo wa kulia (Conservative) Mrongo wa Kati(Liberal) na Mrongo wa Kushoto (Socialists)

Vyama huwa vinasapotiana kutokana na mirongo yao. Mfano: Jeremy corbyn(Socialist) ni mpinzani Ungereza lakini ana support chama kinachotawala Venezuela.

Swali lako halina taja kwamba ukiwa mpinzani lazima usupport wapinzani. Siasa haziendi hivyo ndugu.
WE NEED URINE SAMPLE FIRSTS , AND THEN WE WILL CARRY ON TALKING
Ni jambo la kimantiki tu. CHADEMA wamekurupuka.
WE MIGHT NEED URINE SAMPLE FROM HIM PLEASE
 
Katika watu niliokuwa nawaheshimu katika hili jukwaa ni wewe ila kwa hichi ulichoandika nimegundua Tanzania yangu bado NANGA ni wengi mno. Adui wa adui yako lazima awe rafiki yako. Wewe kweli umesoma sheria kama unavyojinadi? Ila siwezi kushangaa kwani kuna wanaomaliza mlimani hata mkataba wa kuuza shamba hawezi kuandaa.
Mwanasheria amenisikitisha sana hata siamini,hata kama ni masihara sikutegemea yatoke kwake kwasababu siyo kawaida yake.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom