CHADEMA mbona hamueleweki?

CHADEMA mbona hamueleweki?

Mwaka 2016,wakati wa uchaguzi wa kule nchini Ghana, nyinyi CHADEMA mlikuwa mkimuunga aliyekuwa mgombea wa Upinzani, Rais wa sasa wa Ghana Mhe. Nana Akufo-Addo aliyekuwa akichuana na Rais wa wakati huo, Mhe. John Dramani Mahama. Kwakuwa wote mlikuwa wapinzani, uungaji wenu mkono ulikuwa unaeleweka.

Mwaka huu, katika uchaguzi wa Kenya, CHADEMA mmemuunga mkono waziwazi Rais wa sasa wa Kenya na mgombea wa Jubilee Mhe. Uhuru Jomo Kenyatta. Ndiyo kusema, mmeunga mkono chama tawala ili kiendelee kutawala kule nchini Kenya. Mpinzani kuunga mkono chama tawala, ambacho nchini mwake anapambana kukiondoa madarakani, ni jambo la kustaajabisha.

Mwanachama wenu na Mjumbe wa Kamati Kuu, Ndugu Edward Ngoyai Lowassa amejitokeza mubashara jukwaa la Jubilee kukipigania chama tawala Kenya ili kiendelee kutawala. Kama Rais Uhuru Kenyatta atashinda tena, naye atapanda jukwaa la CHADEMA mwaka 2020 kuwanadi? Imekuwaje hadi nyinyi wapinzani muunge mkono chama tawala?

Tuamini kuwa hata Tanzania nyinyi CHADEMA mnazuga tu kupambana na chama tawala CCM huku mkiwa mnapenda CCM iendelee kuongoza? Kwakweli, CHADEMA hamueleweki kirahisi katika hili!
Kweli wewe ni Mwanasheria?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa sababu Raila Odinga siyo Mpinzani.ANgekuwa mpinzani angekuwa wa kwanza kumuonya rafiki yake namna anavyowafanyia wapinzani wake kwa maana hata kule kwao ni mpinzani.

Sasa hakuonyesha any sympathy towards wapinzani "Chadema" why should Chadema support Raila Odinga?Nategemea utawaelewa Chadema
Hongera mkuu, jibu lako limeshiba,sidhani kama kuna mwenye swali tena!
 
Mwaka 2016,wakati wa uchaguzi wa kule nchini Ghana, nyinyi CHADEMA mlikuwa mkimuunga aliyekuwa mgombea wa Upinzani, Rais wa sasa wa Ghana Mhe. Nana Akufo-Addo aliyekuwa akichuana na Rais wa wakati huo, Mhe. John Dramani Mahama. Kwakuwa wote mlikuwa wapinzani, uungaji wenu mkono ulikuwa unaeleweka.

Mwaka huu, katika uchaguzi wa Kenya, CHADEMA mmemuunga mkono waziwazi Rais wa sasa wa Kenya na mgombea wa Jubilee Mhe. Uhuru Jomo Kenyatta. Ndiyo kusema, mmeunga mkono chama tawala ili kiendelee kutawala kule nchini Kenya. Mpinzani kuunga mkono chama tawala, ambacho nchini mwake anapambana kukiondoa madarakani, ni jambo la kustaajabisha.

Mwanachama wenu na Mjumbe wa Kamati Kuu, Ndugu Edward Ngoyai Lowassa amejitokeza mubashara jukwaa la Jubilee kukipigania chama tawala Kenya ili kiendelee kutawala. Kama Rais Uhuru Kenyatta atashinda tena, naye atapanda jukwaa la CHADEMA mwaka 2020 kuwanadi? Imekuwaje hadi nyinyi wapinzani muunge mkono chama tawala?

Tuamini kuwa hata Tanzania nyinyi CHADEMA mnazuga tu kupambana na chama tawala CCM huku mkiwa mnapenda CCM iendelee kuongoza? Kwakweli, CHADEMA hamueleweki kirahisi katika hili!
Yaani weww unataka vyama vya upinzani vijenge urafiki na vyama pinzani tu!!!Sasa huu si utakuwa urafiki wa muda mfupi tu!Mfano chama ambacho ni rafiki yako wew mpinzani,akishinda uchaguzi basi anageuka adui na yule mtawala aliyeangushwa ndio muanze urafiki,!!!;
 
Mazindu Msambule ,

..hoja ya mtoa mada ina matatizo.

..yeye anataka kutuaminisha kwamba CDM kwasababu hawapo madarakani hawapaswi kuunga mkono vyama au wagombea walioko madarakani.

..Ni kweli walimuunga mkono Nana Ado ambaye alikuwa "mpinzani" Ghana. Lakini sasa Nana Ado ni Raisi. Je CDM sasa wanatakiwa waachane naye waunge mkono wapinzani wake?

..Mtoa mada nadhani ameshindwa kuzingatia ukweli kwamba kwenye nchi za wenzetu vyama vya siasa hupokezana madaraka.
 
Huu ujinga umekaririshwa wapi?Huoni hata aibu kuandika upuuzi wa kiwango hiki?Yaani weww unataka vyama vya upinzani vijenge urafiki na vyama pinzani tu!!!Sasa huu si utakuwa urafiki wa muda mfupi tu!Mfano chama ambacho ni rafiki yako wew mpinzani,akishinda uchaguzi basi anageuka adui na yule mtawala aliyeangushwa ndio muanze urafiki,nonsense!!!;
Mkuu, kila mpinzani analenga kuwa mtawala. Mnapaswa kupambana mtawale. Si kuwaunga mkono watawala.
 
Mazindu Msambule ,

..hoja ya mtoa mada ina matatizo.

..yeye anataka kutuaminisha kwamba CDM kwasababu hawapo madarakani hawapaswi kuunga mkono vyama au wagombea walioko madarakani.

..Ni kweli walimuunga mkono Nana Ado ambaye alikuwa "mpinzani" Ghana. Lakini sasa Nana Ado ni Raisi. Je CDM sasa wanatakiwa waachane naye waunge mkono wapinzani wake?

..Mtoa mada nadhani ameshindwa kuzingatia ukweli kwamba kwenye nchi za wenzetu vyama vya siasa hupokezana madaraka.
Kinachoshangaza ni kuunga mkono chama tawala ambacho kinataka kuendelea kuongoza. Si dhambi kumuunga mkono mpinzani hata kama atakuwa mtawala. Nana alikuwa mpinzani, hakukuwa na tatizo na hata sasa hakuna tatizo urafiki ukiendelea. Si kuwaunga mkono Jubilee Mkuu.
 
haha kweli chadema imefulia kila mtu anaikana.
 
kueleweka kwa chadema siyo leo wala kesho.
 
Mkuu, kila mpinzani analenga kuwa mtawala. Mnapaswa kupambana mtawale. Si kuwaunga mkono watawala.

So siku ccm ikishindwa uchaguzi watavunja urafiki walionao na vyama vyote tawala duniani?????

JPM kuunga mkono upinzani Kenya,hii imekaaje?Kwanini asiwaunge mkono watawala wwnzake????

Huu ni upuuzi,Kwa chaguzi kama za marekani,unaweza kujikuta unabadili chama rafiki kila baada ya miaka 5!
 
Mkuu, kila mpinzani analenga kuwa mtawala. Mnapaswa kupambana mtawale. Si kuwaunga mkono watawala.

..but, what if chama cha upinzani kikishinda uchaguzi kama ilivyotokea Ghana?

..Je CDM sasa wanapaswa kuwapinga rafiki zao walioingia madarakani uchaguzi uliopita ili waporomoke na kuwa chama cha upinzani?!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom