CHADEMA mbona hamueleweki?

CHADEMA mbona hamueleweki?

Aisee nimecheka sana baada ya kuona mtu kaanzisha uzi akisema kwamba ushindi wa Uhuru ni ushindi wa CHADEMA.

Hawa watu naona wanaishi kwenye ulimwengu wao peke yao.

..mara nyingi vyama tawala vikishinda CCM huwa wanashangilia sana.

..nashangaa ushindi wa Uhuru Kenyatta CCM this time hawana furaha nao kabisa.

..WHY? Kuna kitu gani nyuma ya hali hii?
 
Huwa wanashangilia sana kivipi?

Kwa kupiga vigelegele na matarumbeta?
 
Hawa wazee wakubadili gia angani mmmmmh. Uhusiano wao na kenyata umeanza lini?Navojua CCM haina uhusiano wowote na NASA wala odinga. Na jpm hana uhusiano wowote na NASA zaidi ya urafiki wao na odinga tena toka jpm ni waziri.

Na mtakumbuka jpm aliwahi kwenda kwenye msiba wa mtoto wa odinga kama Rafiki yake wa karibu na sio kama mwakilishi wa CCM. Mwaka 2013 jpm alimuunga mkono odinga kama chadema walivomuunga mkono odinga. Hapa mmoja ambaye ni JPM alifanya hivo kama muendelezo wa urafiki wao na ukumbuke CCM haikua upande wa odinga na chadema walimuunga mkono odinga kama chama Rafiki. So utaona kila mmoja alimuunga mkono odinga kwa sababu zisizofanana.

Urafiki wa chadema na odinga ulianza kutetereka baada ya 2015. Odinga ni Rafiki yake magufuli na hata ka magufuli asingekuwa Rais bado urafiki wao ungeendelea tu coz urafiki wao hauko ktk mfumo wa kisiasa. Ingekuwa maajabu leo magufuli aache urafiki na odinga kisa siasa kwani wamekuwa wakishare vingi nje ya ulimwengu wa siasa.

Chadema haijawah kuwa Rafiki wa kenyata na urafiki wao hautaweza kudum na hata ukidum hautaleta impact yoyote ktk harakati zao kuelekea ikulu. Huu ni urafiki wa kumkomoa magufuli na haijawah tokea ndoa au urafiki wowote ukadum kama urafiki huo au ndoa hiyo imetokana na kulipiza kisasi au kumkomoa mtu aliyekuacha au kutofautiana naye.

Chadema hawana sababu za msingi kwanini wanamuunga mkono Kenyata .Kipindi odinga anakuja sengerema kuungana na WANACHADEMA ktk kufanya maendeleo ni kipindi hichohicho odinga ni Rafiki wa karibu wa jpm wakati yuko CCM. Je haya mahusiano hawakuyaona?je walitaka baada ya uchaguz odinga ampinge jpm?

Hakuna ccm au chama kama chama kimetoa tamko kuhusu kumuunga mgombea flani huko kenya. Ni chadema tu wamefanya hivo na kwenda kushiriki kampeni. Wao wamechagua kumuunga mkono kenyata na ili kuleta balance wameanzisha propaganda kuwa ccm inamuunga mkono odinga. Waulize ni lini hilo tamko limetoka kuwa ccm inamuunga mkono odinga?

Mimi nafikiri chadema kimepoteza dira na sasa hawajui wasimamie nini na kwann.KUWAELEWA CHADEMA mmmmmmmh Ufanye KAZI SANA.

posti fromu Nokia kitochi yuzingi jamii forum
 
mkuu cjawa mzigo ila nimekua mtaka haki-so sisi tunashindana na mkulu kwa kile anacho takaa-leo mkulu kumsapot odinga kumekua uvunjifu wa katba na kuanza vichuki ,odinga alituunga mkono ila kuna ubaya gani cc tukaonesha msimamo kuliko kuonesha vichuki,ninavo fahamu mm cc chadema tumekua watu wa kukomoa cku izii,msimamo wetu ni muhmu ili kuepuka kusto jifahamu-ukipenda ukweli hata awe mzee wako!! kosa utaliona tuu!!! au ndo tunaona kauli ya chama awezi kukosolewa basi neno demokrasia tuliondoshe,chama ni msimamo
Unaendelea kudhihirisha jinsi ulivyo mzigo,Odinga alikiri kufurahishwa na uteuzi wa Magufuli na kusema chama chake ni rafiki ws CCM,sasa unayegemea kwa akili ya kawaida CDM wamuunge mkono mtu anayemsapoti mtesi wao
 
Wanahubiri SIASA zisizo na visasi

Lakini wanapenda visasi kwa vitendo.

Zitto na Dr.Slaa hawapo

Mheshimiwa Tundu Lissu yupo bizee sana.

Mnyika anaelemewa na nguvu ya wahamiaji.

Wenye Chama wanachungulia palipo na fursa za mda mfupi.

TUWAPE MUDA NDANI YAKE WATAIBUKA WANAOELEWEKA MKUU.
 
Mwaka 2016,wakati wa uchaguzi wa kule nchini Ghana, nyinyi CHADEMA mlikuwa mkimuunga aliyekuwa mgombea wa Upinzani, Rais wa sasa wa Ghana Mhe. Nana Akufo-Addo aliyekuwa akichuana na Rais wa wakati huo, Mhe. John Dramani Mahama. Kwakuwa wote mlikuwa wapinzani, uungaji wenu mkono ulikuwa unaeleweka.

Mwaka huu, katika uchaguzi wa Kenya, CHADEMA mmemuunga mkono waziwazi Rais wa sasa wa Kenya na mgombea wa Jubilee Mhe. Uhuru Jomo Kenyatta. Ndiyo kusema, mmeunga mkono chama tawala ili kiendelee kutawala kule nchini Kenya. Mpinzani kuunga mkono chama tawala, ambacho nchini mwake anapambana kukiondoa madarakani, ni jambo la kustaajabisha.

Mwanachama wenu na Mjumbe wa Kamati Kuu, Ndugu Edward Ngoyai Lowassa amejitokeza mubashara jukwaa la Jubilee kukipigania chama tawala Kenya ili kiendelee kutawala. Kama Rais Uhuru Kenyatta atashinda tena, naye atapanda jukwaa la CHADEMA mwaka 2020 kuwanadi? Imekuwaje hadi nyinyi wapinzani muunge mkono chama tawala?

Tuamini kuwa hata Tanzania nyinyi CHADEMA mnazuga tu kupambana na chama tawala CCM huku mkiwa mnapenda CCM iendelee kuongoza? Kwakweli, CHADEMA hamueleweki kirahisi katika hili!
  • Bro hawa jamaa mi nawaelewa kilichotokea,kenya mpinzani alidai waziwazi kuwa ametengeneza system image cd from Tz.
  • Jamaa wakaona hapana kwanza stop system image to spread then fight the virus.
  • Kwa siasa za muda mrefu ujao kwao ilikuwa ni janga,hatari ni hatari hata kama inafanywa na mwenzio
 
Mwaka 2016,wakati wa uchaguzi wa kule nchini Ghana, nyinyi CHADEMA mlikuwa mkimuunga aliyekuwa mgombea wa Upinzani, Rais wa sasa wa Ghana Mhe. Nana Akufo-Addo aliyekuwa akichuana na Rais wa wakati huo, Mhe. John Dramani Mahama. Kwakuwa wote mlikuwa wapinzani, uungaji wenu mkono ulikuwa unaeleweka.

Mwaka huu, katika uchaguzi wa Kenya, CHADEMA mmemuunga mkono waziwazi Rais wa sasa wa Kenya na mgombea wa Jubilee Mhe. Uhuru Jomo Kenyatta. Ndiyo kusema, mmeunga mkono chama tawala ili kiendelee kutawala kule nchini Kenya. Mpinzani kuunga mkono chama tawala, ambacho nchini mwake anapambana kukiondoa madarakani, ni jambo la kustaajabisha.

Mwanachama wenu na Mjumbe wa Kamati Kuu, Ndugu Edward Ngoyai Lowassa amejitokeza mubashara jukwaa la Jubilee kukipigania chama tawala Kenya ili kiendelee kutawala. Kama Rais Uhuru Kenyatta atashinda tena, naye atapanda jukwaa la CHADEMA mwaka 2020 kuwanadi? Imekuwaje hadi nyinyi wapinzani muunge mkono chama tawala?

Tuamini kuwa hata Tanzania nyinyi CHADEMA mnazuga tu kupambana na chama tawala CCM huku mkiwa mnapenda CCM iendelee kuongoza? Kwakweli, CHADEMA hamueleweki kirahisi katika hili!
Mkuu ulitaka Chadema waunge mkono Raila ambaye kwenye majukwaa ya kuomba kura alikuwa akiwaambia Wakenya iwapo angeshinda angewapelekea kile kinachofanywa na Magufuli hapa, ambacho wao wanakipinga?

Nadhani, hapa ingekuwa ni issue ya kujadili kama Chadema wangemuunga mkono Raila. Sera za Raila katika uchaguzi huu ilikuwa ni kupeleka Kenya tumbuatumbua inayolalamikiwa na Chadema kwa kuwa haizingatii sheria na taratibu (?).
 
..kwenye nchi za wenzetu ambako demokrasia zao zimekomaa kuna VYAMA VYA SIASA.

..wenzetu hawana siasa changa za chama tawala vs chama upinzani.

..Chama kilichoshinda uchaguzi Ghana kilikuwa madarakani wakati wa Raisi John Kuffour.

..Raisi wa Ghana wa sasa hivi Nana Ado alijaribu kumrithi John Kuffour lakini akashindwa.

..CDM wanapaswa kuwa na VYAMA RAFIKI bila kujali vyama hivyo viko madarakani au la.

.

Laiti wangekuwa na fikra za Moyo wako Wenda tungekuwa mbali Mkuu.
 
Hawa wazee wakubadili gia angani mmmmmh. Uhusiano wao na kenyata umeanza lini?Navojua CCM haina uhusiano wowote na NASA wala odinga. Na jpm hana uhusiano wowote na NASA zaidi ya urafiki wao na odinga tena toka jpm ni waziri.

Na mtakumbuka jpm aliwahi kwenda kwenye msiba wa mtoto wa odinga kama Rafiki yake wa karibu na sio kama mwakilishi wa CCM. Mwaka 2013 jpm alimuunga mkono odinga kama chadema walivomuunga mkono odinga. Hapa mmoja ambaye ni JPM alifanya hivo kama muendelezo wa urafiki wao na ukumbuke CCM haikua upande wa odinga na chadema walimuunga mkono odinga kama chama Rafiki. So utaona kila mmoja alimuunga mkono odinga kwa sababu zisizofanana.

Urafiki wa chadema na odinga ulianza kutetereka baada ya 2015. Odinga ni Rafiki yake magufuli na hata ka magufuli asingekuwa Rais bado urafiki wao ungeendelea tu coz urafiki wao hauko ktk mfumo wa kisiasa. Ingekuwa maajabu leo magufuli aache urafiki na odinga kisa siasa kwani wamekuwa wakishare vingi nje ya ulimwengu wa siasa.

Chadema haijawah kuwa Rafiki wa kenyata na urafiki wao hautaweza kudum na hata ukidum hautaleta impact yoyote ktk harakati zao kuelekea ikulu. Huu ni urafiki wa kumkomoa magufuli na haijawah tokea ndoa au urafiki wowote ukadum kama urafiki huo au ndoa hiyo imetokana na kulipiza kisasi au kumkomoa mtu aliyekuacha au kutofautiana naye.

Chadema hawana sababu za msingi kwanini wanamuunga mkono Kenyata .Kipindi odinga anakuja sengerema kuungana na WANACHADEMA ktk kufanya maendeleo ni kipindi hichohicho odinga ni Rafiki wa karibu wa jpm wakati yuko CCM. Je haya mahusiano hawakuyaona?je walitaka baada ya uchaguz odinga ampinge jpm?

Hakuna ccm au chama kama chama kimetoa tamko kuhusu kumuunga mgombea flani huko kenya. Ni chadema tu wamefanya hivo na kwenda kushiriki kampeni. Wao wamechagua kumuunga mkono kenyata na ili kuleta balance wameanzisha propaganda kuwa ccm inamuunga mkono odinga. Waulize ni lini hilo tamko limetoka kuwa ccm inamuunga mkono odinga?

Mimi nafikiri chadema kimepoteza dira na sasa hawajui wasimamie nini na kwann.KUWAELEWA CHADEMA mmmmmmmh Ufanye KAZI SANA.

posti fromu Nokia kitochi yuzingi jamii forum
Mkuu umetoa maelezo mazuri sana,hawa jamaa wamepoteza mwelekeo kabisa,wanacheza mziki wa Lowassa kila CD anayoleta.Ukifatilia huko nyuma sera za cdm kipindi cha Slaa ndo sera za ODM,bahati mbaya au nzuri ikatokea kiongozi wa ODM - Odinga ni rafiki wa JPM toka zamani,Sasa Laigwanan kawapoteza muelekeo,wamesahau na kusapoti umafia wa Uhuru,hebu muulize mfuasi wa CHADEMA muasisi wa kikundi cha Mungiki kilichosumbua 2008 ni nani?,hapo ndo utajua kwanini Mzee Mkapa huwa anawatukana hawa jamaa..
 
Mwaka 2016,wakati wa uchaguzi wa kule nchini Ghana, nyinyi CHADEMA mlikuwa mkimuunga aliyekuwa mgombea wa Upinzani, Rais wa sasa wa Ghana Mhe. Nana Akufo-Addo aliyekuwa akichuana na Rais wa wakati huo, Mhe. John Dramani Mahama. Kwakuwa wote mlikuwa wapinzani, uungaji wenu mkono ulikuwa unaeleweka.

Mwaka huu, katika uchaguzi wa Kenya, CHADEMA mmemuunga mkono waziwazi Rais wa sasa wa Kenya na mgombea wa Jubilee Mhe. Uhuru Jomo Kenyatta. Ndiyo kusema, mmeunga mkono chama tawala ili kiendelee kutawala kule nchini Kenya. Mpinzani kuunga mkono chama tawala, ambacho nchini mwake anapambana kukiondoa madarakani, ni jambo la kustaajabisha.

Mwanachama wenu na Mjumbe wa Kamati Kuu, Ndugu Edward Ngoyai Lowassa amejitokeza mubashara jukwaa la Jubilee kukipigania chama tawala Kenya ili kiendelee kutawala. Kama Rais Uhuru Kenyatta atashinda tena, naye atapanda jukwaa la CHADEMA mwaka 2020 kuwanadi? Imekuwaje hadi nyinyi wapinzani muunge mkono chama tawala?

Tuamini kuwa hata Tanzania nyinyi CHADEMA mnazuga tu kupambana na chama tawala CCM huku mkiwa mnapenda CCM iendelee kuongoza? Kwakweli, CHADEMA hamueleweki kirahisi katika hili!
Upinzani hauna maana ya kupinga kila serikali iliyopo madarakani. Upinzani upo ili kuwepo pingamizi la sera zisizofaa. Chama chochote haijalishi kipo madarakani au lah kinaweza kuungwa mkono na wapinzani wa ndani au nje ya nchi endapo sera zake zitakubalika kwa wapinzani husika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unaendelea kudhihirisha jinsi ulivyo mzigo,Odinga alikiri kufurahishwa na uteuzi wa Magufuli na kusema chama chake ni rafiki ws CCM,sasa unayegemea kwa akili ya kawaida CDM wamuunge mkono mtu anayemsapoti mtesi wao

makamanda waliona hekma yao ni kugeuka geuka kwa kua odinga ni kigeo geo-so ondinga akigeuka na cc tuna geukaa!!!
 
...Tuamini kuwa hata Tanzania nyinyi CHADEMA mnazuga tu kupambana na chama tawala CCM huku mkiwa mnapenda CCM iendelee kuongoza? Kwakweli, CHADEMA hamueleweki kirahisi katika hili!
1100.jpg

[B]Petro E. Mselewa[/B], na wewe hueleweki...je kwa picha hii ulitaka Chadema wafanyeje? Ni swala tu la birds of feather...!
 
makamanda waliona hekma yao ni kugeuka geuka kwa kua odinga ni kigeo geo-so ondinga akigeuka na cc tuna geukaa!!!
Malengo ya urafiki yanapobadilika njia nzuri ni kuvunja urafiki,unafikiri kabla ya Julai 2015 PM Majaliwa alikuwa na imani na yupi kati ya Lowassa na Magufuli?tafuta ile clip ya wimbo "Tuna Imani na Lowassa"
 
tukiunga mkono chama tuunge ila c kwa kukosa sababu za msingi et kwa kua mkulu anaunga kono upinzani au upinzani una unga mkono serikali hiki ni chama wala c masikani kwa kua na vitu vya mihemuko naongea hili nikiwa mwana na mfuasia wa cdm -ila kwa hili cliungi mkono watakao unga waunge watakao jifahamu wataelewa
Hujui hata kile usichounga mkono! Sababu ya kutounga Mkono Odinga ipo, usidhani haipo! Nimeshakueleza kuwa sababu ni Odinga kutokuendelea kuiunga Mkono cdm! Sasa utalazimisha kuunga mkono asiyekuunga mkono? Kuna limitation za kuchagua Marafiki?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naamini jibu unalo ila unataka mjadala kidogo.

Kwa sasa Chadema wamo kifungoni,kamatakamata,zuio la mikutano,bungeni na kwingineko.

Chadema wanaamini ya kuwa anayesababisha yote haya ni JPM na pia wanajua kuwa JPM ni rafiki wa Raila.

Kwa busara ni kuwa si lazima umpinge rafiki wa adui yako lakini kuna wakati inabidi umpinge rafiki wa adui yako,na ndicho wanachofanya CHADEMA!!!!!!!!!!!
Kwa akili ya kawaida tu, mnategemea wakati wa kampeni za 2020 Kenyatta akiwa rais wa Kenya aje kwenye kampeni za upinzani Tanzania na apande jukwaa moja na Lowassa?.
 
Analosema au alofanya EL ndo jambo la CDM cause ni mali yake, alisha uziwa na mbowe. Akiwa Kenya alishatangaza atagombea urais kupitia ' chama chake CDM'
 
Sasa unataka tumuunge mkono anayeungwa mkono na dikteta? Huyo amekuwa adui yangu mara moja baada ua kuwa upande wa dikteta! Namchukia sana dikteta hivyo kamwe siwezi kumpenda rafiki yake.Nenda kaulize Lowassa alichomletea Uhuru kutoka kwa wamasai wa Kenya!
 
Tuwapinge madikteta na marafiki zao! Tuwapinge kwa nguvu zote asilani!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom