Hata alivyokuwa CCM alikuwa fisadi,ndiyo maana bunge ambalo kwa kipindi kile wabunge wengi walikuwa wa CCM walimshinikiza ajuihuzuru na akafanya hivyo,Kamati kuu ya CCM kwa kutambua ufisadi wake ilimla kichwa kwenye mbio za kugombea urais.
Ni ujinga kudhani kuwa kila anaemkosoa Rais ni mpinzani, mimi sina chama mkuu, ni mwananchi, na nikiona kuna kitu cha maana kama sakata la Lugumi linahitaji majibu, naona ni busara na hekima Rais akichukua hatua kama ambavyo amekuwa akifanya
Rais akijibu, anajibu wananchi na sio wananchama au wafuasi wa CHADEMA au chama fulani, kwani yeye ni kiongozi wa nchi, na idadi ya watu wazima ambao hawakupiga kura ni kubwa sana kuliko walioshiriki uchaguzi
Kuwa mwanaCCM na kutofautiana na mwanaCCM mwenzako hata kama ni Rais hakukuondolei sifa ya uwanaCCM bali ni dalili ya ukomavu mkubwa wa akili
Sina hamu na chadema walisema lowassa wa richimond fisadi kwa miaka nane baadaye wakasema lowassa kaonewa si ajabu kesho wakasema lugumi naye ameonewa yaani tabu tupu.
Ni mabigwa flani hivi wa kubadilisha uongo kuwa ukweli na ukweli kuwa uongo.
Ni ujinga kudhani kuwa kila anaemkosoa Rais ni mpinzani, mimi sina chama mkuu, ni mwananchi, na nikiona kuna kitu cha maana kama sakata la Lugumi linahitaji majibu, naona ni busara na hekima Rais akichukua hatua
Rais akijibu, anajibu wananchi na sio wananchama au wafuasi wa Chadema au chama fulani, kwani yeye ni kiongozi wa nchi, na idadi ya watu wazima ambao hawakupiga kura ni kubwa sana kuliko walioshiriki uchaguzi
Kuwa mwanaCCM na kutofautiana na mwanaCCM mwenzako hata kama ni Rais hakukuondolei sifa ya uwanaCCM bali ni dalili ya ukomavu mkubwa wa akili
Richmond corruption scandal
On February 7, 2008, Lowassa was forced to resign after being implicated in the Richmond Energy deal corruption scandal. This followed a parliamentary select committee report on an emergency power generation contract between the Tanzania Electric Supply Company Ltd (TANESCO), a public corporation, and a US company styled Richmond Development Company LLC of Houston, Texas. The five-member select committee, headed by Kyela MP, Dr. Harrison Mwakyembe, found the contract to have been fraudulently concluded, hence unconscionable. Richmond was contracted to provide 100 megawatts of electricity each day after a drought early in 2006 but the Richmond generators arrived late and did not work as expected. In spite of this, the government paid Richmond more than $100,000 a day.[5] Lowassa's office then influenced the government's decision to extend Richmonds contract despite advice to the contrary form TANESCO. Two other cabinet ministers who had held the energy portfolio, Dr. Ibrahim Msabaha and Nazir Karamagi were forced to resign as well.[8][9]
Lowassa however denied that his office was involved in improperly awarding a contract to US-based electricity company Richmond Development in 2006.
Wewe unayejifanya huu ndii ushaidi naomba nikulize unakumbuka mwakembe alisema ninaachia hapa siendelei kusoma kwa maslai mapana ya nchi wewe unaelewa nini hapo
Nilisikiliza majibu ya Kitwanga na Mwema na majibu yao ni mfano wa utetezi dhaifu, maana hawapingi ukweli juu ya ukakasi uliopo bali wanazalisha maswali mengine
Unajua inawezekana umesahau, ila Magufuli aliwahi kusema waziri wake akiwa na kashfa ya ufisadi atamfukuza kazi haraka. Sasa kulikoni hazungumzii 'ufisadi' wa waziri wake?
Wazee wa kuhamisha magoli katika ubora wao, hili la Lugumi likipatiwa suluhisho, litatafutwa lingine tena. Wajipange kwelikweli, bunge likimalizika, watapotea kwa muda mrefu sana. Na wakati huo watu watakuwa wanapiga kazi usiku na mchana. Upinzani ujipange haswa hii ya kutegemea temporary popularity sio silaha sahihi kwao.
Utumbuaji vijipu ndo unaendelea na siyo majipu...na yote hayo ni ku-capture minds za watu wa chini ambao mkuu anaamini ndyo wengi na wengi Hao hawajui lolote....so ili ukurudisha imani iliyokuwa imepotea kwa kwa wananchi dhidi ya serikali yao ...ndo anafanya hivyo kutumbua vijipu...ika in a real sense nadhani majipu hayawezi...ataishia kusema yaliyopita si ndwele....tuange yajayo.......
Nasema mh.mm naomba jicho lako lipeleke mahakamani....kuna watu wanafungu kwa kesi za kupewa..inaumiza sana...tena ndo Hao wewe unao waita watu wa chini....wakubwa hawafungwi hatawafanye kosa gani...
source mtanzania.Naibu katibu mkuu wa chadema ndugu salum mwalimu amesema iwapo rais john p.magufuli hatomuwajibisha mh.charles kitwanga kutokana na kuhusika kwake na suala la lugumi basi wao km chadema watapeleka hoja bungeni ya kumpigia kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu jambo litakalosababisha kuundwa upya baraza la mawaziri,katika kuwasilisha hoja ya kutokuwa na imani na waziri mkuu inatakiwa asilimia 20 ya wabunge wakubali
Yaan ww furaha yako tu livunjwe baraza la mawazir ili nchi iingie kwwnye taharuki bila sababu za mcngi?Pole saana...hupaswi kuwa kiongozi ww.Mbona hajawajibishwa kwanza lowassa na Richmond kabla hata ya kujiunga na chadema?hta hili haliwezekan pole yenu.
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema uzito wa Rais John Magufuli kumwajibisha Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga kutokana na kutajwa kuhusika na Kampuni ya Lugumi inayodaiwa kulitapeli Jeshi la Polisi, utasababisha waanze harakati za kumng’oa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema, Salum Mwalimu aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa Rais John Magufuli hana budi kuchukua hatua haraka kumwajibisha Waziri Kitwanga kama alivyofanya kwa watumishi wengine wa umma katika operesheni ya kutumbua majipu.
Waziri Kitwanga anadaiwa kuwa na hisa kwenye Kampuni ya Infosys Ips Tanzania Limited ambayo ilipewa zabuni ya kutoa huduma za kitaalamu na Kampuni ya Kimarekani ya Biometrica kuhusu uwekaji wa mashine za kielektroniki za kuchukua alama za vidole kwenye vituo 108 vya polisi. Mkataba wa kuweka mashine hizo uliingiwa kati ya Jeshi la Polisi na Kampuni ya Lugumi Enterprises ambayo ililipwa Sh34 bilioni kati ya Sh37 bilioni za mkataba, wakati kazi ya kufunga mashine hizo ilifanyika kwenye vituo 14 tu hadi wakati Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) alipofanya ukaguzi.
Hata hivyo, kampuni hiyo inadai kuwa Kitwanga, ambaye ni mmoja wa waasisi wa Infosys, alijiondoa kwenye uendeshaji tangu mwaka 2010, wakati mkataba huo ulisainiwa mwaka 2011.
Chadema bado inaona kuwa Rais Magufuli anatakiwa kumwajibisha waziri huyo wa Mambo ya Ndani. “Kama Rais akishindwa kuchukua hatua katika hili, Serikali itang’oka madarakani. Sisi Chadema tutaiondoa. Haiwezekani wakati Lugumi inachunguzwa mhusika mkuu (Kitwanga) aendelee kuwa waziri, tena wa wizara inayohusika na mkataba wa Lugumi,” alisema Mwalimu.
Mwalimu alisema, Rais anapaswa kujitokeza hadharani na kueleza uhusiano wake na Kitwanga na awaeleze Watanzania kuwa kutokana na uswahiba wao ndiyo sababu ya kutomchukulia hatua. “Mbona anawatumbua marafiki wa wenzake? Kwa nini marafiki zake anashindwa kuwatumbua? Ukiwa kiongozi mwenye kubagua katika uamuzi ni hatari kwa uchumi wa Taifa, ni sawa na baba anayewabagua watoto wake matokeo yake ni kuzalisha chuki tu.”
Licha ya Mwalimu kutotaka kuweka wazi mpango huo, kwa mujibu wa Ibara ya 53 A(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977, Bunge linaweza kupitisha azimio la kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu endapo itatolewa hoja kupendekeza hivyo.
Kwa mujibu wa Ibara hiyo, hoja ya kupiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu inapaswa kuungwa mkono na wabunge wasiopungua asilimia 20 ya wabunge wote.
Wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni 372, kati yao wabunge wa upinzani ni 118. “Hilo tutalifanya iwapo tu Rais atashindwa kumwajibisha Kitwanga. Ila huyu waziri naye anapaswa ajipime mwenyewe ili kumlinda bosi wake (Waziri Mkuu). Afanye kama Edward (Lowassa-waziri mkuu mstaafu) aliamua kujiuzulu wadhifa wake ili kumlinda Jakaya (Kikwete-Rais wa Awamu ya Nne) kwa kosa ambalo yeye hakulifanya,” alidai Mwalimu.
Mwalimu alidai kwamba Serikali imezuia matangazo ya moja kwa moja ya vikao vya Bunge kuhofia uchafu wa viongozi, likiwamo sakata la Lugumi. “Ndiyo maana tunasema CCM ni ileile maana wametumbua majipu, sasa imebaki mitoki. Ni kama imewashinda maana ipo sehemu mbaya,” alisema.
Licha ya mkakati huo wa Chadema, Aprili 19 mwaka huu, Kitwanga alisema kuwa hahusiki katika sakata hilo na juzi alijibu hoja ya Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha) lililomtaka ajiuzulu, akisema hawezi kuwajibu watoto ili kuonyesha tofauti yake na wao.
Katika maelezo yake, Mwalimu aliorodhesha utumbuaji ambao Rais Magufuli ameufanya tangu aingie madarakani, ukiwamo wa watendaji waliofanya vurugu tu katika vikao kwa kusisitiza kuwa ni ajabu kuona mpaka sasa hajamchukulia hatua yoyote Kitwanga wakati ukweli uko wazi kuwa anahusika na sakata la Lugumi. Baada ya ripoti ya CAG kuibua udhaifu huo kwenye mkataba, Kamati ya Hesabu za Serikali ya Bunge iliunda kamati ndogo kufuatilia tuhuma hizo baada ya kutoridhishwa na maelezo ya Wizara ya Mambo ya Ndani na Jeshi la Polisi kuhusu mkataba huo.
Kampuni ya Infosys ni wakala wa kampuni maarufu duniani ya kutengeneza kompyuta ya Dell, ikijihusisha na usambazaji wa vifaa hivyo, matengeneza na utoaji huduma za kitaalamu.
Kaimu katibu mkuu huyo wa Chadema alisema, chama hicho pia kinajipanga kuanza ziara yake nchi nzima na ajenda kuu itakuwa kuanika mambo yote mabaya yanayofanywa na Serikali
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.