CHADEMA: Magufuli anayo siri LUGUMI

CHADEMA: Magufuli anayo siri LUGUMI

Wananchi wanashindwa kuwaamini tena sababu mmekua vinyonga , sisi tupo na uncle magu tuna imani nae 150% piga kazi.
ww muamini na waamin wengin pia ila siasa ni mchezo na nikibiashara (bidhaa ikiwepo huwa pana nafuu kw nteja ila zikipungua nitatoz kw mtej, namaanisha siasa na wanasiasa hawaaminiki).
Nakunasihi mkuu, fanya kazi kwa bidii ili ujisaidie na uwasaidie wanafamilia yako, hao wanasias wako bize kutekeleza majukum yao kw familia zao tuu.
 
Sina hamu na chadema walisema lowassa wa richimond fisadi kwa miaka nane baadaye wakasema lowassa kaonewa si ajabu kesho wakasema lugumi naye ameonewa yaani tabu tupu.

Ni mabigwa flani hivi wa kubadilisha uongo kuwa ukweli na ukweli kuwa uongo.
Huo wimbo wenu umeishapitwa na wakatii, tungeni mpya
 
nafikiri hii issue lugumi haitawatoa mafichoni baada ya kukumbatia mafisadi sijui mtaeleza nini mueleweke sasa hivi
Wote watumbuliwe pamoja na "waliojificha huko - CHADEMA" iwapo tu unachosema kimetoka ktk akili yako timamu!!

Lugumi ni shida wewe, acha kabisa - jamaa yenu kakamatwa kunako. Atabana weeeeee........lakini mwisho wa siku ataachia tu!!
 
Jana niliweka uzi humu kuwa jpm anapambana na baadhi ya mafisadi na si ufisadi kwani ufisadi mwingine unangusa moja kwa moja
 
mi naomba na hili jipu la kivuko cha BAGAMOYO-MV DAR ES SALAAM litumbuliwe...
kununua kivuko kibovu cha mwaka 1978,kwa bilioni mbili halafu kishindwe kufanya kazi huu ni ufisadi laanifu wa kukejeli kodi za umma !
 
Lugumi ni shetan au malaika?
Swala la Lugumi sio kwamba ni yeye mwenyewe. Ingekuwa ni yeye mwenyewe wangekuwa wameshamtumbua zamani maana mi ninavyomfahm lugumi kurudisha Billion 34 sio issue, tatizo ni wale walio nyuma ya jina la lugumi kuanzia mawazir mpaka Raic wa awamu ya 4.
 
CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeeleza kuamini kwamba, Rais John Magufuli anayo siri ya Kampuni ya LUGUMI na INFOSYS hivyo anapatwa kigugumizi kuchukua hatua.

Pia chama hicho kimeeleza kwamba, ni vema Rais Magufuli ajitokeza hadharani na kuwaeleza wananchi uhusiano wake na Charles Kitwanga, Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi ambaye kampuni yake ndiyo iliyofunga vifaa vya kuchukulia alama za vidole katika Jeshi la Polisi nchini.

“Chama kina mashaka juu ya mahusiano yao kwani licha ya Kitwanga kutajwa mara kadhaa kuwa anahusika na mkataba tata wa Bilioni 37 kati ya Jeshi la Polisi na Kampuni ya LUGUMI Enterprises.

“Lakini bado ameziba masikio. Hivyo, akiendelea kuwa kimya serikali yake itaangushwa kupitia waziri mkuu wake,” Salim Mwalimu, Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA-Zanzibar.

Akizungumza na waandishi wa habari leo ofisini kwake Mwalimu amesema, inawezekana Rais Magufuli anamasilahi binafsi na kampuni hiyo na hivyo kushikwa na kigugumizi jinsi ya kutoa maamuzi.

“Ni kitu cha kushangaza sana kwamba hadi sasa bado hajatoa kauli yoyote. Yeye ni mtaalamu wa kutumbua majipu kwa kupata habari mitandaoni na kwa kusikia tu kama alivyofanya kwa Mkurugenzi wa Jiji lakini majipu yaliyokaribu yake anayaogopa,” amesema na kuongeza;

“Tunamashaka na utumbuaji majipu wake inawezekana anafanya hivyo kwa kulipiza kisasi na kuharibu urafiki wa marais waliopita, ama anajifanya kutumbua watu ili awaweke watu wake waliokuwa wakimsapoti kwenye kampeni.

“Kama kweli anafanya hakimu mbona majipu yanayomuhusu hayatumbui?” amehoji Mwalimu.

Mwalimu pia amemtaka Waziri Kitwanga ambaye anatajwa kuwa ni mmoja kati ya wamiliki wa kampuni ya INFOSYS iliyotumika kufunga mashine za kuchukua alama za vidole (AFIS) , ajitokeze kujibu tuhuma hizo ama ama ajiuzulu kwa kuwa hana sifa za kuwa Waziri tena.

“Kama bado wanafichiana siri yeye na rafiki yake basi aige mfano kwa Edward Lowassa aliyekuwa Waziri Mkuu ambaye alijiuzulu kwa kumstahi rafiki yake aliyekuwa akinuka usifisadi Rais Jakaya Kikwete. Kitwanga ajipime na ajitafakari na kujitoa kwenye uwaziri,” amesema Mwalimu.

Awali, zabuni ya mkataba huo ilitangazwa tarehe 22 Septemba 2011 na kusainiwa terehe 23 Septemba mwaka huo huo ndani ya siku moja mkataba ukasainiwa jambo ambalo ni hatari.

Kampuni ya LUGUMI Enterprises Ltd ilipewa tenda na Jeshi la Polisi kwa ajili ya kufunga mashine za kuchukua alama za vidole katika vituo 108 nchi nzima kwa gharama ya Sh 37 bilioni.Hadi sasa mashine hizo zimefungwa katika vituo 14 tu vya polisi ambapo tayari kampuni hiyo imelipwa Sh. 34 bilioni ikiwa ni asilimia 99 ya fedha za mkataba huo.
Hivi hiki chama cha chadema kinaongozwa na watu kweli? Hivi mnafikiri Mh Magufuli mnadhani ni mpumbavu kama hao viongozi wenu ambao wametawaliwa na unafiki kwa kusema kitu wasichokiamini kwa sauti kubwa. Yalifanyyika hayo kwa kumtuhumu Lowasa na Sumaye, matokeo yake wote tunajua chama na wapumbavu wake wote walianza kumsujudia Lowasa.
Mh Magufuli ni mwanasayansi haamini katika porojo zilizosemwa kwa ufundi bali huongozwa na data halisi. Ufundi wa kipumbavu umetumika kumhusisha Mh Rais na hayo yanayoongelewa ili atoe uamuzi wa papara. Upinzani wataongea sana lakini kwa serikali hii lazima upinzani utachoka tu. Mtu wa kwanza kuipokea taarifa ya CAG ni Mh Rais, aliona mkataba huo na makosa yake ya kiufundi. Huenda haukuwa na sifa yakuushindanisha kwa sababu ya unyeti wake kiusalama kama alivyojibu Mh Kitwanga bungeni
Kabla ya kampeni tuliamini Lowasa alijiudhuru. Baada ya kampeni tumejua kuwa Mh Lowasa alifukuzwa kazi, kwani aliambiwa na mH Kikwete kuwa anachaguwa waziri mkuu mpya. Kama alijiudhuru kweli kwanini alikuwa na chuki na serikali iliyoundwa kwa kutoa matamko ya hovyo. Ushahidi wa pili ni kauli ya Mzee Makamba kuwa walipoenda kumuona Mh Kikwete ili wamshawishi amuondowe Lowasa, waliambiwa kuwa amemwambia Lowasa kuwa anateuwa Waziri Mkuu mpya. Hivyo kwa sasa ni upumbavu kuendelea kuamini kuwa Lowasa alijiudhuru.
CAG kwa sababu za kiufundi huhesabu kitu kwa kuona nyaraka mbalimbali ili kuunga mkono taarifa husika za hoja za kihasibu. Upungufu wa nyaraka hizo hutia mashaka taarifa japo chombo husika kipo. Ndio maana kamati ndogo ya PAC imeenda kuangalia uwepo wa hivyo vifaa vyote kwenye hivyo vituo 108. Hii taarifa itapelekwa bungeni na watu watajua kilichotokea. Sasa ujinga wa chadema wanaona bora hii hali ibaki kimashakamashaka ili waendelee kuwa na cha kuongea vinginevyo wamechoka na kufilisika kwa hoja mpaka CAG atoe taarifa.
Swala la nyumba za serikali limekwisha tolewa maelezo na serikali toka mwaka 2007. Majibu mengi yametolewa. Kwanini sasa? Kwanza wapinzani hawana hoja ya msingi ya kuzungumza na umma ukawaelewa. Pili wanahisi umma utamchukiwa Mh Rais kwakuwa ndiye alikuwa waziri wa ujenzi wakati wa uuzwaji wa nyumba hizo. Hili wapinzani watalia sana na hawata fanikiwa.
 
Hali inabashiri Lugumi ni deal ya chama ndiyomaana kina Aishi wanazongwazongwa na viongozi wa chama na Serikali.
 
Inawezekana Magufuli siyo mpumbavu (kama ulivyoandika wewe hapo juu), bali ni "mtu wa data" na ni "mwanasayansi" asiyeamini ktk porojo!!!???

Nilicho na uhakika nacho baada ya kuisoma hii argument yako ni hiki, kuwa - likely wewe ndiye mpumbavu basi kwa sbb huoni kasoro zozote ktk utawala huu!!
 
Magufuli kwa lugumi chali hana ujanja membe alisema magufuli hatatumbuwa rafiki zake sasa tunamuona anavyokausha haha kumekucha
 
Bakiza akiba ya maneno maana haijulikani siku wala saa ya Mbowe kubadili gia angani na kumteua Lugumi kuwa mgombea urais wa chadema..
Unaniwaza au umenielewa ki UKAWA mimi nawaza kizalendo kwa Inji yangu maana Tanzania sio ya ccm wala ukawa. Achana na itikadi.
 
Back
Top Bottom