Kijana wa Bavicha katelekezwa, Chadema mna jopo la wanasheria msaidieni huyu kijana.
Ludo ni rafiki ake na lwakatare na ni private secretary wa slaa
Mkuu naona ona hoja sana, sasa mie binafsi nakuomba tinga ofisi za CDM kaulize haya yote na kaongee na viongozi alafu lete hapa jamvini. Vinginevyo hata wewe una nafasi ya kumwekea dhamana kijana mwenzako, hamasisha michango toka kwa vijana na hata watu wenye mapenzi mema, angalia vigezo vya utoaji dhamana , tinga mahakamani, utakuwa shujaa sana mkuu na utakuwa umeachana na itikadi za vyama na kufanya tendo la kiutu.WanaJF!
Leo ni siku ya kesi ya bwana Lwakatare kusikilizwa kwenye mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, lakini kesi imehairishwa mpaka July 22, 2013.
Pamoja na hayo, mshitakiwa na.2 bwana Ludovick Rwezahula ameshindwa kupata dhamana kwa sababu ya kutokamilika kwa nyaraka za dhamana, ingawa dhamana yake iko wazi kabisa.
Bwana Ludovick akiwa nje ya mahakama, ameonekana akiwa mnyonge na alikuwa akilia sana kwa uchungu huku akilalamika ndugu zake (ambao hawakufika mahakamani) hawafatilii dhamana yake.
Kwa hali kama hiyo, kijana Ludovick anaendelea kusota gerezani na kuzidi kuangamia, kwani wote sisi ni wanaadamu na tunajua makali ya maisha ya gerezani.
Rai yangu kwa CHADEMA; haijarishi kijana Ludovick kama alikuwa mwajiriwa wa CHADEMA kimkataba ama alikuwa volunteer, jambo la msingi ni kwamba alikuwa ana kitumikia CHADEMA kwa moyo wake wote na nguvu zake zote. Ludovick alijitoa kwa CHADEMA kwa namna ya pekee, ni kijana ambae alikuwa bega kwa bega na Dr Slaa kiutendaji na vile vile alikuwa kama mtoto kwa Dr Slaa.
Katika hali kama hiyo sikutarajia kama CHADEMA kinaweza kumtema na kumkataa kabisa bwana Ludovick Rwezaura. Kwani wote tunafahamu kuwa, kosa aliadhibiwi kwa ubaya, bali kosa dawa yake kukosolewa. Sasa kwanini CHADEMA wana muadhibu kijana Ludovick kwa ubaya? kwanini wasimsaidie hata kwa dhamana ili aweze kutoka kwenye 'jehanamu' ya duniani?
Maamuzi haya ya kumtupa mkono kijana Ludovick katika hali hii mbaya inayo mkabili, inajenga wasiwasi mkubwa kwa vijana wengi walio CHADEMA juu ya hatma yao endapo wakikosea jambo. Je, chama kitawasaidia kwa lolote? Ni wakati vijana wakawa makini sana na namna ambavyo CHADEMA na viongozi wake wana shughulikia nidhamu na makosa ya wanachama wao, hiki anacho fanyiwa Ludovick, hakina tofauti sana na walicho fanyiwa Juliana Shonza na Mtela Mwampamba.
View attachment 101283Kijana Ludovick akionekana amenyong'onyea leo mahakamani, pembeni yake ni bwana Lwakatare wakiwa na askari magereza.
You are NEXT.....
Tatizo lenu ni ujinga na umbumbumbu mkubwa mlionao magaidi wa chadema.
unamuongelea mabere marando na kesi ya LWAX NA LUDOVIC??? hivi una hata chembe ya sheria hata kama hujaenda shule hata siku moja??? labda nikupe tu ufunuo(revelation ) ya kile mnachofanyiwa na marando'
''wakati akiwa kama wakili wa LWAX, angetakiwa atumie uwezo wake wooote kumtoa mteja wake(LWAX) katika tuhuma zile!! yeye anahangaika kutafuta mlolongo wa watuhumiwa wengine ili waunganishwe kwenye kesi ya LWAX. kwa hiyo anachotaka yeye mahakama itambue, sio kwamba mteja wake(LWAX) hajashiriki, laa bali ni kwamba alishiriki lakini hakushiriki peke yake.mpaka sasa hajafanya jitihada zozote(za wazi na za siri) za kujaribu kumtenganisha LWAX na tuhuma bali anacement ushiriki wa LWAX katika tuhuma husika.
mbona kesi ya LWAX mwisho wake uko wazi!!! hata muweke wakili SHETANI na hakimu awe MALAIKA WA SHETANI
mwigulu malipo ni hapa hapa duniani,movies zake kipuuzi...zitamuumbua muacheni atumike huku akijiharibia sifa,sijui atakuwa mgeni wa nani siku yakimkuta.
Duh umeamua kumpa za usoni.Waliomtosa ndo wale waliomtuma akaenda angukia pua kinachopelekea yeye kuwa mahabusu.Hili jinamizi linaloitwa Hammy-D icho anachokiita Jehanamu ya dunia si imetengenezwa na magamba wenzake?Yeye alikubali kuwa toilet paper au mipira ile ambayo Mwigulu aliihitaji wakati akifanya uashereti na mke wa kada mwenzie kwa hivo Ludovick he is the master of himself on what he is facing now.Acha ale matunda ya uhuru ila Ritz si anajua au sio zamu yake kupeleka mamsosi?HAMMY-D, CCM ndio walivyo, ukishawafanyia kazi yao wanakutosa, subiri zamu yako wewe na wenzako hasa yule jamaa anayeongozana na Mwigulu kuonesha majeraha ya tindikali!
Mbona chadema imewasaliti vojana wengi tu waliopata matatizo
Bwn Hamy-D, umeeleza vizuri na ushauri mzuri pia, wewe ni ccm damu na CDM ni mpinzani wako mkubwa, comments zako humu jamvini nyingi zinaonesha pia hua unaichukia CDM, swali, Shetani anaweza kumshauri kitu kizuri mcha Mungu ili aendelee kumcha Mungu? Mlitegemea CDM wafanye kitu kwa huyo kibaraka while anti-Virus ya chadema ika detect mapema huyo virus, hilo hamkulitegemea, nendeni wenyewe mkamtoe, hakuna siri, kila mwenye akili timamu anajua kua yeye alitumika na sasa anavuna alicho kipanda, hongera zake Ludovic, matunda ya usaliti kama Yuda Iskarioti