Mkuu ngoja waje wamwage povu hapa wenyewe kina mohamed mtoi na mwita maranya
japo nina wasiwasi uwepo wa hii thread hapa jamvini dakika chache zijazo.
Ngoja nikasali thread isitolewe maana kuna maslahi ya watu yameguswa hapa.
Kwa kupunguza makali wameiunganisha haraka sana ili isionekane barazani.Mkuu ngoja waje wamwage povu hapa wenyewe kina mohamed mtoi na mwita maranya
japo nina wasiwasi uwepo wa hii thread hapa jamvini dakika chache zijazo.
Ngoja nikasali thread isitolewe maana kuna maslahi ya watu yameguswa hapa.
mwambie mwigulu akamwekee dhamana dhambi ya usaliti itawamaliza vijana wengi wenye tama na maisha ya kifahari bado mtela na shonza
Mkuu kwangu utasubili sana.we endelea kutumia id fake.
mnh! Mkuu wangu JokaKuu hapa naona umenipa historia ya mbali kweli kweli manake, sana sana hapo afadhali Makweta namfahamu angalau kwa kumsikia! Anyway, hao "walitoswa litoswa" vipi? Ni kwamba serikali ilishindwa kuwapa huduma pale walipozihitaji; au?Chris Lukosi,
..mbona CCM waliwatosa makada waaminifu, na mawaziri waandamizi,Jackson Makweta, na Chediel Mgonja?
..pamoja na hao mwingine aliyetoswa ni mkuu wa majeshi mstaafu General.Ernest Mwita Kyaro.
cc: Mchambuzi, Ritz, chama, NasDaz
Aisee!NasDaz,
..Chediel Mgonja ndiye aliyetangaza uamuzi wa Tz kuiunga mkono Biafra. wakati huo alikuwa ni waziri wa nchi Ofisi ya Raisi anayeshughulika na mambo ya nje. baada ya hapo alikuwa waziri wa elimu,na baadaye waziri wa utamaduni,na michezo. nadhani baraza la mitihani lilianzishwa akiwa waziri wa elimu. Taifa Stars iliqualify kwenda fainali za kombe la mataifa ya Afrika zilizofanyika Lagos, wakati Mgonja ni waziri wa michezo na utamaduni.
..Gen.Ernest Mwita Kiaro, alikuwa Chief of Defence Forces. Alitanguliwa na Gen.David Musuguri, na kufuatiwa na Gen.Robert Mboma. Ernest Kiaro alitumikia wakati wa utawala wa Raisi Mzee Ali Hassan Mwinyi. Sifa kipekee ya Gen.Kiaro ni kwamba alitumikia vyeo vyote jeshini, kuanzia private mpaka General. Alirushwa cheo kimoja tu cha Luteni Jenerali wakati alipoteuliwa kuwa mkuu wa majeshi.
..Jackson Makweta umesema umepata kumsikia. Kwa upande wangu nadhani ni kati ya mawaziri wa elimu waliotumikia ktk kipindi kigumu sana. Mh.Makwete ndiye aliyeanzisha mtihani wa sekondari wa kidato cha 2.
..sasa wote hao, Chediel Mgonja, Jackson Makweta, Ernest Mwita Kiaro, waliugua na serikali haikuonekana kuwajali mpaka wanafariki.
Chris Lukosi angeanza kuhoji kwanini wazee hao walitelekezwa na serikali ya CCM, kabla kuwashukia CDM na jinsi wanavyomhudumia Lwakatare. That does not imply kwamba kwamba CDM wasihojiwe.
NasDaz,Aisee!
Hakika kila mmoja ana historia yake inayosisimua....!! Nawakubali sana wanajeshi wanaopitia cheo kimoja baada ya kingine kwani mara nyingi kama sio zote wanajeshi wa aina hii wanakuwa ni wale wanaofika juu si kwa sababu ya elimu yao huku wakiwa goi goi lakini ni kwa ajili ya ukakamavu na utendaji wao jeshini....yaani, more likely wanakuwa wanajeshi mtulinga; correct me if am wrong!
Kuhusu huyo Mgonja, afadhali umenikumbusha! Naisikia sikia tu hii Biafra na Vita vyake lakini sina ufahamu nayo wa kutosha zaidi tu ya kufahamu kwamba ni somewhere in Nigeria! Kuna wakati nilitaka kuisoma historia yake, nikatingwa na mambo....afadhali umenikumbusha; ngoja niiperuzi peruzi kidogo ili nifahamu ABC yake!
YES, huyu Makwetta, namfahamu kidogo ingawaje sifahamu alikuwa ni kiongozi wa namna gani hasa! Sina uthubutu wa kumwongelea vizuri huyu bwana....lakini nazani hadi wakati wa Mwinyi, alikuwapo! Anyway, wakati huo nao flow of information haikuwa mzuri sana na ndio maana hata kama tayari tulikuwa na akili/ufahamu; lakini hatukupata fursa ya kufahamu mengi; unless mzee wako awe mnunuzi wa Uhuru na Mzalendo; au Mfanyakazi...!
JokaKuu,NasDaz,
..Statement ya Tanzania kuitambua Biafra hii hapa:
Tanzania
..Makweta, alianza na Nyerere. Aliteuliwa na Mwinyi kuwa waziri wa elimu. kwa mtizamo wangu he did a lot ukizingatia hali ya uchumi ya wakati ule. Hata kwa nafasi ya ubunge nadhani wananchi wa Njombe wanamkubali, ingawa wanadai mwishoni alikuwa king'ang'anizi.
JokaKuuChris Lukosi,
..mbona CCM waliwatosa makada waaminifu, na mawaziri waandamizi,Jackson Makweta, na Chediel Mgonja?
..pamoja na hao mwingine aliyetoswa ni mkuu wa majeshi mstaafu General.Ernest Mwita Kyaro.cc: Mchambuzi, Ritz, chama, NasDaz
Nilijua tu, ili kupunguza makali lazima ifutwe au iunganishwe na thread nyingine
Hii tabia ya kufagia uchafu chini ya kapeti iko siku mchwa watajenga sebuleni kwenu
Mkuu Chris Lukosi
Tatizo la mods wamegueka watumishi wa Chadema yaani wanalazimisha mambo mengi sana kuzima hoja; ukitukanwa na kamanda unyamaze kimya ukijibu wanapiga ban sasa kama NJAA nipo tayari kulipa mods wawili wa jukwaa hili ili watoe maamuzi ya haki; wanatia aibu sana yaani na wenyewe wamekubali kutumika kama pedi mimi hata wakipiga na wapige lakini kunyamaza kwa kuogopa ban hilo siwezi.
chama,JokaKuu
Hebu tukumbushe watu hao walitoswa vipi? Chadiel Mgonja na Makweta walikuwa wabunge hata nyadhifa zao zilitokana na ubunge kama wananchi waliwakataa kwa njia ya kura ulitaka CCM ifanye kitu gani? Na Mzee Kyaro hebu lielezee jukwaa kama mkuu wa majeshi mstaafu alikosa haki ipi?
chama,
..hawa walitoswa na CCM na serikali yeke wakati wakiwa wagonjwa kwa namna hiyohiyo ambayo Chris Lukosi anadai CDM imewatosa makada wake.