CHADEMA kweli ni shwari au ni kauli za kisiasa tu ?

Ndugu ThinkTwice

Mkwawa, Mirambo, Mputa,Rumanyika, Mangi Sina, Mandara, n.k walikuwa viongozi wazuri na hawakuwa na shule yeyote leader is born, and we all have such ability naturaly because real leadership starts at home!

Inategemea sana wewe unachoita elimu ni kitu gani. Mbona Mwungwana hakuona vyumba vya darasa lakini kesha itwa Dokta mara mbili mbili? Babu yangu alinifundisha namna ya kutengenezea migomba { prooning} hata migomba ikazaa vizuri sana lakini hakuwa na cheti chochote cha shule za kilimo za wazungu. By the way what is education?? Labda tukishapata definition ndiyo tunaweza kuchangia kama huyu jamaa alikuwa nayo elimu au la!
 
Tangia kampeni kuanza za uchaguzi mkuu, Ndg. Slaa alikuwa peke yake kwenye kampeni bila ya kusaidiwa na Mgombea mwenza, tofauti na vyama vingine, je huu sio ubinafsi?. Na habari za uhakika zilizozopo ni kuwa Mgombea mwenza wa Slaa alikuwa na elimu ya darasa la 7 tu, ili hali yeye mwenyewe alikuwa anahubiri elimu ya awali iwe ni form six. Hivi alichokuwa anakisema ndicho alichokuwa anakimaanisha kweli ? inakuwaje utuletee mgombea mwenza wa darasa la 7 ili hali wewe wahubiri elimu ya awali ni form six ?. Huu ni upotoshaji dhahiri ambao CDM waliufanya kwa wananchi, na yaonyesha Slaa alichokuwa anakisema sicho ambacho angetenda endapo angepata urais. Bora Mungu alituepushia mbali mtu huyu !

Hili jambo lilifafanuliwa wakati wa kampeni, lakini kwa kuwa wewe ni mwepesi wa kusahau ua mvuvi wa kufaatilia mambo kwa wakati ngoja nikusaidie. Katiba inayotumika kwa sasa katika Jumhuri ya Muungano inatamka wazi wazi kwamba sifa za mtu atakegombea Ubunge, Urais ina maana hata mgombea mweza ni kujua kusoma na kuandika katika Kiswahili au Kiengereza. Haijataja mtu anatakiwa awe emeenda shule mpaka darasa la ngapi. Hivyo basi hata kama mtu ajaenda shule kabisa lakini anajua kusoma na kuandika katika kiswahili au Kiengereza huyu anaweza kugombea nafasi ya uongozi. Kwa ushahidi zaidi soma Katiba hiyo ibara ya 67 (1) (a). Mwisho wa mjadala.
 
Magazeti yote ya leo yameandika kilicho jiri kwenye mkutano wa wabunge wa CHADEMA uliofanyika kule Bagamoyo. Tutizame yaliyojiri kwa ufupi :

  1. Shibuda kukwidana na Wenje na kutangaza rasmi kuwa atakwenda mwanza kumshitaki kwa wapiga kura kuwa mbunge wao hana adabu , na aheshimu wazee wa kisukuma
  2. Zitto kabwe kung’olewa katika nafasi ya Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni
  3. Wabunge wa CHADEMA kugawanyika kuhusu kususia hotuba ya JK
  4. Shibuda atishia kukihama chama na kusema ushindi wake wa Jimbo la Maswa ulitokana na umaarufu wake na wala siyo CHADEMA
  5. Shibuda awaambia CHADEMA haina haja ya kudai katiba wakati chenyewe hakiendeshwi kwa kufuata katiba
  6. Shibuda amwambia Lissu kuwa hana sababu ya kuwashambulia wenzani kwani hata yeye anayo maovu mengi ambayo watu wanayajua ingawa hawayasemi
  7. Godbless Lema amwambia Shibuda kuwa ni pandikizi la CCM kwa kuwa anatambulika hivyo mkoani Arusha
  8. Shibuda aamini kuwa CHADEMA si Chama, bali ni kikundi cha watu, waliokuwa na misimamo yao kutoka nyumbani, na hawako tayari kujadiliana

Kwa hali hii CHADEMA kweli ni shwari au ni kauli za kisiasa tu ?
 
Mie niliisha yasema haya kitambo kuwa kwa mizizi hii ya CHADEMA wanayo iotesha ya kutumia udini, ukabila, upendeleo na ubinafsi katu hawawezi kuwa chama sahihi cha kisiasa cha kuiondoa CCM madarakani. Kwa hii hali CCM itatutawala milele. Na haya mliyo yaona ni ya firauni tu , ya Mussa yanakuja, wait !!!
 
Kama shibuda kasema na marehemu Chacha alisema ninapata uhalisia kuwa kuna baadhi ya ukweli na mengine yanaweza kutokuwa kweli...CDM kuweni makini
 
Chadema hakuna ushwari. Mbowe na Slaa, kwa kuwa hawa wote ni system, wameshapewa amri ya kukisambaratisha. Amini usiamini. Vyama vya siasa Tanzania vichukulie kama Simba na Yanga, walaaa usiwe na hamasa.
 
Hivi inawauma nini? Kajichimbieni huko CCM.
 
..Shibuda ana tabia za kitemi-temi huyo.

..alishawahi kushikana mashati na Kikwete kabla hajaukwaa uraisi.

..Chadema wanapaswa kuwa makini sana na jinsi wanavyom-handle.
 
Kwa wote tunaochangia thread hii ya kipumbavu wote tuko hopeless na tumetumwa kuja kuichafua CHADEMA na Viongozi wake!!! sure, I should tell you kuwa hamtafanikiwa hata chembe instead mnakiimarisha CHADEMA bila ya nyinyi kujua!

Hii mbinu mnayotumia haiwezi kukubalika maana mliisha itumia kuiua NCCR MAGEUZI, mkawagombanisha, mkawasaidia mliotaka waiyumbishe lakini CHADEMA hamtaweza.
CHADEMA iliisha mfukuza Katibu wake mkuu Warid Kaburu haikuyumba, iliishabadilisha viongozi wakuu mara kadhaa haikuyumba, iliisha tumiwa mamluki kwenye uchaguzi wa baraza la wanawake haikuyumba, iliisha pata majarabio kwenye uchaguzi wa Baraza la Vijana ikabaki salama, sasa haya mnayoleta sasa ni marudio, wala CHADEMA haitatingishika!
 
MWANALUGALI....unaongea kama msimamo wa chama au ushabiki?....mimi nimshabiki na mpenzi watimu ya SIMBA ya dar-es-salaam.....hata ifungwe 10-0 na yanga ama timu yeyote, hata iuze wachezaji wote...hata viongozi wawe wabovu kiasi gani MIMI NI SIMBA NA SIMBA NI MIMI....lakini naamini siasa haina kanuni hii niiamniyo mimi.....THE WHIRLWIND IS NOW SWEEPING ACCROSS CHADEMA
 
Mie niliisha yasema haya kitambo kuwa kwa mizizi hii ya CHADEMA wanayo iotesha ya kutumia udini, ukabila, upendeleo na ubinafsi katu hawawezi kuwa chama sahihi cha kisiasa cha kuiondoa CCM madarakani. Kwa hii hali CCM itatutawala milele. Na haya mliyo yaona ni ya firauni tu , ya Mussa yanakuja, wait !!!

CUF imesambaratishwa kwa udini hasa huku bara zanzibar imeshindikana coz dini moja imeoccupy about 99% ya Zanzibar yote. Sasa wanakuja CHADEMA wameingia na gia Ukabila wameshindwa, Sasa wanakuja na hii ya udini ambayo watashindwa haswa kwa kitendo chao cha kumtumia Rais na Spika wahubiri kuwa kuna udini. Watashindwa kwa kweli watabaki na aibu kama mahimbo alivyojidhalilisha kwenye kesi ya kudai mke wa slaa.
 
Wadau nimefuatilia kwa makini kipindi hiki baada ya uchaguzi na kugundua kwamba sasa CHADEMA wapo kwenye 'kutibu' vijidonda vya uchaguzi kwa vijembe vya hapa na pale kwa serikali na pia ndani ya chadema hasa suala la Zitto kupewa nafasi kubwa zaidi ya hoja za msingi.

Ukiangalia upande wa NCCR ni kama wanapitia mlango ule ambao chadema wanatokea kwa kuanza ku-raise ishu za msingi kama ile ya kafulila juu ya Ngeleja na hili la Leo la kusudio la kupeleka hoja bungeni kuhusu katiba mpya ambayo wao wanadai ndiyo waanzilishi wa vuguvugu hilo huku wakipewa bonge la sapoti na tbc ambayo inawafikia wanachi wengi kupita magazeti,internet etc. CHADEMA wamekaa pembeni na mjadala mkubwa ni ZITTO na matatizo yake..

Je kujenga hoja kwa mtindo wa kuwahi kutoa kusudio la kupeleka mijadala bungeni na hatimaye kujadiliwa NCCR wataleta picha gani kwa watanzania?? assume ajenda yao ikapita,watanzania watawapa pride gani??..na je huo utakuwa mwanzo wa watanzania kuwaamini tena na kuimwaga CHADEMA??

Nawasilisha....
 
NCCR hawana chochote isipokuwa wanajifanya kuwahisha hoja. Hoja ya Katiba ilikuwa ya CDM ambapo mgombea urais wake alizunguka nalo Tz nzima wakati wa kampeni. NCCR wanaposema kuwa wao ni waasisi wa hoja ya katiba siwaelewi. Hoja isiwe nani ni mwasisi bali kama wao wanaona katiba mpya ni muhimu inatosha si lazima wasema wao ni waasisi.

Hili suala la chama fulani kujidai kuwa muasisi wa kitu fulani ni kama CCM nao waliposema kuwa hoja ya kupinga ufisadi ni hoja yao baada kuona kuwa hoja hiyo inakubalika kwa wananchi.
 
Hii ni kwa wote wanaoleta hoja za ajabu hapa JF za kuichokonoa CDM. Vyama vipo kibao lakini kukicha CDM. Mbona UDP, NCCR, TLP, CUF wapo lakini hawaongelewi? Chokochoko nyingi humu ndani zinaletwa na Mafisadi tunhakuna wengine. Tuiache CDM ifanye kazi sasa uchaguzi umepita.
 
Back
Top Bottom