Ritz
JF-Expert Member
- Jan 1, 2011
- 56,762
- 46,273
KATIBU Mkuu wa Waziri Mkuu wa Kenya, Carol Omondi, aliungana na wakazi wa Wilaya ya Nyamagana na kuchangisha kiasi cha Sh50.6 milioni kwa ajili ya kusaidia kumaliza tatizo la madawati kwa Shule za Msingi na Sekondari wilayani humo.
Katika harambee hiyo iliyoandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Nyamagana kwa tiketi ya Chadema, Ezekia Wenje, kupitia mfuko wa maendeleo ya elimu Nyamagana (NEF), Katibu huyo aliandamana na mtoto wa Raila Odinga, Fidel Odinga aliyeweza kuchangia Sh2 milioni.
Mgeni rasmi katika harambee hiyo alikuwa ni Katibu wa Waziri Mkuu wa Kenya Raila Odinga, Carol Omondi, akiwa ameongozana na marafiki zake ambao walichangia fedha za Kenya Sh. laki 6 ambazo ni sawa na Sh. milioni 12 za Tanzania.
Mtoto wa Odinga na Katibu wa Odinga walipewa mualiko na Chadema.