Neema ya BWANA
Senior Member
- Jun 25, 2023
- 129
- 61
Kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, ninapenda kuzungumzia kipengele kimoja kilichonivutia zaidi katika Ilani ya mwaka 2020-2025 ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA); Sura ya 16, Kifungu namba 16.1 Kipengele b (Ukurasa wa 95) ambacho kinasema:
"Katika kutimiza azma ya kujiendeleza katika sekta ya sayansi na teknolojia, Serikali ya Chadema itaweka mkazo katika kuimarisha mahusiano yanayolenga kuiwezesha Tanzania kuiga na kuchota maendeleo ya kiteknolojia yaliyofikiwa katika nchi za Asia na hasa China."
Kipengele hiki ni muhimu sana kwa taifa letu, kwani tunafahamu sote kuwa China ni taifa lililopiga hatua kubwa katika Maendeleo ya Sayansi na Teknolojia duniani; yaliyopelekea uchumi wake kukua kwa kasi kubwa na kuwa imara zaidi.
Ingawa lengo hili lilitolewa na CHADEMA kupitia Ilani yake ya uchaguzi ya mwaka 2020-2025, lakini tukiamua kuweka kando vyama vyetu, dini zetu na ubaguzi wa aina yoyote ile tukabaki kuwa Watanzania ambao ni Wazalendo tunaolitakia mema taifa letu; haijalishi Ilani hii inakaribia kumaliza muda wake, lakini lengo hili linaweza kuhuishwa upya na kutekelezwa nasi sote kuanzia Serikali iliyopo madarakani, Chama Tawala (CCM), Mimi, Wewe, Watanzania, Taasisi, Mashirika, Vyama vya Upinzani na CHADEMA wenyewe haijalishi wako ndani au nje ya Serikali; kupitia SEKTA BINAFSI.
Ni uwekezaji wa aina gani unaweza kulifaa lengo hili?
Taguchi ni nini?
Taguchi ni njia za kitakwimu ambazo zilivumbuliwa na Mjapani aitwaye Genichi Taguchi ili kuongeza thamani ya ubora (quality) wa ubunifu wa bidhaa zinazozalishwa viwandani na katika nyanja mbalimbali kama vile Uhandisi, Bioteknolojia, Masoko, TEHAMA, Mawasiliano, Uchukuzi, n.k.
Sababu ya mimi kuona kuwa maeneo haya matatu yanafaa zaidi katika uwekezaji huu ni kutokana na Elimu, Ujuzi na Maarifa kuwa moja kati ya nyenzo kuu zilizowafanya Wachina wapige hatua kubwa kwenye Maendeleo ya Sayansi na Teknolojia kisha Uchumi duniani.
Mfano; kupitia Falsafa ya Kichina iitwayo CONFUCIANISM iliyoanzishwa na 'Kong Qiu' au 'Zhong Ni' maarufu kama Master Kong, Kong Fuzi au Confucius (551-479 BCE) inayotumika kwenye nyanja maalum nchini humo ambazo ni Utamaduni, Jamii, Biashara na Siasa.
Confucianism ni nini?
Confucianism ni Falsafa ya Kichina yenye lengo la kurejesha, kujaza, kuhamasisha na kuimarisha tabia njema kwenye jamii ya Kichina; ili kuibua matokeo mema na chanya kwenye jamii za Kichina yatakayojidhihirisha dunia nzima. Hakika leo hii sote tunashuhudia mema haya yaletwayo na taifa la China. Falsafa hii ya Kichina inafundisha kuhusu tabia njema mbalimbali kama ifuatavyo:-
REN Confucian
Upendo, Utu na Huruma
YI Confucian
Haki na Kufanya Matendo ya Haki
LI Confucian
Kuwa na mpangilio mzuri wa jambo unalofanya ikiwemo kufuata kanuni au mfumo. (System or Proper Way)
ZHI Confucian
Kuyatafsiri Maarifa, Hekima, Ujuzi na Elimu uliyonayo haijalishi udogo au ukubwa wake; ili yatumike katika kufanya maamuzi sahihi, kujua lipi ni sahihi na lipi si sahihi, kufanya ubunifu (innovation), kuwaza kwa hekima, kufanya uchambuzi na ku-judge mambo kwa hekima.
Kwa tafsiri rahisi, ZHI ni Hekima kwa Vitendo; ku-apply kile ulichonacho kwa kufanya kitu kipya. Hii imepelekea Wachina kuwa watu wenye uthubutu wa kufanya mambo makubwa zaidi duniani.
XIN Confucian
Katika Falsafa ya Kichina; XIN ni Ukweli, Uaminifu na Kutovunja Ahadi. Maneno yaliyonyooka, matendo yaliyonyooka pasipo kupepesa macho na kufanya kile ulichoahidi kufanya ni sehemu ya Utamaduni wa Kichina.
Xin inajenga urafiki, uhusiano na inasimama kama tabia moyo (muhimu zaidi) kwenye Utamaduni wa Kichina.
Ndiyo iwe Ndiyo!
Hapana iwe Hapana!
XIN Confucian inaibua tamaduni nyingine za Kichina ambazo ni Guanxi pamoja na Mianzi. Guanxi ni ujenzi wa Uhusiano Mzuri (Good Relationship or Friendship) ambao ni binafsi, wa kibiashara, wa kijamii, wa kisiasa, n.k. Namna bora ya kujenga Guanxi kwa Wachina ni kwa njia ya kukutana Uso kwa Uso kupitia vikao, mikutano, kutembeleana, kukaribishana, n.k.
Kutengeneza Guanxi ni mchakato wa muda mrefu; mfano ni ule niliowashauri CHADEMA kurudi kwa jamii kwenye andiko langu lililopita. Kujenga Guanxi kunachochea kuibuka kwa Mianzi (Face) Gaining.
Mianzi (Face) Gaining ni kitendo cha kufanya jitihada za kuleta neema na mambo yaliyo mema kwa mwingine ili kulinda 'Social Image' yake. Unapofanya mabaya kwa mwingine maana yake unaharibu 'Social Image' yake; na kwenye Utamaduni wa Kichina huitwa Mianzi (Face) Loosing; ambapo Mianzi Loosing hupelekea kubomoa Guanxi.
XIAO Confucian
Hii ni namna watoto na vijana wa Kichina wanapaswa kuwahudumia wazazi na wakubwa wengine kwenye familia na jamii zao. Kupitia tabia hii njema ya Xiao Confucian, Wachina hufundishwa kuwasikiliza wakubwa, kutumia lugha laini wazungumzapo na mkubwa, kuwasalimia wakubwa, kuwafariji wakubwa kwa maneno na vitendo hasa pale wanapopitia changamoto mbalimbali, kuwahudumia wakubwa kwa fedha na mahitaji mengine, heshima kwa wakubwa, n.k. katika familia na jamii zao.
WEN Confucian
Hii ni sanaa za amani ambazo hutumiwa ili kuleta maendeleo ya mtu binafsi. Confucius (Kong Fuzi) aliamini kuwa sanaa ina nguvu ya kubadili maisha ya mwanadamu. Katika Wen Confucian; sanaa zilizozungumziwa zaidi ni sanaa za Kiutamaduni za China kama via Calligraphy (Sanaa ya Uandishi wa Mkono kwa kutumia mwandiko mzuri), Music (Muziki), Numeracy (Namba au Hesabu), n.k.
Hitimisho
Mpaka sasa nchini Tanzania ipo Taasisi ya Kichina iitwayo Confucius inayopatikana kwenye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM); iliyojikita katika kufundisha Lugha ya Kichina kwa Watanzania.
Ingawa taasisi hii imeleta nuru kwa kufundisha lugha iliyo katika nafasi za juu sana ulimwenguni kwa sasa; mapungufu ya taasisi hii ni kuwa haijachota elimu nzima-nzima iliyobeba maendeleo ya kiteknolojia yaliyofikiwa katika Nchi ya China na kuileta Tanzania, hivyo suluhu ni vyema kuanzisha Shule Binafsi za Mitaala ya Kichina na kuzalisha vitabu vinavyohusu China kwa Lugha ya Kiswahili nchini Tanzania.

- Eneo la kwanza la uwekezaji unaoweza kufanyika kupitia lengo hili ni kuanzisha shule binafsi za kimataifa (International Schools) zenye mitaala (mtaala) ya Kichina inayolenga sanaa, ubunifu, sayansi na teknolojia nchini Tanzania; kuanzia ngazi ya malezi (daycare), awali, msingi, sekondari mpaka elimu ya kati (college) kwani tayari tumekwishaona mitaala kutoka magharibi kama vile Cambridge na International Baccalaureate (IB) ikifanya kazi nchini.
- Eneo la pili la uwekezaji unaoweza kufanyika kupitia lengo hili ni kuwekeza katika Uandishi Bunifu na kuandika vitabu vipya kwa Lugha ya Kiswahili vyenye kuelezea na kuvumbua siri za mafanikio ya China pamoja na bunifu mbalimbali zinazofanyika nchini humo kama vitabu vya ziada kwa wanafunzi ambao hawataweza kusoma katika shule zilizoelezewa katika kipengele namba 1 lakini pia vitabu vinavyoweza kusomwa na mtu yeyote kwenye jamii ya Tanzania.
- Eneo la tatu la uwekezaji unaoweza kufanyika kupitia lengo hili ni kutafsiri vitabu vya Historia ya China na Vitabu vya Taguchi za Kichina vilivyopo katika lugha ya Kichina ili viwe katika Lugha ya Kiswahili kama vitabu vya ziada kwa wanafunzi ambao hawataweza kusoma katika shule zilizoelezewa katika kipengele namba 1 lakini pia vitabu vinavyoweza kusomwa na mtu yeyote kwenye jamii ya Tanzania.
Taguchi ni nini?
Taguchi ni njia za kitakwimu ambazo zilivumbuliwa na Mjapani aitwaye Genichi Taguchi ili kuongeza thamani ya ubora (quality) wa ubunifu wa bidhaa zinazozalishwa viwandani na katika nyanja mbalimbali kama vile Uhandisi, Bioteknolojia, Masoko, TEHAMA, Mawasiliano, Uchukuzi, n.k.
Sababu ya mimi kuona kuwa maeneo haya matatu yanafaa zaidi katika uwekezaji huu ni kutokana na Elimu, Ujuzi na Maarifa kuwa moja kati ya nyenzo kuu zilizowafanya Wachina wapige hatua kubwa kwenye Maendeleo ya Sayansi na Teknolojia kisha Uchumi duniani.
Mfano; kupitia Falsafa ya Kichina iitwayo CONFUCIANISM iliyoanzishwa na 'Kong Qiu' au 'Zhong Ni' maarufu kama Master Kong, Kong Fuzi au Confucius (551-479 BCE) inayotumika kwenye nyanja maalum nchini humo ambazo ni Utamaduni, Jamii, Biashara na Siasa.
Confucianism ni nini?
Confucianism ni Falsafa ya Kichina yenye lengo la kurejesha, kujaza, kuhamasisha na kuimarisha tabia njema kwenye jamii ya Kichina; ili kuibua matokeo mema na chanya kwenye jamii za Kichina yatakayojidhihirisha dunia nzima. Hakika leo hii sote tunashuhudia mema haya yaletwayo na taifa la China. Falsafa hii ya Kichina inafundisha kuhusu tabia njema mbalimbali kama ifuatavyo:-
REN Confucian
Upendo, Utu na Huruma
YI Confucian
Haki na Kufanya Matendo ya Haki
LI Confucian
Kuwa na mpangilio mzuri wa jambo unalofanya ikiwemo kufuata kanuni au mfumo. (System or Proper Way)
ZHI Confucian
Kuyatafsiri Maarifa, Hekima, Ujuzi na Elimu uliyonayo haijalishi udogo au ukubwa wake; ili yatumike katika kufanya maamuzi sahihi, kujua lipi ni sahihi na lipi si sahihi, kufanya ubunifu (innovation), kuwaza kwa hekima, kufanya uchambuzi na ku-judge mambo kwa hekima.
Kwa tafsiri rahisi, ZHI ni Hekima kwa Vitendo; ku-apply kile ulichonacho kwa kufanya kitu kipya. Hii imepelekea Wachina kuwa watu wenye uthubutu wa kufanya mambo makubwa zaidi duniani.
XIN Confucian
Katika Falsafa ya Kichina; XIN ni Ukweli, Uaminifu na Kutovunja Ahadi. Maneno yaliyonyooka, matendo yaliyonyooka pasipo kupepesa macho na kufanya kile ulichoahidi kufanya ni sehemu ya Utamaduni wa Kichina.
Xin inajenga urafiki, uhusiano na inasimama kama tabia moyo (muhimu zaidi) kwenye Utamaduni wa Kichina.
Ndiyo iwe Ndiyo!
Hapana iwe Hapana!
XIN Confucian inaibua tamaduni nyingine za Kichina ambazo ni Guanxi pamoja na Mianzi. Guanxi ni ujenzi wa Uhusiano Mzuri (Good Relationship or Friendship) ambao ni binafsi, wa kibiashara, wa kijamii, wa kisiasa, n.k. Namna bora ya kujenga Guanxi kwa Wachina ni kwa njia ya kukutana Uso kwa Uso kupitia vikao, mikutano, kutembeleana, kukaribishana, n.k.
Kutengeneza Guanxi ni mchakato wa muda mrefu; mfano ni ule niliowashauri CHADEMA kurudi kwa jamii kwenye andiko langu lililopita. Kujenga Guanxi kunachochea kuibuka kwa Mianzi (Face) Gaining.
Mianzi (Face) Gaining ni kitendo cha kufanya jitihada za kuleta neema na mambo yaliyo mema kwa mwingine ili kulinda 'Social Image' yake. Unapofanya mabaya kwa mwingine maana yake unaharibu 'Social Image' yake; na kwenye Utamaduni wa Kichina huitwa Mianzi (Face) Loosing; ambapo Mianzi Loosing hupelekea kubomoa Guanxi.
- Unapomtukana mwingine hii katika Utamaduni wa Kichina ni Mianzi Loosing inayopelekea kubomoka kwa Guanxi.
- Unapomzungumzia mwingine vizuri awe yupo au hayupo hii katika Utamaduni wa Kichina huitwa Mianzi Giving ambayo hupelekea Kujengeka kwa Guanxi.
- Kama wewe ni mwanasiasa na hukufanya kile ulichoahidi kwa wanachi wako hii katika Utamaduni wa Kichina huitwa Mianzi Loosing ambayo hupelekea kubomoka kwa Guanxi.
- Kama una rafiki yako na umeamua kumualika nyumbani kwako aje kula chakula cha jioni hii katika Utamaduni wa Kichina huitwa Mianzi Giving ambayo hupelekea kujengeka kwa Guanxi.