Duh,kumbe kafulila ni presidential material kwako?Huu ni unafiki wa hali ya juu toka kwa Mzee Mtei. Hivi kweli Mzee Mtei anaweza kutuambia kuwa hajui kuwa Mbowe hatagombea urais 2010? Ina maana yote yaliyoandikwa magazetini, JF n.k, ya Mbowe kurudi kwenye ubunge hakuyaona na kumfanya amuulize mkwe wake niaje?
Mtei anafahamu wazi kuwa mgombea uraisi haibuki tu bila kuwa amejijengea umaarufu. Walio maarufu CHADEMA either wanapigwa vita au hawagombei kwa sababu zisizojulikana.
Mbowe si maarufu tena ukiachilia kwa baadhi tu ya mashabiki wa CHADEMA. Kwa hiyo ni wazi kuwa kwenye ligi ya uraisi Mbowe hayumo tena na ndio maana ameamua kukimbilia kwenye ubunge ili ajijenge kwa ajili ya 2015.
Ni wazi pia kuwa, yeyote atakayewekwa kugombea 2010, atakuwa msindikizaji tu au mtu wa kupasha moto hicho kiti kinachoandaliwa na Mtei 2015 kwa ajili ya mkwe wake Mbowe.
Ndio maana wale vijana wengine wote ambao 2015 watakuwa tayari kwa uraisi na hivi sasa wanataka nafasi za uongozi ndani ya CHADEMA, k.m. Kafulila na Zitto, ambazo zingeweza kuwajenga ndani na nje ya chama kwa ajili ya kugombea uraisi, wanapigwa vita na Mzee Mtei na mkwe wake. Kwa Mzee Mtei uraisi ni wa Mbowe tu na atafanya lolote kumlinda mkwewe kwenye hilo. Hii ndiyo demokrasia ya sera ya majimbo.