Chadema kusimamisha mgombea wa Urais 2010; si lazima Mbowe! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema kusimamisha mgombea wa Urais 2010; si lazima Mbowe!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kanda2, Nov 22, 2009.

 1. k

  kanda2 JF-Expert Member

  #1
  Nov 22, 2009
  Joined: Apr 22, 2007
  Messages: 1,318
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Na Hemed Kivuyo, Arusha

  MUASISI wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema), Edwin Mtei amesema kuwa endapo mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe hatagombea urais mwaka 2010 basi chama hicho kitamsimamisha mgombea mwingine ambaye atakuwa imara kama alivyo Mbowe.

  Mtei aliyasema hayo hivi karibuni alipokuwa akizungumza na Mwananchi Jumapili, nyumbani kwake nje kidogo ya Arusha mjini.

  Alisema hayo mara baada ya kuulizwa mustakabali wa chama hicho kumpata mgombea wa kiti cha urais huku aliyetarajiwa kugombea kiti hicho, Freeman Mbowe kutaka kugombea ubunge katika moja ya majimbo mkoani Kilimanjaro .

  Mtei alisema kuwa kama mwenyekiti huyo ameamua au ataamua kugombea kiti cha ubunge anaamini kuwa ndani ya chama hicho kuna hazina ya viongozi `weledi` ambao hawapatikani katika chama kingine cha siasa hapa nchini.

  ``Endapo Mbowe atagombea kiti cha ubunge nitamuunga mkono na kwenda kumpigia kampeni kwa kuwa naamini ni kiongozi mwenye uwezo wa kuongoza katika nyanja mbalimbali kutokana na uzoefu alioupata katika siasa nchini,``alisema.

  Alisema kuwa kutokana na taarifa hizo, wananchi wasishangae kuona chama hicho kikimsimamisha kiongozi mwingine atayegombea kiti cha urais na kwamba atakuwa na uwezo wa kuongoza nchi na kutekeleza ilani ya chama hicho.

  Alisema kuwa pamoja na hayo nia ya chama hicho kwa sasa ni kuongeza nguvu bungeni, kwa kuwa na idadi kubwa ya wabunge ambao watawapigania Watanzania katika kukiondoa chama tawala CCM na kupigania maslahi ya taifa zima.

  ''Mimi naamini ndani ya Chadema kuna hazina kubwa ya viongozi shupavu na kama Mbowe atagombea ubunge pia tunampa nguvu kwa kuwa ana uwezo mkubwa wa kuongoza na wananchi wasiwe na wasiwasi nia yetu ni moja na tutawapa mgombea urais shupavu,'' alisema Mtei.


  NIMESHINDWA KUELEWA KAULI YA MZEE WA CHADEMA MTEI KUWA KAMA MBOWE HATAGOMBEA URAIS 2010,BASI ATATAFUTWA MGOMBEA MWINGINE KWA AJIRI YA NAFASI YA URAIS 2010.

  HIVI CHADEMA TAYARI MNA MTU AMBAYE ANA HAKI YA KUWA MGOMBEA URAIS BILA KUPITISHWA NA KIKAO CHOCHOTE CHA WANACHAMA WA CHADEMA, ZAIDI YA RIDHAA YA MZEE MTEI?

  MKISOMA MWANACHI MTAONA HABARI YOTE.
  http://www.mwananchi.co.tz/newsrids.asp?id=16147
   
 2. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #2
  Nov 22, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  hivi wewe mbona unawashwa sana na mambo ya CHADEMA??cha ajabu nini mbona nyerere alikuwa anaamua nani awe rais na nani asiwe ?umesahau alishinikiza jina na macelela litolewe katika wagombea??achana na CHADEMA bana
   
 3. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #3
  Nov 22, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Our political culture is that of a chairman of a party running for president. Usually it is the party chairman who runs for president unless otherwise stated. So sioni ajabu hapa. Hata kwa CCM mgombea wao wa uraisi eventually anakua mwenyekiti wa chama.
   
 4. B

  Baija Bolobi JF-Expert Member

  #4
  Nov 22, 2009
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 931
  Likes Received: 697
  Trophy Points: 180
  Kanda
  Mbona ukiona habari ya Chadema unaweweseka?
  Nafuu ya Usultani wa Chadema kuliko Umungu-mtu wa CCM.
   
 5. 911

  911 Platinum Member

  #5
  Nov 22, 2009
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 761
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 60
  Tatizo mnanukuu mstari mmoja wa maelezo then unaanzishia mada.Soma habari yote,Mtei alikuwa akijibu swali kuwa inasemekana Mbowe akajitosa kugombea ubunge na asigombee urais.Sasa kanda2 hapohapo anakuja na mambo ya ooh sultan na bla bla nyingine.
   
 6. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #6
  Nov 22, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,844
  Likes Received: 1,110
  Trophy Points: 280
  Hivi kulikuwa na haja ya kuanzisha thread hii?

  Ushabiki wa kisiasa, kidini, kikabila ndo unaoshusha hadhi ya jamvi letu. Tulipaswa kujadili na kutoa mwelekeo wenye manufaa kwa taifa. Sasa limekuwa jamvi la majungu, visasi na personal attacks.
   
 7. M

  Magezi JF-Expert Member

  #7
  Nov 22, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Hii thread haina mashiko
   
 8. M

  Mkandara Verified User

  #8
  Nov 22, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Whaaaat?.....
   
 9. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #9
  Nov 22, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Kwa nini haina mashiko?
   
 10. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #10
  Nov 22, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  washabiki utawajua tu...wanapenda kusikia thread zinazomsifia kilaza wao..duh
   
 11. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #11
  Nov 22, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  wewe na u bright wako umekupeleka wapi?yes ni kilaza but he is far ahead of you..then who is kilaza between you and him??
   
 12. Kilasara

  Kilasara JF-Expert Member

  #12
  Nov 22, 2009
  Joined: Dec 21, 2008
  Messages: 578
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mzee Mtei ametamka kwamba Chadema kuna wanachama wanaoweza kugombea urais endapo Freeman Mbowe hatataka kusimama. Mbona wanaJF wengine mnafadhaishwa na kudhani huyu mzee ndiye analazimisha mambo? Anapenda chama alichoasisi kishinde, na hiyo ndiyo sababu ya kumheshimu.

  Kila Mtanzania ana haki ya kuwa na jina la kiongozi anayem rate kuwa ataweza kuongoza nchi. Hata Kanda2 ana haki hiyo. Kwa hiyo Mzee Mtei ana mtu au watu katika Chadema anaowa rate ni presidential material hata kama mkwewe Freeman hatasimama.
   
 13. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #13
  Nov 23, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Mkuu I don't like it but that is the fact. Niambie vyama vingapi vya upinzani vimewahi kusimamisha mgombea wa uraisi ambae siyo mwenyekiti wap. Niambie ni mara ngapi CCM raisi akawa mtu mmoja na mwenyekiti wa chama akawa mtu mwingine. Sasa kama kila mtu anafanya hivyo si vyema kuisolate chama kimoja kwa kufanya kitu hicho hicho. Kama hatupendi tabia ya mwenyekiti kuwa mgombea uraisi basi tukemee kwa vyama vyote.
   
 14. U

  Upanga Senior Member

  #14
  Nov 23, 2009
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 135
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Tuchape Kazi!!! nadhani Mzee Mtei hayo yalikuwa maoni yake kwa kuwa anaamini hata MBOWE asipogombea watampata mwingine badala yake na wala hajataja nani anatakiwa kugombea nafasi ya u-rais.Hii inaonyesha ni jinsi Chama kilivyo na hazina ya Wagombea na inaondoa ile fikra ya kudhani nisipokuwa mimi basi hakuna mwingine.
   
 15. W

  WildCard JF-Expert Member

  #15
  Nov 23, 2009
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Mama Senkoro yule aliyegombea Urais kwa tiketi ya PPT Maendeleo hakuwa mwenyekiti hata Dr Mvungi yule wa NCCR-MAGEUZI naye hakuwa mwenyekiti. Ujue hata CCM, JK hakuwa Mwenyekiti wakati anagombea Urais 2005!
   
 16. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #16
  Nov 23, 2009
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,686
  Likes Received: 21,951
  Trophy Points: 280
  "NIMESHINDWA KUELEWA KAULI YA MZEE WA CHADEMA MTEI KUWA KAMA MBOWE HATAGOMBEA URAIS 2010,BASI ATATAFUTWA MGOMBEA MWINGINE KWA AJIRI YA NAFASI YA URAIS 2010'.


  Ndio mkuu Kanda2, CHAKAZA ataomba ridhaa ya CHADEMA kugombea. Jee umeridhika sasa?
   
 17. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #17
  Nov 23, 2009
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  NIMESHINDWA KUELEWA KAULI YA MZEE WA CHADEMA MTEI KUWA KAMA MBOWE HATAGOMBEA URAIS 2010,BASI ATATAFUTWA MGOMBEA MWINGINE KWA AJIRI YA NAFASI YA URAIS 2010.

  HIVI CHADEMA TAYARI MNA MTU AMBAYE ANA HAKI YA KUWA MGOMBEA URAIS BILA KUPITISHWA NA KIKAO CHOCHOTE CHA WANACHAMA WA CHADEMA, ZAIDI YA RIDHAA YA MZEE MTEI?

  MKISOMA MWANACHI MTAONA HABARI YOTE.
  http://www.mwananchi.co.tz/newsrids.asp?id=16147[/QUOTE]
  Kanda2
  kweli wewe kichwa maji.
  Mzee Mtei hajasema kwamba Mbowe ana haki ya kugombea Urais mwakani na wengine hawana.Wote tunafahamu kwamba Mbowe ndiye aliyegombea 2005 na tulitarajiandiye angegombea 2010 na ndio maana hata humu JF hili limekuwa likijadiliwa sana na hata wengine kushauri Dk Slaa ndio agombee 2010 kwani yeye ana haki peke yake? Na hata kwa upande wa chama chako CCM tunafahamu JK ndiye atakayegombea 2010 kwani yeye ana haki?Acha uvivu wa kufikiri Bwana Mkubwa.
  Kila mmoja ana haki ilimradi tu atimize matakwa ya kikatiba ya chama husika na ya nchi pia.
   
 18. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #18
  Nov 23, 2009
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
   
 19. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #19
  Nov 23, 2009
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Sio kweli kwa sasa na ndio maana hata Zitto aliamua kugimbea uenyekiti wa chama akijua fika kwamba mwakani hata gombea urais kwani umri wake usingemruhusu kwa mujibu wa katiba ya nchi.labda vyama vingine lakini sio CHADEMA.
   
 20. Kubwajinga

  Kubwajinga JF-Expert Member

  #20
  Nov 23, 2009
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,190
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Huu ni unafiki wa hali ya juu toka kwa Mzee Mtei. Hivi kweli Mzee Mtei anaweza kutuambia kuwa hajui kuwa Mbowe hatagombea urais 2010? Ina maana yote yaliyoandikwa magazetini, JF n.k, ya Mbowe kurudi kwenye ubunge hakuyaona na kumfanya amuulize mkwe wake niaje?

  Mtei anafahamu wazi kuwa mgombea uraisi haibuki tu bila kuwa amejijengea umaarufu. Walio maarufu CHADEMA either wanapigwa vita au hawagombei kwa sababu zisizojulikana.

  Mbowe si maarufu tena ukiachilia kwa baadhi tu ya mashabiki wa CHADEMA. Kwa hiyo ni wazi kuwa kwenye ligi ya uraisi Mbowe hayumo tena na ndio maana ameamua kukimbilia kwenye ubunge ili ajijenge kwa ajili ya 2015.

  Ni wazi pia kuwa, yeyote atakayewekwa kugombea 2010, atakuwa msindikizaji tu au mtu wa kupasha moto hicho kiti kinachoandaliwa na Mtei 2015 kwa ajili ya mkwe wake Mbowe.

  Ndio maana wale vijana wengine wote ambao 2015 watakuwa tayari kwa uraisi na hivi sasa wanataka nafasi za uongozi ndani ya CHADEMA, k.m. Kafulila na Zitto, ambazo zingeweza kuwajenga ndani na nje ya chama kwa ajili ya kugombea uraisi, wanapigwa vita na Mzee Mtei na mkwe wake. Kwa Mzee Mtei uraisi ni wa Mbowe tu na atafanya lolote kumlinda mkwewe kwenye hilo. Hii ndiyo demokrasia ya sera ya majimbo.
   
Loading...