Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,470
- 911,174
Wasiwasi wangu serikali ya CCM itawafanyia mikwala mizito na kuwanyima vibali kwa sababu CCM inategemea mtaji huo huo wa Nyerere kuendelea kuwarubuni wapigakura:-
Endapo Chadema itafanya kweli maandamano hayo itakuwa ni mara ya kwanza kwa chama hicho kikongwe cha upinzani kuweza kuongoza wanachama na mashabiki wake kutoa shinikizo la kisiasa kwa chama tawala. "Wiki ijayo watu ndio watajua juu ya nguvu ya umma" amesema mwaandaji huyo.
Baadhi ya vioongozi wa CHadema ambao wanatajwa kuhutubia mkutano huo mkubwa ni pamoja na Mbowe, Zitto, na mgombea wa Urais Dr. Willibrod Slaa ambaye anatarajia kutoa tamko hilo kwa niaba ya chama chake. Siku na Mahali pa kuanzia maandamano hayo na kuishia bado panajadiliwa na mara vikiwa tayari taarifa itatolewa kwa umma.