Elections 2010 CHADEMA kuitisha Maandamano Makubwa wiki ijayo

Wasiwasi wangu serikali ya CCM itawafanyia mikwala mizito na kuwanyima vibali kwa sababu CCM inategemea mtaji huo huo wa Nyerere kuendelea kuwarubuni wapigakura:-

Endapo Chadema itafanya kweli maandamano hayo itakuwa ni mara ya kwanza kwa chama hicho kikongwe cha upinzani kuweza kuongoza wanachama na mashabiki wake kutoa shinikizo la kisiasa kwa chama tawala. "Wiki ijayo watu ndio watajua juu ya nguvu ya umma" amesema mwaandaji huyo.


Baadhi ya vioongozi wa CHadema ambao wanatajwa kuhutubia mkutano huo mkubwa ni pamoja na Mbowe, Zitto, na mgombea wa Urais Dr. Willibrod Slaa ambaye anatarajia kutoa tamko hilo kwa niaba ya chama chake. Siku na Mahali pa kuanzia maandamano hayo na kuishia bado panajadiliwa na mara vikiwa tayari taarifa itatolewa kwa umma.
 
Maandamano ni kuwasilisha mawazo ya watu kwa vitendo!
Chadema mikoani tunawaungeni mkono, usalama na amani vitawale!
 
Mwanzo wa kufilisika huko! Teh teh teh! :tonguez:

Mnaitana kujitokeza kwa wingi, sasa huo wingi wenu kwenye maandamano ndiyo utasaidiaje kuongeza kura zenu siku ya uchaguzi? Mweee!

Maandamano mema! Tarehe 31 Oktoba maumivu kama kawa! Teh teh teh!
 
Tujitokeze wote ili kutoa msg ya kuonesha chama kukubalika licha ya uhuni wa kuchakachua matokeo feki ya redet
 
Wakuu nitakuwepo Dar kati ya 09/10/2010 mpaka 18/10/2010 utafikiri mi mchawi kwenye maandamoni nitashiriki mkimwona mzee na mkongojo mjuwe ni mimi.shime tushiriki wote kwa pamoja bila kujali vitisho vya vyombo vya dola.
 
This is a very excellent move CHADEMA has taken. This will be a blow to the CCM.

Tunasubiri kwa hamu.
 
Nadhani hizi ni propaganda kujaribu kuwatia wasiwasi ccm, hapa Tutambiwa yamekataliwa kwa sababu kuna dalili za uvunjifu wa amani na chadema wataazia hapo kulalamika jinsi wananavyoonewa.

You're really a great thinker... unafikiri tofauti sana na wengine wenye bongo dhaifu
 
Sina imani na Zitto, kwanza kuna tetesi kwa sasa anamiliki Hummer au ndio kinua mgongo cha mbunge au kutetea kununa mitambo ya Dowans kinyume na sheria au ndio matunda ya kuwa kwenye tume ya madini?

Mkuu maandamano ni mtu au watu?
 
Good idea.Natamani kwenda na mtoto wangu wa miaka minne ili ajifunze mapema kuwa nchi hii sio monarch! Na nguvu za wananchi kuleta maendeleo!
 
Kuna taarifa ambazo zimeingia muda si mrefu ujao ambapo Chama cha Demokrasia na Maendeleo kinaandaa maandamano makubwa na ya kihistoria yatakayolitikisa Jiji la Dar wiki ijayo, wiki ya maadhimisho ya Siku ya Nyerere.

Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali maandamano hayo yataongozwa na uongozi mzima wa Taifa wa Chadema chini ya Mwenyekiti Mbowe ambaye siku za karibuni amekuwa akiwasihi wananchi kuondoa woga wa kusimamia wanachokiamini.

"Mwenyekiti Mbowe ataongoza maandamano hayo akiwa pamoja na Mgombea wetu wa Urais, wagombea wote wa Ubunge na viongozi wengine waandamizi" amesema mmoja wa watu wenye kuandaa maandamano hayo.

Kiongozi huyo ambaye amekataa kutajwa jina lake kwa sababu taarifa hizo hazijatangazwa rasmi amesema kuwa "lengo la maandamano hayo ni kutaka kutoa tamko la kihistoria kuhusu uchaguzi huu mkuu ikiwa ni pamoja na kuuthibitishia ulimwengu kuwa Chadema iko tayari kushika madaraka mwaka huu na kwamba itafanya hivyo kwa njia za amani kabisa".

Kwa mujibu wa vyanzo vingine CHadema inaandaa maandamano hayo ikiwa ni majibu kwa wale wenye kudai kuwa chama hicho hakiko tayari kuongoza. Akijibu swali la tamko wanalopanga kutoa mmoja wa waandaji wa maandamano hayo amesema kuwa "tamko hilo ni silaha yetu ya ushindi ambayo itaiweka siasa za Tanzania katika kiwango kingine kabisa na litatolewa na viongozi wote wa juu wa CHadema".

Endapo Chadema itafanya kweli maandamano hayo itakuwa ni mara ya kwanza kwa chama hicho kikongwe cha upinzani kuweza kuongoza wanachama na mashabiki wake kutoa shinikizo la kisiasa kwa chama tawala. "Wiki ijayo watu ndio watajua juu ya nguvu ya umma" amesema mwaandaji huyo.


Baadhi ya vioongozi wa CHadema ambao wanatajwa kuhutubia mkutano huo mkubwa ni pamoja na Mbowe, Zitto, na mgombea wa Urais Dr. Willibrod Slaa ambaye anatarajia kutoa tamko hilo kwa niaba ya chama chake. Siku na Mahali pa kuanzia maandamano hayo na kuishia bado panajadiliwa na mara vikiwa tayari taarifa itatolewa kwa umma.

Kaka,

U mean unawashauri wafanye hivi ili kutia msisitizo wa kampeni ya kisaikolojia... Natumai utapanda ndege na familia yako mje mshiriki ladha ya siasa hizi....Vilevile angalia tu maandamano kama haya Dar yasije yakasadifisha jungu la kuwa chadema ni chama cha dini fulani ama kama wasemavyo hivi sasa hapa Dar, ni chama cha wakuja....chonde jamani na hizi desparate moves
 
Watu wote wenye mapenzi mema na nchi yetu tujitokeze bila woga katika maandamano hayo
 
Sina imani na Zitto, kwanza kuna tetesi kwa sasa anamiliki Hummer au ndio kinua mgongo cha mbunge au kutetea kununa mitambo ya Dowans kinyume na sheria au ndio matunda ya kuwa kwenye tume ya madini?
Hapo penye RED Tupo pamoja. Mimi mtu huyu simwamini kabisaaaaaaaaaaaaaaa
 
Nadhani hizi ni propaganda kujaribu kuwatia wasiwasi ccm, hapa Tutambiwa yamekataliwa kwa sababu kuna dalili za uvunjifu wa amani na chadema wataazia hapo kulalamika jinsi wananavyoonewa.

Kama itafanyika Octoba 14 kama inavyopangwa na CHADEMA lazima watanyimwa kibali maana najua kisingizio kitakachotolewa ambacho ni kuwa, ''hatuna askari wa kutosha kulinda usalama maana wamepelekwa butiama kulinda usalama wakati wa shughuli za kuzima mwenge wa uhuru''.
 
kwa mwendo huu chaguzi zijazo zitakua zinafanyika kabla ya October 14.... maana wama chetu kitatumia kila mbinu kukwepesha siku hii maalum

Natumai CHADEMA mtaonyesha uzalendo kwa kutotumia siku hii ya Mwalimu kwa ajili ya siasa ama maslahi ya chama.

Kumbukeni kuwa miaka yote mmekuwa mstari wa mbele kupigania kuwa Mwalimu Nyerere ni zaidi ya maslahi ya watu fulani, kundi fulani ama vyama fulani na kuwa siku ama nafasi yake katika taifa letu isichakachuliwe na partisan politics.....

Chonde wandugu, Mwalimu ni nguzo pekee ya Utanzania ambayo hawa jamaa hawajaweza kuiangusha nanyi msiwe wamoja katika jitihada zao....

Siku ya Mwalimu Nyerere isigeuzwe wala kutumika kwa kampeni za kisiasa ama kivyama, ni siku ya Watanzania na Tanzania. Ni siku ya watanzania kujikumbusha misingi yetu na sio vijembe na propaganda za kimakundi. Ni siku ya kuwezesha some sense of sanity to rule over this insanity eroding our nation. Ni mujibu wa kila anayelilia UZALENDO kuilinda na kuitukuza kwa dhati na sio kwa kufanikisha maslahi yake binafsi ama kundi lake....Ni siku ambayo inahitaji UMAKINI na UWAJIBIKAJI wa Watanzania wote bila ya kujali mitizamo ama matamanio yao kisiasa ama kidini...
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom