Elections 2010 CHADEMA kuitisha Maandamano Makubwa wiki ijayo

Good news

kuna taarifa ambazo zimeingia muda si mrefu ujao ambapo chama cha demokrasia na maendeleo kinaandaa maandamano makubwa na ya kihistoria yatakayolitikisa jiji la dar wiki ijayo, wiki ya maadhimisho ya siku ya nyerere.

Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali maandamano hayo yataongozwa na uongozi mzima wa taifa wa chadema chini ya mwenyekiti mbowe ambaye siku za karibuni amekuwa akiwasihi wananchi kuondoa woga wa kusimamia wanachokiamini.

"mwenyekiti mbowe ataongoza maandamano hayo akiwa pamoja na mgombea wetu wa urais, wagombea wote wa ubunge na viongozi wengine waandamizi" amesema mmoja wa watu wenye kuandaa maandamano hayo.

Kiongozi huyo ambaye amekataa kutajwa jina lake kwa sababu taarifa hizo hazijatangazwa rasmi amesema kuwa "lengo la maandamano hayo ni kutaka kutoa tamko la kihistoria kuhusu uchaguzi huu mkuu ikiwa ni pamoja na kuuthibitishia ulimwengu kuwa chadema iko tayari kushika madaraka mwaka huu na kwamba itafanya hivyo kwa njia za amani kabisa".

Kwa mujibu wa vyanzo vingine chadema inaandaa maandamano hayo ikiwa ni majibu kwa wale wenye kudai kuwa chama hicho hakiko tayari kuongoza. Akijibu swali la tamko wanalopanga kutoa mmoja wa waandaji wa maandamano hayo amesema kuwa "tamko hilo ni silaha yetu ya ushindi ambayo itaiweka siasa za tanzania katika kiwango kingine kabisa na litatolewa na viongozi wote wa juu wa chadema".

Endapo chadema itafanya kweli maandamano hayo itakuwa ni mara ya kwanza kwa chama hicho kikongwe cha upinzani kuweza kuongoza wanachama na mashabiki wake kutoa shinikizo la kisiasa kwa chama tawala. "wiki ijayo watu ndio watajua juu ya nguvu ya umma" amesema mwaandaji huyo.


Baadhi ya vioongozi wa chadema ambao wanatajwa kuhutubia mkutano huo mkubwa ni pamoja na mbowe, zitto, na mgombea wa urais dr. Willibrod slaa ambaye anatarajia kutoa tamko hilo kwa niaba ya chama chake. Siku na mahali pa kuanzia maandamano hayo na kuishia bado panajadiliwa na mara vikiwa tayari taarifa itatolewa kwa umma.
 
Back
Top Bottom