Elections 2010 CHADEMA kuitisha Maandamano Makubwa wiki ijayo

Wasisahau kuomba kibali toka kwa RPC anayehusika...

Hilo ni la muhimu maana ndio sheria ilivyo. Sitegemei kama wataamua kufanya bila kutoa taarifa maana Chadema sio kundi la "wahuni". Ni chama halali cha kisiasa.
 
tujiandae kwa maandamo wazalendo wa kweli, kila mmoja aandae bango lake akielezea hisia zake coz naamini si kila mtu ataweza kuwa kwenye jukwaa, bango linatosha kujivunia hapo baadae kuwa umesaidia nchi yako. tuachane kulumbana na hawa kina malaria sugu, kudadadeki, kibunango, mwafrika.........
 
Sidhani kama maandamano haya yataruhusiwa na kile kitengo maarufu cha CCM kinachoitwa "vyombo vya dola" maana umati utakaohudhuria utawamaliza nguvu kabisa mafisadi wa chama filisi na kuona mwaka huu hata wizi hautawafikisha kokote.
 
Go Go Go, chadema Go Go hakuna kurudi nyuma hadi kieleweke. Hapo ndo tunazika kabisa ccm.
 
kwa mwendo huu chaguzi zijazo zitakua zinafanyika kabla ya October 14.... maana wama chetu kitatumia kila mbinu kukwepesha siku hii maalum
 
"lengo la maandamano hayo ni kutaka kutoa tamko la kihistoria kuhusu uchaguzi huu mkuu ikiwa ni pamoja na kuuthibitishia ulimwengu kuwa Chadema iko tayari kushika madaraka mwaka huu na kwamba itafanya hivyo kwa njia za amani kabisa".

siku ya kumuenzi Nyerere na lengo la hayo maandamano mbona tofauti kidogo.
 
Sidhani kama watazuiwa kwani kufanya hivyo watawapa sababu Chadema kusema hata maadhimisho ya mwalimu Nyerere, vyombo vya Usalama au CCM wameyazuia..
Ila itakuwa vizuri kama Chadema watawaalika viongozi wa vyama vingine pia kuihudhuria maandamano hayo ya Kitaifa. Ni wakati wa kuungana pamoja hata kama wazo limetolewa na Chadema...
Bila shaka Mafisadi wataingia mitini.
 
Kuna taarifa ambazo zimeingia muda si mrefu ujao ambapo Chama cha Demokrasia na Maendeleo kinaandaa maandamano makubwa na ya kihistoria yatakayolitikisa Jiji la Dar wiki ijayo, wiki ya maadhimisho ya Siku ya Nyerere.

Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali maandamano hayo yataongozwa na uongozi mzima wa Taifa wa Chadema chini ya Mwenyekiti Mbowe ambaye siku za karibuni amekuwa akiwasihi wananchi kuondoa woga wa kusimamia wanachokiamini.

"Mwenyekiti Mbowe ataongoza maandamano hayo akiwa pamoja na Mgombea wetu wa Urais, wagombea wote wa Ubunge na viongozi wengine waandamizi" amesema mmoja wa watu wenye kuandaa maandamano hayo.

Kiongozi huyo ambaye amekataa kutajwa jina lake kwa sababu taarifa hizo hazijatangazwa rasmi amesema kuwa "lengo la maandamano hayo ni kutaka kutoa tamko la kihistoria kuhusu uchaguzi huu mkuu ikiwa ni pamoja na kuuthibitishia ulimwengu kuwa Chadema iko tayari kushika madaraka mwaka huu na kwamba itafanya hivyo kwa njia za amani kabisa".

Kwa mujibu wa vyanzo vingine CHadema inaandaa maandamano hayo ikiwa ni majibu kwa wale wenye kudai kuwa chama hicho hakiko tayari kuongoza. Akijibu swali la tamko wanalopanga kutoa mmoja wa waandaji wa maandamano hayo amesema kuwa "tamko hilo ni silaha yetu ya ushindi ambayo itaiweka siasa za Tanzania katika kiwango kingine kabisa na litatolewa na viongozi wote wa juu wa CHadema".

Endapo Chadema itafanya kweli maandamano hayo itakuwa ni mara ya kwanza kwa chama hicho kikongwe cha upinzani kuweza kuongoza wanachama na mashabiki wake kutoa shinikizo la kisiasa kwa chama tawala. "Wiki ijayo watu ndio watajua juu ya nguvu ya umma" amesema mwaandaji huyo.

Baadhi ya vioongozi wa CHadema ambao wanatajwa kuhutubia mkutano huo mkubwa ni pamoja na Mbowe, Zitto, na mgombea wa Urais Dr. Willibrod Slaa ambaye anatarajia kutoa tamko hilo kwa niaba ya chama chake. Siku na Mahali pa kuanzia maandamano hayo na kuishia bado panajadiliwa na mara vikiwa tayari taarifa itatolewa kwa umma.

Sina imani na Zitto, kwanza kuna tetesi kwa sasa anamiliki Hummer au ndio kinua mgongo cha mbunge au kutetea kununa mitambo ya Dowans kinyume na sheria au ndio matunda ya kuwa kwenye tume ya madini?
 
Sina imani na Zitto, kwanza kuna tetesi kwa sasa anamiliki Hummer au ndio kinua mgongo cha mbunge au kutetea kununa mitambo ya Dowans kinyume na sheria au ndio matunda ya kuwa kwenye tume ya madini?
Kwa hiyo unataka asiwepo kwenye maandamano?
 
HIMAAAAAA! TANZANIAAAAAAA!! SHIMEEEEEEE! TANZANIAAAAAAA!!
Jamani muda wa mabadiriko ndo huu, bila shaka tunahitaji mabadiriko ya kweli, hainiingii akirini kwa wadogo zetu na wanetu kukaa chini na kula vumbi wakimsikiliza mwalimu darasani huku kukiwa na methali nzuri kuwa elimu haina mwisho, elimu ni mwanga!!! Hivi mtoto atakubaliana vp na misemo hii ikiwa kila ki2 anakiona kuwa ni uzushi na uongo mkubwa kuwa ninalojifunza ni kupotezewa muda! Sasa basi huu ndo muda wa mabadliko na Dr Slaa'ndo jemedari wa hilo.
 
Kama kweli kuna mpango wa kufanya hayo maandamano, basi yana uzito mkubwa kuliko wengi wanavyodhani.

  • (1) It could bring matters to a head. Yaani yanaweza yakaleta UMATI mkubwa Dar es Salaam wa watu ambao wameichoka kabisa CCM na wakaitaka CCM iachie madaraka SASA. UMATI uliokasirika unaweza kufanya lolote. CCM haijui watu walivyoichoka.
  • Shimbo, Mwema na maswahiba wengine wa Kikwete wanaweza kukataza maandamano. Kwa vile CHADEMA lazima ionyeshe Dunia inafanya shughuli zake kwa kufuata tu sheria za nchi na haiwezi kukandamizwa na vibaraka, itakataa kuwatii Mwema na Shimbo. Sasa kwa vile nchi nzima inapenda mabadiliko, hakutakuwepo tena na haja ya kusubiri Oktoba 31.
  • Kama CCM wanapenda amani, itabidi wawaachie CHADEMA haki yao ya kikatiba ya kufanya maandamano. Ila ukubwa wa maandamano na yatakayosemwa pale vitakuwa vimeimaliza kabisa CCM.
A well coordinated CHADEMA rally in Dar would deal CCM a fatal blow. Watabaki na huu upupu wao wa REDET wa kusema wameshinda kura za maoni wakati kura huru ZOTE za maoni ameshinda Slaa kwa karibu 75%. Vibaraka wote wataingia aibu mwaka huu.
 
Thanks Mzee Mwnakijiji,
Ni jambo la busara na linatakiwa kuchukuliwa kwa hali ya tahadhari sana kwasababu watu wamepigika sana kwahiyo kitendo cha kufanya maandamano ni kuudhihirishia ulimwenguni kuwa CHADEMA NI CHAMA MBADALA NA CCM NA WAKO TAYARI KUONGOZA NCHI.
Chadema ina wafuasi wenye elimu ya upeo mkubwa sana wa kuongoza nchi,nyuma ya pazia kuna wafuasi wengi sana wa CHADEMA walioko CCM,
Kwahiyo sidhani kama CHADEMA ikishika DOLA itashindwa kusimamia majukumu ya kiserekali na kusimamia Ahadi ambazo ni muhimu kuzitekeleza.
Kwamfano Ahadi ya Elimu bure na Afya bure ,lazima uwe na kiongozi makini,serekali makini ili uweze kuitekeleza.na inawezekana kabisa.kama kila mtu atafanya kazi kwa juhudi na maarifa na kwa technolojia mpya basi tutafika mbali na karibu na malengo ya MDG.
 
Tunashukuru kwa taarifa mwanakijiji,Chadema wakifanya hivyo itaendelea kuleta mwamko wa mageuzi!Chadema keep it up!
 
Kuna tofauti kati ya malengo ya maandamano, mada zinazotegemewa kuongelewa na siku yenyewe.

Ukiangalia madhumuni hii si lingine bali ni kampeni ya Uchaguzi.

Polisi siyo tatizo ila wanaweza wasiruhusiwe kwani NEC watasema hii ni kampeni ambayo haipo katika ratiba.
 
"lengo la maandamano hayo ni kutaka kutoa tamko la kihistoria kuhusu uchaguzi huu mkuu ikiwa ni pamoja na kuuthibitishia ulimwengu kuwa Chadema iko tayari kushika madaraka mwaka huu na kwamba itafanya hivyo kwa njia za amani kabisa".

siku ya kumuenzi Nyerere na lengo la hayo maandamano mbona tofauti kidogo.
hakuna tofauti mazee... ni utayari tu wa kuyaenzi aliacha baba wa taifa na kuchakachuliwa na wenye nchi yao
 
Kuna taarifa ambazo zimeingia muda si mrefu ujao ambapo Chama cha Demokrasia na Maendeleo kinaandaa maandamano makubwa na ya kihistoria yatakayolitikisa Jiji la Dar wiki ijayo, wiki ya maadhimisho ya Siku ya Nyerere.

Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali maandamano hayo yataongozwa na uongozi mzima wa Taifa wa Chadema chini ya Mwenyekiti Mbowe ambaye siku za karibuni amekuwa akiwasihi wananchi kuondoa woga wa kusimamia wanachokiamini.

"Mwenyekiti Mbowe ataongoza maandamano hayo akiwa pamoja na Mgombea wetu wa Urais, wagombea wote wa Ubunge na viongozi wengine waandamizi" amesema mmoja wa watu wenye kuandaa maandamano hayo.

Kiongozi huyo ambaye amekataa kutajwa jina lake kwa sababu taarifa hizo hazijatangazwa rasmi amesema kuwa "lengo la maandamano hayo ni kutaka kutoa tamko la kihistoria kuhusu uchaguzi huu mkuu ikiwa ni pamoja na kuuthibitishia ulimwengu kuwa Chadema iko tayari kushika madaraka mwaka huu na kwamba itafanya hivyo kwa njia za amani kabisa".

Kwa mujibu wa vyanzo vingine CHadema inaandaa maandamano hayo ikiwa ni majibu kwa wale wenye kudai kuwa chama hicho hakiko tayari kuongoza. Akijibu swali la tamko wanalopanga kutoa mmoja wa waandaji wa maandamano hayo amesema kuwa "tamko hilo ni silaha yetu ya ushindi ambayo itaiweka siasa za Tanzania katika kiwango kingine kabisa na litatolewa na viongozi wote wa juu wa CHadema".

Endapo Chadema itafanya kweli maandamano hayo itakuwa ni mara ya kwanza kwa chama hicho kikongwe cha upinzani kuweza kuongoza wanachama na mashabiki wake kutoa shinikizo la kisiasa kwa chama tawala. "Wiki ijayo watu ndio watajua juu ya nguvu ya umma" amesema mwaandaji huyo.

Baadhi ya vioongozi wa CHadema ambao wanatajwa kuhutubia mkutano huo mkubwa ni pamoja na Mbowe, Zitto, na mgombea wa Urais Dr. Willibrod Slaa ambaye anatarajia kutoa tamko hilo kwa niaba ya chama chake. Siku na Mahali pa kuanzia maandamano hayo na kuishia bado panajadiliwa na mara vikiwa tayari taarifa itatolewa kwa umma.

Natamani siku hiyo ifike haraka. wana JF, wanachama wote wa CCM wanaoipenda Tz, washabiki wa CHADEMA, Hima tujitokeze siku hiyo tumuenzi Mwalimu... Hata kama naumwa, lazima niwepo. Cheers

Siku hiyo viongozi wetu wasisahau kiapo kama kile cha TARIME .... Ee mwenyezi Mungu nisaidie
 
maandamo sio lazima tupewe kibali, tutaandamana bila woga wala hofu, nipo tayari kupigwa virungu lakini kuandamana ni haki yangu ya kimsingi kabisa.

our constitutional, civic and birth right
 
......ngoja nika-book tiketi ya ndege ya Tropical ya Tanga-Dar tarehe hiyo!!!! mwenye sheria inayo-govern maandamo kama hayo atuwekee hapa jamvini.
 
Back
Top Bottom