CHADEMA kuitisha Maandamano Makubwa wiki ijayo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA kuitisha Maandamano Makubwa wiki ijayo

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mzee Mwanakijiji, Oct 7, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Oct 7, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Kuna taarifa ambazo zimeingia muda si mrefu ujao ambapo Chama cha Demokrasia na Maendeleo kinaandaa maandamano makubwa na ya kihistoria yatakayolitikisa Jiji la Dar wiki ijayo, wiki ya maadhimisho ya Siku ya Nyerere.

  Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali maandamano hayo yataongozwa na uongozi mzima wa Taifa wa Chadema chini ya Mwenyekiti Mbowe ambaye siku za karibuni amekuwa akiwasihi wananchi kuondoa woga wa kusimamia wanachokiamini.

  "Mwenyekiti Mbowe ataongoza maandamano hayo akiwa pamoja na Mgombea wetu wa Urais, wagombea wote wa Ubunge na viongozi wengine waandamizi" amesema mmoja wa watu wenye kuandaa maandamano hayo.

  Kiongozi huyo ambaye amekataa kutajwa jina lake kwa sababu taarifa hizo hazijatangazwa rasmi amesema kuwa "lengo la maandamano hayo ni kutaka kutoa tamko la kihistoria kuhusu uchaguzi huu mkuu ikiwa ni pamoja na kuuthibitishia ulimwengu kuwa Chadema iko tayari kushika madaraka mwaka huu na kwamba itafanya hivyo kwa njia za amani kabisa".

  Kwa mujibu wa vyanzo vingine CHadema inaandaa maandamano hayo ikiwa ni majibu kwa wale wenye kudai kuwa chama hicho hakiko tayari kuongoza. Akijibu swali la tamko wanalopanga kutoa mmoja wa waandaji wa maandamano hayo amesema kuwa "tamko hilo ni silaha yetu ya ushindi ambayo itaiweka siasa za Tanzania katika kiwango kingine kabisa na litatolewa na viongozi wote wa juu wa CHadema".

  Endapo Chadema itafanya kweli maandamano hayo itakuwa ni mara ya kwanza kwa chama hicho kikongwe cha upinzani kuweza kuongoza wanachama na mashabiki wake kutoa shinikizo la kisiasa kwa chama tawala. "Wiki ijayo watu ndio watajua juu ya nguvu ya umma" amesema mwaandaji huyo.


  Baadhi ya vioongozi wa CHadema ambao wanatajwa kuhutubia mkutano huo mkubwa ni pamoja na Mbowe, Zitto, na mgombea wa Urais Dr. Willibrod Slaa ambaye anatarajia kutoa tamko hilo kwa niaba ya chama chake. Siku na Mahali pa kuanzia maandamano hayo na kuishia bado panajadiliwa na mara vikiwa tayari taarifa itatolewa kwa umma.
   
 2. Sir R

  Sir R JF-Expert Member

  #2
  Oct 7, 2010
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 2,177
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Tunasubiri kwa hamu
   
 3. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #3
  Oct 7, 2010
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Wasisahau kuomba kibali toka kwa RPC anayehusika...
   
 4. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #4
  Oct 7, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Gud. Bila shaka tutapewa taarifa zaidi.
   
 5. Mpambalyoto

  Mpambalyoto JF-Expert Member

  #5
  Oct 7, 2010
  Joined: Mar 26, 2010
  Messages: 752
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ni jambo jema sana kwa CHADEMA kuandaa shughuli ya kumuenzi Nyerere maana UDSM wamefuta/wamekataza mbongi (palaver) wa Nyerere siku hiyo. Sababu ni kwa kuwa VC Prof. Mkandala na DVC Prof. Maboko hawatakuwepo chuoni na wanafunzi hawapo.
   
 6. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #6
  Oct 7, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  ha ha ha Kibs bana, yaani hapa imebidi nicheke tu
   
 7. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #7
  Oct 7, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 689
  Trophy Points: 280
  Good....wafuate taratibu, then tutajua cha kufanya Jama wakitutolea nje....pipooooooooooz!
   
 8. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #8
  Oct 7, 2010
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Jamaa tayali wameshaanza kulia lia, hivyo ni vema kuwakumbusha taratibu za maandamano, wasije kukurupuka tu na kuanza kuandamana!
   
 9. M

  Mkulima JF-Expert Member

  #9
  Oct 7, 2010
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 698
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 60
  Hawatapa kibali cha kufanya maandamano hayo
   
 10. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #10
  Oct 7, 2010
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,004
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280

  maandamo sio lazima tupewe kibali, tutaandamana bila woga wala hofu, nipo tayari kupigwa virungu lakini kuandamana ni haki yangu ya kimsingi kabisa.
   
 11. Mpambalyoto

  Mpambalyoto JF-Expert Member

  #11
  Oct 7, 2010
  Joined: Mar 26, 2010
  Messages: 752
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tutaandamana kwa imani
   
 12. Uncle Rukus

  Uncle Rukus JF-Expert Member

  #12
  Oct 7, 2010
  Joined: Jun 16, 2010
  Messages: 2,430
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kinana, kumbe upo?
   
 13. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #13
  Oct 7, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Kibali hakiombwi, wanatoa taarifa kwa polisi ili wapatiwe ulinzi.
  Lakini kama ujuavyo IDARA zote zinazosimamia dola zimeshafunga mlango wa demokrasia. utashangaa taarifa ya maandamano itaishia mezani kwa VASCO na watasubiri maamuzi kutoka juu.
  Watu hawana utashi bali wanasubiri maamuzi ya MASULTANI ndipo wafanye kazi
   
 14. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #14
  Oct 7, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Hakuna sheria inayotaka waombe kibali. Wanatakiwa watoe taarifa tu.
   
 15. PayGod

  PayGod JF-Expert Member

  #15
  Oct 7, 2010
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 1,255
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  tunasubir kwa hamu
   
 16. Sir R

  Sir R JF-Expert Member

  #16
  Oct 7, 2010
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 2,177
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Mikoani watuandalie tuko tayari kuandamana.
   
 17. K

  Kidatu JF-Expert Member

  #17
  Oct 7, 2010
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 1,491
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Wana Chadema tujitokeze kwa wingi katika maandamano hayo.
   
 18. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #18
  Oct 7, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  nitaandamana kwa kweli
   
 19. M

  Misterdennis JF-Expert Member

  #19
  Oct 7, 2010
  Joined: Jun 4, 2007
  Messages: 1,521
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160
  Weye ndiye RPC? .... hata aibu huna?
   
 20. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #20
  Oct 7, 2010
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Nadhani hizi ni propaganda kujaribu kuwatia wasiwasi ccm, hapa Tutambiwa yamekataliwa kwa sababu kuna dalili za uvunjifu wa amani na chadema wataazia hapo kulalamika jinsi wananavyoonewa.
   
Loading...