Elias Msuya
Senior Member
- Dec 23, 2011
- 173
- 671
Baada ya Mahakama Kuu ya Masijala ya Dar es Salaam kukubali ombi la upande wa Jamhuri la kuficha majina na taarifa nyingine za mashahidi raia wa upande wa Mashitaka katika kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, chama hicho kimesema kinaipinga Sheria hiyo ya iliyopitishwa kama Mabadiliko ya Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali Namba 2 ya 2018.
Agosti 4, 2025, Jaji Hussein Mtembwa alisema kutokana na uzito wa kosa la uhaini na hofu ya mashahidi kutishiwa, ni haki kwa mashahidi raia kulindwa kwa kutotajwa majina yao, anuani wala mahali walipo katika hatua ya committal, Preliminary Inquiry (PI) na hata wakati wa kusikilizwa kwa kesi hiyo.
Hata hivyo, Kaimu Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, Dk Rugemeleza Nshala amesema leo Agosti 6 kuwa sharia hiyo japo ilipitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano, haikufuata utaratibu wa kutumika.
“Bunge lilipitisha ila liliitaka Serikali kuweka utarratibu wa kuitumia, lakini haikufanya hivyo. Tumefuatilia na tumegundua kuwa sheria hiyo haikutangazwa kwenye gazeti la Serikali jambo ambalo ni kinyume cha Katiba na tumegundua kuna wafungwa 27 wamehukumiwa kunyongwa kwa sharia hiyo,” amedai Dk Nshala.
Lissu anatarajia kufikishwa tena mahakamani Agosti 13, ambapo anatarajiwa kusomewa mashitaka yake (comital) ili ahamishiwe mahakama kuu kusikiliza kesi hiyo ya uhaini.
“Bado hatujachelewa, tutamweleza jaji haya mambo yote, mambo ndiyo yameanza,” amesema Dk Nshala.