Nape, tunajua kwamba ungependa saaana Chadema ife ili chama chenu cha mafisadi kirejee madarakani kirahisi come 2015. Lakini ukae ukijua kwamba migogoro (kama huu wa Arusha) mara nyingii ndiyo inayoimarisha chama. Nadhani badala ya wewe na wenzako ndani ya chama cha mafisadi mngetumia zaidi muda kurejesha imani ya wananchi kwa chama chenu badala ya kuifikiria Chadema. Mna kazi kubwa ya kufanya, ikiwa ni pamoja na kuwatimua mapacha watatu, ingawa kuna taarifa kwamba mnawagwaya. Hakika chama chenu kimepoteza mvuto, na hivi sasa kinashabikiwa na mazuzu tu na wachache kama wewe ambao mnanufaikia moja kwa moja kutokana na hicho chama chenu kinachonuka.