CHADEMA kuchukua nchi ni baadae sana

Rage alipopanda na bastola jukwaan matumizi yake yalikuwa nini?

Zile za CCM sio bastola ila za CDM ndio bastola,magamba wanajitahidi kuichafua CDM lakini wapi,waache waendelee kuweweseka tu.
 
Jingine ni mawazo yako yasiyokuwa na maana.samahani usije kuwa mtoto nikakukosea inawezekana bado uu mtoto sana,hayo utawaeleza wasioona na kusikia wala kuelewa.Unalipwa sh ngapi?zimekusaidia nini wakati ndugu zako wengi wanumiaaaa! acha u.......a
 
Hakuna ubishi kwamba CDM ndio chama kikuu cha upinzani nchini na chama makini na tegemeo la Watanzania na ili ndoto ya tegemeo hili itimie lazima tikiri bado kuna mapungufu ya kimkakati. Pamoja na ukweli huu hatuna budi kuwa wakweli juu ya mambo mbalimbali kama ifuatavyo:

  1. Kujiimarisha katika mikoa isiyo na mwamko wa kisiasa. Ni ukweli usiopingika kwamba kuna umuhimu mkubwa wa CDM kujiimarisha kichama katika mikoa isiyo na mwamko. Baadhi ya mikoa hii ni Dodoma,Tanga,Tabora, Lindi, Mtwara na Pwani. Tukiangalia kwa umakini idadi ya kura katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 utaona kabisa tofauti kubwa sana kati ya CDM na CDM. Mfano mkoa wa Tanga hakuna diwani hata mmoja achilia mbunge toka CDM, kura za Uraisi kwa CDM hazifiki 3,000 dhidi ya zaidi ya 20,000 za CCM kwa jimbo la Lushoto, jimbo la bumbuli ndilo linaongoza kwa mkoa wa Tanga kwa kutoa kura za Uraisi takriban 10,0000 dhidi ya zaidi ya 20,0000 za CCM pamoja na kutokwepo kwa mgombea wa Ubunge wa CDM 2010 na kutofanyika kwa kampeni yoyote. Lakini ieleweke vilevile mkoa wa Tanga ni moja wa mikoa 10 yenye idadi kubwa ya watu Tanzania.
  2. Kujenga mazingira ya kupata kupata viongozi bora.Mwaka 2013 kutakuwa na uchaguzi wa ndani wa chama kwa ngazi ya majimbo/wilaya, Mkoa na Taifa. Ni dhahiri kwamba uchaguzi huu ndio utatoa taswira halisi ya kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, hivyo bila usimamizi makini kwa maana ya uratibu katika mchakato huu CDM itapoteza mwelekeo.
  3. Kujenga mkakati madhubuti wa kienezi kwenye mikoa isiyo na mwamko. Ni dhahiri kwamba CDM imeweka nguvu nyingi kwenye mikoa yenye muamko mkubwa wa kisiasa na kusahau mikoa yenye muamko mdogo na kwa kuzingatia kwamba gap ya kura dhidi ya CCM katika mikoa hii ni kubwa mno ipo haja ya kupunguza idadi hii kama kweli CDM imedhamiria kukamata dola. Ipo haja wa viongozi wa kitaifa wa CDM kutoa elimu ya uraia katika mikoa hii kwa maana ya ushawishi wao mkubwa kuliko viongozi wa Mikoa,wilaya/Majimbo.

  • Bila ya kupunguza gap la kura kati ya CDM na CCM kwenye mikoa isiyo na muamko ya kisiasa kukamata dola itakuwa ni ndoto kwa sababu hata katika maeneo ambayo CDM inaongoza tofauti ya kura ni ndogo na hivyo kuwa recovered kwa urahisi na kura za CCM.

Nakushauri utafute ile orodha ya idadi ya wapiga kura katika mikoa yote ya Tanzania halafu ujipange upya katika hoja yako ukituonyesha ni mikoa gani ina idadi kubwa ya wapiga kura.
 
Bado hueleweki mkuu, mikoa yenye muamko wa kisiasi maana yake nini?

Mikoa ambayo haikuchagua Chadema si kwamba haina muamko wa kisiasa ni kwamba wana vyama vyao CCM na CUF

Mikoa hiyo kwa mfano CUF ina madiwani wingi na imepata kura nyingi za urais? huo si muamko wa kisiasa?

Sema chadema wameshindwa ku-penetrate huko usituambie hatuna muamko kisiasa..
 
Ninachozungumzia ni changamoto kwa CDM kujiimarisha kisiasa, sijakuelewa unachobisha ni nini? na content ya thread yangu inaongelea CDM na hivyo muamko ninaouongelea unahusiana na CDM ambacho hujaelewa ni nn?Sasa kama hakuna mikakati ya ku-penetrate kama ulivyosema tutegemee miujiza?
 
Sasa ungesema chadema umeshindwa ku -convince wapiga kura katika mikoa hiyo; siyo kutuambia sisi hatuna muamko wa kisiasa? kwani muamko wa kisiasa ni kuwa mwana chadema?? WRONG
 
Nimekusoma mkuu.Kwa kweli ni good advice.Kwa hilo hakuna ubishi.Kinachosumaua watu wanakurupuka ktjadili thread hata hawjaisoma na kuielewa.
 
...ni kweli mkuu kuna mikoa cdm iko chini sana...lakini ukifuatilia tayari chadema imeshaanza kufanya kama unavyotaka...mkoa mmoja wapo ambao wameaanza nao ni mkoa wa morogoro hakuna ubishi kwamba huu ni mkoa ngome ya ccm lakini cdm wameiingia huko...ni hivi majuzi tu mwenyekiti wa bavicha na makamanda wengine walikuwa huko na walifungua matawi kibao na kuvuna wanachama zaidi ya 100 kutoka ccm...kabla ya hapo akina tundu lisu walikwenda mzumbe walikofungua tawi chuoni hapo....pia cdm walishaenda pwani maeneo ya kibaha...alikuwa ni peter msigwa na wenzake walionguruma huko....pia kwenda kujitosa zanzibar uzini ni katika hiyo mikakati unayoitaka....,mi nakuomba uendelee kuiamini cdm na cdm iko makini katika mikoa yote uliyoisema.....
 
unapoint ila kumbuka kuwa matokeo yaliyotangazwa 2010 sio matokeo halisi.

Tuache kuganganyana, mimi binafsi nilishiriki moja kwa moja uchaguzi wa mwaka 2010 jimbo la Lushoto kuna baadhi ya maeneo hawajui kuna chama kinaitwa CDM zaidi ya CCM na CUF zaidi na mbaya zaidi kuna wapiga kura walikuwa wanahoji propaganda kwamba CDM ni chama cha wakristo na bendera ya CDM kwanini ina rangi nyekundu ambapo kwa mtizamo wao ni chama cha wamwaga damu kwa kasumba walizoliswa na Magamba....lakini cha zaidi ni kwamba hakuna kampeni ya nguvu iliyofanywa na CDM mkoa wa Tanga (kwa mfano).

Vilevile nilishiriki uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya Funta-Bumbuli na kuona kwamba CDM kinaanza kutambulika na kushika kasi kinachokosekana ni msukumo dhabiti wa kienezi. Pamoja na kuwa ni mara ya kwanza CDM kusimamisha mgombea udiwani kata ya funta CDM kilipata kura 502 dhidi ya 1400 za CCM na CUF kuambulia kura 88 pamoja na uwepo wake wa siku nyingi jimbo la Bumbuli.

Lakini vilevile kwa zipo tetesi kwamba Januari Makamba hawamkubali sana Bumbuli kutokana na gia aliyotumia kuingia kwenye kura za maoni na hatimaye kupata nafasi ya kugombea ikiwa ni pamoja na mambo ya family matters ambapo wanadai aliwadanganya wananchi wa Bumbuli na iwapo atatokea mtu strong kusambaza elimu ya uraia na cocompete na Januari kama atapita kugombea tena ipo dalili kubwa za kummwaga. Najaribu kukusanya baadhi ya data na nitamwaga siku sio nyingi hapa jamvini. Ikumbukwe kwamba Januari alipita bila kupingwa kwa mizengwe iliyafanywa na mgombea wa CDM na taarifa niliyoipata mgombea yule amepewa ukatibu na CCM wilaya moja ya kanda ya ziwa. Pamoja na CDM kutosimamisha mgombea ubunge na kutopiga kampeni jimbo la Bumbuli ndilo linaongoza kwa kumpa kura nyingi Dr.Slaa (takriban zaidi ya 10,000) mkoa wa Tanga.

Iwapo kutafanyika kampeni ya nguvu ya elimu ya uraia bila shaka wilaya ya Lushoto ndio itakuwa kitovu cha mapambazuko ya kifikra mkoa wa Tanga kutokana na mwamko ulioanza kutokea. Wilaya ya Lushoto ina majimbo matatu: Lushoto, Bumbuli na Mlalo. Ikumbukwe kwamba idadi kubwa ya kabila la wasambaa ambao ndio utambulisho wa mkoa wa Tanga wengi wapo Wilaya ya Lushoto.

Tufute fikra ya kuibiwa kura kwanza, CDM iweke malengo kwenye baadhi ya mikoa niliyotaja iwapo CDM itafanikiwa kuwabeat CCM kwa kura nyingi uwezekano wa kuchakachua kama upo UTASHINDIKANA.
 
cdm still uve long way to go................mtafika tu lakini kwakua strategies zenu tunaziona.
 
mmh!
Mwamko mdogo wa kisiasa=CDM kukosa kura?
kweli tuna mbumbumbu katika kaifa hili! ila anyway 9% ndio wenye div 1-3.
 
mmh!
Mwamko mdogo wa kisiasa=CDM kukosa kura?
kweli tuna mbumbumbu katika kaifa hili! ila anyway 9% ndio wenye div 1-3.

Niligraduate kabla wewe hujajua kuandika...anyway rudi kwenye content ya thread yangu mpaka hapa unaonyesha wewe ni mvivu wa kusoma nahisi utakuwa mwanamuziki wa bongofleva...hapa naongelea kujiimarisha kwa CDM kwenye mikoa niliyoitaja na hali halisi juu ya majaliwa ya CDM kushika dola, na nimetoa changamoto acha kugeneralize mambo...muamko ninaoongelea unahusiana na CDM ndio maana title yangu nimeitaja CDM.
 
ni kweli, ni lazima tukubali changamoto ili tuweze kusonga mbele tusiwe watu wa kupinga kila jambo.
 
Tuache kuganganyana, mimi binafsi nilishiriki moja kwa moja uchaguzi wa mwaka 2010 jimbo la Lushoto kuna baadhi ya maeneo hawajui kuna chama kinaitwa CDM zaidi ya CCM na CUF zaidi na mbaya zaidi kuna wapiga kura walikuwa wanahoji propaganda kwamba CDM ni chama cha wakristo na bendera ya CDM kwanini ina rangi nyekundu ambapo kwa mtizamo wao ni chama cha wamwaga damu kwa kasumba walizoliswa na Magamba....lakini cha zaidi ni kwamba hakuna kampeni ya nguvu iliyofanywa na CDM mkoa wa Tanga (kwa mfano).

Vilevile nilishiriki uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya Funta-Bumbuli na kuona kwamba CDM kinaanza kutambulika na kushika kasi kinachokosekana ni msukumo dhabiti wa kienezi. Pamoja na kuwa ni mara ya kwanza CDM kusimamisha mgombea udiwani kata ya funta CDM kilipata kura 502 dhidi ya 1400 za CCM na CUF kuambulia kura 88 pamoja na uwepo wake wa siku nyingi jimbo la Bumbuli.

Lakini vilevile kwa zipo tetesi kwamba Januari Makamba hawamkubali sana Bumbuli kutokana na gia aliyotumia kuingia kwenye kura za maoni na hatimaye kupata nafasi ya kugombea ikiwa ni pamoja na mambo ya family matters ambapo wanadai aliwadanganya wananchi wa Bumbuli na iwapo atatokea mtu strong kusambaza elimu ya uraia na cocompete na Januari kama atapita kugombea tena ipo dalili kubwa za kummwaga. Najaribu kukusanya baadhi ya data na nitamwaga siku sio nyingi hapa jamvini. Ikumbukwe kwamba Januari alipita bila kupingwa kwa mizengwe iliyafanywa na mgombea wa CDM na taarifa niliyoipata mgombea yule amepewa ukatibu na CCM wilaya moja ya kanda ya ziwa. Pamoja na CDM kutosimamisha mgombea ubunge na kutopiga kampeni jimbo la Bumbuli ndilo linaongoza kwa kumpa kura nyingi Dr.Slaa (takriban zaidi ya 10,000) mkoa wa Tanga.

Iwapo kutafanyika kampeni ya nguvu ya elimu ya uraia bila shaka wilaya ya Lushoto ndio itakuwa kitovu cha mapambazuko ya kifikra mkoa wa Tanga kutokana na mwamko ulioanza kutokea. Wilaya ya Lushoto ina majimbo matatu: Lushoto, Bumbuli na Mlalo. Ikumbukwe kwamba idadi kubwa ya kabila la wasambaa ambao ndio utambulisho wa mkoa wa Tanga wengi wapo Wilaya ya Lushoto.

Tufute fikra ya kuibiwa kura kwanza, CDM iweke malengo kwenye baadhi ya mikoa niliyotaja iwapo CDM itafanikiwa kuwabeat CCM kwa kura nyingi uwezekano wa kuchakachua kama upo UTASHINDIKANA.

yaani unaona sifa watu kutokuijua chadema!!!!!!?????? badala uwahurumie hao ambao hawaijui na ufanye jitihada waijue au wajue vyama vingine vya siasa kwa maendeleo yao wenyewe!!!!!
embu jaribu kulinganisha maeneo waliong'ang'ania ccm miaka yote na ulinganishe na hali ya maishi mfano Pwani, Tanga Dodoma, tabora, ruvuma, mtwara, n.k then anghalia maeneo ya Moshi, Karatu, Mwanza N.K. walilie ndugu zako kwa kutokuijua Chadema na sio jambo la kujivunia hata kidogo!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
yaani unaona sifa watu kutokuijua chadema!!!!!!?????? Badala uwahurumie hao ambao hawaijui na ufanye jitihada waijue au wajue vyama vingine vya siasa kwa maendeleo yao wenyewe!!!!!
Embu jaribu kulinganisha maeneo waliong'ang'ania ccm miaka yote na ulinganishe na hali ya maishi mfano pwani, tanga dodoma, tabora, ruvuma, mtwara, n.k then anghalia maeneo ya moshi, karatu, mwanza n.k. Walilie ndugu zako kwa kutokuijua chadema na sio jambo la kujivunia hata kidogo!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

ebu sema jambo moja tu muhimu kwenye points zako zote" cdm haijajipanga kwa wizi wa kura" maana ushindi wa ccm si wa halali bali ni wa wizi, inawezekana watu wa cdm wanamwamko wa siasa wa kutosha na ndio maana siku zote magamba wanajipanga kuiba kura maana wanajua kama sio wizi hawaiwezi cdm hata kidogo
 
Bado hueleweki mkuu, mikoa yenye muamko wa kisiasi maana yake nini?

Mikoa ambayo haikuchagua Chadema si kwamba haina muamko wa kisiasa ni kwamba wana vyama vyao CCM na CUF

Mikoa hiyo kwa mfano CUF ina madiwani wingi na imepata kura nyingi za urais? huo si muamko wa kisiasa?

Sema chadema wameshindwa ku-penetrate huko usituambie hatuna muamko kisiasa..

Mkuu umesaidia sana kumuelimisha huyu aliyeleta huu uzi na kiukweli anahitaji kwenda kujipanga tena kwa sababu hajui hata maana ya neno "mwamko wa kisiasa". Yeye anachoamini ni kwamba mkoa wowote au jimbo ambalo CHADEMA hawajajipenyeza, hauna mwamko wa kisiasa. Hii siyo kweli na umemuelimisha vizuri sana.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom