CHADEMA itasababisha Mauaji mwaka 2015

CHADEMA itasababisha Mauaji mwaka 2015

Joseph Ludovick

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2013
Posts
382
Reaction score
506
Wandugu,
Wengi wamekuwa wanaacha kutazama hoja ninazoweka na kukimbilia kunitusi na kunikashfu binafsi. sijali sana hayo kwa sababu naamini natimiza wajibu mkubwa wa kijamii, kukilinda na kukitetea chama changu CHADEMA, na kuilinda nchi yangu TANZANIA. leo natafakari kile ambacho kitatokea baada ya matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2015 kama chama changu hakitabadilika haraka na kuachana na siasa za ki machiaveli.

"Makamanda" kama tunavyoitana, tumekuwa ni watu wa mihemuko. hatuhoji chochote hasa kikisemwa na viongozi wetu. hoja na ushuhuda wangu ni kuwa nafahamu kuwa mara nyingine na hasa juu ya matokeo ya uchaguzi viongozi wetu husema uongo wa hatari, na huko nyuma mimi mwenyewe nimeshiriki kuupika uongo huo. kwa ajili ya hoja yangu, nitatoa mifano mitatu halisi.

Wakati wa uhaguzi wa ubunge wa mwaka 2010 pale Bukoba mjini, tukijua kabisa kuwa tulikuwa tumeshindwa,tuliamua kuwadanganya wapiga kura na hasa vijana waliokuwa wamefurika kwenye kituo cha kujumlisha kura kuwa tumeshinda, wakaanza kushangilia,wakati ukweli tulikuwa tumeshindwa kwa zaidi ya kura 2000, na kwa haki kabisa. hii ilisababisha vurugu pale wafuasi wa CCM walipoanza kushangilia ushindi halali wa mbunge mteule.

Wakati wa uchaguzi mdogo wa Igunga, tukiwa tumejua matokeo kuwa tumeshindwa usiku, na kulingana na upepo tuliokuwa tumewajaza mashabiki wa CHADEMA pale Igunga, tuliamua kuwadanganya wanachama wetu kuwa tumeshinda na tukapita mitaani na gari la matangazo tukishangilia na kukusanya vijana kwenda halmashauri eti kulinda kura zisichakachuliwe. vijana waliingia mtaani kwa wingi. matokeo yake Matokeo yakasema CCM ndiyo washindi. tulipofika maeneo ya Peak hotel pale igunga wakatokeza vijana wa CCM wakatembeza kipigo cha mbwa mwizi kwa vijana wa CHADEMA. watu walikatwa mapanga na nakumbuka hadi risasi zilifyatuliwa.

Mwisho nakumbuka alichosema mgombea wetu baada ya uchaguzi wa rais uliopita. akisema alikuwa ameshinda ila akachakachuliwa. nchi ilikuwa kwenye tension na nadhani vijana wa CHADEMA tulikuwa tayari kuingia barabarani tukiamini kuwa kweli tuliibiwa kura tu uchaguzi wa rais.

Hoja yangu ni kuwa kutokana na mazingira ya siasa yalivy sasa,hadi mwaka 2015 kutakuwa na kundi kubwa la vijana bila shaka watakaoweza kuitikia mwito wa viongozi wetu wa CHADEMA kuingia barabarani kama watasema kura zimeibwa ama kujitangaza kushinda wakati wakijua hawakushinda. (maana kushinda urais bado sana), mapigano makubwa yatatokea baina ya vijana wa chama chetu CHADEMA, na wale wa CCM, na baina yetu na vyombo vya dola. kama CHADEMA itafanya hivi itakuwa imesababisha mauwaji ya raia wasiyo hatia. natamani chama changu kibadilike kabla ya wakati huo. Inawezekana kufanya siasa safi kama CHADEMA inavyotarajiwa.
 
haki yao ikiporwa 2015,wasifanye kile stahili ambacho si kinyume na sheria?

always CDM pop on ya head,your in love na Ufipani
 
Joseph Ludovick;Kijana unatia hata aibu kwa kuumba uongo dizaini hii! ulaaniwe! nadhani hata wazazi wako wanajutia kuzaa na kulea buyu kiasi hiki! any way ndio njia uliochagua ya kujidhalilisha hatuna cha kukufanya! ila wewe ni mtu hatari sana na utakata roho huku ukiwa umeshika ---- kwa laana za mamilioni ya watanzania waliowekeza wakitarajia Ukombozi kutoka CDM! Mungu na akuweke mahali pabaya sana jehanamu
 
Last edited by a moderator:
Kijana unatia hata aibu kwa kuumba uongo dizaini hii! ulaaniwe! nadhani hata wazazi wako wanajutia kuzaa na kulea buyu kiasi hiki! any way ndio njia uliochagua ya kujidhalilisha hatuna cha kukufanya! ila wewe ni mtu hatari sana na utakata roho huku ukiwa umeshika ---- kwa laana za mamilioni ya watanzania waliowekeza wakitarajia Ukombozi kutoka CDM! Mungu na akuweke mahali pabaya sana jehanamu

Ukombozi walete chadema? Unajidanganya 100%, 2015 mtakimbiana kumtafuta mchawi,
 
Wish tukio lako 1 tu lingekutajirisha but now unajuta kwa kile ulichokifanya koz madhara yake yamekuwa mabaya zaidi....pole wakala wa shetani
 
uongo mweupe....Mbona huongelei Jimbo kama la segerea? kama kweli wewe ni msema kweli tuambie ni nani alishinda jimbo la segerea kwa idadi kubwa ya kura. Kihalali..
 
Huyu jamaa Nate! Hilo nalo haliitaji disc! Wakiiba tu barabaran fasta
 
mawazo ya kiwiziwizi haya!
Kila nikiona uzi unaoanzisha ukijifanya mwana CHADEMA nakumbuka jinsi Mwigulu Nchemba alivyojitapa namna alivyokununua

Kwa mtu aliye wa kawaida, asingeendelea kujitokeza na kujifanya bado mmoja wa kundi alilolitengenezea kashfa.

Una matatizo makubwa sana, wewe ni mtu hatari sana, unaweza hata kuua kwa ajili ya pesa tu.
 
kwa akili yako kwa hiyo mwigullu ndo ludovick? come on!
 
Last edited by a moderator:
Whoever isn't with me is against me, and whoever doesn't gather with me scatters. Mt. 12:30.

Kama ni mwana CHADEMA hutashinda humu kinafiki ukifanya siasa za majitaka dhidi ya CHADEMA.

Wandugu,
Wengi wamekuwa wanaacha kutazama hoja ninazoweka na kukimbilia kunitusi na kunikashfu binafsi. sijali sana hayo kwa sababu naamini natimiza wajibu mkubwa wa kijamii, kukilinda na kukitetea chama changu CHADEMA, na kuilinda nchi yangu TANZANIA. leo natafakari kile ambacho kitatokea baada ya matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2015 kama chama changu hakitabadilika haraka na kuachana na siasa za ki machiaveli.

"Makamanda" kama tunavyoitana, tumekuwa ni watu wa mihemuko. hatuhoji chochote hasa kikisemwa na viongozi wetu. hoja na ushuhuda wangu ni kuwa nafahamu kuwa mara nyingine na hasa juu ya matokeo ya uchaguzi viongozi wetu husema uongo wa hatari, na huko nyuma mimi mwenyewe nimeshiriki kuupika uongo huo. kwa ajili ya hoja yangu, nitatoa mifano mitatu halisi.

Wakati wa uhaguzi wa ubunge wa mwaka 2010 pale Bukoba mjini, tukijua kabisa kuwa tulikuwa tumeshindwa,tuliamua kuwadanganya wapiga kura na hasa vijana waliokuwa wamefurika kwenye kituo cha kujumlisha kura kuwa tumeshinda, wakaanza kushangilia,wakati ukweli tulikuwa tumeshindwa kwa zaidi ya kura 2000, na kwa haki kabisa. hii ilisababisha vurugu pale wafuasi wa CCM walipoanza kushangilia ushindi halali wa mbunge mteule.

Wakati wa uchaguzi mdogo wa Igunga, tukiwa tumejua matokeo kuwa tumeshindwa usiku, na kulingana na upepo tuliokuwa tumewajaza mashabiki wa CHADEMA pale Igunga, tuliamua kuwadanganya wanachama wetu kuwa tumeshinda na tukapita mitaani na gari la matangazo tukishangilia na kukusanya vijana kwenda halmashauri eti kulinda kura zisichakachuliwe. vijana waliingia mtaani kwa wingi. matokeo yake Matokeo yakasema CCM ndiyo washindi. tulipofika maeneo ya Peak hotel pale igunga wakatokeza vijana wa CCM wakatembeza kipigo cha mbwa mwizi kwa vijana wa CHADEMA. watu walikatwa mapanga na nakumbuka hadi risasi zilifyatuliwa.

Mwisho nakumbuka alichosema mgombea wetu baada ya uchaguzi wa rais uliopita. akisema alikuwa ameshinda ila akachakachuliwa. nchi ilikuwa kwenye tension na nadhani vijana wa CHADEMA tulikuwa tayari kuingia barabarani tukiamini kuwa kweli tuliibiwa kura tu uchaguzi wa rais.

Hoja yangu ni kuwa kutokana na mazingira ya siasa yalivy sasa,hadi mwaka 2015 kutakuwa na kundi kubwa la vijana bila shaka watakaoweza kuitikia mwito wa viongozi wetu wa CHADEMA kuingia barabarani kama watasema kura zimeibwa ama kujitangaza kushinda wakati wakijua hawakushinda. (maana kushinda urais bado sana), mapigano makubwa yatatokea baina ya vijana wa chama chetu CHADEMA, na wale wa CCM, na baina yetu na vyombo vya dola. kama CHADEMA itafanya hivi itakuwa imesababisha mauwaji ya raia wasiyo hatia. natamani chama changu kibadilike kabla ya wakati huo. Inawezekana kufanya siasa safi kama CHADEMA inavyotarajiwa.
 
kwa akili yako kwa hiyo mwigullu ndo ludovick? come on!
Ulinunuliwa na Mwigulu kama mkakati wa Mwigulu kuiangusha Chadema, na Mwigulu mwenyewe anajisifia hapa jinsi alivyokutumia kama condomu

Unakataa ushahidi uko wazi?

Hili unalofanya humu JF kupost majitaka dhidi ya CHADEMA, ni mwendelezo wa ushirikiano wako na Mwigulu.

Kijana aliyenunuliwa na kugeuzwa kondomu, kauli zake ni za kinafiki tu......
 
Last edited by a moderator:
Hii nchi haijakaa vizuri,
acha kuota ndoto za mchana usijepotea ukaacha familia yako inateseka;
 
afadhali mimi ni kijana . nafikiria hili likitokea kwa gaidi mwenzangu! itakuwa balaa.

Hapa umedhibitisha kitu kimoja. Kwamba ulitumwa kwa kazi maalumu kumfanya "huyo" gaidi mwenzako aonekane gaidi. Kijana maisha ya kinafiki hayana mwisho mzuri na hilo unalosema afadhali wewe ni kijana litajakuja kukutokea kama halijawahi. Tumia ujana wako vema utaheshimika uzeeni.
 
Molemo hivi huyu kijana ni mwanchama waTawi lipi? kwa nini hawamfuti uanachama na akakimbilia ACT ?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom