CHADEMA: Israel ituombe radhi

CHADEMA: Israel ituombe radhi

Kauli hii jibu lake laenda mbali kidogo na wala mtu akifupisha upana wa fikra ni makosa sana.

Kitendo cha kuruhusu taifa mojawapo la Ghuba kuhamia kwenye mbuga zetu likiwa na viashirio vyote vya tawala zake za kujitegemea kabisa ndani ya nchi yetu, na vile vile jibu la jinsi gani tumekua na mchango kwa taifa la Irani ni tabu tupu hadi hapa.

Wakati tukionyesha kuchanganyikiwa na hiyo kauli tata to kwa taifa teule la Israel, mwenzetu Rostam Aziz kule Kigoma anaelewa fika kitu gani kinachomaanishwa hadi hapo.
kwani ni uongo wametuona hatuna maana siku tulipoonyesha makomandoo wa jeshi letu wakifanya mazingaombwe mbele ya rais eti komandoo anavunja tofali kwa kichwa, eti komandoo anapigwa na kaubao ka msprus kembamba kweli israel ndipo ilituona wajinga na hatuna maana wakaona hawana cha kuungana nasi kiulunzi,
 
Hilo dege la jeshi lina uafadhali, hawa mapacha watatu Richmondi, dowanz na symbioni tunao miaka nenda miaka rudi mkuu wa kaya katuambia hata hawajui!! Lakini anatetea walipwe tuuu pesa yao. Jifanye wewe ni balozi unayewakilisha nchi yako hapa TZ halafu waziri Mkulo anakujia kukuomba uchangie kwenye bajeti yake ya mwaka ujao!! Katika mazingira kama haya nani atakuheshimu? Tunastahili kudharaulika na nchi zingine. Naungana na wachangiaji wengine kwamba wanaostahili kutuomba radhi ni sisiemu iliyotengeneza na kutekeleza sera ambazo zimetufikisha hapa.

Ni aibu sana.

Na ni bora hizo hela tunaomba basi tuzitumie kwa mambo ya maendeleo na yaonekane kwa wananchi..Ni sawa na wanwake wanaoenda pride kukopa hela za kuznzisha biashara lakn wanaishia kununua kanga na vitenge.Sasa ndio maana tunadharaulika kwa kuwa hatujui kupangilia mambo yetu.
 
Pipijojo,

Sina ajenda ya siri, ili kuepusha kumnukuu tofauti, tumeyanukuu maneno yote kwa lugha ile ile ambayo imenukuliwa kwenye vyombo vya habari vya Israel; tafadhali rejea kwenye taarifa kamili.

Kuhusu Ushoga; tulitoa kauli naomba nikuwekee hapa chini kama ilivyo kwa ajili ya rejea yako na ya wengine:

TAARIFA KWA UMMA
Kurugenzi ya Mambo ya Nje na Mahusiano ya Kimataifa ya CHADEMA inatoa mwito kwa Rais Jakaya Kikwete kutumia mazungumzo kuhusu mahusiano baina ya Tanzania na Uingereza yanayotarajiwa kufanyika wakati wa ziara ya mtoto wa Mfalme wa Uingereza Charles na mkewe kuanzia tarehe 7 Novemba 2011 kushughulikia masuala yaliyojitokeza hivi karibuni yenye kuweza kuathiri mahusiano ya nchi zetu.Katika siku za karibuni Serikali ya Uingereza imepunguza misaada yake ya kibajeti kwa Tanzania kwa asilimia 30 kutokana na kutoridhishwa na utendaji wa serikali hususani kuhusiana na masuala ya kuboresha mazingira ya kibiashara na kutoa fursa kwa wananchi kuwawajibisha viongozi. Uamuzi huo wa Serikali ya Uingereza umeelezwa kupitia barua ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Nchi hiyo Andrew Mitchell ya tarehe 3 Agosti 2011 kwenda kwa Mwenyekiti wa Kamati Teule ya Bunge la Nchi hiyo kuhusu Uchumi .“Ni vizuri pande zote mbili Rais Kikwete na Mwanamfalme Charles wakawaeleza watanzania kuhusu sababu za ziada za maamuzi haya. Vyanzo mbalimbali vinaeleza kuwa sababu halisi ni washirika wa maendeleo kutoridhika na kasi ya vita dhidi ya ufisadi kwa upande mmoja na kwa upande mwingine ukanda wa ulaya (Eurozone) kukumbwa na matatizo ya kifedha”.Aidha, Rais Kikwete atumie mazungumzo ya ziara hiyo kuwaeleza watanzania mkakati wa nchi kupunguza tatizo la utegemezi ambalo linasababisha nchi kupewa misaada yenye masharti ya kibeberu, ikiwemo kulieleza taifa namna ambavyo nakisi ya bajeti inayotokana na wahisani kupunguza fedha zao kwa Tanzania itaweza kuzibwa kwa kuongeza uzalishaji, mauzo ya nje na kupunguza ubadhirifu katika serikali.Kwa upande mwingine, pamoja na kauli iliyotolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Mahusiano ya Kimataifa Benard Membe kuwa Tanzania iko tayari kukubali kukosa misaada yote toka Uingereza ikiwa serikali ya nchi hiyo italazimisha kutungwa kwa sheria ya kuruhusu ushoga, usagaji na ndoa ya jinsia moja; ni muhimu kwa Rais Kikwete kutumia mazungumzo hayo kufikisha ujumbe kamili wa kupinga masuala hayo kwa niaba ya watanzania.Kurugenzi ya Mambo ya Nje na Mahusiano ya Kimataifa ya CHADEMA inaunga mkono msimamo wa serikali ya Tanzania wa kukataa kufanya mabadiliko ya sheria ya kuruhusu vitendo hivyo ambavyo ni kinyume cha sheria na utamaduni wetu.“Kwa mujibu wa katiba ya CHADEMA kifungu 3.1.8, kwa falsafa yetu ya nguvu ya umma na itikadi ya mrengo wa kati CHADEMA inaweka umuhimu wa pekee katika familia kama moja ya taasisi muhimu za kijamii. Hivyo, tunapinga vitendo vya ushoga, usagaji na ndoa ya jinsia moja kwa kuwa vinakinzana na misingi ya maadili na uwepo wa familia”.Kurugenzi ya Mambo ya Nje ya CHADEMA inataka ujumbe mahususi utolewe na Rais Kikwete kupitia ziara hiyo sababu wakati wa kujadiliwa kwa ripoti ya ndani ya mustakabali wa Jumuia ya Madola (Internal Report on the future relevance of Commonwealth) katika Mkutano wa Jumuia ya Madola uliomalizika karibuni; Rais Kikwete hakutoa ujumbe mkali kwa Serikali ya Uingereza wakati wa kujadiliwa kwa masuala ya haki za binadamu tofauti na kauli ambayo serikali iliitoa kupitia vyombo vya habari wakati ujumbe wake uliporejea Tanzania.Wenu katika demokrasia na maendeleo, John Mnyika (Mb)Mkurugenzi wa Mambo ya Nje na Mahusiano ya Kimataifa (CHADEMA)06/11/2011

Mhe. Mnyika,

Mbona kauli ya Chama chako dhidi ya ushoga haukuitoa kwa publicity kama hii ya Israel? Isitoshe, mbona katika taarifa hiyo suala la ushoga limepewa uzio mdogi ikilinganishwa na ziara ya Mwana Mfalme na tena katika muktadha wa kmtupia lawama Mhe. Rais? Hata hivyo, wewe ukiwa ndio Mkurugenzi wa Nje wa CHADEMA inaingia akilini kwako kuwa msimamo wa nchi unatolewa na Waziri wa Ulinzi? Lakini, hivi kweli unatarajia Serikali ya Israel iwe na mtazamo mzuri dhihi ya Serikali ya Tanzania? Kwa lipi? Mbona kila mwaka hapa nchini yanatolewa matamko makali tu dhidi ya Israel? Kila mwaka Tanzania inapiga kura maazimio ya kuunga mkono Palestina dhid ya Israel, ni kwa vipi Tanzania itakuwa relevant kwa Israel? Je, tuna shauku ya Tanzania kuwa relevant kwa Israel? Ndio sera ya mambo ya nje ya CHADEMA?
 
Ehud Barak kazungumza......na keshasema habadili msemo/lugha yake......nchi nyingine zilizoendelea mfano UK.....ni wanafiki kweli kweli wao hawasemi ila wanatenda.....kutuonyesha kuwa sisi si lolote na si chochote...........

Ndio maana ninawaheshimu sana Viongozi wa Afrika waliopigania na wanaopigania Afrika tuungane (Kwame, Gadaffi, JKN etc)...........only then hizi dharau za akina Barak na nchi kama hizo.....zitatutambua...........
 
dah! yaani taifa linatukanwa watu tunafurahia!

hapa huyu eudi kapotoka. naamini kama huyu jamaa asingekuwa na lengo la kuitukana
tanzania angeweza kabisa kutumia maneno mengine na mifano mingine.

jamaa anastahili kuomba radhi. na kama asipoomba radhi, tanzania tuweke kumbukumbu
(natumaini watawala wetu bado hawajaua "kumbukumbu ya kitaasiss") na ipo siku hawa
watu wataingia tu katika "anga" zetu nasi kama taifa tutapata nafasi ya kuwakumbusha hilo.
katika masuala ya kidiplomasia hilo lawezekana sana. muulizeni mzee salim a. salim yaliyompata
alipogombea ukatibu mkuu umoja wa mataifa. dah!
 
Kisa cha chuki na hasira dhidi ya Tanzania kilianzia enzi ya Mwalimu Nyerere alipoamua kutokuwa na ubalozi wa Israel nchini Tanzania.

Ila sasa mkianza kuuza Uranium yenu kwa nchi kama Iran, ndio mtatambulika na kuonekana wa muhimu.
 
Tz kweli haina maana,kama bushi kaja kujijengea kigamboni!..juzi mkurugenzi wa ewura anatangaza kuwa taifa lina akiba ya mafuta ya siku33,just imagine marekani ina akiba ya mafuta miaka500 ijayo. je waweza kusema taifa ina lolote? bongo kuna ndege moja ya taifa,na dege ilo ni bovu...Hata mi siamini kama Tz ina maana!
 
WATUOMBE RADHIi?hawawezi hata siku moja kufanya hicho kitu,wanamfahamu vizuri sana raisi tuliyenaye na wametamka hivyo wakijua JK akisikia atacheka tu!na kurudi kwao kuomba tena msaada mwingine.
Kingine ninachokiona hapa inatakiwa yujiulize huyu raisi wetu anavyoenda huko nje huwa anawaambia nn?kwa sababu naona sasa nchi yoyote ikiamua kututukana wla haisiti kufanya hivyo,
Mimi naona kuna ruhusa wameipata kutoka kwa raisi wetu kufanya lolote wanaloweza na kutupa vijimsaada vyao kwa matusi na kebehi wanazozitoa.
Ni kwa nini hii serekali inatudhalilisha kiasi hiki?SIKU YAJA TENA I KARIBU SANA!!!!!!
 
Mbona Membe yuko Kimya? namjua ni Hodari wa Kutoa Matamko pale Mtu anapoichokoza ama kuidharau Tanzania. Naona Kanywea wapi Mbopo?
 
Kuna nyumba ya kanisa masaki kapangishwa muisrael kwa kodi za nhc lakini yeye anapiga dola na yeye hakai anakula vichwa.

Waumini na viongozi wao wanamshobokea sababu ni muisrael na wala hafanyi kazi za kanisa inaonekana kabisa ni shushushu.

Kuna kampuni QTE imedhulumu watu kibao zaidi suppliers hawafanywi kitu eti ni ya waisrael.

Michache tu bado watu wanatutusi, hawa wana makusudi tu!
 
Hapo Mnyika (CHADEMA) wamepotoka.

Tz ikijiheshimu itaheshimika. Ni kanuni ya kawaida..... kwanza nyumbani kisha nchi jirani na baadaye mataifa mengine wataona na kuthamini. Lakini kwa ukweli wa hali ya sasa na Serikali hii; naamini Wananchi (Watanzania) wengi wanatoa maneno makali sana dhidi ya nchi yao kuliko maneno aliyotumia Ehud Barak.




yalikuwa ya upole sana maana
 
Nafurahi kuona michango mingi imelenga kwenye mada, ukweli na weledi.

Wengi nilosoma michango yao usually ni pro-Chadema, lakini wameonesha ukomavu mkubwa kwa kuainisha kuwa ktk hili CDM wamekosea. Sasa ni busara nao CDM wakisoma upande wa pili wa shilingi wa tamko lao na kuchukua hatua stahiki.
 
Nafurahi kuona michango mingi imelenga kwenye mada, ukweli na weledi.

Wengi nilosoma michango yao usually ni pro-Chadema, lakini wameonesha ukomavu mkubwa kwa kuainisha kuwa ktk hili CDM wamekosea. Sasa ni busara nao CDM wakisoma upande wa pili wa shilingi wa tamko lao na kuchukua hatua stahiki.

hiyo ni kweli mkuu, mi nilidhani chadema wangemgeukia ombaomba asiyetumwa na wale anaojifanya kuwaombea na kummnyooshea kidole kuwa yeye ndiyo chanzo cha sisi kudharauliwa. hivi enzi za nyerere wangesema hivyo pamojaa na umasikini 2liokuwa nao?

wengine wanasema eti ni maoni ya waziri na siyo msimamo wa Israel, hivi nani amemmsikia statesman yeyote wa Israel akikanusha au kulaani? kwa hiyo hata ushoga ni maoni 2 ya akina Cameron na Obama? 2kijiheshimu 2taeshimika, nahisi wachina wana2fananisha ni moja ya vitongoji vyao na huo ndiyo ukweli. ni angalau kiongozi wa mtaa anayeweza kuona ujiko kupiga picha na Cris Tucker au 50 cents.........siyo raisi wa nchi
 
Taifa teule,litamdhalilisha mtu yoyote na haliombi radhi,hamna mtu yoyote wa kumfanya kitu chochote
 
Back
Top Bottom