THREAD hii nimeikuta ikiwa imefika mbali sana kiasi cha kunilazimisha nianze kupitia post moja hadi nyingine ili nipate kile nilichokuwa nakitafuta! Hata hivyo, sikukipata.....si kwenye michango ya members tu bali hata kutoka kwenye main thread! Interest yangu ni kufahamu msingi wa swali uliomfanya Ehud Barak Kuitaja nchi yetu kwamba haina maana wala umuhimu wowote kwa Israel! Kwavile msingi wa swali haupo wazi basi inaonesha wazi kwamba wachangiaji wengi michango yao imetawaliwa na USHABIKI WA KIPUMBAVU, MAPENZI YA KIPUMBAVU na CHUKI ZA KIPUMBAVU za wachangiaji!
USHABIKI WA KIPUMBAVU!
Sio siri kwamba baadhi ya mashabiki wa CHADEMA wana ushabiki wa kipumbavu kiasi kwamba inapotokea yeyote akaisema serikali (ingawaje hapa imesemwa TZ, na kwao wao TZ is all about serikali) kwa mabaya basi wao watashangilia hata kama kusemwa huko nao kunawahusu! Hawa ni wale wanaoamini katika nadharia kwamba ADUI WA ADUI YAKO NI RAFIKI! Kutokana na ushabiki huo wa kipumbavu, inaonekana kana kwamba Ehud Barak ametamka kwamba Tanzania haina umuhimu wala maana kwa Israel kwakuwa ni ombaomba; kitu ambacho hakijawekwa wazi! Kwavile sababu haikuwekwa wazi, je ikidhihirika kwamba ameyasema hayo kwa sababu tu Tanzania ipo Afrika na watu wake ni Waafrika bado mtaandelea kushangilia?!
MAPENZI YA KIPUMBAVU
Wakati ushabiki wa kipumbavu unatokana na itikadi za kisiasa, mapenzi ya kipumbavu yanatokana na itikadi za kidini! Wapo baadhi ya Wakristo, kutokana tu na itikadi zao za kidini na kule kuaminishwa kwao kwamba Israel ni taifa teule na kwamba ndiko chimbuko la Jesus Christ, basi wao kila kinachosemwa au kufanywa na Israel wao watakifurahia na kukipamba kwa maua!! Yaani Mwafrika mwenye ngozi nyeusi anajishadidia na Myahudi mwenye ngozi nyeupe na kumshabikia kwamba eti ni taifa teule!
CHUKI ZA KIPUMBAVU!
Hii ni sawa na hapo juu ingawaje hili lipo kwa baadhi ya Waislamu ambao nao msingi wake ni itikadi za kidini! Kwavile Wayahudi wana chuki na Waarabu ambao wengi wao ni Waislamu basi chochote kinachofanywa ama kusemwa na Israel kitabezwa kwavile tu Wayahudi wana chuki na Waarabu ambao ni waislamu wenzetu!!!
HIVYO basi, kwa vile wengi wetu (including mtoa mada) tumedandia mada tusiyoijua chanzo, basi ningemuomba Mheshimwa Mnyika atueleze chanzo cha Ehud Barak kutoa kauli hiyo! Mathalani, tuseme Uhud Barak aliulizwa swali kwamba ana maoni gani kuhusu Tanzania kuiunga mkono Palestina....mnatarajia atajibu nini?! Lazima tu atoe kauli ya sizitaki mbichi hizi!