CHADEMA: Israel ituombe radhi

CHADEMA: Israel ituombe radhi



kumbuka anaposema tanzania aina umuhimu duniani.. anamaana na wananchi wa tanzania,hakuna TANZANIA BILA WATANZANIA SO for ur info. wewe kama mtanzania umekuwa included ndani kwamba you are nothing! .. ni kama ile karatasi ya toi... sasa nashangaa unaposhabikia hawa wapumbavu walivyo tutukana .. labda mwenzetu mkenya!

AU Kama unadhani weye hauna umuhimu kivyako ... ni weye peke yako... $%$&:embarassed2:
...pole sana NJIWA,"acha kupoteza muda na nguvu zako nyingi kutetea hili li-nchi tz"...njoo uku tusubiri basi{katiba mpya} lije, tupande turudi zetu kwetu TANGANYIKA...

uko nyumbani {TANGANYIKA} mtu akitutukana ndo itabidi tupigane kulinda heshima yetu,lakin kilipigania hili lidubwasha tanzania ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu coz lilishauzwa siku nyiiiiiiiiiiiiiingi...
 
Mkuu Njiwa,
Umeona unafiki huu wa Mitanzania na ujinga watu wao, wanatukanwa wanashangilia kisa alietukana kipenzi chao Isarel.

Inawezekana kabisa humu kuna watu hata akikuta mke wake kajazwa mimba na Muisrael au Mzungu, atashangila sana na kutoa pongezi
Mimi wakwangu bora achalazwe na waarabu kwa kuwa wawo wanafaida,wanatuleteaga tende harua na nyama ya mbuzi!
 
Pipijojo,

Sina ajenda ya siri, ili kuepusha kumnukuu tofauti, tumeyanukuu maneno yote kwa lugha ile ile ambayo imenukuliwa kwenye vyombo vya habari vya Israel; tafadhali rejea kwenye taarifa kamili.

Kuhusu Ushoga; tulitoa kauli naomba nikuwekee hapa chini kama ilivyo kwa ajili ya rejea yako na ya wengine:

TAARIFA KWA UMMA
Kurugenzi ya Mambo ya Nje na Mahusiano ya Kimataifa ya CHADEMA inatoa mwito kwa Rais Jakaya Kikwete kutumia mazungumzo kuhusu mahusiano baina ya Tanzania na Uingereza yanayotarajiwa kufanyika wakati wa ziara ya mtoto wa Mfalme wa Uingereza Charles na mkewe kuanzia tarehe 7 Novemba 2011 kushughulikia masuala yaliyojitokeza hivi karibuni yenye kuweza kuathiri mahusiano ya nchi zetu.Katika siku za karibuni Serikali ya Uingereza imepunguza misaada yake ya kibajeti kwa Tanzania kwa asilimia 30 kutokana na kutoridhishwa na utendaji wa serikali hususani kuhusiana na masuala ya kuboresha mazingira ya kibiashara na kutoa fursa kwa wananchi kuwawajibisha viongozi. Uamuzi huo wa Serikali ya Uingereza umeelezwa kupitia barua ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Nchi hiyo Andrew Mitchell ya tarehe 3 Agosti 2011 kwenda kwa Mwenyekiti wa Kamati Teule ya Bunge la Nchi hiyo kuhusu Uchumi .“Ni vizuri pande zote mbili Rais Kikwete na Mwanamfalme Charles wakawaeleza watanzania kuhusu sababu za ziada za maamuzi haya. Vyanzo mbalimbali vinaeleza kuwa sababu halisi ni washirika wa maendeleo kutoridhika na kasi ya vita dhidi ya ufisadi kwa upande mmoja na kwa upande mwingine ukanda wa ulaya (Eurozone) kukumbwa na matatizo ya kifedha”.Aidha, Rais Kikwete atumie mazungumzo ya ziara hiyo kuwaeleza watanzania mkakati wa nchi kupunguza tatizo la utegemezi ambalo linasababisha nchi kupewa misaada yenye masharti ya kibeberu, ikiwemo kulieleza taifa namna ambavyo nakisi ya bajeti inayotokana na wahisani kupunguza fedha zao kwa Tanzania itaweza kuzibwa kwa kuongeza uzalishaji, mauzo ya nje na kupunguza ubadhirifu katika serikali.Kwa upande mwingine, pamoja na kauli iliyotolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Mahusiano ya Kimataifa Benard Membe kuwa Tanzania iko tayari kukubali kukosa misaada yote toka Uingereza ikiwa serikali ya nchi hiyo italazimisha kutungwa kwa sheria ya kuruhusu ushoga, usagaji na ndoa ya jinsia moja; ni muhimu kwa Rais Kikwete kutumia mazungumzo hayo kufikisha ujumbe kamili wa kupinga masuala hayo kwa niaba ya watanzania.Kurugenzi ya Mambo ya Nje na Mahusiano ya Kimataifa ya CHADEMA inaunga mkono msimamo wa serikali ya Tanzania wa kukataa kufanya mabadiliko ya sheria ya kuruhusu vitendo hivyo ambavyo ni kinyume cha sheria na utamaduni wetu.“Kwa mujibu wa katiba ya CHADEMA kifungu 3.1.8, kwa falsafa yetu ya nguvu ya umma na itikadi ya mrengo wa kati CHADEMA inaweka umuhimu wa pekee katika familia kama moja ya taasisi muhimu za kijamii. Hivyo, tunapinga vitendo vya ushoga, usagaji na ndoa ya jinsia moja kwa kuwa vinakinzana na misingi ya maadili na uwepo wa familia”.Kurugenzi ya Mambo ya Nje ya CHADEMA inataka ujumbe mahususi utolewe na Rais Kikwete kupitia ziara hiyo sababu wakati wa kujadiliwa kwa ripoti ya ndani ya mustakabali wa Jumuia ya Madola (Internal Report on the future relevance of Commonwealth) katika Mkutano wa Jumuia ya Madola uliomalizika karibuni; Rais Kikwete hakutoa ujumbe mkali kwa Serikali ya Uingereza wakati wa kujadiliwa kwa masuala ya haki za binadamu tofauti na kauli ambayo serikali iliitoa kupitia vyombo vya habari wakati ujumbe wake uliporejea Tanzania.Wenu katika demokrasia na maendeleo,John Mnyika (Mb)Mkurugenzi wa Mambo ya Nje na Mahusiano ya Kimataifa (CHADEMA)06/11/2011

@PIPIJO.......... Mh John (hata kama we ni mdogo wangu) .... People might not notice the difference..... nimeonya kabla.... huyo pipijo hasomi taarifa za CDM ana arrage...!!!
 
Watanzaia kama sio wapumbavu au kama si wa tripolitania wangechaguaje chama ambacho viongozi wake wanongeza kodi kwenye mafuta ya taa an kupunguza au kufuta kodi kwenye madini? Big up waisraeli

hivi tahir square nzuri kwa bongo ni wapi? ..bora tukutane hapo!
 
Hiyo ndio taswira ya Tanzania kimataifa. Nafikiri kauli ya waziri wa Ulinzi wa Waziri wa Israel ametutanabahisha ni namna gani wanatufahamu. Sasa ni wajibu wetu kungalia tulipojikwaa na tusingalie tulipoangukia. Kuombwa radhi hakuwezi kujenga hadhi na hesshima ya Tanzania
 



you are so thick mate aren't you ...?!! nishakwambia hapo umetukanwa wewe kama mtanzania... ni sawa anakuja mtu anakuita MBWA WE! na wewe unashangilia na kurukaa YEEY !! NIMEITWA MBWA ... hebu jifunze kuwa patriotic na nchi yako!.. sahau u ccm na uchadema, U cuf pale mgeni anapokutukana na kukudharau usishangilie unapotukanwa wawapi weye ..??, alafu wauliza nini umuhimu wa Dactari katika nchi hii ya tanzania! are u serious mate..?!


Njiwa try 2 b a real DR. afadhali tu anieleze ukweli sitachukulia kama tusi.....!!!! kuliko anaye kusifia kwa kinywa huku akikutukana ki-matendo (RICH... SOMETHING. DOWANS, SYMBION; unakumbuka Mama Crinton siku ile alisemaje ...!!!, Wabeba nyara..... the list is too long....)
NASIKIA KULENGWLENGWA NA MCHOZI..
 
YES Tanzania sio nchi ya maana na muhimu...well said minister barak

Na viongozi wetu hawajiulizi kwa nini uzalendo na mapenzi ya wananchi kwa nchi yetu nzuri ya Tanzania vimepungua!
Kama hawaoni hivyo wajaribu kutuhamasisha tufanye maandamano kulaani kauli ya Waziri huyo wa Israel. Naamini hata UV-CCM hawatajitokeza kwenye hayo maandamano!
 
Sioni haja ya Israel kuomba radhi kwa chochote na
much less kwa irrelevant country kama Tanzania.

Hivi watasikia hata kilio chenu hicho?
 
Ndiyo uzuri wa Izrael maana hawajui kuuma uma maneno kama UK au USA.

USA ni hii WIKILEAKES tu imewaumbuwa kuja kujua kumbe walikuwa wanabwabwaja ovyo.

NAMSIFU BARAK kwa kusema ukweli kama ulivyo na ndiyo maana nimebadili hata SAHIHI yangu hapa chini....
 
Watanzaia kama sio wapumbavu au kama si wa tripolitania wangechaguaje chama ambacho viongozi wake wanongeza kodi kwenye mafuta ya taa an kupunguza au kufuta kodi kwenye madini? Big up waisraeli

Ha! Ha! Ha! Leo umekubali kuwa Chadema hawakushinda Watanzania waliichaguwa CCM?
 
kwa hiyo wewe muisrael akija nyumbani kwako na kumchukuwa mke wako wewe nafsi yako kwatu tu!

mimi bora mwarabu mkuu,kwa kuwa waarabu wanatuleteaga tende harua na nyama ya mbuzi!
 
Hi Mh. Mnyika yuko sahihi; Tanzania imepoteza mwelekeo na nafasi yake katika nyanja ya kimataifa baada ya kauchana na sera za Self-reliance na kuto fungamana na upande wowote. Tanzania ilikuwa msemaji wa maskini na wanaoonewa, ikikataa kuchaguliwa marafiki na maadui. kwa msimamo huu, Tanzania iliweza kuwa rafiki wa Israel pomaja na kwamba iliiambia wazi wazi inapashwa kuhama/kurudisha ardhi ya Palestina, Syria na Jordan ambayo iliikalia kimabavu na vile vile ilikuwa mstari wa mbele kutetea kuwepo kwa Taifa la Wapalestina. Nafikiri msimamo huu bado tunauendeleza kwa kugharimia ubalozi wa palestina hapa Tanzania.

Pengine huu ni wakati muafaka kurudi na kuingalia sera yetu ya mambo ya nje. Sera hii ya sasa ya "Economic Diplomacy" iliyoasisiwa na rais mstaafu Mkapa na kuendelezwa na serikali ya Kikwete si lolote si chochote bali ni sera iliyobuniwa kuidhinisha uomba omba na inadharirisha sana nchi yetu.

The major Tanzania Foreign Affairs speech to have been made by our First President and perhaps is still relevant today, ilitolewa kwenye mkutano wa TANU uliofanyika Mwanza, mwaka 1967.

Wale wadau wenzangu wanaopenda kudadisi na kujua mambo mnaweza kwenda hapa mkaisoma speech hii. Unaweza pia kudownload

Mwalimu Nyerere | Speeches and Statements - Tanzania Policy on Foreign Affairs in 1967

Wanatakia Heri ya Mwaka Mpya
 


mi nawashangaa sana hawa watu! hapo hajatukanwa kikwete wala CCM wala serikali ya CCM hapo aliyetukanwa ni MTANZANIA... nasikitika nikiona wakishangilia..



Hebu issue ya udactari weka pembeni weye unavyoona hapa nani hapa ni mpumbavu! yule anayeitwa Mbwa / toilet paper na anashangilia kuitwa hivo ... au yule anayepinga kwa si hivyo unavyonifikiria ....

mkuu hakikwanza narudia tena aliyetukanwa sio serikali bali wewe MTANZANIA..! nakushangaa ukikubali na kushangilia kuitwa mpumbavu! ... jitahidi basi utoke ndani ya huo upumbavu kwani mimi sipo huko.. nakushauri ujifunze nini maana ya patriotism..

ADIOS

Ok. Wewe Njiwa omba omba sana. Ndio maana kila kukicha hodi kwa majirani. Hadi wamekuchoka wanaanza kukuona huna maana wala umuhimu wowote katika maisha yako,ya familia na hata kwa binadamu wenzako.
 
umaskini ni janga Baya.. mtu anatembea na kaptula iliyotoboka nyuma kiasi cha kuacha sehemu kubwa ya makalio yake kuonekana, ukichukulia hata uwezo wa kununua kufuli hana, sasa akipita kunako kadamnasi la watu, kisha wananchi wakamcheka anakasirika huyoo na kuanza kudai aheshimike..
wewe TZ wewe, amka wewe, chapa kazi, acha ufisadi, tunza uzalendo, jenga miundombinu, kusanya kodi halali, trafiki waache maujingajinga yao, kisha tukishaimarisha utu, tujenge uchumi na uchumi ukikomaa shilingi yetu itapanda.. lazma ipande hadi tuipige kumbo sterling.. kisha nambie nani ambaye hatatuheshimu.. maskini anayekilia kuheshimiwa
.. anaudhii!
 
Back
Top Bottom