CHADEMA: Israel ituombe radhi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA: Israel ituombe radhi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by issenye, Dec 29, 2011.

 1. i

  issenye JF-Expert Member

  #1
  Dec 29, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 1,151
  Likes Received: 992
  Trophy Points: 280
  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimemtaka Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, kuitaka Serikali ya Israel kuwaomba radhi Watanzania kutokana na kauli ya Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo, Ehud Barak, kudai kuwa Tanzania si nchi ya muhimu wala ya maana.

  Aidha, chama hicho kupitia Kurugenzi yake ya Mambo ya Nje na Mahusiano ya Kimataifa kimemtaka Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Hussein Mwinyi, kueleza iwapo hatua hiyo ndiyo msingi wa mahusiano yaliyopo kati ya nchi hizo, hasa ikizingatiwa kuwa serikali imekuwa ikieleza kwamba Tanzania ina mahusiano mazuri ya kiulinzi na Israel.

  Kauli hiyo ilitolewa jana na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mambo ya Nje na Mahusiano ya Kimataifa wa CHADEMA kupitia mtandao wake wa kijamii.

  Waziri Barak alifanya mahojiano na Radio Israel na kutoa kauli ambayo imenukuliwa na vyombo mbalimbali vya habari vya nchi hiyo kuwa Tanzania si nchi ya muhimu wala ya maana hata kufikia hatua ya kuilinganisha na eneo ndani ya Libya linaloitwa Tripolitania.

  Mnyika alisema kupuuzwa huku kwa nchi yetu katika medani ya kimataifa kunatokana na sera mbovu ya mambo ya nje chini ya utawala wa sasa wa Chama cha Mapinduzi (CCM).

  "Tanzania imepoteza heshima katika siasa za dunia kutokana na diplomasia yetu kujikita katika kuomba omba kimataifa; pamoja na kuwa kimaneno na maandishi serikali inazungumza kuhusu diplomasia ya kiuchumi, kivitendo mahusiano yetu yamejengeka katika misingi ya utegemezi, kupungua kwa urari wa kibiashara na kuachia mianya ya uporwaji wa rasilimali," alisema.

  Alieleza kuwa kauli ya Waziri Barak ni muendelezo wa mataifa mbalimbali kuifanya Tanzania na baadhi ya nchi nyingine za Afrika kukosa heshima wala sauti katika siasa za kimataifa kama ambavyo serikali za Uingereza na Marekani zilivyoweka masharti yenye mwelekeo wa ukoloni mamboleo kuhusu masuala ya ushoga na usagaji.

  "Barua pekee ya Balozi wa heshima wa Tanzania nchini Israel, Kasbian Nuriel Chirich, kwenda kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel, Avigdor Lieberman ya kulaani matamshi hayo na kumkaribisha mwakilishi wa Israel kutembelea Tanzania haitoshi kuifanya serikali ya nchi hiyo kutambua athari za kidiplomasia za kauli iliyotolewa," alisema Mnyika.

  Mbunge huyo alieleza kuwa wakati wa uongozi wa awamu ya kwanza wa hayati Mwalimu Julius Nyerere, Tanzania ilikuwa na heshima na sauti kimataifa si tu katika jitihada za ukombozi kusini mwa Afrika bali pia katika mahusiano ya kisiasa, kiuchumi na kijamii baina ya nchi za Kusini na mataifa mengine duniani.

  Kutokana na hali hiyo, alisema iwapo hatua hazitachukuliwa kurejesha heshima na sauti ya Tanzania kimataifa, maamuzi mengi yatafanyika yenye athari kwa wananchi wengi bila ushiriki wao thabiti kama yanayoendelea hivi sasa kuhusu Mikataba ya Kiuchumi na Nchi za Jumuia ya Ulaya (EPA) yenye madhara kwa wakulima na wenye viwanda nchini.

  "Ni wakati sasa kwa Watanzania kuendelea kuunganisha nguvu ya umma kusimamia uwajibikaji na kufanya mabadiliko ya kimsingi ya kiuongozi, kisera na kimfumo ya kitaifa, ili kurejesha nafasi na heshima ya Tanzania kimataifa katika mazingira ya sasa ya ushindani wa kiuchumi, kiulinzi, kijamii na kisiasa," alisema.

  Source: Mimi mwenyewe mwana CHADEMA
   
 2. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #2
  Dec 29, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  hivi tunaposema dar sio itigi... tunakosea?? au msaki sio kambi ya fisi pia tunakosea sio?

  na kweli, kweli kabisa yani kweli tunategemea Membe atawaaambia jamaa watuombe radhi? na hata akisema wataomba?
   
 3. SOBY

  SOBY JF-Expert Member

  #3
  Dec 29, 2011
  Joined: Sep 19, 2011
  Messages: 1,265
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Tatizo letu mkuu hatujijui how irrelevant we are as a country.
   
 4. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #4
  Dec 29, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Hizo ni hisia za Israel,hata kama tukiwalazimisha waombe radhi,hizo zitabaki kuwa hisia zao siku zote!
   
 5. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #5
  Dec 29, 2011
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Hali hii ni matokeo ya serikali ya JK kuwa omba omba sana dunian
   
 6. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #6
  Dec 29, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,337
  Likes Received: 19,507
  Trophy Points: 280
  tanzania nchi ya vilaza..sisi tunaomba omba kila siku kwenye uombaji tupo level moja na afganistani huko kwa nini wasiwadharau
   
 7. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #7
  Dec 29, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  hilo nalo neno na pia njaa zetu kuzionesha mbele za watu...
   
 8. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #8
  Dec 29, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  kweli kabisa daily mkuu wa kaya anazunguka na kikombe cha kuomba kama matonya vile..
   
 9. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #9
  Dec 29, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  tutake tusitake... hata washikaji (type ya akina Musafiri Diof) huwa wanadharaulika!!!

  what we hear from this one minister may be a common word from europe na north america.... ukishakuwa ombaomba, kubali kudhalilika
   
 10. Mkuu wa chuo

  Mkuu wa chuo JF-Expert Member

  #10
  Dec 29, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,253
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  sasa Israel iwaombe radhi kwa kuwachana ukweli!
   
 11. F

  FUSO JF-Expert Member

  #11
  Dec 29, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,856
  Likes Received: 2,333
  Trophy Points: 280
  mi huwa natolea mifano tangu level ya kaya -- nyumba omba -omba au ukoo umba -omba huwa hauna heshima katika jamii. sasa sioni kosa walilofanya islael. huwezi kuwa unaomba omba tu bila kuwa na misingi yoyote ya kujitegemea ni aibu - wanatuaibisha watanzania pamoja na utajiri wote huu tunadhalilishwa?

  hii ni aibu kubwa sana, tena ukiunganisha na ile ya cameroon kwamba tuheshimu mashoga na wasagaji kuoana kama hatutaki hakuna pesa. aisee hii nalo linafunga mwaka 2011. njaa wakuu ni mbaya mno ukiendekeza.
   
 12. F

  FUSO JF-Expert Member

  #12
  Dec 29, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,856
  Likes Received: 2,333
  Trophy Points: 280
  israel ipo sahihi kabisa, serikali ya CCM ndiyo ituombe radhi sisi wananchi kwa sera zake zake mbovu zinazopelekea kutembeza bakuri kila kukicha as if sisi ni viwete.
   
 13. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #13
  Dec 29, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 0
  Kwani Israel imeongea uongo? Kama dege la kijeshi linatua nchini na Usalama wa Taifa wapo na linapakia Twiga na kupaa tena bila rais kujua hii nchi ina maana kweli?
   
 14. R

  Rafikikabisa JF-Expert Member

  #14
  Dec 29, 2011
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 252
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  jamani, tumedhalilika vya kutosha, tumenyanyswa na matamshi haya vya kutosha. Hatuwezi kuvumilia. Mimi kama mtanzania napendekeza tutangaze mgogoro na hiyo nchi sijui inaitwa Israel.

  Hiyo nchi haina maana yoyote katika medani ya maisha ya kila siku ya mtanzania. Nasi tuwaambie kuwa Israel si nchi muhimu Tanzania. kuomba radhi tu hakutoshi maji yakiisha mwagika hayazoleki.

  Huyu jamaa katamka haya maneno kutoka rohoni mwake hata akiomba radhi haitasaidia kesha tudharirisha. Cha muhimu tuangalie tumejikwaa wapi, kesho na mwingine atatamuka hivi hivi.

  Tatizo kubwa letu tumekuwa watu wa kuwasujudia hawa watu weupe. Mtu akisha kuwa mweupe sisi kila goti litapigwa sasa tukome. Kila siku tumebaki katika kushabikia siasa za maji taka basi.
   
 15. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #15
  Dec 29, 2011
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Dar si Itigi
   
 16. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #16
  Dec 29, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  YES Tanzania sio nchi ya maana na muhimu...well said minister barak
   
 17. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #17
  Dec 29, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mkuu SOBY, hata siku moja sintonunua fikra kama hizo!!!

  Hizo wenzangu kazipelekeni hukooo!!! Kinachotufanya tuwe irrelevant ni nini hasa kama taifa? Labda kama kuna baadhi ya mambo ambayo wakuu wetu hutenda kinyume na matarajio ya ulimwengu hivyo kutufanya tusukumwe moja kwa moja jalalani.

  Lakini hata tukihisiwa jalala, ni jukumu letu kukataa huo muonekano wa ujala machoni mwa ulimwengu kwa kuwa sisi tunawathamini sana tu tena kwa uzito wote hivyo ni matarajio yetu kurudishiwa heshma endapo hakina cha ajabu kilichofichama machoni mwetu wananchi.

   
 18. F

  FUSO JF-Expert Member

  #18
  Dec 29, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,856
  Likes Received: 2,333
  Trophy Points: 280
  mkuu hata ukitangaza mgogoro na nchi ya islael haitasaidia kitu, wewe umeambiwa ukweli mwamba ni omba-omba kwani uongo? na ndiyo maana mataifa mengine yakasema kama hautaukubali ushoga na usagaji basi BAKURI lako likipita nchi zao hupati kitu, upo? je utatangaza mgogoro na huko nako?
   
 19. Lighondi

  Lighondi JF-Expert Member

  #19
  Dec 29, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 585
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Hilo dege la jeshi lina uafadhali, hawa mapacha watatu Richmondi, dowanz na symbioni tunao miaka nenda miaka rudi mkuu wa kaya katuambia hata hawajui!! Lakini anatetea walipwe tuuu pesa yao. Jifanye wewe ni balozi unayewakilisha nchi yako hapa TZ halafu waziri Mkulo anakujia kukuomba uchangie kwenye bajeti yake ya mwaka ujao!! Katika mazingira kama haya nani atakuheshimu? Tunastahili kudharaulika na nchi zingine. Naungana na wachangiaji wengine kwamba wanaostahili kutuomba radhi ni sisiemu iliyotengeneza na kutekeleza sera ambazo zimetufikisha hapa.

  Ni aibu sana.
   
 20. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #20
  Dec 29, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kauli hii jibu lake laenda mbali kidogo na wala mtu akifupisha upana wa fikra ni makosa sana.

  Kitendo cha kuruhusu taifa mojawapo la Ghuba kuhamia kwenye mbuga zetu likiwa na viashirio vyote vya tawala zake za kujitegemea kabisa ndani ya nchi yetu, na vile vile jibu la jinsi gani tumekua na mchango kwa taifa la Irani ni tabu tupu hadi hapa.

  Wakati tukionyesha kuchanganyikiwa na hiyo kauli tata to kwa taifa teule la Israel, mwenzetu Rostam Aziz kule Kigoma anaelewa fika kitu gani kinachomaanishwa hadi hapo.
   
Loading...