Chadema Iringa Mei 19, 2011: Picha na Matukio

MAANDAMANO ya kufunga mikutano ya kitaifa ya mikoa ya yanda za juu kusini ya chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) yatikisa mji wa Iringa huku chama cha mapinduzi (CCM) kikikwama kuhujumu maandamano hayo pamoja na kujaribu kuwachanganya wananchi kwa kuwatoa madarasani wanafunzi shule ya sekondari ya wazazi Mwembetogwa ili kuushikiria kwa muda uwanja wa Mwembetogwa .

Mbali ya mbinu hizo pia baadhi ya vijana wanaosadikika kuwa walipandikizwa na CCM kuingia katika maandamano hayo ili kuvuruga waliishia kunusurika kichapo baada ya mmoja kuangusha kofia na skafu ya CCM iliyochanwa na kuchomwa moto majira ya saa 5 asubuhi kabla ya kuanza maandamano hayo eneo la Kihesa .

Uchunguzi uliofanywa na mtandao huu wa Francis Godwin ni mzee wa matukio daima umebaini kuwepo kwa njama za hali ya juu kwa CCM kutaka kuvuruga maandamano hayo ambapo njama ya wazi ni ile ya kuuzuia uwanja wa Mwembetogwa ili Chadema isitumie kwa mkutano huo na badala yake kuwatoa wanafunzi madarasani na kuutumia uwanja huo huku baadhi ya wazazi wakilalamikia hatua hiyo ya uongozi wa shule hiyo kukubali kutumiwa kisiasa na CCM.

Mtandao huu wa Francis Godwin ni mzee wa matukio daima ulimshuhudia mkuu shule hiyo Ahmed Mbata akiwa na mwalimu mmoja katika uwanja huo wa Mwembetogwa akisimamia zoezi la wanafunzi hao kufanya tamasha ambalo linadaiwa kuanza kuandaliwa ndani ya wiki moja baada ya kutokana na agizo la CCM mkoa kama njia ya kuhujumu maandamano hayo ya Chadema Taifa.


Hata hivyo baadhi ya wananchi ambao walizoea uwanja huo wa Mwembetogwa kama uwanja mkuu wa mikutano ya Chadema walionyesha kubabaika na kujikuta wakisubiri kwa muda katika uwanja huo bila kuona rangi ya bendera za Chadema zaidi ya sare za wanafunzi hao hali iliyopelekea kutoka barabara kuu ya Iringa -Dodoma na kuungana na maandamano hayo huku baadhi yao walilazimika kuwauliza viongozi wa Chadema kwa simu.


Hata hivyo katika tamasha hilo lililobatizwa kuwa ni tamasha la kusaka vipaji kwa wanafunzi baadhi ya wanafunzi walisema kuwa tamasha hilo limeandaliwa na CCM na sio uongozi wa shule hiyo kama inavyoelezwa na baadhi ya watu.

"….Jana vionngozi wa CCM walifika shuleni kwetu na kushinda katika ofisi ya mkuu wa shule kwa ajili ya kuandaa tamasha hili …japo tunashindwa kujua lengo la CCM kuandaa tamasha hili kwani kama lingekuwa ni tamasha la shule tuna ukumbi mkubwa wa shule na siku zote tumekuwa tukifanyia katika ukumbi huo ila leo tumeshangazwa kuambia tuje hapa uwanjani ambako hatujawahi kufanyia tamasha kama hili la ghafla ….wana sema ni bonanza la shule mbona katika ratiba za mabonanza yetu hakuna kitu kama hiki"

Mmoja kati ya walimu wa shule hiyo alimweleza mwandishi wa habari hizi kuwa suala hilo limezua mgawanyiko mkubwa katika shule hiyo baada ya mkuu wa shule kuingiza ratiba ambayo haikuwepo na ndio sababu ya walimu wote kutofika katika uwanja huo kuungana na mkuu wa shule ambaye ni kada wa CCM.

Jitihada za kumpata mkuu wa shule hiyo ili kuweza kuelezea malengo ya tamasha hilo hazikuweza kuzaa matunda .

Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Iringa mjini Abed Kiponza alipotafutwa kwa njia ya simu na mtandao huu wa Francis Godwin ni mzee wa matukio daima ili kujibia madai ya wanafunzi hao kuwa viongozi hao wa CCM walifika shuleni hapo ili kupanga mbinu hiyo ya kuhujumu mkutano wa Chadema ,alikanusha madai hayo na kuwa kwa sasa yeye yupo chuo kikuu huria cha Tanzania akijisomea kwa zaidi ya wiki sasa na hajapata kupata muda za kuacha darasa hata siku moja.

"mimi ni mwisilam na sijazoea kusema uongo mimi nasoma huku Openi Universt hata sasa nikija hapo ulipo nitakuwa na vifaa vyangu vya shule"

Mbunge wa jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa na mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Chiku Abwao walisema kuwa CCM ilipanga kuvuruga maandamano hayo ila imeshindwa na nguvu ya umma baada ya wananchi kukubali kutembea umbali wa zaidi ya kilometa zaidi ya 5 kutoka Kihesa hadi Mlandege .



Imewekwa na Francis Godwin ni Iringa na matukio
 
aka mabanzi......

si mchezo mkuu mambo ya ipamba. asante mkuu tupo pamoja ktk ukombozi wa taifa, huku wazungu wananiambia hawaifagilii kabisa CCM. Kinachoendelea huko jamaa wanafuatilia dakika kwa dakika na ripoti inatumwa kila siku, wamechoshwa na hao gambas, hawana mchezo CCM lazima iondoke madaraki hata kama itachukua muda.
 
IMG_8142.JPG
 
hapa ni kazi tu


IMG_8110.JPG

Chadema eti chama cha Wachanga, aka chama cha ukoo, hawa nao wenye ngozi nyeupe wanashagilia ukoo wa nani? Hawa wanaoandamani ni wachaga? Sikujua kama kuna wachaga wazungu, hehehe mwaka huu watu maduka ya madawa yaongezee vidonge vya kuteremsha BP.
 
si mchezo mkuu mambo ya ipamba. asante mkuu tupo pamoja ktk ukombozi wa taifa, huku wazungu wananiambia hawaifagilii kabisa CCM. Kinachoendelea huko jamaa wanafuatilia dakika kwa dakika na ripoti inatumwa kila siku, wamechoshwa na hao gambas, hawana mchezo CCM lazima iondoke madaraki hata kama itachukua muda.


wakumbushe kuhusu hela yetu ya rada kaka......
 
wazee hawa ni kamati ya shule ya mwembetogwa walikuwa wamtumwa na ccm ili kuzuioa chadema kutumia uwanja wa shule hiyo kwa shughuli ya leo


IMG_8179.JPG

Nyuso za wasiwasi na dalili ya kukata tamaa inaashiria mkao wao ulivyo
 
sorry, nilikuwa ninamjibu mafilili anayedai CDM haiwapendi wakulima lakini ujumbe wangu ukaenda sehemu ambayo sikutarajia.
 
Sita alisha iba pesa wakati akiwa waziri wa ujenzi kwahiyo yeye as well ni fisadi papa... tuangalia history tusirukie habari na kuwasafisha hao viongozi papa; nadhani yeye ni same as the owner of RAI Newspaper
 
Chadema eti chama cha Wachanga, aka chama cha ukoo, hawa nao wenye ngozi nyeupe wanashagilia ukoo wa nani? Hawa wanaoandamani ni wachaga? Sikujua kama kuna wachaga wazungu, hehehe mwaka huu watu maduka ya madawa yaongezee vidonge vya kuteremsha BP.
kwa mujibu wa nape ni lazima wafuatao wapewe majina yafuatayo ili cdm ikae vizuri:dr w. Silayo
-Mabere Marandu
-Prof.A. Sawaya
-Zitto Kavishe
-FRendriki Mnganya
-Tindu Laswai
 
  • Thanks
Reactions: Bob
wazee hawa ni kamati ya shule ya mwembetogwa walikuwa wamtumwa na ccm ili kuzuioa chadema kutumia uwanja wa shule hiyo kwa shughuli ya leo


IMG_8179.JPG
Haa haa haa!!!!!!!!!!!. Ama kweli chadema kinawakosesha watu usingizi wasiokuwa na maisha magumu. Kwa stahili hii utafikiri wanaomboleza kifo cha ccm. Halafu mbona wanajihami hami sana au wanaogopa nguvu ya umma. Inaelekea hawajaisoma historia ya Tarime ikawaingia akilini. Na wahehe, wabena walivyo kama moto wa kifuu.
 
Back
Top Bottom